Tatizo siyo "Elimu ndogo ya Wananchi" au "Elimu ya Uraia"!

Mwanakijii swali lako ni gumu sana. Kuna mambo mengi sana yanendelea kwenye jamii yetu, lakini moja kubwa ni kuwa ni lazima tukubali kuwa "ujinga" na "umasiki" tulionao watanzania tulio wengi ndio unatufanya tuwe hapa tulipo.

Kuna watu ambao mpaka leo wakisikia neno wapinzani wanaona kuwa wapinzani ni watu wahuni, lakini is it true kuwa ni wahuni? May be yes may be No, lakini generally kwa majority of Tanzanians ni wahuni. Na hii inaanza toka siku Nyerere alipomuweka Mzee Zuberi Mtemvu kwenye kundi hilo. Kuna watu mpaka sasa hawana critical minds za kuweza kuchanganua yanayoendelea TAnzania. Kama tungekuwa na watu hao wa kutosha CCM at thsi moment ingekuwa na wakati mgumu.

Umasikini nao unachangia sana, leo hii kuna watu wanaweza kumpigia mtu kura kwa kupewa Pilau, Nyama (yes wapo wengi sana hasa maeneo ya Pwani ambako vyakula kama hivi ni almasi). Kuna wengine huko bara wakipewa kitenge, Tshirt, lita moja ya mafuta ya kupikia wanaunulika kiurahisi sana. hata wengine wanahingwa nyadhifa au pesa kuisaliti nchi. Kwa hiyo siwezi kukataa kuwa kuna ujinga mwingi na umaskini ndio unawafanya watanzania tuburuzwe.

Kuna mwanasiana mmoja alifurahi sana na kusema hayo ya jamiiforums yanaishia kwenye internet tu, hayafiki kwa watu wanaotupigia kura hata mkitaka kuandika andikeni usiku kucha. So he knew that what was said in here was the truth and still he was confident that pamoja na wizi wote huo na dhuluma yote ya EPA Rada Richmond ndege etc, bado wanatamba kuwa watachaguliwa tu. Kisa ni kuwa wananchi bado hawana elimu ya yanayotokea kwenye nchi yao.

Ukitaka kujua angalia hiki. Nenda nje ya sehemu unayokaa, picha picha 100 maeneo ya karibu, halafu do the same baada ya miaka mitano(unaweza kuona kuwa hali imebadilika for worse) lakini angalia kwenye upigaji kura, CCM ile ile inapata ushindi tena mkubwa zaidi. Why? umasikini na ujinga ni political capital ya wanasiasa.
 
Kwanini vijijini watu wameweza kuwaangusha vigogo wakati tunaambiwa hawana elimu au ujuzi mkubwa wa mambo ya elimu ya kiraia?
 
Back
Top Bottom