Tatizo siyo "Elimu ndogo ya Wananchi" au "Elimu ya Uraia"!

Mmh! Mwanakijiji wakati mwingine bwana! Hoja zake zimekaa mshazari.

Wewe ongea/andika tu mbele ya laptop. Mimi nakula vumbi huku uswekeni. Nakuhakikishia wananchi wetu hakuna wanaloelewa. Wapo wapo tu. Kutumia kigezo cha kura za Mrema 1995, hiyo ni flaw mzee wangu. Kama wananchi wangekuwa wana uelewa, Mrema hakustahili kura, kwani hakuwa kiongozi mzuri. Alikuwa dikteta, na ndumila kuwili.
 
Nyerere alileta mwamko wa upinzani, sidhani. Nyerere enzi zake aliweka wapinzani kizuizini,

Haya madudu jamani mnayatoaga wapi? Wapinzani waliowekwa kizuizi ni kina nani pasipo sababu?

akasema makabila makubwa km wachagga, wahaya nk ni wakabila

Duh.. haya aliyasema haya lini na wapi?

na akaunda utaratibu unatumika hadi leo ambapo minority ndio hutoa maraisi.

Minority wa kitu gani? hizi dhana nyingine sijui zinatoka wapi? Rais lazima awe mmoja tu kila baada ya miaka 5, sasa makabila yenyewe yako zaidi ya 120.. kila Kabila likisema liweze kutoa Rais japo mara moja guess what.. kuna makabila hatutaishi kuona yakitoa marais!
 
Hebu ngoja turudi nyuma nadhani watu wanafikiri tunazungumza tu; kabla ya kuja mfumo wa vyama vingi kulikuwa na vitu kadhaa ambavyo vimefanyika kwa Tanzania nzima.

  • Elimu ya kujua kusoma na kuandika ilikuwa imeenea karibu sehemu zote
  • Radio ambacho ndicho kilikuwa chanzo kizuri cha habari kilikuwa na vipindi vyenye kutoa elimu sana kwa wananchi hadi kule madarasani watoto nchi nzima waliweza kukitumia kujifunza. Vipindi kama "Mikingamo" na matangazo ya kuhamasisha vita dhidi ya ufisadi "Liangalieni limbukeni hili, halina haya".. yalikuwa yanajulikana. Wananchi walikuwa na taarifa za yanayoendelea nchini na uongozi wao
  • Wananchi waliweza kuwakataa viongozi wabovu kiasi kwamba kwa sababu mfumo wa wakati ule uliruhusu kura kupigwa kwa kuangalia mtu na utendaji wake masuala ya rushwa katika kampeni hayakuwa pervasive kama ilivyo sasa. Matokeo yake nina mifano mingi ya viongozi ambao waliangushwa katika kura
  • Somo la siasa lilifundishwa nchi nzima na kuwafanya wananchi wajue mfumo wa utawala wao na siasa za kimataifa. Mwamko wa kisiasa ulipandikizwa katika majeshi yetu, na taasisi mbalimbali za siasa, tulikuwa na mikutano ya kisiasa na mijadala ya kisiasa. Kiasi kwamba ukiangalia hata wengi wetu ambao leo tunaona tumeamka kwa kweli ni mazao ya mfumo ule wa kisiasa kiasi kwamba waliopingana nao bado wanapingana nao, na wengine wanauelewa vizuri zaidi. Na utaona kumbe wengi wanaotaka mabadiliko sasa hivi ni wale wa kizazi kile. We fikiria vijana wa "kizazi kipya" ndio leo wanasimama kutukuza CCM!
Mara nyingi watu wanashtushwa wakisikia sijui mwanakijiji fulani kambana waziri au rais kijijini huko wanashangaa! Mimi sishangai kwa sababu najua kwa muda mrefu vijijini kumekuwa na siasa za ndani sana na uelewa mkubwa. Uelewa kwamba uongozi mbaya haufai. Ndio maana utaona hata leo hii ni vijijini kuna mwamko mzuri zaidi wa kupokea sera za upinzani kuliko mijini. Kigoma mjini, Karatu, na maeneo mengine wananchi wamechagua wapinzani kwa muda mrefu!

Haiitaji shahada au diploma kujua uongozi mbovu, tangu zamani vijijinii wananchi wamewaelewa viongozi wabovu na kuwatimua. Tatizo liko kwa hawa wenzetu wa mjini ambao kwa kweli wamezoea kuishi katika mfumo wa kitawala wa ufisadi, wamevuna matunda yake na wanayafurahia.. Hawa ndio wagumu kuiachilia CCM kwani mafanikio yao yamefungamana kabisa na mafanikio ya CCM.
 
Wakuu zangu,
Kwanza inabidi sisi wenyewe hapa kuwa wasikivu na wenye kukubali hoja kwa mtazamo wake kisha kupambanua ukweli. Swala la kupembua linahitaji sana muda wa kufikiri kwa sababu tunapobishana juu ya hulka ya Watanzania kwa ujumla wake inakuwa kazi kubwa zaidi kwa sababu sii swala la kupembua pumba na mchele tu isipokuwa kuna mchanga ndani yake na kama mjuavyo Pilau lenye mchanga haliliki.

Mimi naamini kabisa kwamba Watanzania tuna matatizo makubwa sana ya EXPOSURE na hakika elimu yaweza kuchangia lakini kikubwa zaidi ni UTUMWA wa akili na ULIMBUKENI ambavyo vyote hivi havitokani na elimu ya darasa isipokuwa - Elimu ya Uraia. Ifike wakati watu tukubali kwamba mambo mengi yanayotokea ama tunayoyafanya nchini hayana dawa ya elimu ya darasa, isipokuwa wananchi bado wana fikra za KUTAWALIWA kiasi kwamba leo hii hata ukiwauliza Watanzania wakupe tofauti baina ya kutawaliwa na mkoloni au na CCM sidhani kama wengi wanafahamu.

CCM wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kupotosha elimu ya Uraia kwa wananchi wake na kuwajaza ujinga wa Unyenyekevu kiasi kwamba CCM imekuwa ni IMANI ya watu badala ya chombo hiki kuwa ni chama cha Kisiasa. Unyenyekevu wa wananchi kutoka kutawaliwa na mkoloni umehamia ktk utawala wa chama CCM na viongozi wote wa chama wanatisha baada ya kujazwa woga (fear) hivyo kunyenyekewa kama wakoloni na hakika wanapenda na kuridhika na mfumo huu..

Utawala wa CCM umeweza kujenga imani ya Unyenyekevu kama mbinu ya kuhakikisha Amini na Utulivu nchini badala ya kufundisha Uzalendo. Na ndio maana mafisadi wote kina Lowassa na mzee wa vijisenti Chenge na wengineo wameweza kupokelewa kwa shangwe huko makwao baada ya kuwaibia wananchi Mabilioni. Waulize wasomi watakwambia bora kaiba Lowassa fedha itazunguka humu humu badala ya mwekezaji ikiwa kama ni unyenyenyevu kwa viongozi hawa..Hii ndio mind set ya wananchi kwa ujumla.

Na kwa sababu CCM haina tofauti na utawala wa mkoloni ambao ilani yao ya kwanza ni kulindana imeshindwa kuchukua hatua yeyote dhidi ya mafisadi hao. Hakuna sababu ya ndugu, mzazi au rafiki kufurahia mtu anapoiba fedha toka shirika au benki akapewa sifa za ujasiri kama sii akili ya kitumwa. Na hakuna sababu hata kidogo ya mtu kuwanyanyasa wananchi na fedha ya wizi au dhulma pasipo sheria huru kuchukua mkondo wake. Hivyo basi tumeendeleza mfumo wa Unyenyekevu ktk utawala wa ukoloni mamboleo, badala ya uhuru wetu kuzaa Uzalendo.

Na ukitazama enzi za mkoloni, watawala wetu iwe wazungu au waarabu waliweza kunyenyekewa na kulindwa hata wakifanya makosa makubwa dhidi ya watawaliwa. Na hakika kuwaibia wakoloni au mzungu ilikuwa sifa kubwa kwa wananchi kwa sababu iliweza kudumaza uchumi wao. Leo hii watu wanaibia serikali yetu kwa mtazamo sawa na mkoloni. tazameni kina RA na matajiri wote nchini, wote hawa wananyenyekewa sii kwa mchango wao ktk uchumi wa nchi yetu isipokuwa kwa nguvu ya fedha zao kuweza kununua sheria ya unyenyekevu. Nimewahi kusema kwamba Unyenyekevu ni wa Mungu pekee, binadamu tunapeana heshima. Tukitumia Unyenyekevu kama msingi wa amani kwa binadamu uta replace heshima ambayo ndiyo chachu ya Uzalendo kwa jamii iliyokuwa huru na yenye kuthamini haki na usawa.

Hivyo, kutokana na akili hii ya Utumwa (Unyenyekevu) ambayo uhuru wetu umeshindwa kuukana na kufundisha Uzalendo utakao hakikiwa na sheria kama vile miiko na maadili ya viongozi, tumejikuta taifa zima tukirudi ktk kutawaliwa kiakili. CCM imekuwa kama dini badala ya chama cha kisiasa na yawezekana pia Nyerere amechangia kwa kiasi kikubwa sana kukifanya chama hiki kiwe Mtawala badala ya kuongoza Umma wa Kitanzania..nasi sote tumejenga IMANI ya kuabudu chama ambayo haiwezi kuondoka tu kwa sababu viongozi wake sii waadirifu. Sasa pima utakavyoweza kupima lakini kama mjuavyo IMANI ya dini haina uelewa wa juu ktk elimu ya dunia isipokuwa nafsi zetu kulingana na mazingira tuliyopo na kama ingekuwa imani hutokana na elimu ya darasa basi bila shaka sisi wote duniani tungefuata dini moja.

Kisha kuna hili swal la Ulimbukeni ambalo linatokana na tamaa ya kuwa kama wao - Wonna be!
Hili ni tatizo kubwasana ambalo naweza kusema linatokana na asili (genetic) aidha iwe ni uvivu wa kufikiri na ubunifu au ndio kama wanavyodai wengi kwamba utumwa ndio ulichangia sana. Mimi sina uhakika sisi Watanzania tumepatwa na nuksi gani kwani wavivu kupita kiasi. Kila kitu tunategemea kuletewa na matumaini ya namna hii ndio yanapelekea watu kufikiria kwamba hakuna maendeleo isipokuwa kwa
msaada..

Kila mmoja wetu anategemea KUTOKA kwa kupitia mgongo wa fulani iwe familia, marafiki hadi serikali kuu. Na hakika ktk kila Familia mwenye nacho ndiye hutukuzwa, mzazi atampenda sana mwanaye, ndugu au rafiki aliye nacho na sii mwenye elimu na huyo ndiye atakuwa role model..Mwenye akili ni yule aliyefanikiwa kifedha, kwa maana nyingine kiongozi mzuri na atakaye pewa kura ni yule aliyejiwezesha utajiri -Money talks, haijalishi mtu huyo kazipata vipi. Ukiwauliza Watanzania wana prefer urafiki wetu na nchi za nje watakwambia Marekani (the richest) pasipo hata kufikiria mara mbili..

Tatizo hili lipo deep, ktk kina kikubwa cha Umaskini zaidi ya kufikiria kielimu. Sioni sababu ya kuchukua mbegu za maabala kuja panda mahindi au mpunga nchini..Sioni sababu ya wananchi kufuga ng'ombe na kuku wa kizungu kuliko wa asili wakati wenzetu walishindwa kufanya hivyo kutokana na hali ya hewa huko makwao. Imefikia tunajaribu kuishi maisha ya four season kwa kuiga tamaduni za Ulaya ili mradi tu tufanane nao na sii kwa lengo la maendeleo. Imefikia wakati vita yetu dhidi ya Ujinga, maradhi na Umaskini tumeikabidhi missionaries (wawekezaji) kwa matumaini kwamba wao wataweza kupigana kwa niaba yetu. Tazama mavazi yetu jinsi watu wanavyojichubua na kadhalika haya yote yanatokana na Ulimbukeni ambao asili yake ni kutojiamini (inferiority complex) - Na wanaopitisha yote haya ni wasomi tena wana hayo ma Phd..Aidha tumeshindwa kuelemika tuliposoma tukakariri sana masomo pasipo reasoning au ndio Ulimbukeni wenyewe ambao hauna elimu.

Kwa hiyo wakuu zangu itachukua muda mrefu sana kuweza kuondokana na adha hizi kama sisi wenyewe hatutakubali mapungufu haya na kujaribu kuyapa elimu ya Uraia kulingana na mazingira yetu. Na hakika Dr.Slaa na viongozi wengine wote wenye nia njema na Taifa letu wanatakiwa kuhutubia Uzalendo, kupiga vita Ulimbukeni kwani hata nchi tajiri kama Marekani wanapiga vita Ulimbukeni. Hawaruhusu vitu kutoka nje kuingia kwao pasipo kuvitazama kwanza ATHARI zake wakati sisi tunapima umuhimu wake kwetu kabla ya athari zake. Na kwa haya nasema hivi kuwa mbali na akili ya kitumwa (Unyenyekevu), wananchi wanaichagua CCM kwa kutazama umuhimu wake badala ya kutazama athari zake.
 
Nakubaliana na hoja zako Mwanakijiji.Suala la kujiuliza hapa je baada ya mfumo wa vyama vingi,elimu hii imefikishwa kwa wananchi kwa mapana yake?hivi wananchi wanafahamu dhana ya vyama vingi,wanfahamu pros and cons za vyama vingi?Tumepita kwenye operesheni sangara huko vijijini watu hawajui kabisa vyama vingi,Katibu wa CCM,au Mtendaji wa Kijiji au Mwenyekiti wa Kijiji ni Mungu mtu..Kifupi ni kwamba sehemu nyingi hasa ambako watu hawapati magazeti,au wanasoma magazeti yamichezo tu,au hawasikilizi redio vya kutosha hali ni mbaya.Na hata vyombo vyetu hivi vya habari bado havijaelezea dhana ya vyama vingi kwa mapana yake.Wanaandika stori za Dr Slaa kafanya hivi,sijui fulani kafanya vile basi.Havichambui vya kutosha ili Mtanzania wa kawaida aelewe.Achague kiongozi kwakuwa anataka maendeleo na si vinginevyo.Sehumu ulizozitaja zimechagua watu na sio upinzani,baada ya watu hao kupita ndipo wakakuza upinzani katika maeneo husika...
 
Jamani eehh mi nawaomba kila mmoja wetu hapa........honestly ajaribu kuongea na watu watatu anaowafahamu kule kijijini kwao kuhusu ufahamu (elimu au mwamko) wa siasa zinazoendelea........tuweke maswali hapa ya kuwauliza (ili kila mmoja wetu ayatumie maswali hayo hayo)halafu kila mtu aje na majibu......lets try this approach
 
Kisha kuna hili swal la Ulimbukeni ambalo linatokana na tamaa ya kuwa kama wao - Wonna be!
Hili ni tatizo kubwasana ambalo naweza kusema linatokana na asili (genetic)

Mkuu Mkandara nachukulia maneno yako kwa uzito sana, una scientific sources ku validate hii claim ?
 
Wakuu zangu,
Kwanza inabidi sisi wenyewe hapa kuwa wasikivu na wenye kukubali hoja kwa mtazamo wake kisha kupambanua ukweli. Swala la kupembua linahitaji sana muda wa kufikiri kwa sababu tunapobishana juu ya hulka ya Watanzania kwa ujumla wake inakuwa kazi kubwa zaidi kwa sababu sii swala la kupembua pumba na mchele tu isipokuwa kuna mchanga ndani yake na kama mjuavyo Pilau lenye mchanga haliliki.

Mimi naamini kabisa kwamba Watanzania tuna matatizo makubwa sana ya EXPOSURE na hakika elimu yaweza kuchangia lakini kikubwa zaidi ni UTUMWA wa akili na ULIMBUKENI ambavyo vyote hivi havitokani na elimu ya darasa isipokuwa - Elimu ya Uraia. Ifike wakati watu tukubali kwamba mambo mengi yanayotokea ama tunayoyafanya nchini hayana dawa ya elimu ya darasa, isipokuwa wananchi bado wana fikra za KUTAWALIWA kiasi kwamba leo hii hata ukiwauliza Watanzania wakupe tofauti baina ya kutawaliwa na mkoloni au na CCM sidhani kama wengi wanafahamu.

CCM wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kupotosha elimu ya Uraia kwa wananchi wake na kuwajaza ujinga wa Unyenyekevu kiasi kwamba CCM imekuwa ni IMANI ya watu badala ya chombo hiki kuwa ni chama cha Kisiasa. Unyenyekevu wa wananchi kutoka kutawaliwa na mkoloni umehamia ktk utawala wa chama CCM na viongozi wote wa chama wanatisha baada ya kujazwa woga (fear) hivyo kunyenyekewa kama wakoloni na hakika wanapenda na kuridhika na mfumo huu..

Utawala wa CCM umeweza kujenga imani ya Unyenyekevu kama mbinu ya kuhakikisha Amini na Utulivu nchini badala ya kufundisha Uzalendo. Na ndio maana mafisadi wote kina Lowassa na mzee wa vijisenti Chenge na wengineo wameweza kupokelewa kwa shangwe huko makwao baada ya kuwaibia wananchi Mabilioni. Waulize wasomi watakwambia bora kaiba Lowassa fedha itazunguka humu humu badala ya mwekezaji ikiwa kama ni unyenyenyevu kwa viongozi hawa..Hii ndio mind set ya wananchi kwa ujumla.

Na kwa sababu CCM haina tofauti na utawala wa mkoloni ambao ilani yao ya kwanza ni kulindana imeshindwa kuchukua hatua yeyote dhidi ya mafisadi hao. Hakuna sababu ya ndugu, mzazi au rafiki kufurahia mtu anapoiba fedha toka shirika au benki akapewa sifa za ujasiri kama sii akili ya kitumwa. Na hakuna sababu hata kidogo ya mtu kuwanyanyasa wananchi na fedha ya wizi au dhulma pasipo sheria huru kuchukua mkondo wake. Hivyo basi tumeendeleza mfumo wa Unyenyekevu ktk utawala wa ukoloni mamboleo, badala ya uhuru wetu kuzaa Uzalendo.

Na ukitazama enzi za mkoloni, watawala wetu iwe wazungu au waarabu waliweza kunyenyekewa na kulindwa hata wakifanya makosa makubwa dhidi ya watawaliwa. Na hakika kuwaibia wakoloni au mzungu ilikuwa sifa kubwa kwa wananchi kwa sababu iliweza kudumaza uchumi wao. Leo hii watu wanaibia serikali yetu kwa mtazamo sawa na mkoloni. tazameni kina RA na matajiri wote nchini, wote hawa wananyenyekewa sii kwa mchango wao ktk uchumi wa nchi yetu isipokuwa kwa nguvu ya fedha zao kuweza kununua sheria ya unyenyekevu. Nimewahi kusema kwamba Unyenyekevu ni wa Mungu pekee, binadamu tunapeana heshima. Tukitumia Unyenyekevu kama msingi wa amani kwa binadamu uta replace heshima ambayo ndiyo chachu ya Uzalendo kwa jamii iliyokuwa huru na yenye kuthamini haki na usawa.

Hivyo, kutokana na akili hii ya Utumwa (Unyenyekevu) ambayo uhuru wetu umeshindwa kuukana na kufundisha Uzalendo utakao hakikiwa na sheria kama vile miiko na maadili ya viongozi, tumejikuta taifa zima tukirudi ktk kutawaliwa kiakili. CCM imekuwa kama dini badala ya chama cha kisiasa na yawezekana pia Nyerere amechangia kwa kiasi kikubwa sana kukifanya chama hiki kiwe Mtawala badala ya kuongoza Umma wa Kitanzania..nasi sote tumejenga IMANI ya kuabudu chama ambayo haiwezi kuondoka tu kwa sababu viongozi wake sii waadirifu. Sasa pima utakavyoweza kupima lakini kama mjuavyo IMANI ya dini haina uelewa wa juu ktk elimu ya dunia isipokuwa nafsi zetu kulingana na mazingira tuliyopo na kama ingekuwa imani hutokana na elimu ya darasa basi bila shaka sisi wote duniani tungefuata dini moja.

Kisha kuna hili swal la Ulimbukeni ambalo linatokana na tamaa ya kuwa kama wao - Wonna be!
Hili ni tatizo kubwasana ambalo naweza kusema linatokana na asili (genetic) aidha iwe ni uvivu wa kufikiri na ubunifu au ndio kama wanavyodai wengi kwamba utumwa ndio ulichangia sana. Mimi sina uhakika sisi Watanzania tumepatwa na nuksi gani kwani wavivu kupita kiasi. Kila kitu tunategemea kuletewa na matumaini ya namna hii ndio yanapelekea watu kufikiria kwamba hakuna maendeleo isipokuwa kwa
msaada..

Kila mmoja wetu anategemea KUTOKA kwa kupitia mgongo wa fulani iwe familia, marafiki hadi serikali kuu. Na hakika ktk kila Familia mwenye nacho ndiye hutukuzwa, mzazi atampenda sana mwanaye, ndugu au rafiki aliye nacho na sii mwenye elimu na huyo ndiye atakuwa role model..Mwenye akili ni yule aliyefanikiwa kifedha, kwa maana nyingine kiongozi mzuri na atakaye pewa kura ni yule aliyejiwezesha utajiri -Money talks, haijalishi mtu huyo kazipata vipi. Ukiwauliza Watanzania wana prefer urafiki wetu na nchi za nje watakwambia Marekani (the richest) pasipo hata kufikiria mara mbili..

Tatizo hili lipo deep, ktk kina kikubwa cha Umaskini zaidi ya kufikiria kielimu. Sioni sababu ya kuchukua mbegu za maabala kuja panda mahindi au mpunga nchini..Sioni sababu ya wananchi kufuga ng'ombe na kuku wa kizungu kuliko wa asili wakati wenzetu walishindwa kufanya hivyo kutokana na hali ya hewa huko makwao. Imefikia tunajaribu kuishi maisha ya four season kwa kuiga tamaduni za Ulaya ili mradi tu tufanane nao na sii kwa lengo la maendeleo. Imefikia wakati vita yetu dhidi ya Ujinga, maradhi na Umaskini tumeikabidhi missionaries (wawekezaji) kwa matumaini kwamba wao wataweza kupigana kwa niaba yetu. Tazama mavazi yetu jinsi watu wanavyojichubua na kadhalika haya yote yanatokana na Ulimbukeni ambao asili yake ni kutojiamini (inferiority complex) - Na wanaopitisha yote haya ni wasomi tena wana hayo ma Phd..Aidha tumeshindwa kuelemika tuliposoma tukakariri sana masomo pasipo reasoning au ndio Ulimbukeni wenyewe ambao hauna elimu.

Kwa hiyo wakuu zangu itachukua muda mrefu sana kuweza kuondokana na adha hizi kama sisi wenyewe hatutakubali mapungufu haya na kujaribu kuyapa elimu ya Uraia kulingana na mazingira yetu. Na hakika Dr.Slaa na viongozi wengine wote wenye nia njema na Taifa letu wanatakiwa kuhutubia Uzalendo, kupiga vita Ulimbukeni kwani hata nchi tajiri kama Marekani wanapiga vita Ulimbukeni. Hawaruhusu vitu kutoka nje kuingia kwao pasipo kuvitazama kwanza ATHARI zake wakati sisi tunapima umuhimu wake kwetu kabla ya athari zake. Na kwa haya nasema hivi kuwa mbali na akili ya kitumwa (Unyenyekevu), wananchi wanaichagua CCM kwa kutazama umuhimu wake badala ya kutazama athari zake.

Mkuu, unaposema tuna matatizo makubwa sana ya EXPOSURE, ina maana bila ya Watanzania kuwa na EXPOSURE basi hawawezi kuelewa tofauti ya uongozi mbovu na uongozi mzuri? Ina maana katika yale majimbo ambayo yameweza kuchagua viongozi kutoka vyama vya upinzani basi wapigakura wa majimbo hayo waliopigia upinzani wamepata EXPOSURE? Exposure inaweza tu kusaidia kwa kiwango fulani lakini hata Watanzania wote wangelikuwa na exposure bado tatizo la CCM kubaki madarakani lingeliendelea kuwepo tu.

Pia kusema tatizo letu Watanzania ni UTUMWA wa akili; kwamba wananchi bado tuna fikra za KUTAWALIWA ni kutowatendea haki Watanzania. Kwa maoni yangu, haya ni matusi kwa historia ya nchi yetu na kwa Watanzania unaodai hawajui tofauti baina ya kutawaliwa na mkoloni au na CCM! Tuchukue mfano alioutoa Mwanakijiji wa Mrema. Je, ina maana wakati huo ambao nusura Mrema apate urais (Mkapa amshukuru Mwalimu), wananchi walisitisha kidogo kuwa na Utumwa wa akili, hawakuwa na fikra za kutawaliwa na walianza kujua tofauti baina ya kutawaliwa na mkoloni au na CCM?

Wakati mwingine tunapozungumzia Elimu ya Uraia huwa sielewi ni elimu ipi hasa inayozungumziwa? Wananchi ambao hujitokeza na kwenda kujiandikisha kupiga kura na kuwa na malumbano ya kishabiki ya vyama vyao wanafanya hivyo kwa kujua wanachokifanya . Kuchagua chama kibovu si sababu ya kutokuwa na elimu ya uraia. Ni tatizo la kutoelewa huo upinzani unaweza kufanya kipi tofauti na CCM? Elimu ya Uraia haiwezi kuwa na impact yoyote kubwa kwenye chaguzi zetu iwapo vyama vyote vya siasa na zaidi CCM hawatabadilika na kujali maslahi ya wananchi na mustakabali wa Taifa kwa ujumla na kuacha kutumia mbinu chafu za kutaka kushinda kila chaguzi. Halikadhalika, vyama vya upinzani vinawajibu mkubwa wa kuonyesha na kujinadi kwa usafi wao vikilinganishwa na CCM.

Mbali ya ufisadi unaofanywa kwenye chaguzi na wagombea wa CCM wasio na uzalendo, ushindi wanaoupata unatokana na factors kadha wa kadha ikiwemo ya muundo wa Chama chenyewe ambao uliwekwa tangu enzi za TANU. Tatizo la vyama vyetu vya upinzani ni kwamba hawachukui muda wa kutosha kutumia nguvu za ziada kuanzisha mifumo ya vyama vyao na matawi madhubuti ya vyama tangu ngazi za mtaa, shina hadi Taifa. Kutegemea tu kampeni za kipindi cha uchaguzi ndizo zisaidie kuishinda CCM yenye mizizi iliyokomaa itakuwa ni kujidanganya na tutaendelea kuwa frustrated na kulaumu ama kutafuta mchawi kila kukicha.

Kijijini kwangu ninakoishi hivi sasa, wakati nahamia niliambiwa kwamba eneo letu tuna mjumbe wa CHADEMA. Sikumuona mjumbe huyo kwa muda wote tangu nihamie. Siku niliyomuona ni siku aliyokuja kutaka kumega kipande cha ardhi yangu kumgawia mtu mwingine! Maana yangu ni kwamba kuweza kuwa na chama madhubuti kitakachoweza kukishinda CCM chenye mizizi inahitaji moyo wa uzalendo na usafi wa viongozi na wanachama tangu ngazi ya chini hadi juu ambao watakuwa tayari kufanya kazi kubwa ya kuwahamasisha wananchi wajiunge na chama ili chama kiweze kupata nguvu zaidi. Hamasa kutoka kwa viongozi wa juu kitaifa peke yake tena katika kipindi cha uchaguzi haitoshi.

Mkuu Mkandara, kuhusu ‘Ulimbukeni’ nakubaliana nawe kabisa kwamba Watanzania ulimbukeni umetuzidi mno kiasi cha kuathiri maendeleo yetu wenyewe. Ulimbukeni ndio uliofanya tuue viwanda tulivyojengewa na Serikali ya Awamu ya Mwalimu Nyerere, badala ya kufanya juhudi za kuvifufua, kuboresha bidhaa zinazotengenezwa na kuwahamasisha wananchi wanunue bidhaa hizo kwa manufaa yao na ya taifa kwa ujumla. Ulimbukeni wa viongozi wetu ndio uliosababisha benki ya Taifa (NBC) ibinafsishwe kwa Makaburu na kuua madhumuni mazima ya kuanzishwa kwa benki hiyo. Naamini CHADEMA tukiwapa uongozi watatufanyia kazi kubwa ya kuua ulimbukeni wa Kitaifa uliokithiri na unaotia kinyaa.
 
watz sasa wana uelewa sana tena sana kuliko miaka ya 90+!.... si mnaona wenyewe yanayoendelea ndani ya chama kiasi cha kuwafanya takukuru kufunga idara zao zote na kufanya kazi moja tu ya kukimbizana na ccm? mnadhani kama si uelewa kukua ni nini? kama ukivaa shati la kijani na ccm ikashika madaraka siku za umasikini kwenye familia yako zinaanza kuhesabika, wewe utachagua upinzani uozee kwenye umasikini? anayoyafanya mrema sasa ndiyo wanayofanya wa tz wote, au na mrema naye hana uelewa? tieni akili vichwani sawasawa!!!
 
Mkuu Mkandara nachukulia maneno yako kwa uzito sana, una scientific sources ku validate hii claim ?
Mkuu wangu niliyoyaandika hapo juu ndio scientific yenyewe kwani unataka yapimwe na mzungu au? sisi wavivu wa kufikiri isipokuwa kutafuta urahisi mkuu wangu hata sindano na glass zinzotengenezwa kwa udongo tunaagiza toka nje unataka scientific source ipi ikiwa sisi wenyewe ndio source!
 
Kwa leo nikubaliane na ndugu mwanakijiji. Tatizo si Elimu ya uraia wala ya Darasani. Hilo liko very clear na tujaribu kuangalia mbali zaidi ya hizi hisia zilizoenea ambazo mimi naona zinasababishwa zaidi na mitazamo hasi tuliyonayo kuhusu watu wa vijijini. Watu wengi hapa tunawazungumzia watu wa vijijini kama si watu. Hatuna touch na maisha ya vijijini na hatujui watu wa vijijini ni watu wa kawaida kabisa. Mimi niseme tu kwa uwazi kabisa, watu wa vijijini ndo wako tayari zaidi kwa mabadiliko kuliko watu wa mijini.

Historia imejaa mafunzo mengi kuwa wanaofaidika na mifumo dhalimu huwa hawawezi kusaidia kuiondoa mifumo hiyo. Watu wa mijini kwa hapa tukubaliane ndo kuna kiwango kikubwa cha watu wanaonufaika na huu udhalimu na ufisadi, rushwa na mifumo mibovu iliyopo. Chaguzi nyinigi zimetuthibitishia kuwa si watu wa mijini hasa wanaolilia mabadiliko, bali wa vijijini. Mifano mingi imeshatolewa kuwa wabunge wengi wa upinzani nchi hii wanatokea mashambani. Pemba si mjini, tarime si mjini, kigoma kaskazini si mjini, Mpanda magharibi si mjini, Karatu si mjini n.k. Pengine katika chaguzi zote ni majimbo machache sana ya mjini yamewahi kupigia kura mabadiliko. Moshi, Arusha, Ubungo na Temeke, mji mkongwe huko Zanzibar na Kigoma. Je jumla ya majimbo ya mijini ni Mangapi??

Ukitaka kujua kuwa tatizo si wananchi au tatizo si elimu, angalia quality ya watu walioshinda katika majimbo hayo. Jamani tuwe wakweli, siasa za vyama hasa uongozi wa vyama haujajikita sana kwa watu huko kwenye ground zero. Hii ina apply kwa vyama vyote, CCM inanufaika tu kwa sababu sehemu nyingi katika nchi hii huwezi kutenganisha CCM na serikali. Ni kama kitu kimoja. Hakuna chama chenye uwezo wa kulirudufu hilo kwani serikali ni moja tu. Vile vile tutakuwa hatujitendei haki tusiposema ukweli kuwa vyama vingi huko vijijini ama havipo au wanaoviwakilisha hawachaguliki.

Nakumbuka kule kwetu vyama vya upinzani vilipoingia kwa mara ya kwanza wale waliokuwa wakorofi kwenye jamii ndo walivikimbilia. Wengine walikuwa ni known criminals. Picha hii ya vyama vya upinzani ilizagaa maeneo mengi kwani wale ambao walikuwa wanaonekana si watu wa kuaminika sana ndo waliokimbilia huko. Sasa ukiangalia hali hiyo na ukweli kuwa wasomi wengi wa mjini mngependa kuendeleza status quo, ni watu wachache sana walikuwa tayali kuingia upinzani openly. Maana yake ni kuwa vyama vya upinzani havipati wagombea wanaouzika. Wananchi wa vijijini si perfect ila wanawapigia kura wagombea wazuri.

Kule Kigoma kaskazini, Zitto alitokea shuleni na kupata Ubunge, hao wananchi hiyo elimu wao wameisomea wapi? Suala ilikuwa ni quality ya mgombea. Si kuwa kila mwenye elimu ana quality ya kuchaguliwa. Kuna mfano Mwingine kule Kigoma kusini alishashinda mbunge wa upinzani kwenye misimu iliyopita (Kiffu Gulam) naye alikuwa tu katokea chuoni, hao wananchi wa huko elimu walikuwa wamepata wapi? Suala si elimu ni quality ya mgombea. Kule kigoma mjini Kaburu waliwabwaga CCM enzi zile kabla ya kununuliwa. Na huyu alikuwa ni mtu mwenye uwezo wa kujitetea. Kule Kigoma kama Kaburu angesimama imara na kuijenga Chadema kama alivyoanza miaka ile ya tisini, leo pengine kutokea pale Kigoma nzima ingeshachukuliwa na wapinzani. Lakini hilo halikuwezekana.

Kule kote ambako wananchi wamewahi kupigia kura mabadiliko, kulikuwa na wagombea wanaochagulika. Sasa angalia vyama vyetu vya upinzani, je vimeweka wagombea wangapi wanaochagulika? Ukiachia wave ya mabadiliko ndani ya Chadema hivi karibuni sehemu nyingi, kama anavyosema Mbogela hapo juu, wagombea wa vyama vya upinzani huwa ni waliochoka na wasiouzika. Nasema sehemu nyingi. Kwa hiyo tusitarajie miujiza.

Suluhisho lililopo ni kwa vyama hivi vipya kujijenga kitaasisi kiasi cha kuweza kuvutia wasomi. Mbinu walizotumia kupata wagombea machachari wa aina ya Kina Zitto, Kina Slaa, Kina Ndesamburo, n.k. zitumike katika majimbo yote. Hili si rahisi na linahitaji financial resources za kutosha kulitekeleza. Wakati mwingine haya yanatokea si kwa sababu ya sera nzuri, utaona kuwa kuingia Chadema kwa Slaa hakukutokana na kupenda sera zake, zaidi ya kuenguliwa na CCM kwenye kura za maoni.

Siamini kuwa kuwachagua wapinzani ndo holy grail ya kuleta maendeleo. Naamini kuwa maendeleo yanapatikana pale mfumo unapotoa nafasi kwa BEST BRAINS katika jamii kuleta mchango wao. Chaguzi huru zinazoshirikisha vyama vingi ndo njia pekee ya kuleta BEST BRAINS ndani ya political systems ambazo ndo decision making organs zinazoongoza nchi.

Wananchi, wote wa vijijini na mijini pia, huchagua mara nyingi personalities. Mfumo wa maisha ya kitanzania, uwezo wetu wa kiuchumi, n.k. bado hazitoi nafasi kwa sera. Watu mara nyingi hawachagui sera, wanachagua wagombea bora. Sera za vyama sehemu nyingi zimeshaonekana kuwa ni ahadi hewa ambazo hutolewa na baadaye waliozitoa wakazikana. Hivyo watu huchagua zaidi watu kuliko sera au chama. Kazi za vyama vyote ni kupata wagombea bora, sera si muhimu sana kwa Tanzania.

Kwa mfumo uliopo ndani ya CCM, WORST BRAINS NDO ZINAFLOURISH NA TUSITARAJIE MABADILIKO POSITIVE.
 
Mkuu Kiranga, hivi unafikiri wenzetu Marekani wanaelewa sana civic education ndio maana walimchagua Bush na baadaye wakaamua kumchagua Obama? Watu wale wale waliojipanga kuimba "yes we can" leo wanampa Obama approval rating ya 44% huku congress waliyoichagua wanaipa approval rating ya 11%. Wale wale walioipeleka congress toka kwa republican na kuwa democrat leo wanatabiriwa kuirudisha tena kwa republican comes November.

Sidhani kama Wamarekani wengi wanajua all the complexities za siasa zao zaidi ya kujua kuwa walichonacho hawakitaki. Sidhani ukimuuliza mpiga kura wa Marekani ataeleza vizuri how recession imetokea na jinsi gani stimulus package doesn't work.. wao wanachoelewa utaona ni kuwa kuna vitu hawataki serikali yao ifanye..

Watu wetu wengi wa vijijini wanaweza wasieleze vizuri kitaalamu suala la recession na mfumuko wa bei.. lakini wanajua kuna tatizo pale mazao yao yanapokosa soko au wanapojikuta wanauza bidhaa zao kwa bei ya chini kuliko mwaka uliopita.. wanachotaka kumbe ni mabadiliko tu.

So, naamini tatizo siyo elimu.. kwa sababu kama elimu ingekuwa ni suluhisho Nigeria... Nigeria...
 
Na miye nitatabiri tena kuwa wabunge wengi wa CCM watakaoangushwa watakuwa ni wale wa vijijini siyo wa mjini na sababu iko very simple.. wa kijijini wanaelewa uhusiano wa matatizo yao na viongozi wao wakati wa mjini hawaoni hilo kwa urahisi.
 
Bibi Ntilie,
Shukran sana kwa kunichambua pale ulipoona kuna makosa au kupotosha lakini nadhani itakuwa haki yangu kujieleza pamoja na kwamba mara nyingi huandika maelezo marefu ili nipate kueleweka.

Kwanza nitaanza na EXPOSURE, hapa mkuu wangu sijui kama unaelewa impact inayotokana na exposure ktk jamii..Sidhani kama unaweza kumweleza kipofu ukubwa wa Tembo akakuelewa kwa ufasaha wake ndivyo ilivyo exposure kwa wananchi. Unapoweza kuyaona maendeleo ya wenzetu, freedom na rightts walizokuwa nazo wao na mahusiano baina ya viongozi, vyombo vya usalama na vya kijamii ni maajabu ya Mussa kwa Mtanzania.

Swala la Mrema kukaribia ushindi mwaka 1995 halina mahusiano kabisa na exposure isipokuwa walimchagua mtu Mrema dhidi ya Mkapa kutokana na sura, umaarufu na ahadi za mgombea kuwatajirisha. Hivyo, Mkapa alipwaya kuwashawishi wananchi Utajiri jambo ambalo linaturudisha palepale kujiuliza kwa nini Mrema aliweza kupata kura za wananchi. Tatizo sio Mrema isipokuwa sisi wananchi wapiga kura kutoelewa kiongozi bora ana sifa zipi, tunarudi ktk tatizo la exposure yaani kipofu husikia sauti lakini haoni uzuri wa kitu.

Kuhusu Kutawaliwa. hapa mkuu wangu situkani isipokuwa nasema ukweli ambao hatupendi kuusikia. Nitashuru sana kama wewe utanieleza tofauti zilizopo za kiutawala wakati wa mkoloni na leo hii zaidi ya sisi kukabidhiwa Uhuru on a silver plate..Viongozi wetu walichokifanya ni kuchukua nafasi walizoacha wakoloni tukaendeleza yale waliyoaacha chini ya mkono wa mtu mweusi. Toka mfumo, mihilili ya nchi yetu bado inafuata mila za mkoloni na hao viongozi wetu wamehamia majengo yaliyokuwa yaiishi wakoloni. Nambie haki Lilaah, hivi kweli sisi tuna ONGOZWA au tuna TAWALIWA?.. that should be the different au nakosea?..

Kwa hiyo wewe nambie tofauti unazoziona wazi ikiwa uchumi wetu ulikuwa bora zaidi chini ya mkoloni kuliko leo hii kimebadilika kitu gani kama sio sisi wananchi wenyewe kubadilika makuzi ya kimaumbile. Tulikuwa naviwanda leo hii hatuna, tulikuwa ktk nchi kuu za uzalishaji wa katani, pamba na kahawa leo hii hatupo hata kwenye ramani.. What good independence has brought us!.. nambie na wala situkani kwa sababu na mimi ni Mtanzania vile vile ambaye nashuhudia haya pengine tofauti yangu na wengine ni hiyo exposure unayoikataa.
Na ndio maana nakataa KUTAWALIWA naomba KUONGOZWA.

Mwisho ni maajabu ya Mussa kutegemea CCM wabadilike, kama ndivyo unavyotegemea ni ktk fikra hizo hizo za woga unaotokana namfumo wa kiutawala unaotufanya tunyenyekee. Hivi kweli unategemea mtu anayekutawala anaweza kubadilika ikiwa yeye ananufaika zaidi na kukutawala?..Kwa nini utegemee CCM na viongozi wake wabadilike na sio wewe ubadilike ili CCM wawe forced kukubali matokeo ya kutokubaliana nao. Ndivyo tulivyopigania Uhuru wetu iwe South Afrika, Ghana au Misri kote wananchi ndio walikataa kutawaliwa na sio chombo tawala kukubali kubadili mfumo wa utawala wake.

Elimu ya Uraia ni pamoja na kufahamu freedom maana yake mapana yake na Rights zote zinazoambatana na haki miliki na usawa wa binadamu. Utawala kazi yake kubwa ni kulinda vitu hivi hushindwa pia kusimamia uchumi wa nchi hiyo na ndipo unakuta maswala ya Ufisadi yakiibuka. Mkuu hadi leo hii mimi sielewi kabiusa kwa nini mtu anakuwa na houseboy/girl akimlipa Tsh30,000 kwa mwezi kwa kazi zote za ndani ya nyumba na maisha sawa na ukoloni kama sio kubadilishana mashati na mkoloni..Nenda katika bar na hotel jinsi tunavyo wa treat wafanyakazi hawa kama mbwa. Vijana wanavyo treat girlfriends zao yaani umaskini ni utumwa mpya..what else can I say!

Swala la Ulimbukeni tupo pamoja, nadhani nimejieleza vya kutosha na ushahidi mama Ntilie tunao wenyewe
 
Nimesikia mara kwa mara tena kwa lugha ya dharau ya aina fulani kuwa "Watanzania hawaju" na kuwa "Huko kijijini watu hawaelewi" na wengine wamefikia mahali pa kudai kuwa "wananchi hawana elimu ya kutosha ya uraia" na kuwa vitu hivyo ndivyo vinavyosababisha CCM ishinde.

Nimejiuliza swali moja: Mwaka 1995 (Nyerere akiwa bado hai) kwanini kulikuwa na mwamko mkubwa wa upinzani kuliko 2000, 2005 hasa tukiangalia matokeo ya Urais? Hili ukizingatia kuwa matumizi ya cellphones hayakuwepo, internet ndiyo kabisa, na vyombo vya habari bado vichache?

Hivi kweli tukilinganisha kuwa wananchi wa 1995 hawakuwa na uelewa wanachokitaka zaidi kulinganisha na hawa wa "digital age"?

Nakataa tatizo haliko katika uelewa wa Watanzania.. na tutadagangana tukifiria ati tukitoa elimu zaidi, matangazo ya kwenye TV kuhusu "usia wa Nyerere" n.k utawafanya watu waamke zaidi. Ni makosa kudhania kuwa elimu zaidi ya uraia itawafanya watu wachague upinzani na kuwa kueleza zaidi mabaya ya CCM kutawafanya waichukie.

Labda hatuangalii vitu kwa usahihi?

Mkjj

Tatizo la uchaguzi Tanzania si tatizo la watu bali ni la kimfumo. Mfumo mzima wa uchaguzi umekaa kwa ajili ya chama kimoja tu nacho ni chama tawala kushinda. Ninaamini leo hii hata wananchi wote wasipigie kura chama tawala bado itashinda kwa kishindo na sababu kuu tatu:

1. Mwaka 1995: Uchaguzi ulikuwa 65% huru na haki kabla matokeo hajawa satified, na kuamua kuyabadili kwa nguvu na sehemu walizoona ni ngumu waliamua kuuvuruga kwa makusudi. Mfano Dar wabunge wote wa upinzani walishinda kabla ya kuvurugwa kwa kuficha karatasi na kutofungua vituo makusudi. Hili lilitoa mwanya kwa kufanyika review kabla ya uchaguzi wa marudio na jinsi ya kuhadaa ulimwengu.

2. Baada ya yaliyotokea 1995, vyombo vya usalama wa Taifa vikapewa role mpya ya kuangalia ni jinsi gani ya kuhadaa ulimwengu kwa kura huru na haki na wakati huohuo chama tawala ibakie kuwa mshindi wa kishindo. Mkakati huu upo kuanzia kwa wakuu wa wilaya, mikoa, wakurugenzi wa maendeleo na mabosi wa tume ya uchaguzi. Nafasi hizi hupewi mpaka ihakikishwe kuwa wewe ni muumini wa mbinu hizi na itakuwa ni siri kubwa. Unakuta kijiji kini wakazi 1000, wanasajiliwa wapiga kura 15,000 wanaojitokeza ni 12,456 kukiwa na "bogus electorates 11,456 katika vituo fake", na 456 wanapewa wapinzani wakati chama tawala inabakia na "11,000 bogus electorates", waangalizi wanapelekwa kwenye vituo halisi vilivyo na transparent ballot boxies na kuridhika. Ukweli utabaki kuwa katika kila vituo kumi vya ukweli basi kuna bogus ishirini na ndiyo maana wana ule usemi wa kusubiri kura makao makuu ya wilaya kwa majumlisho wakati barabara hazipiti. Ukweli ni kwamba kunakuwa na pre-casted votes kama 65% ya kura zote out of which 64% ni infavour of chama tawala. Wenyewe wana usemi mmoja kuwa 80% ya watanzania wapo vijijini na huko ndipo kwenye kura za CCM. Hili bao ambalo mpaka bahari ya hindi ikauke ndipo wapinzani watalirudisha.

3. Watanzania ni wepesi wa "kuchana na", give up: Unakuta kabisa CCM haichaguliki sehemu ila mwisho mkurugenzi wa uchaguzi anaitangaza mshindi, tunalalamika, tunapigwa virungu, tunamwagiwa maji ya kuwasha, na wakati mwingine wanatolewa kafara wawili watatu miongoni mwenu na wengine kukamatwa mnalazwa ndani wiki moja, baadae mnasamehewa then mnashangilia kuwa mwizi wenu wa kura ni mtu mwema kawaachia na kila mtu kuingia porini kusaka uyoga na matunda mwitu kwa ajili ya njaa mpaka miaka mitano inaisha.

Ninaamini kabisa si wote wanaogombea uongozi kupitia CCM mioyoni mwao wanaipenda CCM, bali wanajua kuwa bila kugombei kupitia CCM huna chako. matokeo yake ni watu kuanza kuuana ndani ya chama kwa "invisible scuds" na ikishindika visible kwa kutumia assassins (mnakumbuka ya kule Isamilo mwanza)
 
Hosftede,
Mkuu umenitisha sana na nikiangali hii habari ya kupelekea TAKUKURU hadi vijijini ati kuzuia rushwa za kura inaonyesha wazi ni utekelezaji wa agenda nyingine tusoijua hadi siku ya siku..
Kisha jamani naomba kuuliza..inakuwaje TAKUKURU chombo cha serikali wafanye kazi ya kusimamia uchaguzi wa chama CCM kuhakikisha hakuna Takrima!... inahusu?...Kwa nini wasisubiri mkosefu au mashtaka yanyohitaji upelelezi badala yake wanafanya kazi ya kuzuia Takrima ndani ya chama kimoja kwa gharama ya walipo kodi wote au mimi ndio nazipata habari hizi vibaya!.
 
CCM inayo turufu moja tu inayoiwezesha kubaki madarakani nayo ni katiba inayoipa mamlaka ya kuimiliki dola. Katiba imeiwezesha CCM kuihodhi mihimili yote mitatu ya dola - serikali, bunge na mahakama. CCM kwa upande wake imetumia nguvu yake yote kulinda hii katiba kwa kuzitumia serikali, bunge na mahakama. Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa tulipofika kamaTaifa ni vigumu kupata jibu jepesi kwa matatizo tuliyonayo.

Katiba imeweza kujenga tabia ya hofu kwani kuipinga CCM kunachukuliwa kama kosa la jinai na ni sawa na kwenda kinyume cha katiba. Wapinzani wa CCM wanaonekana kama watu wakorofi wanaotaka kuvunja amani na kwa namna hiyo vyombo vya dola lazima viwabane wananchi wasipate mwanya huo. Ndio maana Polisi wako wepesi kukamata watu kama Mtikila na kumfungulia mashtaka kwa uchochezi au waziri kulifungia gazeti.

Katiba imeweza pia kuinufaisha CCM kwa kujenga tabia ya woga miongoni mwa wananchi na imefika pahala ambapo hata wale wanaojua haki zao, wanashindwa kuzitumia. Kwa mfano mwananchi wa kijijini afanye nini anapopiga hodi katibu wa tarafa wa CCM na kutaka apewe kadi ya mpiga kura anakili namba yake. Mkazi wa kijijini afanye nini anapogombana na balozi wa CCM hata kwa jambo binafsi, anaswekwa ndani.

Katiba pia imeweza kuwa chachu ya tabia ya unafiki na tamaa miongoni mwa wasomi wengi na wafanya biashara. Utamwelewaje Profesa mzima ambaye jana tu alikuwa akiiponda uongozi wa CCM lakini leo yuko wa kwamza kwenye ofisi ya CCM kuchukua fomu ya uongozi. Kwa nini mfanya biashara ambaye usiku analalama kwa kuombwa rushwa na viongozi wa CCM kila kukicha lakini mchana awe mwepesi kukichangia mamilioni.

Lakini kinacholeta faraja ni kwamba wananchi wanaonyesha dalili kuwa wakipata nafasi ya kuiweka benchi utawala wa CCM watafanya hivyo. Mwaka 2005 walikuwa bado na tumaini na CCM kuwa mabadiliko yangewezekana kwa kumchagua Kikwete lakini hivi sasa wengi wanajuta. Dr. Slaa amekuja kwa muda mwafaka kabisa kwani wengi sasa wamekata tamaa kabisa na hawana tena ndoto ya mabadiliko kupatikana chini ya CCM.
 
Mambo yaliyofanywa na CCM katika kuua upinzani ni mabaya sana, na mbaya zaidi ukiyaangalia kijuujuu utayaweza kuyaona. Mimi nakumbuka miaka ya 1990 vyuo vikuu ndio vilikuwa chachu ya mabadiliko, kama mtakumbuka wakina Mtikila walibebwa juu juu baada ya hotuba yake pale Nkurumah Hall. Chama cha Mapinduzi kuona hivyo wakapitisha sheria inayosema ni marufuku kwa mwanasiasa yeyote kuhutubia au kufanya mdahalo katika maeneo ya vyuo vikuu. Wenye akili tulisikitika sana kwani tulifahamu hiyo ilikuwa ni mbinu ya dhahiri ya kuvifanya vyuo vyetu kuwa museum. Kitendo hiki kiliua kabisa chachu ya mabadiliko (inquisitive minds), wanafunzi wa vyuo vikuu wakakosa nafasi ya kukutana na policy makers wao.

Wakaja na mbinu nyingine ya kuwatesa wananchi katika majimbo yaliyowachagua wapinzani . Jamani nendeni mkaulize wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro walivyoteseka katika kipindi cha kwanza cha Mkapa. Serikali iliamua kwa makusudi kuwapunish wale wote waliochagua wapinzani. Kwa hiyo tatizo sio elimu ya uraia tuu, bali ni zaidi ya hapo. Jambo la kusikitisha ni kuwa usalama wetu wa taifa badala ya kuangalia ni kwa jinsi gani wanaweza kudefend interest za taifa letu, wao wako pale kudefend interest a CCM. Na ndio maana afisa wa usalama wa taifa anaweza kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM na wakati huo huo bado anaendelea kuwa afisa wa usalama ..only in Tanzania where this kind of crap can be allowed to flourish!
 
Leo hii "wasomi" ndio wamejitokeza kukimbilia CCM ili wachaguliwe.. wengine na kuandamana kupita huku na huku ili wamchangie mtu wa CCM.. wakati huo huo kule Biharamulo watu wapya zaidi ya 26,000 kama sikosei waliipigia kura Chadema!
 
Back
Top Bottom