Tatizo ni Balozi Ngemera ama Wizara ya Membe?

Basi mie naomba mwenye kumjua huyu mzee atupe data maana kaelezwa na ndugu Mugisha kwamba dikteta anatoa ma amri tu bila ya kujali .Yeye na u boss kwisha kazi ukichanganya na Uhaya .

Kwani Ngemera kabla ya kuwa balozi alikuwa nani ?

mzee hatuwezi kuonesha prejudice zetu namna hii.. kuchanganya na uhaya ndiyo nini? wengine tumechumbia uhayani.. so tuna maslahi..tushtuane mapema. Vinginevyo si sahihi ku generalize tabia ya mtu mmoja kuifanya ibebe tabia ya kabila zima.
 
Kwa kweli labda nimsaidie mtoa hoja .Kuna wakati mwaka huu nimetembelea hapo ubalozini katika shughuli zangu za kawaida nikawa naona watumishi walivyo achilia mbali jengo chakavu na wakubwa wanafika hapo bila kujali nimemsikia mjerumani secretary anateta kwamba balozi ni mtu wa ajabu .anakurupuka na anaweza kukufokea hata mbele za watu .

So nikagundua stress za wale watumishi kumbe si maisha magumu ya kazi pekee kumbe hata boss wao anaonyesha uhaya hadi huko Ulaya .Nadhani wale watu wana kabiliwa na matatizo mazito .Sikuweza kupata wa kusema naye ila kwa sasa nitafanya kazi ya ziada .Mugisha umesema uko Ujerumani ? basi tuwasiliane pembeni nikupe kazi .Lazima tujue kwamba kwanza ubalozi unaendeshwa kama familia ya Ngemera na si Ofisi ya Serikali .

Wengine mnaweza kusema pia ili tupate ukweli maana JF si haba kwa kufuatilia .Mliyoko Majuu umulikeni Ubalozi huo hautoi huduma kwa kuwa watumishi wana ogopa kuchukua majukumu .JK hawa ndiyo washikaji zako ambao umewaleta huku wanavuruga wala hawajengi .

Na wewe wahaya wamekukosea nini?
 
hii.. kuchanganya na uhaya ndiyo nini? wengine tumechumbia uhayani.. so tuna maslahi..tushtuane mapema.


Yooooh! sasa wandugu imekuwaje tena na mambo ya mugambire enough, mmeanza sasa, ngoja nitafute pop-corn!
 

Msema Ukweli Siku Zote huwa ni Mpenzi wa Mungu, mkuu sema ukweli acha dhambi za bure bila sababu.

Unajua nikisema ooooh, we ndio muongo, mimi mkweli, itakuwa habari ya he say, she say. Basi wewe mkweli, mimi muongo. Tuliache hilo la yaliyotokea NY siku ya zoezi la kutoa pasi.

Labda hili la administration ya ofisi ya UN pale NY ndio liko substantive zaidi, na halihusishi old hearsay.

Unatetea ile ofisi. Unasema tatizo ni wanao enda pale hawajui kizungu.

Kwanza, tungekuwa tumetoka katika nchi zinazoheshimu utandawazi, na uwajibikaji, na zinazojua maana ya conflict of interest, ingebidi kabla hujafungua mdomo kutetea ile ofisi ya Ubalozi wa UN na wafanyakazi wa pale, ingebidi kwanza utangaze uhusiano wako na mtu yeyote anaefanya kazi ubalozini pale. Ili kuonyesha imani kwamba hutetei maslahi ya mtu wa karibu. Lakini mimi na wewe tunajua nini kinachoendelea. Anonymous forum hii hapa itaku stahi.

Some people are going, what? What is he talking about? Well, a handful of people know what I mean, and it's alright.

Ingekuwa wewe ndo mimi ungesha nianika na kunilipua zamaaaani sana. Lakini kuna wengine tunajaribu ku maintain a modicum of fair-mindedness, na tunajaribu kutunza heshima za watu, heshima ambayo wewe huwapi wengine. Kwa hiyo kwenye ma low blow ya ajabu ajabu, you will always come out on top, kwa sababu watu hawatarudisha majibu. Lakini kuna siku ndege mjanja...yana mwisho!
 
Naomba mwongozo wa forum
Mada ni ubalozi wa Ujerumani kuwa taabani sana na hii nyingine inakuwaje inakuja hapa ?
 
...kutumia majina na kusema Mama kilango amebakwa ni ustaarabu?

FMES, nani kasema Mama Kilango kabakwa?

Mimi ninaepigana na "dataz" zisizothibitishwa naweza kutunga kitu kama hicho ndugu?

Nimemkosoa Anne Kilango kwa ishu tupu tokea siku alipokuja kwa Mwnkjj. Kabla ya hapo nilikuwa namu admire sana. Lakini baada ya kumsikia anaongea nikamwona ni kama anatetea tetea Kikwete administration huku ana posture kama mpiganaji. Nikasema ni msanii. Lakini hata siku moja siwezi kumtungia bizzare story eti sijui. Halafu hata kama karepiwa, hilo ni dongo kwake au kwa hao majambazi walio mrepu?

Hicho ki udaku cha Mama Kilango karepiwa nilikisikia hapa na mimi. Wakasema sijui ni Mtandao ndio ulimtumia mamluki wampore hela za kampeni akiwa kwenye highway ya kwenda Dodoma or something like that. I couldn't manufacture a story like that. For what? Mi nammaliza Anne Kilango kwa ishu tu. Tosha.

Na hili la kutumia majina sijui unapata wapi hiyo idea. Unadai Kuhani ndio huyo huyo Kubwajinga, Sam, Paparazi Muwazi, Mwanatanu, KadaMpinzani, Jobo, Bangusule, Mchelea Mwana....all these people at some point umetu lump up together kama mtu yule tule. Duuh! I don't know what's up man!
 
Mimi sijaona ambae katulia, sehemu nyingine yeyote.

Kuna mtu anaweza kututajia Balozi ambae anajua anachokifanya?

Kuhani naona Balozi wa UN pale New York ni mtu anaejua anachokifanya. The guy is very Intelligent
 
Wenye data zaidi ya Mugisha watupe juu ya huyu Ngemera na kuendesha ubalozi kikomandoo na Serikali kuacha ubalozi kuwa kama boma la kimasai na watumishi kuishi under fear .Mahiga ni halili si kama hawa wengine wanao pewa kwa kujuana ama misingi ya ufahidhina .
 
Wenye data zaidi ya Mugisha watupe juu ya huyu Ngemera na kuendesha ubalozi kikomandoo na Serikali kuacha ubalozi kuwa kama boma la kimasai na watumishi kuishi under fear .Mahiga ni halili si kama hawa wengine wanao pewa kwa kujuana ama misingi ya ufahidhina .

Huyu mugisha ndio mwenye data zote yeye inaelekea yuko karibu sana na balozi na kila jambo linapo kuwa haliendi sawa upande wake, unakurupuka na kuja kuanzisha thread hapa.
Unakumbuka ile thread ya Mama Karume? Ni yeye aliianzisha nayo inaonekana ni baada ya kukosa kitu..kisha jina lake..ni kabila moja na huyo balozi ndio maana kaingia mitini..
 
...naona Balozi wa UN pale New York ni mtu anaejua anachokifanya. The guy is very Intelligent

Kabisa. Ile kete ya ushindi ile. Kazi anayofanya pale UN haina mfano.

Lakini ubalozi unavyoendeshwa pale NY ni Kitanzania Tanzania. Kienyeji enyeji. Ndio maana I have my misgivings on his administrative credentials.

Hili la kuwa intelligent nalo halihajawahi kuswalishwa kuhusu Mahiga. Lakini chonde chonde kidogo kwenye maswala ya intelligence na leadership.

Ngoja nichagua randomly "vichwa" fulani katika historia ya viongozi: aahhh....Benjamin Mkapa, Joseph Warioba, Dr. Ibrahim Msabaha, Marehemu Prof. Kighoma Malima, Prof. Philemon Sarungi, na Prof. Costa Mahalu. Unaonaje, ni watu intelligent? Sio majuha wale watu, au sio?

Performance, lakini, ilikuwa mediocre, kama sio mbaya zaidi. Wengine walifukuzwa, wengine walilazimika kukimbia kazi kwa shutuma za uzembe au ufisadi, wengine, kina Sarungi, walipotelea potelea kwenye Mabunge, hawasikiki tena. 'Baba lao' ndio mpaka leo Wayahudi wanalia ajieleze, asulubiwe, ajieleze, asulubiwe!

Intelligence kuna wakati haiendi sambamba na uwezo wa uongozi. Lakini Mahiga inaonekana intelligence anaitumia ipasavyo, ukiachalia ishu ndogo ndogo kuhusu ofisi yake inavyo endeshwa kienyeji enyeji.
 
Ubalozi wa NY kazi yake ni kutuwakilisha UN, wanaotuwakilihsa wa-Tanzania USA ni ubaloiz wa DC, sasa ukisema wanashindwa kazi UN sawa, lakini anything else ni majungu,

kuhusu majina yako, nafikiriunaelewa sasa kuwa kila mtu hapa fourm sasa anakuelewa vizuri na hasa tofauti ya majina yako 100, na 100 ya huyo jamaa yako ambaye wote mna beef kubwa na malecela na mkewe, ila ningeomba tu mseme waeiba hela ngapi za taifa?
 
Kwa muda wa miaka sasa Ubalozi wetu Ujerumani umekuwa kama boma la mmasai kuanzia jengo na hata watumishi wake .Ubalozi huu ni mmoja kati ya Balozi kubwa lakini ukifika utadhani si Ubalozi wenye hadhi .Jumba liko kia ajabu na watanzania hapa Ujerumani tumepiga kelele sana lakini alikuwa hapa Karume yeye ilikuwa safari tu hadi amekuja Ngemera sasa ni balaa mtu huyu .

Ujerumani tuna bahati mbaya sana kupata mabalozo vichwa maji ama hawajali ama hawajui wanacho kifanya .Ninajiuliza kwamba hata wakiwa mawaziri hapo Ubalozini sijui hawaoni hali hali halisi ya jengo lao hilo ama wao huwa wanawa perdiem yao na kuabudiwa na watumishi wa Ubalozi ila mazingira ya watumishi si kazi yao .

Majuzi mkewe Karume alikuwa ana vinjari hapo , waziri wa Utalii na hata Matilda katoka Ujerumani juzi lakini wote wana acha hali ikiwa duni kabisa .

Sasa kaja Ngemera kila mara yeye yuko kama mlevi .Mambo yake hayaeleweki hata kukaa akaona namna tunavyo ona aibu hap Ubalozini tukienda haangalii.Ukimuona anatembea utadhani ni balozi kweli kaa naye uone .Anatoa amri kama Mhindi na hata hamalizi kazi moja anarukia nyingine .Nina wasi wasi mkubwa na huyu Mzee sijajua kabla ya kuwa Balozi alikuwa na huko utawala wake ulikiuwaje .Kwa kuwa na watu vichwa maji wa aina yake ndiyo maana Ubalozi unakosa hadhi kwa kuwa anaye uongoza hana hadhi .

Membe na kundi lako kama ulikuwa hujui Ujerumani kuna matatizi basi anza upya kuutafuta ukweli utaupata ni aibu kuanzia nje hadi ndani .
we ni kichwa maji na si balozi wa germany unafikiri kubadili mambo ni pupara pupara ka wewe fikiria kabla ya kulopoka inaonesha wewe huna maendeleo yoyote na kichwa chako ni ziro
mambo mazuri yanaitaji maji kama we ni mkereketwa wa ubalozi wenu na nchi yenu badala ya kupiga domo nenda katafute njia za kuisaidia nchi yako na sio domo mbele tu ka mjinga. nyie ndo mnaotakiwa kuenda vijijini mkalime na muwaachie hao mabalozi wajuao wafanyalo waendelee kuisaidia nchi yenu kwa mambo ambayo yako kwenye uwezo wao si kwamba tanzania ni marekani bado tupo kwenye nchi maskini na hao wanaigeria amabao bado wako maskini wanamafuta sembuse tanzania
kaa chini ukuwe unaonesha elimu yako bado changa rudi shule au chukua jembe ulime na uache kuzungumzia masuara yasiyo ndani ya uwezo wako maana ni kujiaibisha na unabaati umeweka no status mende we.
 
Huyu Ngemela nakumbuka kama alikuwa ni Katibu mkuu kilimo wakati mmoja na hata anachaguliwa kati ya wale makatibu wakuu watano alikuwa kaachwa katika ukatibu mkuu kama sikosei. Yeye ni mmojawapo kati ya wale watano wateule walioteuliwa akiwamo yule mama wa Uingereza na yule Adadi na yule jamaa aliyeshabikia Magereza kula mkong'oto akasusiwa na wanahabari. Wote si mnajua uchaguzi huo? huko ndiko Ngemela alitokea. Muulizeni kikwete anamjua na anajua sababu ya kuteua mtu ambaye hakuwa na uzoefu wa mambo ya diplomasia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom