wa UDOM
Member
- Apr 10, 2011
- 34
- 2
MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU TATIZO LA SIKIO
Ameanza kuugua ugonjwa wa sikio kuuma na ku_discharge mara kwa mara na doctors wamekuwa wakimpa atibiotics ambazo nimeona hazimsaidii.
Mara hii anaumwa ni awamu ya 3 ugonjwa kumrudia, nifanye nini jamani?
---
---Kwanza natanguliza shukrani kwa JF wote na hasa madokta wa JF kwa moyo wao wa kujituma.
Mimi nina tatizo la sikio langu la kulia kutoa usaha, na hili tatizo limeshakuwa la muda mrefu,nimeshajaribu kutumia dawa za kienyeji mpaka za hospitalini lakini ninachoambulia ni kustop kwa mda and then tatizo unirudia tena.
Naombeni msaada tafadhali.
---Wadau naomba mnisaidie,
Nina mwanamke wangu, yeye si mwanaJF ila ana matatizo ya masikio. Anadai kwamba yanamuuma sana kwa ndani na hayatoi usaha. Tatizo lilimuanza mwaka jana na analo kwa mwaka mzima sasa. Kwa anayejua dawa hasa ya mitishamba au ya kienyeji naomba anisaidie ili my wife to be apate nafuu.
Anateseka sana.
---Wakuu!
Mwenzenu nasumbuliwa na tatizo(ugonjwa) wa masikio kutoa usaha, tangu nikiwa mtoto mdogo kabla hata sijapata ufahamu sikio langu moja hutoa usaha.
Tatizo hili nimeishi nalo kwa kwa muda mrefu mpaka hivi sasa nina 20's bado tu linanisumbua...... nimetumia dawa kibao za hospitali na mitishamba lakini wapi mpaka hivi sasa nimechoka kiasi kwamba wakati mwingine nawaza aliyeniloga ashakufa hatua niliyofikia naona kawaida tu na nishakata tamaa ya kupona .....kwa ujumla huwa linanikosesha uhuru sana kwani muda wote popote nilipo lazima niwe kimachalemachale na pamba zangu na vijiti ili kudhibiti huo uchafu......
MWENYE KUIFAHAMU TIBA YAKE YA UHAKIKA TAFADHALI!
CC. MziziMkavu
---Habari wakuu...
Naamini Mungu bado anatupenda na kutupa uzima ndo maana tunakutana hapa
Samahan naomba kuuliza hii hali ya kusikia kelele nyingi masikioni( kama mashine ya kusaga mahindi) n hali ambayo natakiwa kuikubali na kuishi nayo?
Hali hii ilianza mwaka juzi(2016) na nmetumia dawa nyingi lakin sion mafanikio
Kuna wakat nashindwa hata kufanya kazi kwa sababu ya usikivu kuwa mdogo kwa sababu ya kelele hizi
Hivi naandika uzi huu ikiwa ni siku chache tangu niache kibarua changu kwa sababu ya shida Hii
Najaribu kufikir kama swala hili n halipon( kama wengi wasemavyo) bas nitaishi maisha ya namna gan
Najikuta nakata hata tamaa ya kuishi
Naomben mtazamo wenu ndugu zangu kama kuna mtu anaijua hii shida au alishawahi kukutana nayo na aliipona vipi
Ahsante
Sent using Jamii Forums mobile app
---Nimekua nikisumbuliwa na hili tatizo kwa zaidi ya mwaka wa 10 nikilichukulia poa tu. masikio yangu sigusishi maji kabisa, ikitokea kwa bahati mbaya hasa kwenye wakati wa kuoga maji ya kugusagusa kwa ndani basi kinachofata hapo ni maumivu kwa siku nzima japo kua hua simakubwa. Je hili nikawaida au ni tatizo? Kwa kifupi naishi mbali na maji karibu na sikio.
Na pia sewezi eka headset and headphone kwenye sikio langu kwani dakika moja tu itanitosheleza kuleta maumivu ya masikio kwa masaa na muda mwengine yakiambatana na maumivu ya kichwa. Ila kila nikitizama wenzangu wanajifanyia vizuri tu. Hata simu nikizungumza kwa muda mrefu kiodogo tu au simu ikiawa na sauti kubwa basi matokezeo ndio hayo hayo.
Je hii ni hali ya kawaida au ni ugonjwa? na kama ugonjwa naomba msaada wakuu.
Habari wakuu,
Naamini Mungu bado anatupenda na kutupa uzima ndo maana tunakutana hapa
Samahan naomba kuuliza hii hali ya kusikia kelele nyingi masikioni( kama mashine ya kusaga mahindi) n hali ambayo natakiwa kuikubali na kuishi nayo?
Hali hii ilianza mwaka juzi(2016) na nmetumia dawa nyingi lakin sion mafanikio. Kuna wakat nashindwa hata kufanya kazi kwa sababu ya usikivu kuwa mdogo kwa sababu ya kelele hizi. Hivi naandika uzi huu ikiwa ni siku chache tangu niache kibarua changu kwa sababu ya shida Hii
Najaribu kufikir kama swala hili n halipon (kama wengi wasemavyo) bas nitaishi maisha ya namna gan
Najikuta nakata hata tamaa ya kuishi
Naomben mtazamo wenu ndugu zangu kama kuna mtu anaijua hii shida au alishawahi kukutana nayo na aliipona vipi
Ahsante
Sent using Jamii Forums mobile app
Sikio ni sehemu ya mwili inayowezesha kusikia sauti. Wanadamu na wanyama mamalia wana masikio mawili kichwani. Wanyama wengine husikia sauti kupitia viungo vingine kama vile buibui kupitia nywele za miguu au samaki kupitia neva ndefu iliyopo chini ya ngozi kando ya mwili.
Sikio la binadamu huwa na sehemu ya nje inayoonekana na sehemu isiyoonekana iliyopo ndani ya fuvu. Usikivu wenyewe hutokea kwenye sehemu ya ndani.
Sehemu ya nje yenye kazi ya kupokea na kukusanya mawimbi ya sauti na kuyaelekeza ndani ya njia ya sikio inayoishia kwenye kiwambo cha sikio ambacho ni ngozi inayotikiswa na sauti.
Kucheza kwa kiwambo kunatikisa mifupa sikivu ambayo ni mifupa mitatu midogo inayoungwa nacho na mwendo wa mifupa sikivu unapokelewa na mishipa ya fahamu ya sikio la ndani ukibadilishwa kwa mishtuko ya umeme inayopita kwenye neva hadi ubongo. Chumba cha sikio la kati kimeunganishwa na koromeo kwa njia ya neli ya koromeo.
Sehemu ya kiwambo cha sikio pamoja na chumba nyuma yake penye mifupa sikivu huitwa sikio la kati. Nyuma yake kuna sehemu ya sikio la ndani. Kiungo cha mwili kinachobadilisha mwendo wa mishipa sikivu kuwa alama za neva huitwa komboli.
Kazi nyingine za masikio
Pamoja na kupokea sauti, sikio la ndani pia lina kazi ya kutunza uwiano wa mwili likiweza kutofautisha kati ya juu, chini, kulia na kushoto.
Wanyama mbalimbali hutumia masikio pia kwa kupoza mwili. Hivyo tembo anatumia masikio yake kama feni.
Matatizo na magonjwa ya sikio
Sehemu zote tatu za sikio zinaweza kuathiriwa na magonjwa na maumivu.
- Sikio la nje huwa na ngozi laini ambayo inaweza kuumizwa na vidonda na kuambukizwa. Njia ya sauti inaumizwa kama watu wanajikuna ndani yake kwa kidole kichafu au kwa kutumia vijiti. Mara nyingi inajazwa hasa na nta ya mwilini inayokusanyika hapa na kuzuia sauti kupita vema. Daktari anaweza kusaidia kwa kuondoa nta au uchafu mwingine uliokusanyika akitumia mpira mdogo na maji ya vuguvugu.
- Sikio la kati linapata matatizo yafuatayo: kiwambo cha sikio kinaweza kuumizwa, kwa mfano kwa kuingiza kitu ndani ya sikio, kutokana na mlio mkubwa mno kama mtu yuko karibu na mlipuko na pia kutokana na magonjwa. Magonjwa inayotokea mara yingi ni mchonyoto wa chumba cha mifupa sikivu kwa sababu bakteria zinaweza kupitia neli ya koromeo na kuingia ndani; wakati wa magonjwa ya shingoni neli hii inaweza kuvimba na kufunga bakteria ndani ya sikio la kati ambako zinasababisha mchonyoto. Mchonyoto katika sehemu hii inaleta maumivu makali. Isipotibiwa ambukizo linaweza kuathiri hata kuharibu mifupa sikivu.
- Sikio la ndani huumia kama makelele yanazidi. Kuzidi kwa makelele au pia kupokea mlio mkubwa wa mlipuko wa karibu unaweza kuharibu neva ndogo zinazobadilisha mwendo wa mishipa fahamu kuwa alama za neva. Sehemu hii inaweza kushambuliwa pia na maambukizi ya virusi mbalimbali.
Pia watumiaji wa earphones ni rahisi kuumia sikio ukitumia sauti kubwa.
MAONI NA USHAURI ULIOTOLEWA NA WADAU KUHUSU TATIZO HILI
----Pole man .... Ingawa sijamuona mwanao thats sounds like typical chronic otitis media a.k.a middle ear infection ipo hivi katika ear canal kabla hujafikia ngoma kuna lil bastards "bacteria" wamefanya inflammation .. nime suspect hii bcz huwa ni common kwa watoto .. nakama hiyo pus inayotoka ni ya njano thn i might be right . nenda kwambie doc. wake .. jaribu ku suggest tu ask him "doc could be otitis media?" do not make conclusion maana ma doc wengine visirani. soma zaidi hapa Otitis Media (Middle
N;B- jitahidi anapokoga ama anapoogeshwa maji yasiingie sikioni..
wakati unatafuta tiba fanya hivi .. msafishe sikio "kwa pamba sio maji epuka maji ndani ya sikio", then weke dawa fulani inaitwa mupirocin ointment cheki picha hapa ni anti bacterial atumie asubuhi na jioni wakati unaiweka unatumia zile pamba za kutoa nta masikioni . kamulia dawa katika ile pamba ya mbele ipake kwa style ambayo inakaa katika kuta za middle ear sababu infection ipo katika kuta zamiddle ear sio ndani kwenye ngoma, baada ya nusu saa muweke ear drops. ofloxin ear drops cheki image hapa
kwa masaada zaidi fanya haraka nenda kwa dactari... suggest to him about otitis media
KUTOKWA NA USAHA SIKIONI: Ikiwa utaweka kitu kama ujiti wa kiberiti au mfano wake sikioni, unaweza kusababisha jeraha kwenye sikio na damu kuanza kutoka. Baadae usaha unaweza kutungwa sehemu ya jeraha na kutoka kidogokidogo. Lakini pia mashambulizi ya bacteria sikioni yanaweza kusababisha kutokwa na usaha.
TIBA ZA MAUMIVU YA MASIKIO NA KUTOKWA NA USAHA:
Kanuni ya kwanza: Chukua maji masafi ujazo wa kijiko kimoja cha chai halafu uchukue chumvi kidogo kiasi cha vidole viwili uchanganye ndani ya maji hayo kisha hayo maji uchanganye na asali kijiko kimoja kidogo cha chai. Weka tone moja ya dawa hii ndani ya sikio
lenye kuuma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu.
Kanuni ya pili: Dondoshea tone moja ya mafuta ya kitunguu saumu ndani ya sikio ambalo linauma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu.. Kanuni ya tatu: Chukua mafuta ya habat soda na ufanye kama kanuni ya pili. Kanuni ya nne: Ikiwa maradhi ya sikio ni kwa ajili ya bacteria, kunywa antibayotiki asilia kama vile juisi ya Aloe vera, kitunguu saumu, n.k. E.
Na pia nenda hospital kitengo cha ENT hapo Muhimbili kawatafute Ma-Daktari mabingwa hawa mmoja wapo Dr Edwin, Dr Kimario au Prof. Mushi Wataweza kukusaidia hayo Matatizo yako Pole sana.@mpalu
----
---Sikio (Ear) limegawika katika sehemu tatu kuu. Sehemu ya nje ya sikio, sehemu ya kati ya sikio na sehemu ya ndani ya sikio.
Kuna aina mbili ya matatizo ya masikio nayo ni:
Otitis media : ambayo hutokea katika sehemu ya kati ya sikio na mara nyingi huwatokea watoto wachanga
na watoto wadogo.
Otitis externa: ambayo hutokea katika sehemu ya ndani ya sikio na mara nyingi huwatokea waogeleaji, na
hutokea zaidi wakati wa baridi.
Ishara za Matatizo ya masikio kwa Otitis media:
Kuumwa na kuchomwa kwa sikio
Kutokwa na uchafu ndani ya sikio
Kutosikia kwa ghafla
Homa
Sababu za Otitis media:
Sababu kubwa ya maradhi hayo ni kuziba kwa bomba la sikio(Eustachiantube)
kutokana na baridi, allergy pamoja na kuingia takataka. Hii inababisha maji maji ya sikio kujaa maji hayo
nayo husababisha uvimbaji wa (ear drum) sikio.
Sababu za Otitis externa:
Hii husababishwa na baketeria au fungi, maji maji yanayoingia ndani ya sikio ndio sababu kuu ya kufanya
bakteria na fungi kuzaana pia Skin allegies husababisha maradhi hayo.
Na sababu nyengine ni ulaji mbovu wa chakula pamoja na upungufu wa usafi wa mwili.
DAWA ZA KUJITIBU MARADHI YA MASIKIO:
Nyunyiza juisi ya Kitunguu saumu katika sikio linalouma
Nenda Hospitali ukapigwe bomba ili maji na uchafu upate kutoka
Pasha moto mafuta ya Zaituni (Olive oil) na yasubiri yapowe
na ujitie drops mbili hadi 3
Na usafishe masikio yako kila baada ya kutoka kukoga.
KUTOKWA NA USAHA SIKIONI: Ikiwa utaweka kitu kama ujiti wa kiberiti au mfano wake sikioni, unaweza kusababisha jeraha kwenye sikio na damu kuanza kutoka. Baadae usaha unaweza kutungwa sehemu ya jeraha na kutoka kidogokidogo. Lakini pia mashambulizi ya bacteria sikioni yanaweza kusababisha kutokwa na usaha.
TIBA ZA MAUMIVU YA MASIKIO NA KUTOKWA NA USAHA:Kanuni ya kwanza: Chukua maji masafi ujazo wa kijiko kimoja cha chai halafu uchukue chumvi kidogo kiasi cha vidole viwili uchanganye ndani ya maji hayo kisha hayo maji uchanganye na asali kijiko kimoja kidogo cha chai. Weka tone moja ya dawa hii ndani ya sikio
lenye kuuma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu. Kanuni ya pili: Dondoshea tone moja ya mafuta ya kitunguu saumu ndani ya sikio ambalo linauma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu.. Kanuni ya tatu: Chukua mafuta ya habat soda na ufanye kama kanuni ya pili.
Kanuni ya nne: Ikiwa maradhi ya sikio ni kwa ajili ya bacteria, kunywa antibayotiki asilia kama vile juisi ya Aloe vera, kitunguu saumu, n.k. E.

TIBA MBADALA YA MAGONJWA YA MASIKIO
Sikio (Ear) limegawika katika sehemu tatu kuu. Sehemu ya nje ya sikio, sehemu ya kati ya sikio na sehemu ya ndani ya sikio.
Kuna aina mbili ya matatizo ya masikio nayo ni:
i.Otitis media : ambayo hutokea katika sehemu ya kati ya sikio na mara nyingi huwatokea watoto wachanga na watoto wadogo.
i.Otitis externa: ambayo hutokea katika sehemu ya ndani ya sikio na mara nyingi huwatokea waogeleaji, na hutokea zaidi wakati wa baridi.
Ishara za Matatizo ya masikio kwa Otitis media
i.Kuumwa na kuchomwa kwa sikio
ii.Kutokwa na uchafu ndani ya sikio
iii.Kutosikia kwa ghafla
iv. Homa
Sababu za Otitis media:
· Sababu kubwa ya maradhi hayo ni kuziba kwa bomba la sikio(Eustachiantube), kutokana na baridi, allergy pamoja na kuingia takataka. Hii inababisha maji maji ya sikio kujaa maji hayo nayo husababisha uvimbaji wa (ear drum) sikio.
Sababu za Otitis externa
·Hii husababishwa na baketeria au fungi, maji maji yanayoingia ndani ya sikio ndio sababu kuu ya kufanya bakteria na fungi kuzaana pia Skin allegies husababisha maradhi hayo.
Na sababu nyengine ni ulaji mbovu wa chakula pamoja na upungufu wa usafi wa mwili.
DAWA ZA KUJITIBU MARADHI YA MASIKIO:
i. Nyunyiza juisi ya Kitunguu saumu katika sikio linalouma
ii.Nenda Hospitali ukapigwe bomba ili maji na uchafu upate kutoka
iii.Pasha moto mafuta ya Zaituni (Olive oil) na yasubiri yapowe na ujitie drops mbili hadi 3
iv.Na usafishe masikio yako kila baada ya kutoka kukoga.
KUTOKWA NA USAHA SIKIONI:
Ikiwa utaweka kitu kama ujiti wa kiberiti au mfano wake sikioni, unaweza kusababisha jeraha kwenye sikio na damu kuanza kutoka. Baadae usaha unaweza kutungwa sehemu ya jeraha na kutoka kidogokidogo. Lakini pia mashambulizi ya bacteria sikioni yanaweza kusababisha kutokwa na usaha.
TIBA ZA MAUMIVU YA MASIKIO NA KUTOKWA NA USAHA:
Chukua maji masafi ujazo wa kijiko kimoja cha chai halafu uchukue chumvi kidogo kiasi cha vidole viwili uchanganye ndani ya maji hayo kisha hayo maji uchanganye na asali kijiko kimoja kidogo cha chai. Weka tone moja ya dawa hii ndani ya sikio lenye kuuma au kutokwa na usaha kutwa mara tatu