Tatizo la Maji Ubungo na Jitihada za Mbunge Mnyika

Asante kwa taarifa. Hata sisi wakazi wa ubungo kibangu opp na Amec Dispensary hatujawahi kupata maji tangu mwaka jana. Mimi napendekeza hivi ifanyike uhakiki wa wateja wapi wanaopata maji na wale wasiopata japo wameunganishiwa bomba(ya wachina). Na baada ya hapo hao Dawasco watupe mikakati ya dharura na kudumu ili kutatua tatizo hilo
 
Mnyika wewe ndo mbunge bora tz nzima...hakuna wa kukukaribia...na ndo maana ukaongoza bunge lililopita kwa kutoa michango mingi na hoja za maendeleo...hata kama watu wa ubungo wakikutema njoo ugombee nyumbani kanda ya ziwa sie utashinda kwa kishindo...twatamani tuwe na mbunge kama wewe
 
Jamani hivi viporo vya mwezi wa 8 mnaviamsha leo.Muwe mnangalia jamani
 
HOJA binafsi iliyowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyik (CHADEMA), kutaka hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na uondoaji wa maji taka jijini Dar es Salaam, itatolewa uamuzi katika kikao kijacho cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya jiji hilo.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na katibu wa mbunge huyo, Aziz Himbuka, ilieleza kuwa Mnyika aliwasilisha hoja hiyo kwa Mkurugenzi wa Jiji, Mussa Natty.
Himbuka alisema kuwa katika hoja hiyo, Mnyika alieleza kwamba kati ya mwaka 2003 mpaka 2010 serikali ilitekeleza mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya majisafi na majitaka jijini Dar es Salaam na maeneo ya Bagamoyo na Kibaha.
Alisema kuwa mradi huo ulitumia dola za Kimarekani milioni 164.6, lakini hata hivyo hadi sasa katika maeneo mengi mabomba yake hayatoi maji.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Wizara ya Maji iliandaa waraka maalumu wa kuiomba serikali kutenga kiasi cha sh bilioni 653.85 katika mpango maalumu wa 2011-2013 wa kuboresha huduma za majisafi na uondoaji wa majitaka uliopitishwa na Baraza la Mawaziri.
 
Mhe Mnyika kuhusu maji mtaa wa Kilimani, Kata ya Manzese bado siielewi serikali na wewe pia. Kinachohitajika ni kuunganisha pale Kindo system yenye maji na system mpya ya Kilimani (ambapo source pipe ya maji ilikatwa kabula ya ujenzi wa daraja la Kindo). Baada ya kukata bomba halikuunganishwa kwa watu wa Kilimani kwa maelezo kuwa maji hayatoshi. Huu ni ubaguzi kwani kama hayatoshi ni kwa wote, tusiwe na double standards. Ni miaka isiyopungua mitano tangu mradi uishe bila kutumika ikiwa ni kinyume cha lengo la mradi. Baadaye utakuja kumpata wapi mkandarasi kwa ajili ya making good deffects zitakazo jitokeza pale maji yatakapounganishwa maana ni mabomba mapya yanayoendelea kuoza ardhini bila kutumika. Mnyika tuokoa wakazi wa Kilimani. Imebaki kuendeleza mradi wa kutuuzia maji kwa ndoo ya bei ghali na mara nyingi yanayopatikana ni ya chumvi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom