tatizo la breeding

farida29

Member
Dec 4, 2008
34
29
nilikuwa nimechoma sindano ya kuzuia ujauzito mwaka jana mwezi wa tano. ila nikawa naenda breeding kwa muda wa miezi mitatu bila kusimama. baada ya hapo siku zikabadirika kwa mwezi ninakuwa nina breed mara tatu. na siwezi kushika ujauzito ninataka kujua je ninatatizo gani.
 
Tatizo ni hiyo sindano, athari yake inaweza kuchukua muda kuisha. Pia kumbuka athari hutofautiana baina ya watu husika, kwa ushauri zaidi kamwone daktari wako.
 
nilikuwa nimechoma sindano ya kuzuia ujauzito mwaka jana mwezi wa tano. ila nikawa naenda breeding kwa muda wa miezi mitatu bila kusimama. baada ya hapo siku zikabadirika kwa mwezi ninakuwa nina breed mara tatu. na siwezi kushika ujauzito ninataka kujua je ninatatizo gani.

Samahani naomba usahihishe. Unaongelea bleeding au breeding? Hivi ni vitu viwili tofauti. Bleeding ni kutokwa damu wakati breeding ni mambo yanayohusiana na kuzalisha viumbe mfano mimea au wanyama kwa kutumia wazazi wa koo (breeds) tofauti ili kupata chotara ambao wana sifa na ubora zaidi ya wazazi wao. Wafugaji wa ng'ombe wanajua vizuri mambo ya Friesian anavyokuwa bomba akitengeza chotara kwa kupandishwa kwa ng'ombe wa kimasai. Hii inanikumbushwa mwalimu wangu aliyemwambia jamaa kuwa makini kwani alikaribia kuchanganya election na erection!!
 
Sasa hata kama kasema breeding tuseme hukumuelewa? nadhani kama unafahamu kiswahili usingeshindwa kuelewa kamaanisha nini? kama wewe ni Mtanzania unajuwa wazi kuwa matamshi ya herufi 'L' na 'R' yanawapiga chenga wengi, isiwe sababu ya kuanza tasnifa.
Wewe ulitakiwa umwambie kakosea spelling sio sijui wafugaji friesian........ Grrrrrrrrr!
 
Nimekuelewa ila tatizo linakuwa kwamba kichwa cha habari kinapokesewa kama hapo juu kinasababisha matatizo makubwa sana. Kama mimi ni mtaalamu wa breeding nitakimbilia kujua nini kinaongelewa na labda nisingefungua kama angeandika kwa usahihi. Pamoja na maoni yako, ambayo nayakubali na kuomba msamaha kwa yeyote ambaye nimemuudh au kumkwazai; bado naamini kuwa tunatakiwa kusaidiana katika matumizi sahihi ya maneno kama nilivyotoa mifano kwenye post yangu iliyopita.
 
tatizo la kutokwa damu ya uzazi bila mpangilio ambalo lina sababisha nisiweze kushika mimba.
 
Pole sana Farida. Tatizo lako linaweza kusababishwa na mambo mengi. Mojawapo ni hormone zako kutokuwa katika viwango vinavyofaa kwa wakati muafaka (hormonal imbalance). Ila kama ulivyosema, linaweza kutokana na matumizi ya hormones za kuzuia mimba (contraceptives). Kutokana maelezo yako inaonekana matatizo yako yalisababishwa na hizo sindano. Kwa kawaida, inategemewa mama apate uja uzito kati ya miezi 6-12 baada ya kuacha sindano. Sasa kama mfumo wako wa hormones umeshindwa kurudi kwenye hali ya kawaida kiasi cha kutopata uja uzito basi jaribu kumwona Doctor ambaye akishachunguza hali yako kwa makini anaweza kukupa matibabu ya hormones nyingine ili kukurudisha kwenye hali ya kawaida.
 
Farida, kama upo Dar na unaweza kwenda pale hosp ya TMJ, please go. Nafahamu kuna Daktari mzuri wa matatizo kama hayo (I have friends who had similar problems and were helped). Baada ya kutapona, nakushauri ujaribu njia nyingine (tofauti na sindano au vidonge) katika kujaribu kupanga uzazi (I fully understand the practical difficulties of other methods but I believe you will be able to cope and be spared of these harmonal problems).
 
Back
Top Bottom