Tatizo la Umeme - Tuondokane na shirika moja kushika hatamu za huduma

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,885
6,885
Kuondokana na tatizo la umeme ni kuruhusu mashirika mbalimbali na watu binafsi kutoa huduma hiyo. Siku za nyuma tulikuwa na matatizo ya shirika la simu nchini na huduma yao ilisumbua mno watu, lakini baada ya mashirika binafsi mengi kuanza kutoa huduma hizo sasa tatizo la simu imebaki historia tu.
Iwapo watu binafsi wataruhusiwa kutoa huduma ya umeme ni matumaini yangu gharama za umeme zinazolalamikiwa zitapungua kutokana na ushindani.

Gharama ya umeme kwa sasa ni kubwa zaidi kwa sababu ya mzunguko wake na kila unakopitia kila mmoja anataka ulaji. Makampuni yanayosaidia kuchangia umeme kwenye grid ya taifa yanauza umeme huo kwa kampuni ya Tanesco na Tanesco inatuuzia sisi. Ingekuwa bora Makampuni hayo yatoe huduma hiyo moja kwa moja hivyo gharama zingepungu.

Katika utawala wa Mzee Ruksa kulikuwepo na matatizo makubwa sana ya usafiri na alitumia utashi kuruhusu watu binafsi kusaidia kutoa huduma kwa watu na leo imebaki ni hadithi za kusimuliwa tu.

Kuna mitambo ya kufua umeme ya gharama za kawaida tu ambayo wengi wanaweza kumudu kununua na kusambaza huduma hizo kwa majirani. Kuna mitambo inayoendeshwa kwa nguvu ya upepo inaendeshwa kwa gharama nafuu kwani katika maeneo mengi Tanzania yanakubalika kwa kufua umeme kwa njia hiyo.

Watu binafsi wafunzwe namna ya kuhifadhi umeme wanaonunua toka makampuni ya umeme kama Tanesco nk. Wawe na bettery za kuhifadhi umeme huo hivyo wakati unapokatika wanatumia umeme waliouhifadhi.

Njia nyingine ni kununua mitambo solar energy ya kufua umeme kifamilia. Hiyo ni kwamba unagharimia mara moja for life. Bills za umeme itabaki historia vinginevyo kama una mashine kubwa ndani ya nyumba yako.

Bila makampuni binafsi kuanza kusambaza huduma za umeme mchezo wa kisiasa utabaki palepale kama mchezaji anayecheza danadana ndani ya pernalt area badala ya kutandika mkwaju golini.
 
Back
Top Bottom