Tatizo la Umeme: Ushauri Kwa Mnyika Na January

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Kutokana na nafasi zao, hawa ni moja ya viongozi muhimu sana katika sekta ya nishati na madini, ambao sisi wananchi tunawategemea wawakilishe vilio na mawazo yetu, hasa yanayolenga uboreshaji wa sera katika sekta husika. Wengi tunapenda na kuthamini zana kazi za vijana wenzetu hawa, ya kuhakikisha Serikali inakuwa makini katika uendeshaji wa sekta hii muhimu kwa uchumi wa nchi yetu. Sasa kwa vile binafsi siwafahamu wote ‘in person' (nadhani nina wenzangu wengi humu katika hili), nimeonelea pengine njia yetu nzuri ya kuwafikishia mawazo yetu juu ya ni JamiiForums. Iwapo wataona mawazo haya ni ya maana, basi litakuwa jambo jema wakienda bungeni wiki ijayo wakawakilishe mawazo yetu pia. Mada hii inamlenga zaidi Mh. Mnyika, ambae hivi karibuni amefanya ‘uamuzi mgumu', wa kuirejesha hoja ya Richmond bungeni. Katika hatua yake hiyo, ninapendekeza pia aliangalie suala la umeme kwa mapana zaidi, kwani sekta hii inakabiliwa na matatizo kubwa kuliko la Richmond, ambayo jamii haiyafahamu. Matatizo haya yakipatiwa ufumbuzi, haitakuwa rahisi kwa mikataba tata kama hii kujitokeza tena.

Kabla ya Sheria mpya ya umeme ya Mwaka 2008 kupitishwa na bunge, Tanesco lilikuwa ni kampuni pekee yenye mamlaka ya kujishughulisha na yafuatayo kwa pamoja: Kuzalisha, Kusafirisha na Kusambaza Umeme Tanzania. Sheria mpya ya Umeme ya Mwaka 2008, imelegeza masharti haya, ambapo sasa sekta binafsi inaruhusiwa kufanya shughuli kama za Tanesco. Lakini pamoja na nia nzuri ya serikali katika hili, Sekta ya Umeme bado haina mvuto mkubwa kwa wawekezaji binafsi kwa sababu kuu zifuatzo:

Moja, pamoja na uwepo wa Sheria Mpya ya Umeme ya Mwaka 2008, sekta hii inakabiliwa na tatizo la mrejesho mdogo wa mtaji (Low Return on Investment). Na kama tunavyoelewa, moja ya kanuni kuu za uwekezaji, ni kupeleka mitaji kwenye maeneo yenye mirejesho ya juu (kwa mfano kama ilivyo katika Sekta ya Mawasiliano, chini ya TCRA).

Je hali ya Sasa Ikoje?

EWURA ina tarrifs za aina mbili: ‘Feed in Tariff'; na Small Power Project Tariff (SPPT). Tatizo linalowakabili wawekezaji binafsi katika sekta ya umeme, ni uwepo wa tariffs za kiwango cha chini sana kuleta mvuto. Kwa mfano, SPPT ni kama Shillingi 124 kwa Kilowati. Chini ya kiwango hiki, mrejesho wa mtaji (Return on Investment) ni kati ya asilimia 2.5% na 2.8%. Kwa mrejesho huu, ukipiga mahesabu, unapata PayBack Period ya miaka sio chini ya 30. Kwa maana nyingine, mwekezaji katika sekta ya umeme atarudisha hela za mtaji wake baada ya miaka 30. Sasa kutokana na uhalisia wa mambo kwamba mazingira ya kisiasa katika nchi zetu hayaeleweki, leo vita, kesho amani, miaka 30 ni mingi sana kwa mwekezaji kusubiri kurudisha hela yake.

Ili mwekezaji apate mrejesho mzuri kwa kuwekeza kwenye sekta ya umeme Tanzania, kwa mfano mrejesho wa asilimia 20%, hivyo kupekea hela yake irudi katika miaka 5 hadi 7, inabidi EWURA iweke kiwango cha SPPT Tarrifs sio chini Shillingi 3,000 per Kilowatt hour, kutoka kiwango cha Sh. 124.

Ni muhimu pia hapa kuangalia suala la ruzuku ya serikali katika sekta ya umeme, kitu ambacho pia kinachangia sekta ya umeme kutokuwa na mvuto kwa wawekezaji. Kwa mfano, katika mazingira ya sasa, ruzuku ya Serikali kwenye sekta ya umeme inapelekea uwepo wa asilimia kati ya 40 hadi 50 ya watumiaji (consumers), kutolipia umeme wa Tanesco. Hii ni idai kubwa sana.

Pili – kikwazo kingine ni tabia ya benki nyingi Tanzania kutokuwa tayari kutoa mikopo kwa wawekezaji wenye nia ya kujishughulisha katika na uzalishaji umeme. Hii ni kwa sababu mbalimbali, lakini kubwa mojawapo tumeshaiona – mrejesho mdogo wa mtaji. Ndio maana hata mradi kama wa Richmond, ulitegemea Government Guarantee.

Tatu – kikwazo cha tatu ni bureaucracy na rushwa. Mwekezaji anapitia mchakato wenye taabu sana, kabla ya kupewa ‘a go ahead' na serikali kuanza shughuli zake. Kwa mfano, kupata vitu kama, ‘water rights', ‘land rights', ‘generation permits', na Environmental Impact Assessment (EIA) Clearance, Tanzania, ni mchakato ‘pasua kichwa'. Kwa mfano, Clearance ya EIA inayotolewa na National Environmental Management Council (NEMC), huchukua kati ya 2-3 years.

Katika hali ya kawaida, Tanzania ina vyanzo vingi sana vya kuzalisha umeme, pengine kuliko nchi zote za maziwa (Great Lakes). Tuna uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha mahitaji ya mijini na vijijini, na kubakisha mwingine mwingi wa kwa ajili ya kuuza nchi jirani, hivyo kuongeza pato letu la taifa. Lakini tatizo letu ni utegemezi wa mvua. Kama jinsi tunavyotegemea ‘KILIMO CHA MVUA', sisi pia ni mabingwa wa kutegemea ‘UMEME WA MVUA' (Hydro). Hydro ni chanzo muhimu lakini hakitoshi, na serikali haiweki jitiada za kweli to ‘diversify' vyanzo vya nishati. Tanzania inategemea umeme wa mvua kwa asilimia karibia 60%. Hiki ni kikwazo kikubwa kwa Maendeleo ya uchumi wetu.

Pia katika mazingira ya sasa (due to disinvestment in the sector), miundo mbinu ya uzalishaji na usambazaji wa umeme Tanzania ipo katika hali uchakavu mkubwa. Kutokana na hali hii, karibia asilimia 25% ya umeme unaozalishwa katika vyanzo mbalimbali, vinapotea wakati wa usafirishaji na usambazaji, hivyo kupelekea asilimia 80% tu, au chini ya hapo ya umeme unaozalishwa kufika kwa watumiaji. Kama tutakavyoona punde, installed capacity ya umeme Tanzania ni kama MW 948, sasa zikipotea 25% ya hizo, ina maana actual capacity ni kama 710 MW.

Mahitaji ya Umeme Tanzania:

Kwa wastani, watumiaji wa umeme Tanzania kama tunavyofahamu sio zaidi ya asilimia 15% ya watanzania. Lakini muhimu zaidi ni kwamba, vijijini, ambapo ndipo watu zaidi ya milioni 30 wanaishi na kufanya hsughuli zao mbalimbali, ni asilimia 2% tu ndio wana umeme.

Tukiachana na hayo, mahitaji ya umeme Tanzania ni kama megawatts 800 (Plus/Minus), lakini jumla ya vyanzo vyote vilivyopo sasa kuanzia vile vya umeme wa mvua (Mtera n.k, Gesi ya ubungo, IPTL), havifikii kiwango cha mahitaji ya sasa i.e. MW 800. Nitafafanua.

Tutazame ‘Numbers' Zifuatazo:
Jumla ya installed capacity ya Umeme Tanzania hivi sasa ni kama Megawati 948, na iwapo zimeongezeka, basi ni kwa kiasi kidogo sana kwani kwa miaka mitatu iliyopita, hapajawa na mradi wowote mkubwa wa kuongeza capacity hii. Katika hizi 948 MW, peak huwa haifikii kiwango cha MW 948 (kutokana na sababu tulizokwishaona i.e. about 25% is lost in transmission and distribution). Peak huwa ni around MW 708.

So What?

Tumekwisha ona kwamba Umeme wa Mvua (Hydro) unachangia karibia asilimia 60 ya vyanzo vyote, huku diversification ya vyanzo vingine ikiwa ndogo sana. Sasa, kama tunavyofahamu, IPTL ni kama haipo kwani kuna kesi mahakamani dhidi yake na serikali ya Tanzania. Sasa ukitoa umeme wa IPTL ambao ni MW 100, ukizitoa hizi MW 100 katika installed capacity i.e. MW 948, tunapata Megawatts 848, against peak demand ya MW 708. Bear in mind kwamba, hapa hatuja take into account of the 25% loss in transmission.

Sasa nini maana ya takwimu hizi:

Kwa kuanzia, tunafahamu tayari kwamba kutokana na uchakavu wa miundo mbinu ya umeme, uzembe, manejimenti mbovu, n.k, hakuna chanzo chochote kinachopeleka umeme at Maximum Capacity per agreement. Ni jambo la kawaida sana kwa umeme mwingi kupotea potea ovyo tu. Ndio maana unakuta kwamba, inapotokea chanzo kimoja (mfano mtera, kidatu n.k), kinapata itilafu ndogo, hata kama ni utapelekea upungufu wa MW 50 tu (hamsini), maana yake ni kwamba nchi inaingia gizani, kwani kwa mahesabu tuliyokwisha yaona hapo juu, itilafu ndogo tu ya namna hii, inaleta vurugu kubwa sana katika mlinganyo wa Supply and Demand (Ugavi na Mahitaji) ya umeme.

Umeme na Uchumi:

Hapa sina haja ya kuingia kwa undani kwani sote tunaelewa umuhimu wa umeme katika uchumi. Ila niseme tu mwamba - kwa miaka karibia kumi na mbili sasa, uchumi wa Tanzania kwa wastani unakuwa kwa asilimia kati ya 6% na 7% kwa mwaka.
Lakini je, kasi ya ukuaji wa uchumi inaenda sambamba na kasi ya ukuaji wa umeme?

Kasi ya ukuaji ya umeme wa Tanesco kwa mwaka ni kati ya asilimia 8% na 10%. Kwahiyo, tukichukua mahitaji ya umeme ya mwaka ambayo tumeona hapo juu ni kama megawati 708, hii ina maana kwamba, ili Tanesco iende sambamba na ukuaji wa uchumi Tanzania, kila mwaka, Tanesco inatakiwa kuongeza uzalishaji Umeme kwa kiwango sio chini ya MW 64 (nimepata MW 64 kwa kuchukua wastani wa asilimia 8 na 10 na kupata asilimia 9; kisha asilimia 9 mara MW 710 ni sawa MW 64).
Ni jambo lisilo na ubishi kwamba Tanesco haina uwezo wa kutikiza hili, lakini mbaya zaidi ni kwamba mazingira ya sasa ki-sera pia hayawezi fanikisha sekta binafsi kuziba pengo la Tanesco.

EWURA na Sakata la Umeme

Sote tunaelewa EWURA ipo kwa ajili gani. Lakini kwa jinsi inavyoendeshwa, ni dhahiri kwamba EWURA nayo inahitaji another 'Watch Dog', kuithibiti, kwani imeanza kuendesha sekta ya umeme kwa kuendekeza mapungufu yaliyopo katika sekta hii, badala ya kuiboresha. Uamuzi wa EWURA kupandisha gharama za umeme majuzi haukuwa uamuzi endelevu bali uamuzi wokovu kwa Tanesco, huku EWURA ikiacha matatizo ya msingi yaendelee kuwepo.

Wakati wanatangaza bei mpya ya Umeme, EWURA ilitoa maelekezo yafuatayo kwa Tanesco kuyatekeleza for the next year:

1. Tanesco ihakikishe ‘Voltage Variation' isizidi 10 Volts.
2. Tanesco ihakikishe upotevu wa Megawatts wakati wa usafirishaji na usambazaji hauzidi asilimia 10 (upotevu huu kwa sasa ni asilimia karibia 25%).
3. Tanesco wahakikishe kwamba hawakati umeme kwa zaidi ya mara mbili kwa mwezi.
4. Tanesco iongeze wateje wapya 100,000 (laki moja) kwa mwaka ujao wa fedha.

Ni dhahiri kwamba maelekezo haya ya EWURA kwa Tanesco hayatatekelezeka kwa sababu nyingi, baadhi yake ambazo tumekwisha ziona. EWURA imejaribu kuja na justification mbalimbali juu ya ongezeko la bei ya umeme zisizo na mashiko, huku pia ikitoa maelekezo kwa Tanesco, kama vile hili litapelekea unafuu kwa mtumiaji wa umeme. Hali haitakuwa hivyo. Sana sana hali itaendelea kuwa mbaya kwetu watumiaji wa umeme, na EWURA itazidi kutumiza na bei mpya kwa kutupa sababu nyingine mpya.

Ni dhahiri Tanesco inakabiliwa na changamoto kubwa sana, nje ya Richmond, IPTL n.k. Matatizo ya mikataba yenye utata ni matokeo ya udhaifu wa kisera wa sekta ya umeme, kama tulivyokwisha ona.

Tunakumbuka kuna kipindi Tanesco iliingia ubia na sekta binafsi (NetGroup Pty), lakini hatua hii haikuleta ufumbuzi wa kudumu. Sasa tufanye nini na shirika letu la Tanesco, tuingie tena ubia tena? tufanye privatization ya Tanesco? Tuliache kama lilivyo lakini kuhimiza lipate more autonomy (less political interference), huku tuki modernize management?

Vingineyo, tangia mwaka 2008, ni ruksa kwa sekta binafsi kushindana na Tanesco, hivyo kupelekea ufanisi zaidi. Lakini tumeona vikwazo vilivyopo kwa sekta binafsi. Kutokana na hili, ni dhahiri tutaendelea kuwa na miradi ya umeme wa ‘zima moto' kwa muda mrefu.

Mwisho, miaka mitano iliyopita, kabla tu ya sakata la Richmond, tulisoma kwenye vyombo vya habari kuwa kampuni kubwa ya umeme kutoka Canada "ENERGEM", ime-express interest kuanzisha mradi mkubwa wa umeme (900 MW) katika bonde la mto rufiji - Stiglers Gorge, kwa gharama zao wenyewe, na huku wakiipa serikali hisa kubwa. Mradi huu ungekamilika mwaka 2012. Lakini kwa sababu tusizozijua, mradi huu ukayeyuka, na baadae kusoma kwenye Internet kwamba Energem wamejitoa. Vinginevyo, kuanzia 2012, suala la mgao wa umeme lingekuwa ni historia.

Ni muhimu kwa serikali sasa kuondoa siasa katika sekta ya umeme. Na vile vile ni muhimu kwa serikali kuanza kuiangalia sekta hii kama ni moja ya mahitaji ya msingi ya mtanzania, badala ya kuichukulia kama ni anasa kwa mtanzania. Tusaidieni bungeni kupigania effective policy ya umeme itakayotuokoa watanzania.

Nawasilisha.
 
Great Analysis Mchambuzi!!! Umetusaidia wengi wetu kuelewa undani wa janga hili. Sijui kama hao walengwa wana ufahamu wa kina juu ya suala hili. Haya yakiwekwa mezani mle mjengoni kwa ufasaha, wananchi watafunguka sana. Bravo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom