TATIZO KWENYE Vitambulisho vya taifa: Je ni alama ya utanzania?

environmental

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,054
137
Wana bodi,

Nimekipitia kitambulisho cha taifa kwa haraka haraka na kubaini kuna TATIZO, naweza kuwa wrong. Ni wazo zuri kuwa na kitambulisho cha taifa lakini tukitengeneze kwa umakini. Kuna sehemu ya kitambulisho inasema " CITIZEN IDENTITY CARD".

Maswali

1. Je, kuwa na kitambulisho hiki ni alama ya uTanzania? ni uthibitisho kuwa ni mTanzania? Na kama ni citizenship identity,kwa nini kuwe na expiration date? Kwani Uraia unaexpire? Au cheti cha kuzariwa kina expiration date?
2. Masharti ya upatikanaji wa kitambulisho hiki ni yapi? Kama kitakua kinamtambulisha Raia wa Tanzania. Je unahita cheti cha kuzaliwa, passport au kithibitisho chochote ili upate kitambulisho hiki

Mwisho,

Nashauli serikali itoe hilo neno "CITIZEN IDENTITY CARD", tuwe na namna nyingine ya kumtambua mTanzani. Nashauri iwe " KITAMBULISHO CHA TAIFA" au "KITAMBULISHO CHA TANZANIA" kwa mantiki kuwa ni kitambulisho cha Taifa la Tanzania lakini haki signify CITIZENSHIP.

Pia matumizi ya lugha ya kigeni, nivizuri, lakini tuwe waangarifu. Mfano penye jina la kati imeandikwa hivi: MAJINA YA KATI/MIDDLE NAME. Nazani hapa inabidi tuzingatie
singular and plural nouns.

Na kwa kuongeza, inaonyesha hakuna issued date/ tarehe ya kutolewa! Hii kweli zimamoto

Ni wazo tu
View attachment 82394

nalidhani hiyo sentensi ya "citizen ID" inasimama pamoja na sentensi zilizotangulia. Mambo ya explicity na implicity haya.

bila shaka wahusika wamekusoma kiongozi, wataona namna watakavyozingatia ushauri wako
 
Inaelekea hata pale kwnye Jinsia/Sex wameandika Jinsi badala ya Jinsia.............!!

Hakika, imekosewa kabisa. Binafsi nilifedheheshwa sana nilipoliona hili. Na hii inathibitisha namna tunavyokosa umakini hata kwenye mambo ya msingi. Kila kitu ni zimamoto tu.
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    60.1 KB · Views: 215
Inaelekea hata pale kwnye Jinsia/Sex wameandika Jinsi badala ya Jinsia.............!!

Hapana. Kiswahili fasaha ni JINSI na wala sio JINSIA kama tulivyozowea. Linaweza kuleta ukakasi fulani masikioni, lakini ndivyo lugha ya Kiswahili inavyotaka.

"Umejaaliwa mtoto wa jinsi gani?" na sio "umejaaliwa mtoto wa jinsia gani?". Hebu tamka hizo tungo mbili kwa umakini utaona hiyo ya mwanzo imekaa vizuri kuliko hiyo ingine
.
 
wameajiliwa watoto wa wakubwa wasio na ujuzi na utaalam kwa kazi hiyo.
Hata hivyo pesa ya huo mradi ilishaliwa ikaisha.
Wapi masha!
 
Hapana. Kiswahili fasaha ni JINSI na wala sio JINSIA kama tulivyozowea. Linaweza kuleta ukakasi fulani masikioni, lakini ndivyo lugha ya Kiswahili inavyotaka.

"Umejaaliwa mtoto wa jinsi gani?" na sio "umejaaliwa mtoto wa jinsia gani?". Hebu tamka hizo tungo mbili kwa umakini utaona hiyo ya mwanzo imekaa vizuri kuliko hiyo ingine
.

Cha msingi si neno hilo linavyotamkika bali mahitaji ya kiswahili fasaha. Neno hili "JINSIA/SEX" limetumika hata katika PASIPOTI YA JMT. Sasa hata ukitulazimisha tuamini hivyo unavyotaka wewe (JINSI/SEX) bado unazidi kuthibitisha namna Wizara ya Mambo ya Ndani ilivyokosa umakini.

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    34 KB · Views: 203
Hii kitu inasemekana ni mpango wa wajenzi huru!huwezi uza wala kununu kama hauna identity.
 
Hapana. Kiswahili fasaha ni JINSI na wala sio JINSIA kama tulivyozowea. Linaweza kuleta ukakasi fulani masikioni, lakini ndivyo lugha ya Kiswahili inavyotaka.

"Umejaaliwa mtoto wa jinsi gani?" na sio "umejaaliwa mtoto wa jinsia gani?". Hebu tamka hizo tungo mbili kwa umakini utaona hiyo ya mwanzo imekaa vizuri kuliko hiyo ingine
.

Etimological origin of the word ni pi? from there we can judge what is correct
 
Watu wa Ikulu hawajifunzi kabisa. Huko nyuma kulikuwa na aibu ya ile cheque ya Exim, maneno tofauti na tarakimu, sasa naona wamerudia kosa lile lile. Hawakagui hivi vitu kabla rais hajafika?

'Majina ya kati' hapo hapo kuna 'middle name'. Hata ingekuwa ni direct translation 'name' haiwezi kuwa 'majina'!
dudus, sex, translation yake ni jinsi (means?). Tangu lini?
 
Last edited by a moderator:

Cha msingi si neno hilo linavyotamkika bali mahitaji ya kiswahili fasaha. Neno hili "JINSIA/SEX" limetumika hata katika PASIPOTI YA JMT. Sasa hata ukitulazimisha tuamini hivyo unavyotaka wewe (JINSI/SEX) bado unazidi kuthibitisha namna Wizara ya Mambo ya Ndani ilivyokosa umakini.

[/SIZE]

Hicho ndio kiswahili sahihi. Kwa hakika passport ya JMT imekosewa.
 
Kwenye Kamusi ya Kiswahili Sanifu iliyotolewa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Dar es Salaam mwaka 1981 inafafanua kama ifuatavyo: JINSI (namna; aina; mwenendo, njia) wakati JINSIA (hali ya kuwa -a kiume au kike.... ) Sasa wataalamu wa kiswahili watufahamishe kama kumetolewa maana tofauti na hiyo na lini na inapatikana wapi. Kama yameonekana makosa yarekebishwe mapema kabla vitambulisho havijachapishwa/kutolewa kwa wingi
 
Hapana. Kiswahili fasaha ni JINSI na wala sio JINSIA kama tulivyozowea. Linaweza kuleta ukakasi fulani masikioni, lakini ndivyo lugha ya Kiswahili inavyotaka.

"Umejaaliwa mtoto wa jinsi gani?" na sio "umejaaliwa mtoto wa jinsia gani?". Hebu tamka hizo tungo mbili kwa umakini utaona hiyo ya mwanzo imekaa vizuri kuliko hiyo ingine
.

Asante Mzee kwa ufafanuzi.

Si unajua tena Bongo, Kiswahili tabu na Ung'eng'e tabu, tupo tupo tu!!
 
Wana bodi,

Nimekipitia kitambulisho cha taifa kwa haraka haraka na kubaini kuna TATIZO, naweza kuwa wrong. Ni wazo zuri kuwa na kitambulisho cha taifa lakini tukitengeneze kwa umakini. Kuna sehemu ya kitambulisho inasema " CITIZEN IDENTITY CARD".

Maswali

1. Je, kuwa na kitambulisho hiki ni alama ya uTanzania? ni uthibitisho kuwa ni mTanzania? Na kama ni citizenship identity,kwa nini kuwe na expiration date? Kwani Uraia unaexpire? Au cheti cha kuzariwa kina expiration date?
2. Masharti ya upatikanaji wa kitambulisho hiki ni yapi? Kama kitakua kinamtambulisha Raia wa Tanzania. Je unahita cheti cha kuzaliwa, passport au kithibitisho chochote ili upate kitambulisho hiki

Mwisho,

Nashauli serikali itoe hilo neno "CITIZEN IDENTITY CARD", tuwe na namna nyingine ya kumtambua mTanzani. Nashauri iwe " KITAMBULISHO CHA TAIFA" au "KITAMBULISHO CHA TANZANIA" kwa mantiki kuwa ni kitambulisho cha Taifa la Tanzania lakini haki signify CITIZENSHIP.

Pia matumizi ya lugha ya kigeni, nivizuri, lakini tuwe waangarifu. Mfano penye jina la kati imeandikwa hivi: MAJINA YA KATI/MIDDLE NAME. Nazani hapa inabidi tuzingatie
singular and plural nouns.

Na kwa kuongeza, inaonyesha hakuna issued date/ tarehe ya kutolewa! Hii kweli zimamoto

Ni wazo tu
View attachment 82394

hayo ni ya msingi..kwengine kote nimegundua spelling mistakes tu..
 
mimi sina tatizo na vitambulisho, nataka kujua ni sh.ngapi zimetumika hadi sasa hivi - na zitatumika ngapi mpaka zoezi linakamilika.
 
Uchakachuaji imekuwa ni sehemu muhimu katika shughuli zote za kiserikali za hawa magamba.
 
Kiswahili cha "Majina" ni cha Kenya, hawa jamaa huwa wanajitambulisha kama ifuatavyo "Kwa Majina naitwa..........."

Tuchunguze vizuri labda hapo NIDA kuna Mkenya kajipenyeza. Sasa kulikuwa na maana gani kuandika "Majina ya Kati" na huku chini wanasema Middle Name? Kilishindikana nini kuandika tu "Jina la Kati?" Au wanatupa nafasi ya kuweka Mengi kadri tutakavyopenda? Si mnajua tena majina yetu mengine ya Shule tu "Hamisi Nassoro Kigwangalla sasa itakuwa Hamisi Nassoro Said Bagaile Kigwangalla" = Majina ya Kati "Said Bagaile" Au "Mwigulu Nchemba" = Mwigulu Lameck Madelu Nchemba" (Majina ya Kati = Lameck Madelu).

Hapo vipi wadau si watakuwa sahihi na hiyo "Majina ya Kati?" Basi kama walimaanisha hivyo wabadilishe tu kwenye Kiingereza badala ya Middle Name iwe Middle Names watakuwa wameua!!

Na hii mambo ya Expiry Date tena ya nini jamani, haya siyo matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi? Au wanatuzuga baadaye vitakuwa vya kulipia hivi? Hapo watakuwa wametukamata na hivi wa-TZ tu wapole kama Kondoo tutapelekwa pelekwa tu!! Hapo naona kuna mtego tutegemee haya.
 
Hapana. Kiswahili fasaha ni JINSI na wala sio JINSIA kama tulivyozowea. Linaweza kuleta ukakasi fulani masikioni, lakini ndivyo lugha ya Kiswahili inavyotaka.

"Umejaaliwa mtoto wa jinsi gani?" na sio "umejaaliwa mtoto wa jinsia gani?". Hebu tamka hizo tungo mbili kwa umakini utaona hiyo ya mwanzo imekaa vizuri kuliko hiyo ingine
.

Hicho Kiswahili fasaha ni kwa mujibu wa mamlaka gani? Maana kamusi za TUKI na Oxford zina "jinsia" badala ya "jinsi".
 
Back
Top Bottom