Wana JF naomba msaada wa mawazo mimi nina tatizo la kuishiwa nguvu na kizunguzungu, sometime nahisi kupoteza network kabisa na huwa naweza poteza fahamu, nilienda hospital wakanipima kila kitu wakasema hamna shida, but mimi naona siko sawa, baadae wakaja kunipima tena wakasema sukari yangu iko chini na nilitumia dawa ikawa sawa kabisa. Baadae hiyo hali ikarudi tena but nikienda hospital wanasema sina tatizo, sasa nashindwa elewa nini inasababisha hali hii? Na pia nikikichelewa kupata kifungua kinywa asubuhi inakuwa balaa, maana ndio huwa napoteza network kabisa kwa kifupi siwezi vumilia njaa maana ndio huwa nahisi kuzimika kabisa(siwezi kaa zaidi ya saa moja bila kula chochote).