Tatizo la umeme Tanzania kuhusishwa na vita kati ya Serikali na Askofu Kakobe

Yonjolo

Member
Jan 19, 2012
79
6
Umeme wa Tanesco haupiti ktk kanisa la FGBF chini ya kiongozi wake Ask. Kakobe. Kama gazeti moja lilivyoripoti leo kwa kichwa 'KAKOBE AFANYA KWELI'
:Ule umeme wa 132kv uliolazimishwa kupita kanisani kwa Kakobe wagoma
:Kwa mwaka mmoja sasa Kakobe ajichimbia kwa maombi ya Prayer Retreat
:Yaelezwa yaliompata Jairo ni madogo kama Ngereja hatotubu.

Wana Jf wenzangu, jambo hili limenigusa sana hasa ukichunguza sana kuna ukweli ndani yake. Matatizo ya umeme hayaishi nchini mbaya zaidi UMEME WAPANDA BEI, huku huduma bado hafifu.

Tukumbuke Ask. Kakobe alitangaza kuwa bila ya Ngeleja na wenzake kutubu tatizo la umeme halitokwisha.

Maoni yangu: Ngeleja na jopo lake wanapaswa kuwajibika kwa kutubu na kurudisha mabango ya kanisa la mtumishi wa Mungu Ask. Kakobe kama walivyofanya ktk makaburi ya machifu kwa kupitisha pembeni nyaya na umeme kupita baada ya kugoma kama ktk kanisa la Kakobe. Serikali inapaswa kuwaheshimu viongozi wa dini kwani amani ya watanzani imekuwepo baada ya uongozi wa Nyerere kuheshimu din
 
Anayejua ishu hii hebu aseme ukweli jama!...
Mbona hakuna maelezo ya kiufundi?
 
Kakobe! watu wenye kudanganyika kirahisi kama wewe ndio wanaokimbilia kikombe cha babu! TAFAKARI
 
Kwa wenye akili timamu peke yao.

Kama kakobe ndie anaesababisha kuwe na matatizo ya umeme eti kwa kuwa ana bifu na serikali kupitia wizara ya nishati na madini je wanaoumia ni kina Ngeleja au Wananchi pamoja na waumini wake? Je kuna utumishi wa Mungu au Uchawi hapo?
 
wangapi mnaamini kakobe ni mtumishi wa Mungu? Na miujiza yake yatoka kwa Mungu?

Kakobe anaanzia mbali sana mtu mwerevu utamjua kuwa anataka kuhusisha matatizo ya umeme na mgogoro wake na tanesco aseme yeye ndie amefanya iwe kuna matatizo ya umeme! Naogopa asije na kikombe watu wakafumbika macho kwa swala la umeme wakamwagika kama walivyomwagika samunge matokeo yake tukapoteza mamia ya watu.
 
Wakuu hii mbona sio mahala pake. Wanajamvi kabla ya kupost thread naomba tuangalie sana, tuwe makini. JF IS FOR GREAT THINKERS. IS NOT FOR STUPING THINKERS.
 
Kwa wenye akili timamu peke yao.

Kama kakobe ndie anaesababisha kuwe na matatizo ya umeme eti kwa kuwa ana bifu na serikali kupitia wizara ya nishati na madini je wanaoumia ni kina Ngeleja au Wananchi pamoja na waumini wake? Je kuna utumishi wa Mungu au Uchawi hapo?

duu... hivi mchawi anaweza kuroga umeme? na kama inawezekana, je itakuwa ni dhambi au sio dhambi? maana karoga kitu kisicho hai(umeme)!
 
Kwa wenye akili timamu peke yao.

Kama kakobe ndie anaesababisha kuwe na matatizo ya umeme eti kwa kuwa ana bifu na serikali kupitia wizara ya nishati na madini je wanaoumia ni kina Ngeleja au Wananchi pamoja na waumini wake? Je kuna utumishi wa Mungu au Uchawi hapo?

Mungu akiwa anatoa adhabu kwa mtu mmoja inakuwa ni kwa kizazi kizima mfano kidogo tu kosa la Adamu adhabu mpaka kwako wewe ambaye ukula tunda.
 
Yaani Kakobe anafanya maombi (sijui anaroga) sisi tusipate umeme....halafu anataka sadaka?
 
Haya matatizo ya kiufundi yasigeuzwe kuwa ya kiimani...........

Umeme haupiti hapo wakati tayari unapoozwa makumbusho sub station tayari kusambazwa na unasambazwa tangu mradi ukamilike

Hayo Mengineyo ni utendaji wa watu na watahukumiwa kwa utendaji mbovu.
 
Kama angejitokeza Kabobe na kukiri hilo kidogo ingeleta sense. Mengine itabaki kuwa ni hisia za mtu binafsi au mmoja mmoja.
 
Back
Top Bottom