Tatizo la Watoto wa Mitaani : Nini Kifanyike

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,194
1,355
Wakuu kila mara nikipita mitaani na kuona watoto wamejaa mitaani naona "Time Bomb" tunatengeneza majambazi wa kesho na watu ambao hawana skills wala mbele wala nyuma.

Ni mengi yamefanywa kama ifuatavyo:-

  • Kutengeneza NGOs za kuwalea watoto (ingawa hizi nyingi zimekuwa kama njia ya wachache kujipatia kipato)
  • Jamii kusaidia kulea watoto yatima (kuna jamaa yangu mmoja alijitolea kumchukua mtoto wa mitaani na kumsomesha lakini huyu mtoto alitoroka akamuibia na kurudi mtaani
Hivyo basi kama hayo yote hapo juu hayafanyi kazi ni nini kifanyike?
Sababu hawa watoto bado ni wadogo inabidi maamuzi magumu yafanyike, inabidi kama jamii tutengeneze homes zenye ulinzi mkali wa kuwaweka watoto huko (kuhakikisha kwamba hawatoroki) na huko wapewe elimu, wafundishwe attitudes nzuri, na skills tofauti (we are loosing a lot of talent) na wakae huko mpaka pale wakiwa wakubwa (graduate ndio waachiwe waingie mitaani) na kama serikali iwape first priority katika kazi tofauti. Na pesa na misaada yote iwe inapelekwa huko, na kuwa na ardhi ya kutosha kuwafundisha kilimo na ufugaji pia.

Ninachomaanisha yaani hiki kiwe ni kama chuo cha kufundisha hawa ndugu zetu maadili mema ili tusaidiane nao kujenga taifa na sio kubomoa

Any more Suggestions Please, sababu what we are doing now don't seem to work., na tusiporekebisha leo kesho itakuwa too late...
 
kwanza kabisa wajitokeze wanasheria au serikali iwe na wanasheria maalum wa
kutetea watoto wanaodhulumiwa mali kama nyumba na ndugu wa wazazi..
pindi wazazi wakishakufa
 
Rule of "Law" and "Good" governance inaweza kupunguza idadi ya watoto wanaoishi mitaani!

Kwa Tanzania - Sifahamu vizuri ni ipi kazi ya Wizara ya Ustawi wa Jamii? Kama hii Wizara "ingeshikia bango" - kisheria - wale wote wanaozaa na wanawake na kutelekeza watoto - wangepungua sana...

Vyanzo viikubwa vinavyozalisha watoto wanaoishi wenyewe mitaani ni:-

1. Mimba za "utotoni"
2. Ndoa kuvunjika
3. Wazazi kufariki - either mmoja or wote wawili"

Yote hayo matatu hapo juu yanaweza kutatuliwa kama "watawala" watatoka usingizini na kusimamia sheria za malezi na makuzi ya watoto...
 
Mkuu hii huenda ikapunguza wengine kuongezeka lakini vipi wale ambao bado tupo nao sasa hivi mitaani, pili sio kweli kwamba watoto wote wa mitaani ni yatima wengine tu wanapenda kukaa bila sheria..., kuna jamaa yangu ninamfahamu watoto wake walipotea kama wiki akaja kuwakuta wapo mitaani kisa tu ni kwamba alimfokea mtoto wake...

Ndio maana nikasema kama tukiwa na homes za kutosha (ingawa wengine wataziita prisons) huku kutakuwa hakuna kubembelezana bali ni kufundishana maadili na skills tofauti na mtoto akishakuwa mkubwa tutakuwa tumempa zawadi ya ufunguo wa maisha
 
kwanza kabisa wajitokeze wanasheria au serikali iwe na wanasheria maalum wa
kutetea watoto wanaodhulumiwa mali kama nyumba na ndugu wa wazazi..
pindi wazazi wakishakufa
Ni kweli mkuu lakini watoto wakiwa wadogo wanaitaji zaidi mtu wa kuwafundisha what is right or wrong sababu bila hekima soon hao watoto wakifikisha miaka ya kujitegemea hata hizo mali watazipiga bei
 
Watoto hawa wa mitaani watasaidiwa vipi? Tuseme ndo serikali imeshindwa kabisa kupata ufumbuzi ama?

Nashangaa sana jinsi ambavyo hao watoto walivyo. Nilipokuwa Mwanza sikufurahishwa na hali yao maana wanalala hadi uvungu mwa daraja.

Hii hali sio Mwanza tu bali Tanzania nzima na vitongoji vyake. Nimefika Moshi na Arusha hali ni hiyohiyo.
 
Kabla ya serikali tujiangalie sisi kama jamii tumewajibika vipi kupunguza tatizo la watoto wa mtaani?
Hawa watoto hawatoki porini wanatoka ktk majumba na mitaa yetu,

Sababu za Tatizo:
1.kuvunjika kwa ndoa
2.kufariki kwa wazazi
3.umaskini ulikithiri

Kabla ya kutibu tatizo ni vyema kuwekeza nguvu ktk vyanzo vya tatizo.
 
Halafu maajabu yao ni kwamba, wakisha kuwa wakubwa wanapotea kabisaaa hawaonekani.

Kuna mwalimu mmoja alinifundisha kuwa, kabla hujamleta mtoto duniani hakikisha umemuandalia mazingira mazuri ya kuishi.
Na ni wajibu wa wazazi kuwatunza watoto na sio watoto kutunza wazazi.

Kila wakati unapofikilia kuzaa fikiri, unaweza kumhudumia mtoto?
Unaweza kumudu mikiki mikiki yake?
Ukiona maisha wewe mwenyewe tu yanakushinda basi usizae na ni vizuri uende kwenye vituo vya afya ukawekwe vijiti ili usizae bila kutarajia.

Malengo yangu yakitimia ntawahitaji sana hawa watoto nikae nao, naomba MUNGU anisaidie.
 
alafu iyo number 1 naona kama ndo inaongoza maana ndoa ndoano daily!
 
Kabla ya serikali tujiangalie sisi kama jamii tumewajibika vipi kupunguza tatizo la watoto wa mtaani?
Hawa watoto hawatoki porini wanatoka ktk majumba na mitaa yetu,

Sababu za Tatizo:
1.kuvunjika kwa ndoa
2.kufariki kwa wazazi
3.umaskini ulikithiri

Kabla ya kutibu tatizo ni vyema kuwekeza nguvu ktk vyanzo vya tatizo.

4. Watu wanaowapa mimba mabinti na kuwakana

Tabia mbaya sana hii, kama kila mwanaume angewajibika kwa watoto alioshiriki kuwaleta hapa duniani tatizo lingelipungua
 
Kwa kweli hili ni tatizo kubwa sana hapa TANZANIA maana ni kweli kila kona hawa wapo. Hawa watoto wengine wazazi wao walidead kwa #ukimwi na walezi/waangalizi waliobaki wanawanyanyasa ndo maana wanakimbilia mitaani na kuwa watoto kama hao. Jambo jingine kuna baadhi ya wazazi ambao wamezaa watoto wengi na kuwalea kukawa ni shida na hatimaye kutoroka nyumbani na kukimbilia mitaani. Wazazi tutafute njia mbadala kuwaokoa hawa watoto. Unakuta mwanaume mmoja anaoa wanawake wengi then matunzo kuwa shida. Nimewahi kushuhudia mkaazi mmoja katika kijiji kimoja huko #Shirati_Rorya aliyeoa wanawake #22 na hakuna hata mtoto mmoja aliyesoma na kuwa na elimu nzuri. Sasa hali kama hii imepitwa na wakati. Tuelimishane ili tupunguze kasi ya hawa watoto maana wanatutia aibu.
 
Watawala kama wanavyotafuta wafadhili kwenye mambo mengine,wakati umefika wajenge kituo kikubwa hapa
nchini kitachokuwa chini ya ustawi wa jamii-kikusanye watoto wote wa mtaani na wawekwe hapo kuwe na shule kuanzia chekechea hadi form six na vyuo vya ufundi.ardhi tunayo kubwa tu ili alishindikani.halafu kuwena kikosi maalumu cha kukamata hawa macharii mtaani hasa wale wanaolala pale nmb house posta mchana kweupe na pale mnazi mmoja usiku.na wale wamama wapewe kazi ya kufua na kupika ili tumalize kazi ya kuomba omba mtaani.badae watoto hawa wakimaliza elimu yao tunaweza watumia jeshini.wakawa walimu na kazi zengne hapa kwetu.jk akiruka safari hii ajitahidi kutafuta wafadhili wa hili.au Kama tumechoka kusaidiwa vitu vidogo kama hivi matajiri wa ndani watusaidie kwa pamoja kama Rostam,Mengi,riz,bakheresa,dewji,mitandao ya simu,mabank,ila kituo hiki kijengwe mbali na makazi ya raia wa kawaida
 
Watoto wa mitaani wameongezeka, na wengi.wametokea mikoani kukimbilia kwenye majiji.
Tatizo linaanzia kwenye familia, malezi kufikia mpaka binti kupata mimba, inakuja kijana aliyempa mimba na kuikataa.
Hapo ndio familia inatakiwa isimamie malezi ya mtoto hata kama kijana kakataa, kinyume cha hapo, binti akifukuzwa ndio anamtupa mtoto.

Wanawake km unaona huwezi kutunza mtoto tumia protection, matatizo yakikupata huyo kijana hutomuona.
Mnatesa tu watoto mitaani.
Nyingine ni wamama wa kambo nao wanachangia watoto kutoroka majumbani.
Mwisho mimi nalia na Wizara ya Jinsia wanawake na watoto, hii wizara iko butu sn kushughulika na watoto wa mitaani.
 
Kabla ya serikali tujiangalie sisi kama jamii tumewajibika vipi kupunguza tatizo la watoto wa mtaani?
Hawa watoto hawatoki porini wanatoka ktk majumba na mitaa yetu,

Sababu za Tatizo:
1.kuvunjika kwa ndoa
2.kufariki kwa wazazi
3.umaskini ulikithiri

Kabla ya kutibu tatizo ni vyema kuwekeza nguvu ktk vyanzo vya tatizo.
Sababu nyingine
1.Ukatili uliokithiri kwa watoto
2.Domestic violence-vitendo vya unyanyasaji kijinsia[Mfano baba kumpa kipondo mama kila siku]
3.Ulevi uliokithiri wa wazazi
4.Harmful traditional practises -mfano female genital mutilation
 
Watoto wa mitaani wameongezeka, na wengi.wametokea mikoani kukimbilia kwenye majiji.
Tatizo linaanzia kwenye familia, malezi kufikia mpaka binti kupata mimba, inakuja kijana aliyempa mimba na kuikataa.
Hapo ndio familia inatakiwa isimamie malezi ya mtoto hata kama kijana kakataa, kinyume cha hapo, binti akifukuzwa ndio anamtupa mtoto.

Wanawake km unaona huwezi kutunza mtoto tumia protection, matatizo yakikupata huyo kijana hutomuona.
Mnatesa tu watoto mitaani.
Nyingine ni wamama wa kambo nao wanachangia watoto kutoroka majumbani.
Mwisho mimi nalia na Wizara ya Jinsia wanawake na watoto, hii wizara iko butu sn kushughulika na watoto wa mitaani.

#Bantu Lady hiyo wizara imelala ni kama haijui kazi yake maana hawa watoto wanazidi tu na wzara husika iko kimya.
 
Watawala kama wanavyotafuta wafadhili kwenye mambo mengine,wakati umefika wajenge kituo kikubwa hapa
nchini kitachokuwa chini ya ustawi wa jamii-kikusanye watoto wote wa mtaani na wawekwe hapo kuwe na shule kuanzia chekechea hadi form six na vyuo vya ufundi.ardhi tunayo kubwa tu ili alishindikani.halafu kuwena kikosi maalumu cha kukamata hawa macharii mtaani hasa wale wanaolala pale nmb house posta mchana kweupe na pale mnazi mmoja usiku.na wale wamama wapewe kazi ya kufua na kupika ili tumalize kazi ya kuomba omba mtaani.badae watoto hawa wakimaliza elimu yao tunaweza watumia jeshini.wakawa walimu na kazi zengne hapa kwetu.jk akiruka safari hii ajitahidi kutafuta wafadhili wa hili.au Kama tumechoka kusaidiwa vitu vidogo kama hivi matajiri wa ndani watusaidie kwa pamoja kama Rostam,Mengi,riz,bakheresa,dewji,mitandao ya simu,mabank,ila kituo hiki kijengwe mbali na makazi ya raia wa kawaida

Wazo lako ni zuri sana. Tatizo kubwa ni uaminifu kwa wale watakaopokea misaada kwa ajili ya hawa watoto. Mungu atusaidie tuwe na roho ya upendo.
 
Hivi umejiuliza endapo tukipendana na alienacho kumjali asienacho tunaweza kuondosha watoto wa mitaani?
 
Watoto hawa wa mitaani watasaidiwa vipi? Tuseme ndo serikali imeshindwa kabisa kupata ufumbuzi ama? Nashangaa sana jinsi ambavyo hao watoto walivyo. Nilipokuwa #Mwanza sikufurahishwa na hali yao maana wanalala hadi uvungu mwa daraja. Hii hali sio Mwanza tu bali TANZANIA nzima na vitongoji vyake. Nimefika #Moshi na #Arusha hali ni hiyohiyo.

tunasikilizia obama atakapo rudi tena ufumbuzi utapatikana..
 
Back
Top Bottom