Tatizo la umeme na hatma ya CCM

Msema hovyo

Senior Member
Jul 3, 2011
195
86
Hatimaye CCM imefika mwisho baada ya kuchukiwa na watu wa kada zote kufuatia tatizo kubwa la umeme linaloikabili nchi. Watu wa rika, kada, kabila na dini zote hivi sasa wanajuta kuipa kura CCM na hasa Kikwete. wengi ninaokutana nao hivi sasa wanatamani uchaguzi urudiwe ili wafanye maamuzi tofauti. hatimaye CCM Imefika mwishowe.
 
haha hali yenu ni mbaya. kama hamtawapa wananchi umeme mapema iwezekanavyo basi maandamano ya kuwatoa madarakani yanakuja.
Nasikia ile kamati ya Nishati ikiongozwa na Januari inarudi tena Mtera kuangalia kama kweli hakuna maji,
Taarifa zinazoaminika zinasema, watakwenda na Mbunge wa Mtera yule anayeamini kwamba matatizo katika nchi hii yanaletwa na kuwepo kwa picha ya nyoka kwenye baadhi ya noti za fedha za Tanzania
 
Wananchi ndo wamemwambia asee! sio yeye!!
Hajanunuliwa laptop huyu!!! hata shati hajapewa, ajinunulia sarawili mwenyewe huyu, hapewi na CHAMA!
Bora umwambie, anafikiri na mimi nimehongwa chumvi na kapelo.
 
Nasikia ile kamati ya Nishati ikiongozwa na Januari inarudi tena Mtera kuangalia kama kweli hakuna maji,
Taarifa zinazoaminika zinasema, watakwenda na Mbunge wa Mtera yule anayeamini kwamba matatizo katika nchi hii yanaletwa na kuwepo kwa picha ya nyoka kwenye baadhi ya noti za fedha za Tanzania
haha! Kikwete keshauza nchi kwa lusifeli (shetani). Ndiyo maana tangu aingie ni matatizo tu, mara njaa, mara ajali, mara umeme etc etc
 
Back
Top Bottom