Tatizo la Kukosa Usingizi (Insomnia) na tiba yake

huo ni ugonjwa unaitwa INSOMNIA..subiri wataalamu waje wakujulishe kitaalamu
meanwhile nenda kagoogle usome kuhusu hiyo na sababu zake
Asante sana Sweety. As tunawasubiri wataalam nasoma soma google kidogo.
 
Hamjambo wana JF

Ningependa kupata ushahuri toka kwenu. Kwa almost mwezi mmoja sasa mwenzenu sipati usingizi. Ulianza kupotea mwezi wa tatu kati kati nilipoanza competition fulani kubwa tu. Nilifikiri ni uoga wa competition na nikapuuza. wakati huo nilikua nalala kwa saa 1 ao 2, alafu usingizi unakata, naupata tena asubuhi mapema. :frown:
Baada ya wiki 2 matokeo yakatangazwa na nikadhani nitapata usingizi ila ndio ikawa mbaya zaidi. Sasa silali kabisa, mchana nashindwa ku-concentrate kwa kazi yangu, nakua na hasira. Usiku nikilala ni dakika chachetu alafu najigeuza usiku kucha. Sasa hivi nimefikia hatua mbaya: sitaki kuona mtu, usiku ukija nakua na hasira na nadhani imeanza ku-affect personal relation yangu. :angry:

Kama kuna mtu ana idea yoyote naomba msaada coz kinacho fata hapa ni kuomba leave nika jifungie chumbani hadi usingizi utakapo patikana. Asanteni kwa msaada.

Pole sana, je huna maumivu yoyote kama kuumwa kichwa, mgongo, etc?
 
Baada ya usingizi kupotea kwa wiki nzima nilianza kuumwa kichwa ila nikipumzika (hata bila kulala) kinapona kidogo. Shida kubwa ni Irritability. Nimekua na hasira sana na mood inakatika kabisa, nashindwa hata kukaa na watu kwa usalama.
 
Tafuta demu wa kukupa usingizi. Unagonga ukimaliza unalala. pole sana ndugu
 
Anza kwa kuchange avata yako, itakusaidia kutibu hasira ulizonazo kwa sasa.. mengine wadau wataongezea..
 
tafuta asali mbichi yenye masaga,tafuta na maziwa fresh ambayo hayajachanganywa na maji,kila grass 1 ya maziwa changanya na vijiko 3 vya asali kologa kunywa,asubuhi na jiono kwa muda wa siku 7 nadhani itakusaidia.
 
pole sana, huo ushauri wa kumeza dawa sio mzuri hata kidogo.. unaweza ukawa ndio unazitumia maishani mwako mwote..

ushauri wangu ni kula biringanya kwa wingi, hasa zikiwa kwenye mboga au unaweza kukaanga biringanya pamoja na mayai. ukala kwa wingi husaidia kuleta usingizi..
mawazo pia nakushauri upunguze usiwaze sana..
 
Tafuta demu wa kukupa usingizi. Unagonga ukimaliza unalala. pole sana ndugu
Hi Lutala. Mi mwenyewe mwanamke hapa. ao ulimaanisha nini hasa? niko tayari kwa kujaribu kitu chochote, kama nitapata usingizi. embu nifafanulie plz.
 
pole sana, huo ushauri wa kumeza dawa sio mzuri hata kidogo.. unaweza ukawa ndio unazitumia maishani mwako mwote..

ushauri wangu ni kula biringanya kwa wingi, hasa zikiwa kwenye mboga au unaweza kukaanga biringanya pamoja na mayai. ukala kwa wingi husaidia kuleta usingizi..
mawazo pia nakushauri upunguze usiwaze sana..
Asante Bliss. Sasa sijui nikila biringanya nichanganye na maziwa na asali baadae, si nitakua natengeneza bomu tumboni? ngoja nipime. I am desperate, hivi usiku umeingia tena...
 
tafuta asali mbichi yenye masaga,tafuta na maziwa fresh ambayo hayajachanganywa na maji,kila grass 1 ya maziwa changanya na vijiko 3 vya asali kologa kunywa,asubuhi na jiono kwa muda wa siku 7 nadhani itakusaidia.

KIchomiz, wewe ni mtu wa 3 kunambia kuhusu maziwa, ila wakwanza na wapili hawakusema kuchanga asali. Ngoja kesho nikatafute hiyo asali nianze dozi aisee. Asante kwa ushauri
 
huko ulipo hamna kinywaji cha HORLICS???mie huwa ndio nakunywa nalala.kingine anza mazoezi during the day ili mwili uchoke utalala tu
 
Hi Lutala. Mi mwenyewe mwanamke hapa. ao ulimaanisha nini hasa? niko tayari kwa kujaribu kitu chochote, kama nitapata usingizi. embu nifafanulie plz.
Dadaa unaposema kuwa upo tayari kujaribu kila kitu, una maana gani...!?

Kuna mtu amekushauri utumie maziwa ya moto na mwingine akaongeza na asali, nadhani ilio mbichi...!

Dadangu kutokulala kunasababishwa na mkizano wa mawazo (stress) na wasi wasi wa kimaisha...!
Punguza mawazo, na jishughulishe sana kipindi cha mchana, na hakikisha unachoka ili mwili wako, upate kupumzika usiku. Fanya hata mazoezi ya viungo, asubuhi na jioni.

Mimi pia niliwahi kuwa na tatizo kama lako na haswa kama unasumbuliwa na mambo muhimu ya kimaisha...!

Mimi nakunywa Maziwa ya moto, robo saa kabla ya kwenda kulala kila siku, na pia naweka kwenye mto manukato ya Lavender kila ninapotaka kulala...!

Na sasa napata usingizi mzuri na ndoto za hapa na pale tena Coloured in Hi Definition in 4D
dreams.

Taadhari:
Hali yako ikiendelea itakupelekea kupata ugonjwa wa Sononi au unyogofu (Depression).
 
Mi nasikitishwa zaidi na hzo hasira ndg yangu! Hebu fanya walvyokushaur hapo juu, ila mi ushauri wangu, nenda pia kwa watu wa iman yako kwa maombi.
 
Mkuu tafuta kamtu ukashughulikie haswa,baada ya kazi usingizi utakuja wenyewe.
 
Hebu jaribu meditation. Kama wachangiaji wengine walivyosema, matatizo ya usingizi hutokana na stress n.k. Huyo aliyesema ukigonga/gwa (ukinanhii) unalala hajakosea sana. Tatizo linakuja inapobidi ugonge/ugongwe kila usiku ili upate usingizi. That will be too much. Mara moja moja sawa lakini haitakusaidia sana in the long run!
 
Asante Mayasa, nimebadilisha avatar yangu (took me some time)

Kifuatacho sasa ni kujaribu kubadili mfumo wa maisha yako, inaonekana unawaza sana negative ndio maana unapatwa na hasira na kuona kama kila kitu hakiendi sawa. Kushindwa/kutofanikiwa ni sehemu ya maisha, hata vitabu vya dini vinasema TUSHUKURU KWA KILA JAMBO. Kama hukufanikiwa kwa kile ulichokuwa unatarajia haiimanishi ndio mwisho wa maisha, think positive na maisha yaendelee. Fanya mazoezi ili kuchosha mwili, angalia hata sinema nzuri nzuri sio za kutisha, toka nenda jichanganye na watu etc.. zaidi ya hapo tafuta mtaalam wa saikologia akushauri. Tatizo lako ni la ki saikologia zaidi. Kila la kheri
 
Nunua asali na mdalasini kwenye duka la TAFOPA lipo hapo mtaa wa bibi titi barabara ya morogoro, tumia mdalasini robo kijiko cha chai, asali vijiko vitatu vya chakula weka kwenye maji yaliyochemshwa (maji nusu kikombe/glass), yasiwe ya moto sana, tumia kutwa mara tatu, kwa siku saba au hata zaidi ukipenda uliza kama mlonge wa unga upo weka kijiko kimoja cha chai kwenye huo mchanganyiko bila shaka utakuwa mzima kwa muda mfupi.
 
Niliwahi kupata tatizo kama hilo la kukosa usingizi tena ni mwezi mmoja uliopita, kusema ukweli mie sikwenda kwa dr kwa sababu kwa ukoo wangu tuna hilo tatizo. Nilijaribu tu kuuliza kwa watu nikaambiwa niywe maziwa nichanganye na asali niywe nusu saa kabla ya kulaa imesaidia kidogo lakini bado tatizo lipo. Nilichongundua tu kwa mwenye tatizo la usingizi asinywe pombe hii ndio inaharibu kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom