Tatizo la Mihimili mitatu (3) Tanzania hili hapa

Indume

Member
Apr 11, 2011
81
36
Uwajibikaji wa Mihimili Tanzania kwa ile falsafa ya eti kuna mihimili 3 inayojitegemea imekumbwa na dosari ambayo inasababisha kutokuwepo na uwajibaji mzuri kwa kila mhimili.
Kwanza ; Rais na Makamu wa Rais kama mhimili wa kwanza wanachaguliwa na wananchi ambao tunategemea kuwa wao na serikali yote inawajibika kwa umma uliowaweka madarakani.

Pili; Spika wa Bunge na Naibu Spika wa bunge wanachaguliwa na wabunge na kuwajibika ipasavyo ndani ya bunge kwa kufuata kanuni za bunge zilizowekwa.

Tatu; Jaji Mkuu..............hapa ndo kituko kinapoanzia. Anateuliwa na Rais. Anawajibika kwa nani??

Dhana ya kusema kuwa Mahakama ni mhimili unaojitegemea ni Uongo/siyo kweli. Tulitegemea kuwa Jaji mkuu achaguliwe na Majaji au mahakimu wote nchini ili kuwa na nguvu na kuwajibika ipasavyo kwa kufuata misingi ya sheria.

Tatizo la mihimili hii ni kwa sababu mhimili mmoja (Mahakama) huchaguliwa au mhimili huu unawekwa na Rais. Kwa hali hii mahakama inawajibika kwa Rais. Na kwa nini hakuna Naibu Jaji Mkuu au Makamu Jaji mkuu kama ilivyo mihimili mingine?? Hapo ndo kuna matatizo ya kiutendaji.
 
Back
Top Bottom