Tatizo la vumbi nchini

Quemu

JF-Expert Member
Jun 27, 2007
984
128
Inawezekana tatizo la joto liko nje ya uwezo wa kiutaalam kulithibiti. Lakini kweli hatuwezi kutatua tatizo la vumbi? Maana duh...hili vumbi sasa limezidi hapa Bongo. Nilikuwa Arusha wikiendi hii, yaani nimebugia vumbi mpaka likanikaba koo... Dar ndo usiseme.... yaani hata uwezi kuvaa kiatu chako cha mng'aro...lol

Kamanda Kibunango, mwanamazingira maarufu hapa JF, na wanamazingira wote waliopo humu, hebu tushushieni mtiririko wa kitaalam kuhusu ni nini kinaweza kufanyika ili kupunguza vumbi bongo?
 
...duh, ndio maana niliona umepotea siku mbili tatu!! kumbe umejitia minazi mirefu bila kuaga lol. Vipi hukupata funza huko Arusha??

Ha ha ha ha ukiaga uchelewi kusubiriwa airport na wakulu...nilitonywa kuwa wakulu wana usongo na wana jf wote....kwa hiyo siku hizi mwendo ni kuibuka bongo kimya kimya tu...maana uchelewi kufanywa mfano...lol

Bana Arusha kuna vumbi kinoma yaani. Cha kushangaza watu wanausifia kuwa ni msafi, sijui wanasahau kuwa vumbi ni sehemu ya uchafu.

Mzee unazungumzia funza au "FUNZA?"
 
hahahahaha, we nae!! ushahidi binafsi....lol, nakusubiri chini ya ngazi nikubebe!!:)


domo lako lawezana na NN NM LB, hizo lugha uwapelekee wale wapaka wanja wa mkaa kule mikahawani njia ya kwenda soweto au kule ol matejooo
 
...haya nimekubali!! nilikuona siku ukimtoa kamasi kamanda manyota injaji a.k.a FMES a.k.a Msee wa Ze Dataz, basi toka siku ile mie nimezima fagi!! Sina ubavu mama na rasmi nabadili kauli yangu ya kuwa Arusha kuna funza...jamanieeee, Arusha hakuna funza!!!

YNIM....mkia katikati ya miguu!


hujatulia unahitaji kupepewa;)
 
wewe sio wa kwanza kusema hivyo! bila shaka sijatulia kweli, hahaha itabidi leo nikirudi home nijiangalia vizuri kwenye kioo:confused:

nahitaji kupepewa na vile vipepeo vya kiswahili vyenye maneno kama ya kwenye kanga....kiwe kimeandikwa, "vitu vitamu havitaki pupa, hebu tulia wewe kaka."[B]:D[/b]


haswaaa, ulijuwajeee. Kwenye scale ya kumi ya utulivu, yako iko kwenye sifuri au inaendea kwenye hasi. Hivyo basi, nahisi unahitaji zaidi ya hicho kipepeo kukutuliza :)
 
....hahahahaha, haya niwekee sawa huyo mtu wangu!! mupe dozi...:D, mie ni mdengestani natokea Nanjilinji, babu yangu alikuwa mganga wa mahaba. LOL


ha ha haaa, sio wa rika langu.

Jibu lako kwa QM lilikuwa muafaka. Till then.
 
QM

Tatizo la vumbi mijini linachangiwa na mambo mengi, kuanzia maziringira ya mji hadi miundo mbinu yake. Hali kadhalika namna ya uendeshaji wa miji hiyo katika suala zima la utundazaji wa mazingira.

Kwa mji wa AR kuwepo kwa vumbi huko ni dalili mojawapo ya mabadiliko ya hali ya hewa na uchakavu mkubwa wa mazingira katika mji huo. Miaka ishirini iliyopita Arusha ilikuwa ni nadra kukumbana na vumbi. Kwa mfano ilikuwa unaweza kutoka Kijenge hadi mjini pasipo kuchafua kiatu chako cha ngozi cha Bora kwa kutembea kwa miguu.

Hali kadhalika ilikuwa sio rahisi kuchafua kiatu chako ama kubanwa na kikohozi cha nguvu na chafya za hapa na pale iwapo utatembea kwa miguu toka Ngarenaro hadi mnara wa saa (New Arusha Hotel) kupitia barabara ya Uhuru aka Sokoine.

Upanukaji wa mji wa Arusha pasipo kuzingatia athari za kimazingira, uchakavu wa barabara, ongezeko la watu, uanzishaji wa viford ni mojawapo ya sababu ambazo zimechakaza mji wa Arusha na kuwa mkavu kiasi cha kusababisha vumbi.
 
Inawezekana tatizo la joto liko nje ya uwezo wa kiutaalam kulithibiti. Lakini kweli hatuwezi kutatua tatizo la vumbi? Maana duh...hili vumbi sasa limezidi hapa Bongo. Nilikuwa Arusha wikiendi hii, yaani nimebugia vumbi mpaka likanikaba koo... Dar ndo usiseme.... yaani hata uwezi kuvaa kiatu chako cha mng'aro...lol

Kamanda Kibunango, mwanamazingira maarufu hapa JF, na wanamazingira wote waliopo humu, hebu tushushieni mtiririko wa kitaalam kuhusu ni nini kinaweza kufanyika ili kupunguza vumbi bongo?



Mkuu kumbuka kwamba nchi yetu bado ipo nyuma kimaendeleao na mpaka kufikia kudhibiti vumbi nadhani itachukua more than 10 years not now....Sasa hilo swala ndio inabidi apatikane rahisi mwenye kuaminika zaidi maana sasa kila mtu akiingia madarakani anajiangalia yeye na familia yake basi wengine watajijua wenyewe ndio tatizo lilipo hilo........Kwa hiyo nadhani tutachukua time kidogo mpaka kufikia kudhibiti hilo swala.........
 
Back
Top Bottom