Tatizo la utumbo mpana kuwa mrefu kuliko kawaida

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,257
9,878
Wanabidi wataalamu wa afya naomba msaada wenu, mtoto wa ndugu yangu anaumri wa miaka 5, alikuwa analalamika sana kuwa anapata maumivu ya tumbo baada ya kula chakula na walipompeleka Hospitali madaktari walikuwa wanamuandikia antbiotic lakini hata huvyo hazikuweza kumsadia mpaka wiki mbili zilizopita alipokwenda hospitali na kumkuta dr. mmoja aliweza kubaini tatizo la huyo mtoto kuwa anatatizo la utumbo mpana ni mrefu kuliko kawaida hali inayopelekea uchafu kubaki tumboni na kumsababishia maumivu ya tumbo.

Kwa hiyo Dr. amemuandikia dawa za kutumia kwaajili ya kutoa uchafu then waangalie uwezekano wa kufanyiwa upasuaji.

Tokea kupewa taarifa hiyo wazazi wa mtoto wamekuwa na majonzi na hajui hatima ya mtoto wao. Napenda kwa niaba ya familia hiyo kuomba msaada wa mawazo na ushauri kwa wale ambao wanalijua au wamekumbana nalo tatizo hili tuweze kushare hapa,

Natanguliza shukrani za dhati.
 
Baada ya kumpeleka hospitali kadhaa tumekutana na Dk mmoja ameshauri afanyiwe upasuaji na kabla ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa tatizo wakati huo watabadilishe mfumo wa utoaji taka kuwa chini ya kifua kwa muda wa miezi mitatu, hapo tumepata mtihani kwani pamoja na mambo mengine huenda hali hiyo ikamuadhiri sana mtoto kisaikolojia pamoja na wadogo zake pia ni changamoto kwa wazazi wake.

Ikiwa kunamdau yoyote ambaye ana alishakabiliana na ugojwa huu nitafurahi sana kama atatupa maelekezo ya jinsi alivyokabiliana nao

Ni hayo tu.
 
kuwa mvumilivu tu akina mzizi watakuja soon, bt poleni na Mungu atamponya mtoto, punguzeni wasiwasi na majonzi ili kumtia moyo mtoto
Baada ya kumpeleka
hospitali kadhaa tumekutana na Dk mmoja ameshauri afanyiwe upasuaji na
kabla ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa tatizo wakati huo watabadilishe
mfumo wa utoaji taka kuwa chini ya kifua kwa muda wa miezi mitatu, hapo
tumepata mtihani kwani pamoja na mambo mengine huenda hali hiyo
ikamuadhiri sana mtoto kisaikolojia pamoja na wadogo zake pia ni
changamoto kwa wazazi wake.

Ikiwa kunamdau yoyote ambaye ana alishakabiliana na ugojwa huu
nitafurahi sana kama atatupa maelekezo ya jinsi alivyokabiliana nao

Ni hayo tu.
 
kuwa mvumilivu tu akina mzizi watakuja soon, bt poleni na Mungu atamponya mtoto, punguzeni wasiwasi na majonzi ili kumtia moyo mtoto

Shukrani sana , tunaendelea kumuomba MUNGU.
 
Kaka yangu ali survive baada ya surgery pale Seliani ALMC Arusha.
Alikua anaingiziwa mpira kwenye mqundu
 
Back
Top Bottom