Tatizo la Maji Ubungo na Jitihada za Mbunge Mnyika

Communist

JF-Expert Member
Jun 1, 2012
5,400
1,181
DAWASCO NA DAWASA WASHUGHULIKIE MATATIZO YA MAJI MBEZI
Posted: 28 Aug 2012 12:14 AM PDT


Nimefuatilia Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) na kujulishwa kuwa hatua zimeanza kuchukuliwa kuhusu matatizo ya maji yanayoendelea katika maeneo mengi ya kata za Mbezi Luis na Msigani kwa takribani wiki tatu kufuatia ratiba ya mgawo wa maji kuathiriwa na kuhamishwa kwa huduma ya maji kutoka katika bomba la maji la inch 24 mpaka la inch 30. Hali hiyo imeathiri zaidi maeneo ya Magari Saba, Kibanda cha Mkaa, Kwa Msuguri, Temboni na maeneo mengineyo.



Aidha, kuhusu maghati ya umma na maeneo ya pembezoni ambayo yalikuwa na matatizo makubwa ya maji kabla hata ya kipindi husika ikiwemo maeneo ya Bwaloni na Msingwa, nimeiandikia barua Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) kuwaalika kufanya nao ziara ya kikazi mapema iwezekanavyo katika maeneo husika kwa ajili ya kutoa maelezo ya kiutendaji kuhusu hali iliyopo na kueleza mipango inayopaswa kutekelezwa ya kupata ufumbuzi wa haraka.


Natoa taarifa hii kwa kuzingatia kuwa tarehe 25 Agosti 2012 nilipokutana na wananchi katika eneo la Mbezi kwa Msuguri wakati nikiwa katika kazi ya kuhamasisha wananchi kushiriki katika sensa, kujiandaa kutoa maoni ya katiba mpya na kupata mapendekezo yao kuhusu masuala ya kuyapa kipaumbele baada ya kurejea kutoka katika mkutano wa nane wa Bunge nilielezwa kuhusu matatizo ya maji katika maeneo tajwa.


Kufuatia maswali yaliyoulizwa na masuala yaliyoelezwa nilitoa majibu ya ujumla kwamba: Mosi, kuhusu matatizo yaliyojitokeza nilieleza kuwa chanzo chake ni marekebisho yaliyokuwa yakiendelea ya kuondoa baadhi ya watu waliokuwa wamejiunganisha maji kinyemela katika mabomba makuu pia kuhamisha huduma kwa wananchi wa maeneo tajwa kutoka bomba la inch 24 mpaka la inch 30, hata hivyo kwa kuwa matatizo hayo yameendelea niliahidi kuwasiliana na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) na kutoa majibu ya hatua za kuharakisha huduma ya maji kurejea katika hali ya kawaida.


Pili, kuhusu maeneo ambayo yalikuwa hayatoki maji hata kabla ya wiki tatu ikiwemo baadhi ya maghati ya umma na maeneo ya pembezoni nilieleza chanzo cha hali hiyo kwa kadiri ya majibu niliyoelezwa na DAWASCO nilipofanya nao ziara katika kata ya Msigani tarehe 1 Machi 2012 na kwa kuwa matatizo katika maeneo hayo yanahitaji hatua kubwa zaidi niliahidi kwamba nitawaalika Watendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) ili kufanya nao ziara ya kikazi karibuni kuweza kutafuta ufumbuzi.


Izingatiwe kwamba kazi ya mbunge ni kuwakilisha wananchi na kuisimamia serikali na vyombo vyake kuwezesha maendeleo, na katika muktadha huo Machi Mosi 2012 niliungana pamoja na DAWASCO kwenye kata za Sinza, Makurumla, Mburahati, Msigani, Mabibo, Saranga, Kwembe na Makuburi kufuatilia kazi za kuboresha upatikanaji wa maji katika Jimbo la Ubungo.


Kupitia ushirikiano huo tuliona bayana kwamba mtandao wa biashara haramu ya maji unaohusisha kujiunganisha mabomba ya maji kinyemela nao unachangia katika matatizo ya maji katika baadhi ya maeneo, mathalani tuliona mota za biashara hizo katika maeneo ya kata ya Makurumla hususani mtaa wa Kagera, Makuburi kwenye nyumba yenye matanki yaliyounganishwa chini chini kwa ajili ya biashara ya maji na Kata ya Saranga eneo la Kimara B ambapo mtandao wa maji ulitolewa toka kwenye maeneo ya wananchi na kupelekwa nje ya makazi ya watu kwenye mtandao wa wafanyabiashara wakubwa wa maji. Mitandao hiyo ilianza kukatwa na majalada yalifunguliwa polisi kwa ajili ya wahusika kuchukuliwa hatua za kijinai.


Hali hiyo ilishamiri kutokana pia na vishoka na tulikubaliana kwamba kuanzia wakati huo yoyote anayekwenda kugusa bomba la DAWASA lazima kwamba aripoti kwenye serikali za mitaa na pia popote anapofanya kazi hizo lazima awe na kitambulisho cha DAWASCO na pia kadi ya kazi (job card) yenye saini ya meneja wa eneo ya kueleza aina ya kazi na ruhusa iliyotolewa kuifanya. Nachukua fursa hii kuwakumbusha wananchi kuchukua hatua dhidi ya yoyote anayekwenda kinyume na makubaliano hayo kama ilivyo kwa wahalifu wengine wanaokiuka sheria.


Katika kazi tulizofanya Machi Mosi 2012, ilionekana bayana kwamba bado yapo maeneo ambayo mtandao wa mabomba ya wachina hautoi maji kutokana na msukumo mdogo na matatizo ya mfumo mzima, kama ilivyo katika majimbo yote ya Dar es salaam, Kwa upande wa Jimbo la Ubungo hali hii imeathiri maeneo ya Malambamawili, kwa Msuguri, Makoka na mengine. Aidha, yapo maeneo ambayo hayakufikiwa kabisa kwenye awamu ya kwanza ya utandazaji wa mabomba husika mathalani ya Msingwa, Mbezi Msumi na mengineyo katika jiji la Dar es salaam.


Haya ni masuala yanayohusu mwenye mali na miundombinu ambaye ni Serikali kupitia Wizara ya Maji na DAWASA, zaidi ya DAWASCO ambayo pamoja na kuwa nalo ni shirika la umma ni mwendeshaji tu. (Maji DSM ni kama duka, kuna mwenye bidhaa ambaye anawajibika kujaza duka lake ili wateja wasikose-DAWASA na muuza duka ambaye ana kazi ya kuuza duka lenye bidhaa chache-DAWASCO malalamiko mengi ya wateja yanamuangikia yeye).


Kufuatia hali hiyo niliwasilisha kwa Katibu wa Bunge hoja Binafsi kwenye mkutano wa nane wa Bunge uliomalizika kutaka bunge lipitishe maazimio ya hatua za haraka zaidi za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jimbo la Ubungo na Jiji la Dar es salaam; hata hivyo hoja hiyo haikupangiwa kujadiliwa bungeni kutokana na ufinyu wa muda baada ya ratiba ya bunge kufanyiwa marekebisho na kipengele cha hoja za wabunge kuondolewa. Kutokana na hali hiyo, wakati nikisubiri mkutano tisa wa bunge unaofuata niendelee na kazi zingine ikiwemo kuwaandikia DAWASA ili wafike jimboni Ubungo na kuchukua hatua kwa masuala ya maendeleo yaliyo ndani ya uwezo wao.


Wenu katika uwakilishi wa umma,


John Mnyika (Mb)
27 Agosti 2012

 
Asante sana Mnyika kwa juhudi zako katika kutatua matatizo yanayo likabili jimbo la ubungo.

Mungu akuongoze uendelee kutatua matatizo mengine nazaidi hasa ya maji.

Big up
 
nasubiri kwa hamu kuona maji safi yakitoka kwenye mabomba ya wachina. Vipi kuhusu sehemu za jimbo la ubungo hasa kata ya Kimara ambazo zilienguliwa kutoka kwenye mradi wa wachina na hivyo kutofikiwa na mabomba? kuna mpango gani juu ya maeneo hayo?
 
wewe piga sound miaka 5 inakwisha, usisahau kujenga hata kakibanda mdogo wangu jimbo limekushinda, kwa sound tu unajitahidi, lakini wanainchi wengi wameishaanza kukuchoka kwa sound.
 
Mnyika kama ni wewe naomba badilisha jina la Communist kwani hiyo system ndiyo iliyoleta umasikini duniani wa ajabu.
 
Mnyika kama ni wewe naomba badilisha jina la Communist kwani hiyo system ndiyo iliyoleta umasikini duniani wa ajabu.
Communist ni mimi na Mnyika ni mbunge wangu. Usichanganye majina. Mimi ni communist wa mrango wa kati, nakubaliana na Gobachove. Bepari wa mrango wa kati = Comunist wa mrango wa kati. Ndio maana naipenda CDM. Consevertive communist ndio wabaya walioleta umaskini (Soma animal farm)
 
Mh kazi nzuri lakini bado hatuna maelezo mazuri ni kwa nini katika mtaa wa Kilimani, Kata ya Manzese, mabomba mapya hayana maji karibu miaka mitano tangu yawekwe. Inawezekana hata ile retention for making good deffects imerudishwa na hivyo pamoja na mengi unayofanaya saidia nasi tupate maji kama wengine. Tunatumia maji ya kununua akatika ndoo ambayo ni ghali sana (yapata Shs 500/= kila ndoo na ni ya chumvi.
 
Chapa kazi MH.MNYIKA
Usifumbie macho udhaifu wao wa KIUTENDAJI hao DaWASA NA DaWASCO.
Hongera kwa kufuatilia Wananchi wako, hakika USIACHE daima kuwatembelea maana Utajua mengi huko Uraiani kwa kuongea nao katika Mikutano ya Hadhara.
DAIMA SONGA MBELE....KAMANDA...WA UKWELI.
 
I think wananchi wa Ubungo wanapaswa kumuunga mkono mbunge waokwani swala la maji ni nyeti na lina mlolongo mrefu wa ufisadi kuanzia serikali kuu, Dawasa, Dawasco na kibaya zaidi ni kwa wananchi wenyewe ambao wengi wamekuwa wakijiunganishia maji na kutumia pamp ambazo hupeleka kiasi kiukubwa cha maji kwao huku wengine wakikosa!!
Wabunge wengine tunaomba pia waeke wazi mipango na jitihada zao kwa wananchi, either kwa mikutano or through Media... Big up Mnyika!!
 
hongera mh. mnyika kwA jitihada unazofanya . kaza buti..... maneno yawe machache....vitendo vingi.. .... tupate matokeo....MAJI
 
Mnyika muamshe usingizini (msaidie) Mdee. Nyanda za juu za Kawe kuna matatizo kama haya haya, lakini kimyaaa!
 
Mh. Mnyika nakupongeza sana kwa juhudi zako. Big up mate.
Lakini ubungo kibo/rombo sasa ni miezi miwili hatuna maji. Last time nivikuandikia kesho yake maji yakatoka na tangu hapo mpaka leo hakuna kitu.
 
ni kweli jama anajitahidi kufwatilia hili swala lakini sio kwamaba amelitatua ili tatizo! kwani ni bado kabisa mana maji yamezidi kuwa ya taabu mno maeneo hayo husika aliyoyataja, hata kama wewe humu jf ni mkazi wa maeneo hayo tuo yako yalio ya kweli kutoka moyoni je? nikweli hii kero imetatuliwa?, ki ukweli maji bado ni shuu wakuu, tunalipa bili sana tu, na sasa wameanza mtindo hawatoi maji kabisaaa alafu ikifika karibia na mwisho wa mwezi wanatoa maji kama marambili ili mita zisome tu watu walipe! ukweli kamanda wetu mnyika bado hili swala hajalitatua wakuu.
 
Mh. Mnyika nakupongeza sana kwa juhudi zako. Big up mate.
Lakini ubungo kibo/rombo sasa ni miezi miwili hatuna maji. Last time nivikuandikia kesho yake maji yakatoka na tangu hapo mpaka leo hakuna kitu.
Uzuri mmoja mbunge wetu, kwa sasa, yuko katika ziara ya Jimbo lake. Imeingiliwa kidogo na vibali kwa kisingizio cha sensa. Naamini atafika maeneo yote. Tunasubiri muendelezo wa ratiba yake baada ya kikao cha Kamati kuu. Nafikiri mnaelewa hizi vurugu zinazofanywa bila sababu na wapinga maendeleo. Kamati kuu inashughulikia masuala yote ya mikutano, hii imegusa ziara ya Mbunge wetu.

Mbunge wetu yuko pamoja nasi.
 
Back
Top Bottom