Iceberg9
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 24,565
- 47,012
Mshana jr, vipi unatoa tiba mkuu, kuna dogo langu yani huwa nampiga mingumi ila hasikii, huyu ni mgonjwa type gani chronic ama?View attachment 387667
Hiki kitu kina waathirika wengi sana wake kwa waume wakubwa kwa wadogo. Tunaweza kudhani tu kuwa ni tabia mbaya au mazoea! La hasha kutafuna kucha za vidole vya mikononi ni tatizo la kisaikolojia linalomla mtu ndani kwa ndani kwenye ufahamu wake ambapo hupelekea viashiria hivi:-
-woga
-mawazo/msongo wa mawazo
-kutojiamini
-fadhaa/sononi
-kukosa la kufanya
-taharuki
-mapepe/restless mind
-hulka ya kuiga
Hivyo ni viashiria vikuu vya mtafuna kucha na hili jambo hufanya bila kupenda ni involuntary action. Kuna baadhi hufanya wakiwa pekeyao kwenye upweke na wengine hufanya pindi anapokutana na mtu kwa mara ya kwanza ama hadhira.
View attachment 387681
Kwakuwa hili ni tatizo la kisaikolojia zaidi basi hata tiba yake ni ya kisaikolojia, hasa hasa
-councelling/ushauri nasaha
-kumjengea uwezo wa kujiamini mwathirika
-kutafiti kupitia yeye mwenyewe chanzo cha tatizo lake hilo na muda
Wengine hukutana na hii hali katika hatua fulani ya makuzi na ikipita tatizo hujitibu lenyewe!
Je una tatizo kama hili ama ndugu yako? Ama rafiki? Usikimbilie kwa mganga wa kienyeji utaambiwa una jini njaa..! Tiba unayo mwenye