Tatizo la Kukojoa Kitandani kwa Watoto - Ushauri, Tiba na Namna ya Kukabiliana Nalo

Ua kanyoka kadogo afu mlaze pembeni yake asubuhi akiamka akimkuta ndo bye bye kukojoa.
 
Nilimuona mtoto wa kaka yangu alikojoa kitandani mpaka tukamzoea, anasoma primary school lakini bado anatandikiwa mipira!! ss nae yupo darasa la nne ndio ameacha mwenyewe!

Kabla ya yeye kuacha, tulimpeleka hospitali sana, mpaka tuliambiwa tumlaze na chura.
 
Kwanza ni kwa nini mlimpeleka boarding school huku mkijua matatizo yake? Nyie wenyewe hamtendei haki mtoto, anatakiwa kupata mapenzi yenu nyie kama wazazi kwa kuwa hakuna mtu yeyote atakaekulelea mwanao kama mzazi mwenyewe, (samahanini kwa kutoka nje ya topic)

Back to topic: Kaa naye mwenyewe jizoeshe kumuhamsha usiku kwenda kujisaidia hata mara 2 kwa usiku, atazoea kuhamka kwenda kujisaidia na hapo ndipo tatizo litakwisha.
 
Mkuu hilo sio tatizo na wala msikae na kufikiria vibaya na kuanza kuangaika huku na huku no just mpeni time na wala msimpige au kumlaumu ni hali ya kawaida kama mtoto wa sister alikuwa anakojoa mpaka alivyofika na miaka 15 then ikafikia akaacha tu. Huo sio ugonjwa zaidi ungekaa nae then ungekuwa unafanya kazi ya ziada kumuamsha kila siku usiku ungeona tu kaacha ghafla. So jaribu kufanya hivi mkuuu wala usihofie kama ni ugonjwa huo.
 
Mkuu hilo sio tatizo na wala msikae na kufikiria vibaya na kuanza kuangaika huku na huku no just mpeni time na wala msimpige au kumlaumu ni hali ya kawaida kama mtoto wa sister alikuwa anakojoa mpaka alivyofika na miaka 15 then ikafikia akaacha tu...huo sio ugonjwa zaidi ungekaa nae then ungekuwa unafanya kazi ya ziada kumuamsha kila siku usiku ungeona tu kaacha ghafla. So jaribu kufanya hivi mkuuu wala usihofie kama ni ugonjwa huo.

Nashukuru kwa kunifumbua swla hilo, kwani huyo mtoto anasoma boarding darasa la tano, sasa nilivyomuona anaathirika kisaikolojia, inga waalimu wamesema wapo watoto wengine wa form one na two bado wanendelea na tatizo hilo.
Asante
 
Dawa ya Kumtibu Mtoto kukojowa Kitandani Vifaa vyake upate hivi:

Upate Kwato La N'gombe tiya ndani yake Kaa La Moto kisha yule mgonjwa wa kukojowa Kitandani alinuse lile kwato la N'gombe lilio na Kaa la Moto ndani yake, kisha Avue nguo zake awe uchi Apande juu ya mti kisha juu ya huo mti akojoe mkojo ushuke chini afanye hiyo Dawa kwa Muda wa siku 7 atapona kabisa.

Hakuna dawa Mahospitalini kutibu mtoto kukojowa kitandani
 
Wadau nina mtoto sasa anatimiza miaka kumi lakini anamwaga mkojo kitandani hadi nachanganyikiwa ,tafadhali mwenye njia mbadala ya kutatua tatizo hili NAOMBA ANIPATIE USHAURI ili kusaidia tatizo hili kwisha.

Asanteni.
 
Muone daktari wa watoto atakusaidia. Alternatively, waite marafiki zake anaosoma nao au walio jirani hapo kwenu ile asubuhi mfano jumamosi kisha mtoe mbele yao akiwa amelowa mkojo halafu wasisitize wamcheke sana na kumzomea, nilishawahi kuona mtoto aliyefanyiwa hivi, akalia sana na kuona aibu na baadae akaacha kukojoa mara moja.
 
Jaribu kuhakikisha anakojoa kabla ya kwenda kulala na kumuamsha saa fulani akojoe.
 
Muone daktari wa watoto atakusaidia. Alternatively, waite marafiki zake anaosoma nao au walio jirani hapo kwenu ile asubuhi mfano jumamosi kisha mtoe mbele yao akiwa amelowa mkojo halafu wasisitize wamcheke sana na kumzomea, nilishawahi kuona mtoto aliyefanyiwa hivi, akalia sana na kuona aibu na baadae akaacha kukojoa mara moja.

Nadhani jambo la kumuona daktari specialist wa watoto ni la msingi. Ila kumfanya azomewe na wenzie ni kumdhalilisha na kukiuka haki za mtoto. Nalaani tabia kama hizi.
 
Umejaribu kuangalia historia ya kwako na ya mkeo, pengine mlikuwa na tabia hizo.
 
Muone daktari wa watoto atakusaidia. Alternatively, waite marafiki zake anaosoma nao au walio jirani hapo kwenu ile asubuhi mfano jumamosi kisha mtoe mbele yao akiwa amelowa mkojo halafu wasisitize wamcheke sana na kumzomea, nilishawahi kuona mtoto aliyefanyiwa hivi, akalia sana na kuona aibu na baadae akaacha kukojoa mara moja.
Huu ni ukatili wa hali ya juu. Kama unampenda mwanao usimdhalilishe kiasi hiki. Never!!

Kuna namna za kumsaidia. Wengine haya huwa ni matatizo ya kisaikolojia. Mtazame na ongea nae, na ujiulize anakojoa kila siku au siku kukiwa na tukio fulani.

Ukimaliza hapo, jitahidi anza kumwamsha usiku kukojoa na aparticipate kwenye kufanya usafi wa nguo zake. Pia unaweza kumuhimiza kunywa maji mengi mchana na ikianza kufikia jioni apunguze.

Pia vinywaji vyenye caffein kama coca au kahawa usiku apunguze.
 
Nadhani hii inaweza saidia. hakikisha hanywi maji kuanzia mida ya saa 11 jioni. kisha wakati anaenda kulala hakikisha anakojoa kabisa. pia jaribu kumjenga kisaikolojia kuhusu kutokukojoa kitandani. Siamini katika kumletea marafiki zake manake inamdhalilisha na hiuenda ikam-haunt maishani mwake. Dhana hii inasumbua saikolojia yake na kumfanya usiku ashikwapo na mkojo aamke lkn ni sawa pia na wewe kumjenga kisaikolojia ili bado aweze kuamka na kwenda kujisaidia. kwa kuanzia unaweza kuwa unamwamsha mida ya saa 9 huko. mara nyingi kukojoa kitandani huja mida hiyo kuelekea asubuhi.
 
Jamani this is a psychological disorder, the more u try to embarass the child au ukizidi kumgombeza ndo hatoacha. Jaribu kumzawadia zile cku ambazo hatakojoa na cku akikojo mpe moyo kuwa ipo cku ataacha.hii inampa confidence na determination ya kuacha hiyo tabia.
 
Muone daktari wa watoto atakusaidia. Alternatively, waite marafiki zake anaosoma nao au walio jirani hapo kwenu ile asubuhi mfano jumamosi kisha mtoe mbele yao akiwa amelowa mkojo halafu wasisitize wamcheke sana na kumzomea, nilishawahi kuona mtoto aliyefanyiwa hivi, akalia sana na kuona aibu na baadae akaacha kukojoa mara moja.

Sio kila mtoto anayejikojolea kitandani ni kosa lake, na hivyo kumuadabisha kwa kumdhalilisha mbele ya wenzake. Ni uongo uliokithiri kusema kuwa mtoto anayejikojolea kitandani akihadhibiwa kwa bakora au kudhalilishwa kwa kuchekwa na marafiki basi anakoma mara moja kujikojolea. Kuna watoto wenye ulemavu, na wengine kwa matatizo ya kisaikolojia wanakuwa na adha hiyo ya kujikojolea.

UTI pia ni moja ya sababu ya watoto kujikojolea mara kwa mara kutokna na muwasho wa kibofu.

Mpeleke mtoto kwa daktari apate msaada.
 
Kuna mimea inaota maeneo ya mkoa wa kagera, akikojoa usiku unampaka, zinawasha, hapo hatarudia tena make akipatwa na mkojo kisoikologia anakumbuka kuwashwa na hivo anaamka mwenyewe. mmea huo unaitwa'engenyi'
 
kuna mimea inaota maeneo ya mkoa wa kagera, akikojoa usiku unampaka, zinawasha, hapo hatarudia tena make akipatwa na mkojo kisoikologia anakumbuka kuwashwa na hivo anaamka mwenyewe. mmea huo unaitwa'engenyi'

(VAC) Violence Against Children. Hivi karibuni kutakuwa na uzindizi wa ripoti ya VAC Tanzania na statistics zinatisha. Nadhani mfanye juhudi kuisoma itakapozinduliwa na mzingatie mapendekezo yake.
 
Back
Top Bottom