Tatizo la ukosefu wa madawati mashuleni, ni umaskini wa uchumi au wa busara?!

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,450
487
Kwanza kabisa nimshukuru Mungu kwa kunipa nafasi ya kuweza kuizunguka nchi yetu hii kwa takribani 99%. Nasema hivyo kutokana na kufanikiwa kwangu kufanya kazi katika mikoa karibu yote pamoja na wilaya zake hasa vijijini (in health and social market in the Community bases rural areas). Kati ya vitu ambavyo vimekuwa vikiiteka akili yangu ni hili la kuona watoto wetu wakikaa kwenye vumbi huku wengine wakiota vibiongo kutokana na kujipinda kwa kuandikia magotini huku wakiwa wamezungukwa na misitu yenye miti ya mbao ambayo unaweza kutembea kwa muda wa zaidi ya masaa sita kwa gari!

Tunavyo vyuo vya VETA ambavyo ni vya serikali na vikundi vingine vya kijamii vinavyojihusisha na masuala ya useremala, Sasa swali langu hizi Halmashauri zetu zinashindwaje kutumia vituo hivyo kutengeneza madawati kwa kila wilaya husika? Mbona kuna magogo mengi sana yanavunwa hapa kwetu na kuuzwa nje ya nchi kwa magendo na watu hao hao wanarudi kutuuzia samani za ndani kwa gharama kubwa wakati mbao zimetoka kwetu?
Ndiyo maana sasa najiuliza swali hilo hapo juu. Wanajamvi changieni mawazo yenu ili ujumbe huu uwafikie waliokaakwenye viti vya enzi.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom