Tatizo la Kukosa Usingizi (Insomnia) na tiba yake

mwambie muda ule usingizi utakapomwishia, ashuke kitandani achukuwe maji (siyo ya baridi), kikombe 1 (ml 250) anywe kisha achukuwe kipande cha chumvi aweke juu ya ulimi halafu taratibu kama anamung'unya pipi hivi arudi kitandani alale, ajaribu kama siku 3 hivi, atalala fofofo!!!. muulize pia kuhusu chakula au vinywaji anavyokunywa mara nyingi ni vipi na ulete hapa tuone kama inaweza kuwa sababu.
 
amesema anakula vyakula vya kawaida ila aliacha pombe miaka mitano iliyopita anakunywa soda tuu
 
amesema anakula vyakula vya kawaida ila aliacha pombe miaka mitano iliyopita anakunywa soda tuu

vizuri, mwambie aache kwanza soda ya aina yeyote au juisi yeyote ya kiwandani, ataacha pia kinywaji chochote chenye kafeina(chai ya rangi, kahawa na vinywaji vingi vya viwandani), atavirudia vinywaji hivi baadaye atakapokuwa supa tena kama atavihitaji.

mwambie maji ni uhai na kuwa anapaswa kuyanywa kabla ya kusikia kiu walau glasi 1 ya maji mara 8 kwa siku bali asianze na zote 8 kwa siku ya kwanza, aanze na glasi 1 (ml 250) siku ya kwanza na aongeze moja moja kila siku mpaka atakapofikia zote 8 na aendelee kunywa hivyo.

Moja ya kazi mhimu za maji mwilini ni kutupatia usingizi mororo na usio na ndoto za kutisha (nightmares), kukosa usingizi na kuota ndoto za kutisha usingizini ni ishara mojawapo za mwili kupungukiwa maji!, maelezo zaidi ya namna ya kunywa maji utayasoma ukifunguw: http://www.maajabuyamaji2.artisteer.net/jitibu-kwa-kutumia-maji.

kumbuka kurudi kutupa feedback
 
Mwambie asiwaze sana pesa kwa ujumla mawazo mengi yanaathiri usingizi.
 
hapana...miaka 4 lazima angekuwa amekufa maana hypothalumus ingekuwa imeshavurugika sana.....sio lisaa limoja strictly hii nakataa kabisa....aachane na sigara, vinywaji vyote toka kiwandani isipokuwa maji...apumzike ...na hii inatakiwa aifanye kwa taratibu aache kimoja baada ya kingine itamsaidia.....narudia kwa miaka minne mfululizo analala lisaa limoja haiwezekani...
 
Hata mimi kuna wakati nilikosa kabisa usingizi ila umerudi sasa, namshukuru Mungu. Mwambie ajaribu kulala kila siku at the same time na anywe kikombe cha maziwa ya vugu vugu saa 2 au saa 3. Kama ataweza atafute chai yenye "camomille" ndani, inasaidia pia.
Ila miaka 3 naona ni nyingi mno, maybe anatakiwa kuonana na daktari atakae kua kidogo more serious, ampe ma lexotan na valium kwa muda.




wewe ulikuwa na tatizo la kisaikolojia tunaita insomnia

huo ushauri unaompa wa valium na lexotan sio mzuri......kwa kuwa huyu anatatioz kubwa huyu si wa kumpa vidonge hata kidogo....
 
hapana...miaka 4 lazima angekuwa amekufa maana hypothalumus ingekuwa imeshavurugika sana.....sio lisaa limoja strictly hii nakataa kabisa....aachane na sigara, vinywaji vyote toka kiwandani isipokuwa maji...apumzike ...na hii inatakiwa aifanye kwa taratibu aache kimoja baada ya kingine itamsaidia.....narudia kwa miaka minne mfululizo analala lisaa limoja haiwezekani...
mkuu hata mi inaniwia vigumu kuamini kwa miaka 4 mtu alale lisaa 1 tu ndani ya masaa 24!, duh!! hii kali, wakuu usikubali kuuguwa chochote kwa muda mrefu, tatizo likidumu mwezi mmoja tu uliza yeyote unayemuona!!
 
mkuu hata mi inaniwia vigumu kuamini kwa miaka 4 mtu alale lisaa 1 tu ndani ya masaa 24!, duh!! hii kali, wakuu usikubali kuuguwa chochote kwa muda mrefu, tatizo likidumu mwezi mmoja tu uliza yeyote unayemuona!!


miaka hiyo nasoma mzumbe(5 na 6) kulikuwa na jamaa tunasoma nae ..yeye alikuwa anakesha anapiga msuli kila siku kulala kwake ni ule mda wa mchana baada ya chakula cha mchana hadi saa kumi namoja hivi....hata michezoni alikuwa haendi jamaa....kweli jamaa alikuwa kichwa ..tukasoma na kumaliza kidato cha sita ..tukarejea nyumbani...wote tulitokea mwanza na tulienda kwa treni...ile kufika nyumbani kwao akapokelewa kafuraha sana maana tangu ajiunge na advance alikuwa hajawahi kurudi home(hata mimi) so kwao wakafurahi kuona mwanao amerudi..wakampokea..akaoga ...akalala..kisha akawambia akapumzike kidogo ..akaenda kulala....hiyo ndyo ikawa mwisho wa safari yake duniani..hakuamka tena alipitilza kimoja....

mwili ukafanyiwa uchunguzi bugando na kugundulika kuwa hypothumus ilikuwa imeshaharibika( hiki ni kiungo kidogo ssana lakini muhimu sana na ndio cotrol center ya ubongo na kila kitu)......

so miaka minne mtu analal strictly lisaa limoja ...big NO
 
nimezoea kuona watu waliorogwa ndo inawatokea......muulize hakuwahi kuwa mchawi au hahisi karogwa?
 
miaka 4 ni mingi angeruka kichaa. hata hivyo kwa hali ya kawaida ya kukosa usingizi kuna baadhi ya watu hushauri moja ya njia hizi au zote: 1. kuondoa akilini kitu kinachosumbua kwa ku take action sio kuahirisha - mfano wa kipuuzi ni kama dirisha umesahau kulifunga ni heri amka lifunge ili uendelee na amani ya usingizi. 2. ingia kitandani halafu vuta pumzi za mtu kama vile uko usingizini - yaani vuta pumzi nzito na uachie kwa vituo - rudia rudia hadi utajikuta unaamka baada ya kupata usingizi. kuna kipindi kifupi niliwahi tumia njia hii. 3. Kabla ya kulala unywe maziwa mgando a.k.a maziwa lala. maziwa mgando yanaaminika kuwa digestion yake ni cumbersome na hivyo kukupa ulegevu au uzembe fulani hadi unajikuta umepata usingizi.
 
asanteni sana kwa ushauri na nimemweleza ameshaanza kutumia baadhi ya maelekezo mliyonipatia na anaimprove.
 
Daw ya kutibu Ukosefu Wa Usingizi

Mgonjwa wa ukosefu wa Usingizi Atachukua kijiko cha unga wa Habbat-Sawdaa (Nigella Sativa) achanganye na gilasi ya maziwa moto yaliochanganywa na asali, baada ya kupoa kiasi atakunywa.


 
Wadau siku izi nasumbuliwa sana na nguv ya usingiz mara nyingine huwa inakuwa asubh tu nnapoingia library tu nakushika kitab usingiz unanisumbua HIV NITUMIE NINI KUAMSHA KICHWA KIWE ACTIVE NNAPOHIJAJI?
 
Unalala vizuri usiku?
Unalala masaa ya kutosha?

Inawezekana unaufanyisha mwili wako kazi kupitiliza. Au una mapungufu wa madini...hii ilinipata miaka kadhaa iliyopita. Nilikua nahisi uchovu mpaka basi wee. . . nikiwa darasani nafunga macho kidogo tu napotelea usingizini. Sikutilia sana maanani mpaka siku nipoanguka asubuhi na kuishia kupata kizunguzungu mchana kutwa. Baadae nikaja kugunduliwa sikua na madini ya chuma ya kutosha mwilini which resulted in anemia.

So kama sio kazi zimekuzidia au kushindwa kulala muda wa kutosha go and see a doctor.Better safe than sorry.
 
Kutopata usingizi husababisha wazimu (sio kukesha siku moja kwa wale wenye tabia ya kukosa usingizi siku zote). Kukesha kunaweza kumkondesha mtu na hudhurika ubongo.

YENYE KULETA USINGIZI:

1. Miongoni mwa vinavyosababisha usingizi ni mafuta ya tango, hufaa sana kwa wale wenye usingizi mchache wajipake mafuta hayo.

2. Vilevile mafuta ya busanji yanasaidia kuleta usingizi, pia ukitia miguu katika maji ya Uvuguvugu .

3. Pia kunusa manemane na kunywa maji yaliorowekwa manemane.

4. Kunusa zafarani na tufaha (apple) na pia maji ya zafarani ukayatia kichwani husaidia kuleta usingizi.

5. Kunya maziwa yaliyochemshwa ukatia kidogo sukari huleta usingizi

6. Asali safi ya nyuki kunywa kabla kulala kwa saa huleta usingizi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom