Tatizo siyo watu wanaoishi "mabondeni" bali ni wale wanaoishi "magogoni"

Naona hawa ni political accessories pia......imagine ukiwaondoa msimbazi yoote ni jinsi gani Zungu atapungukiwa kura....maana jimbo lake haliwezi kupimwa viwanja vipya na hivo wapiga kura wake watahamia majimbo mengine.......ndio maana haishi kelele wanapotakiwa kuhama hawa watu......na sasa yuko kimya kwenye haya majanga
 
Watu wa Magogoni hawana kosa hata kigogo, wamepiga baragumu la kutosha kuhusu hatari za kuishi mabondeni, lakini watu wa mabondeni wameweka pamba masikioni. Isitoshe baadhi ya watu wa mabondeni wana nyumba za thamani sana na ni waeleewa ambao wangeonyesha mfano, lakini wanendelea tu kuweka pamba masikioni.
Kwa hiyo Magogoni, pamoja na mamlaka aliyokuwa nayo, watu wakikaidi amri halali hana uwezo wa kuwafanya chochote? usitake kuniambia kuwa hatuma mamlaka zenye nguvu za ku-enforce sheria na maagizo halali
 
Watanzania ni rahisi kusahau sana.

Nakumbuka Mzee Makamba alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alikemea sana swala la watu kuishi kwenye mabonde. Alisema hivi, "Nyie mnoapenda sana kujenga na kuishi kwenye mabonde mmekuwa vyura?"


Tuna mazoea ya kufanya vitu kienyeji kienyeji tu kwa kutumia short cuts na kutofuata sheria na hao wanaosimamia hizo sheria za mipango miji na kutoa vibali vya kujenga mabondeni ni watu wanaotakiwa kushitakiwa na kutupwa jela.

Hii culture ya impunity inatumaliza sana.
 
Kuishi dalisalama raha!!

Nini maana ya Serikali au Watawala. Hawa wetu ni watawala wanaotumia utawala wa mapenzi. Kama nchi haina sheria, sheria ndogo basi waseme ili tuhamishie lawama kwa wanaojenga mabondeni kwa 100% la sivyo waliojenga mabondeni wanabeba 30% ya lawana na wa Magogoni 70.
 
Ni vigumu kuwalaumu watu waliojenga mabondeni. Nyumba haijengwi kwa siku moja, serikali ilikuwa wapi wakati wanajenga? Na huwezi kusema kuwa wamevunja sheria kwa kujenga mabondeni kwa sababu serikali ipo! Kama serikali inaweza kutabiri vurugu, na uwepo wa Al-shaabab wanashindwaji kusimamia ujenzi wa nyumba sehemu za mabondeni? Watu hawa wanapata huduma muhimu za jamii, i.e umeme, sasa leo wanawakana kwa vipi?
yaani mtu unakwenda kujenga mahali ambapo unajua pana hatarii ili serikali ikuzuie, akili kweli hizo?
 
Tatizo ni wewe Mwanakijiji.
Wewe unataka kupolitisize hili swala bila sababu za msingi,
Kama kweli tunataka solution kamilifu ya kuepuka aina ya janga lililotokea ni kuyainua
maeneo ya mabondeni ili dar yote ama iwe tambalale au iwe milima, na hii
maana yake ni kwamba Mungu alifanya kosa kubwa sana wakati analiumba eneo
hili la dunia kwa kuliwekea bonde/mabonde.

Nani yuko tayari kuona serikali inajiingiza kwenye project kama hiyo, wewe
mwanakijiji utakuwa ni mtu wa kwanza kuipinga project hiyo. Bisha.

Tutalazimisha kwamba watu wa magogoni wanawajibu wa kuhakikisha miondombinu
inaboreshwa ili kuepuka majanga haya, lakini ukweli ni kwamba Janga likija hata miundombinu
iwe bora namna gani ni lazima liache madhara, wote tunakumbuka kilichotokea Japani
recently, nani anaweza kuwalaumu watawala wa Japani kwa madhara yaliyotokea?

Au tutataka watu wa mabondeni wahame, alafu ardhi hiyo itumike vipi? ibaki ukiwa?

Ndio maana nasema tatizo ni wewe mwanakijiji sababu, itafikia hatua tutamlaumu Mungu
kwa kuumba mvua.
 
Hii serikali bwana! Lipi wataliweza iwapo wameshindwa kuwaondoa ndugu zetu wanaoishi mabondeni na kuwatafutia sehemu zingine ambazo ni salama zaidi? Mimi naona hapa ni lack of seriousness. Serikali ikiwa serious watu wataondoka mabondeni. Najua kuwa watu watasema kuwa wananchi nao wanachangia. Hii si kweli serikali makini husimamia sera na sheria zake. Hapa Tanzania sheria hazifuatwi na hakuna anayezisimamia. Matokeo yake watu wataendelea kuteseka huku serikali ikisingizia kuwa watu watu hawataki kuhama mabondeni.
Tatzo ni la hawa waishio 'magogoni',kwasababu:-

1. Wanadai watu wanakatazwa kujenga mabondeni,mbona wanawapelekea huduma muhimu kama vile umeme kama kweli watu hawatakiwi kujenga mabondeni wasingewapa huduma hizo muhimu kuonesha kuwa hawatakiwi kuishi kule..

2. Ukiona serikali imewafukuza watu mabondeni ujue wana maslahi na hicho kiwanja(kuna kigogo ana shida nacho/kuna mzungu kapewa kwa jina la uwekezaji)..

CONCLUSION:-
serikali legelege haiwezi ikafanya maamuzi sahii/yenye msimamo..
 
Mimi sasa naona sasa it is time hawa watu wahame, kazi ya magogoni ni kuhakikisha inalinda raslimali yake ambayo watu pia ni resource.

Ila kama wanataka ku depopulate watu ok,wawaache watu waendelee kuishi huko.

Climate change ina effect mbaya sana, nayo ni pamoja na uwepo wa ELNINO. In ten years to come mafuriko huenda yakatokea. This time degradation itakuwa haina mfano.

Anyway Japan ipo kwenye eneo la kutokea earthquake but still wanaishi, ila wame-take measures kama kuwa na nyumba nyepesi, hata likiwaangukia hampati madhara.

HAPO MABONDENI WAJENGE MAGOROFA na watu waishi kuanzia floor ya tano ila msingi uwe umeenda shule
 
Ardhi haiwezikosa cha kufanyia ni ubunifu na uamuzi tu.tutafufua kilimo cha mpunga! Ilimradi maisha ya wenzetu yawe salama
 
Tatizo ni wale wa Magogoni! Kikubwa hapa ni umasikini ambao visababishi vyake kwa kiasi kikubwa ni wale wa magogoni kwani ndio wanaosimamia rasilimali za wale walio ona ni bora wajenge jangwani, Msimbazi (mabondeni) ili wawe karibu na mjini aka Kariakoo ambapo ndipo ofisi za wanyonge zilipo.

Katika hali hii kila mmoja anaangalia uwezekano wa kulipa nauli ya gari moja ama kutokulipa kabisa kwa maana ya kutembea kwa miguu.

Pili ni kwamba wa Magogoni njia za rushwa zinasababisha mpaka kukaba mpaka serikali za mitaa kutoa namba za nyumba ili wapate pesa. Nyumba zote zilizosombwa ama zilizozingirwa na maji zina namba.
 
mabondeni vs magogoni.
swali, nani ni dependent variable na nani ni independent variable??
 
-Mlitakiwa kuviendeleza vijiji vya ujamaa hata kama visingejenga ujamaa. Mkaviacha.
-Mlitakiwa kuyaendesha vizuri mashirika ya umma ili angalau tulinde na kuendeleza ajira. Mkayatafuna. Yakafa.
-Dar imejaa. Watu bado wanazidi kuja. Hakuna namna ya kuwazuia. Hawawezi kuhama mabondeni leo.
 
Tanzania ina maeneo mengi sana,hawawezi kosa pa kwenda.Mimi nilishawahi wauliza baadhi yao,walinijibu kuwa wanapenda kuishi pale jangwani kwa sababu ni karibu na mjini,so wanakwenda kwa mguu tu.Hiyo siyo sababu ya kumfanya mtu ariski maisha yake.

Hiyo ni sababu kubwa sana. Hata hivyo Serikali haina msaada kwa wanaotaka kujenga sehemu Salama. Hata wewe ukitaka kiwanja jaribu kuulizia mamilioni utakayoambiwa. Hata hivi karibuni serikali ilipima viwanja kule Tabata, bei ilikuwa Mimnimum ni milioni tisa. Kwa maisha haya ya waTZ wangapi watajenga sehemu salama?
 
Chama legelege huzaa serikali legelege, nenda Zambia Lusaka ukitaka kujenga tu kuna vigezo usipovifikia huwezi kujenga hata kama ni maeneo ambayo hayajapimwa, mfano wa vigezo ni upitishaji wa umeme, maji, uhifadhi wa maji taka nk. Kwanini sisi tunashindwa ni kwamba sheria hazipo au hazisimamiwi? MM mimi binafsi nasema tatizo liko Magogoni kwakuwa wamekuwa walegevu hata katika mambo ya msingi ya nchi yetu.

Leo hii kuna mpango wa kuendeleza kigamboni sijui ni ndoto au kweli lakini ukiangalia jiji la dsm lingesimamiwa vizuri miaka ya 80/90 leo tusingekuwa hapa tulipo, hofu ya kupoteza madaraka ya kisiasa ni moja ya vigezo vinavyofanya ujenzi holela uendelee maeneo mengi ya nchi yetu kwa kuogopa kuwabugudhi wapiga kura. Kazi ya serikali sio kupiga kelele ila ni kutekeleza kwa vitenhaado, huwezi kusema serikali imepiga kelele kiasi cha kutosha bila utekelezaji halafu itoshe..

Tanzania ya leo inataka chama imara kitakochokuwa na serikali imara ili kuweza kutekeleza kwa vitendo malengo ya maendeleo yaliyokwama kwa miongo kadhaa.
 
Watu wa magogoni ndio wana makosa!!
Utajuaje kuwa eneo fulani si makazi kulingana na mpango mji? Ni lazima uende ardhi wakafanye survey na ikibidi wakupimie eneo lako.
Juzijuzi tu nina kashamba kangu huko Bunju kabla sijaanza kuweka kanyumba kangu nikajaribu kufanya utaratibu wa kukapima, niliambiwa niandae Tsh 1'500'000/=. Nikaongezea Tsh 500'000/= ikawa mil. 2 nikanyanyua chumba sebule ndo nakokaa nikimuomba Mola lisitokee la kutokea!
Gharama za upimaji viwanja ziko juu mno!

Hii Serikali ni Mabwege sana. Nchi za wenzentu suala la kupima ardhi si suala la mwananchi. Sasa kazi yao ni nini?
Wanatakiwa wapime maeneo kabla ya kufuatwa ofisini. Hata nguzo za umeme inabidi unue wewe.
Kweli hii Serikali inamfurahisha Faiza Foxy na Na Vichwa maji wengine.
 
Watanzania ni rahisi kusahau sana. Nakumbuka Mzee Makamba alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alikemea sana swala la watu kuishi kwenye mabonde. Alisema hivi, "Nyie mnoapenda sana kujenga na kuishi kwenye mabonde mmekuwa vyura?" Tuna mazoea ya kufanya vitu kienyeji kienyeji tu kwa kutumia short cuts na kutofuata sheria na hao wanaosimamia hizo sheria za mipango miji na kutoa vibali vya kujenga mabondeni ni watu wanaotakiwa kushitakiwa na kutupwa jela. Hii culture ya impunity inatumaliza sana.

Ukifuata utaratibu ni Kero kubwa zaidi maana ni kama unaenda kubembeleza huduma wakati ni haki ya Msingi. Hivi serikali imeshindwa nini kupima viwanja???
 
Unajua serikali ikiona watu wanajenga kwenye njia ya mto,kwa mfano,halafu ikakaa kimya,nyumba zikaisha,
halafu bila aibu inaenda kukusanya kodi za viwanja,na kujenga miundombinu huko,basi serikali hiyo ni wauaji!!!
MY TAKE:
1:Wananchi walio jenga mabondeni ni wajinga
2:Serikali kilema hii ni katili na pumbavu
 
-Ujamaa haukutufaa. Mwalimu akashindwa. Sasa hivi tunamtukana kwelikweli.
-Tunajenga ubepari sasa. Wa mabondeni lazima wawepo. Wa Masaki, Mbezi, Tegeta Masaiti watahangaishwa na madaraja tu.
-Wa mabondeni kuhamia Pugu Kinyamwezi, Kongowe,..., nauli ya kuja mjini watatoa wapi?
 
Tatizo lipo kwa wakazi wa magogoni. Serikali inajua sababu za kuwa legelege katika kuwahamisha watu wa mabondeni. Hii ni kwa sababu sheria ya kuwahamisha wakazi hao wa mabondeni inawagusa pia waliojenga kwenye fukwe za bahari na wale waliojenga mabangalow kwenye mito mbali mbali nchini hasa wanapoishi vigogo.

So kama ni kuwahamisha waliovunja sheria za mipango miji na sheria za mazingira. Ni vyema wote hawa wachukuliwe hatua, serikali isilaumu tu walojenga kwenye kingo za mto msimbazi na kuwaacha waliojenga kwenye fukwe za bahari ya hindi. Prof. Tibaijuka alijipambanua km waziri ambaye angeweza kulishughulikia hili tatizo, lakini sijui kaishia wapi. Serikali legelege hufanya mambo lege lege siku zote.
 
Back
Top Bottom