Tatizo kwenye ndoa yangu naomba msaada

Achana na huyo firauni asije akakuambukiza magonjwa. Ni bora ujipange tu kuwaandalia watoto wako future.
 
Pole sana dada.

Kwanza elewa kwamba nyie ni wazazi, mna wajibu mkubwa sana kwa watoto wenu, especially wewe mama. Kama mumeo ameona ni bora awe na kimada, basi mi nakushauri wewe bora uwe na Mungu wako!Lea watoto wako na mlilie Mungu wako, nakuhakikishia ATAKUJIBU!
 
Miaka 30 watoto wawili bado unajiita kabint? kua mama na simamia ndoa yako, acha utoto
 
Peleka mahakamani that Ba.s.ta.rd! Kwanza hiyo mimba ya mwanamke wa nje ni proof ya kutosha ya ground ya divirce kwa sababu ya ADULTERY! Mtagawana mali na kuhusu watoto atawatunza! Tena kwa asilimia kubwa hao watoto watakaa na wewe! Huyo mwanaume ni hatari sana atakuletea ukimwi aisee! Ila kama unakubali kuwa na wake wadogo itakucost baadae utakapoenda kuomba divorce kwani utakuwa ume-connive hali ile! Tafakari chukua hatua!

Kweli Ubinadamu kaazi kweli... Uyo mume Angepewa nafasi ya kuvaa viatu anavokuvalisha naamini angejua nini tamu au chungu ya hayo anayotenda juu mkewe.. Ila wazo kusema kupelekana mahakamani wapeane talaka naona ni mapema. Kwanza si dhani kama uyu dada alikubali kuolewa ili aje apewe TALAKA, na hata ukisema wagawane mali ikilazimu kutalikiana, itakua vipi kama hawajajenga na pengine labda aseti walizonao ni gari na vitu vya ndani? Uyu dada anatafuta suluhisho namna ya kumbadilisha mume atulie.

Nafkiri Uyu dada afuate utaratibu wa kuwashirikisha washenga wao, wazazi kama wapo na viongozi wa dini \baraza la usuluhishi parokiani kama lipo. Yakishindikana, mimi namshauri KWA KUA ANAYO KAZI, ANAPATA KIPATO FULANI, Basi ajikusanye, ANUNUE ENEO, aanze kujenga makazi yake. Afikirie MBALI. NA kama mume mwenyewe tabia ni hizo, inavyoonekana bila shaka ATAWATELEKEZA NA HAO WENGINE ATAKAOWAZALISHA nje ya ndoa. Ivyo uyu dada akiendelea kumwendekeza, Yeye ndie ATAKAEKUA ANALETEWA WATOTO WA NJE ALEE.
Bora uyo dada aanze kuangalia namna gani ya kuishi INDEPENDENTLY kulingana na kipato chake katika maisha yake na hao watoto ajitahidi kuwalea kadri ya uwezo wake, maana kwa inavyoonekana, kama juhudi za maksudi zisipofanyika mume anaelekea kutelekeza familia nzima.... Ila ZUNGUMZENI KWANZA MEZANI kabla ya kuchukua uamuzi mwingine. Ila pia MUULIZE SWALI, KWAMBA "Je,YUKO TAYARI KUISHI AHADI ya UAMINIFU ALIYOAPA MADHABAHUNI na KUWAACHA WENGINE WOTE AWE NA WEWE....AU HAYUKO TAYARI....?
 
Smile uko wapi unayeachika kila siku! Umpe ushauri wa maana, kwani sioni cha kumshauri zaidi ya kuvunja ndoa. Mume hana mapenzi kabisa sasa yeye sioni anamng'ang'ania wa nini.

Kama uchumi anao, kama urembo naamini kila siku matongozo hayaishi. Smile mshauri akimbie haraka kabla roho haijaacha mwili baada ya maumivu makali ya mtandao wetu>

ndimi Bazazi!
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini ulisubiri tatizo liwa kubwa ndio ulitatue? hapo juu nime underline dalili zote za mvua inayo kunyeshea sasa hivi. It is very sad you did not take any action when you could. Hata hivo wanasema it is never too late to act.

Kwanza kabisa elewa kua wewe hujakosea (zaidi ya kumuonesha uvumilivu wa kupindukia). Kama ndoa yenu inayumba leo ni kosa lake yeye, sio lako. So stop feeling guilty for something you did not cause. and stop trying to fix somebody else's mess.
Hata kama hujajipanga kulea watoto bila baba nadhani umefika hatua ya kubadili mipango sababu hawana baba tena. Mtu anakaa miezi 2 bila kuja home wakati anaweza, na akija anaondoka bila kuacha pesa. Na pale unapo jaribu kuongea nae anakujibu kuny* hafai kuitwa baba tena, amesha jitoa kwenye ndoa hiyo.

Mwache aendelee na huyo dada mngine, wewe jipange upya tu. Unaweza kuamua ku-divorce kabisa au unaweza kuamua separation tu (Ningeshahuri separation tu hadi pale utakapo kua na uhakika). Umesema unafanya kazi, basi anza kubadili taratibu zako za maisha ili mshahara wako uweze kufunika expences zako. Kama utakwama kabisa unaweza kuongea nae juu ya mahitaji ya watoto.
Usilazimishe, huyo mtu hakupendi, na inaonekana hajawahi kupenda in 5 years of marriage. Ukiendelea kua nae utapata magonjwa ya kila aina, kuanzia BP, moyo, depression hadi magonjwa ya zinaa. Don't let anyone ruin your life, move on!

Umepewa ushauri mzuri sana bidada, ongezea na signature yake pia ili ikusaidie katika kufanya maamuzi

A%20S-heart-2.gif
♪♪If you want to be happy, BE! ♫ ♫(Leo Tolstoy)
A%20S-heart-2.gif


 
Pole sana dada yangu, hiyo ni sehemu ya tatu ya ndoa, itapita halafu ndoa yako itakuwa na furaha tele. Ndoa inasehemu kuu tatu. Kizungu, kuchinachina na kienyeji. Ndoa yako ipo ktk hatua ya kienyeji, ikivuka hapo, inaanza tena mwanzo (kizungu) vumilia bado miaka michache ibadirike.
 
pole rafiki! wakati mwingine kufanya maamuzi magumu ndio kipimo cha ukomavu wa akili, hakuna duka la moyo sehemu yoyote ile.Hakikisha unapata haki yako mfano mali mliyopata pamoja na uachane na huyo jamaa haraka iwezekanavyo vinginevyo utavuna mabua! Hasitahiri kuwa na mke mwema kama wewe mwache achezee dunia ninaimani haitaacha kumfunza!
 
Pole dada sina la kuchangia bt namuomba MUNGU nikijaingia taasisi ya ndoa mke wangu ajisifu amepata mume anaempenda
 
Mi naona wakuwajali zaidi ni watoto, huyo mume ni mtu mzima anaelewa fika kuwa ana mke na bado amefanya uashrati wake huko nje mpaka kumpa mimba mwanamke.

Mumeo ndo ameshakupa msimamo wake na wewe amua moja for the sake of your childrean get out of that chaos, kukaa kwenye hiyo 'ndoa' ni kukubali kuishi na machungu daima na hiyo haisaidi makuzi kwa watoto sababu wataona jinsi ambavyo hamko kwenye good terms na hicho kitawaumiza wao pia.

My mum had the same problem in her marriage, she chose to stay but I tell you I wish she would have left. Sheria itakulinda kupata matunzo ya watoto lakini kumuondoa huyo kimada kwenye maisha ya mumeo ni mpaka mumeo mwenyewe aamue na sasa itakuwa vigumu zaidi kama ana mimba yake.

Mungu akupe kujua lipasalo kutenda.
 
Pole sana kwenye mahusiano wanaume wanalalamika sana wasichana si waaminifu wanakuwa na wanaume zaid ya 1,kwenye ndoa wanawake wanalalamika sana wanaume si waaminifu.sijui tatizo litakuwa wapi ila moyo unasiri kubwa na MUNGU ndiye ajuaye siri zake.alafu mi thread kama ihi SMILE akiisoma ndo anazidi kuchukia wanaume agrrr mliokwenye ndoa mnatuaribia bana ambao bdo atuja wowa kwakwelii.
 
Dah dada pole sana. Jamani wanaume wengine sijui wakoje! Nway hebu mkalishe chini mpe ya moyoni mwako point black mweleze kuwa asikutishie na huyo hawara kwa kuwa wewe ndo mke halali wa ndoa na kiimani haruhusiwi kuwa na mwingine bila kuterminate nawe. Mweleze achague moja wewe au yule angalia upole wako usijekufikisha kaburini!

Mwombe sana Mungu
 
kuna mifano ya watu wengi waliolea watoto peke yao, usiogope u can do it. kubaki na huyo mwanaume utawaach watoto yatima
 
mimi nakukulaumu wewe,,, umeeeleeeza ubaya weeeee wa mumeo, as if weye ni malaika, haya nimekusikia na watu wamekushauri kama ulivyowasilisha, wamekuamini na kukuonea huruuma, wamemhukumu mumeo, wamekufariji!

unafiki,,, mabint wengi ni mateso, hawana maadili na wanakompit na waume zao, ni wenye hila hasa wakishakuwa na kinga ya watoto, unafanywa mtumwa, amri na kiburi, over communication, kujali wa kwao, inafikia staji hata mkitofautiana ndugu wanafurahi,,,

Huwa mshakuwa juu wajibu wa mke huelewi makuzi na tabia msingi za akuoaye, hamfundishiki ukisasa mwiingi,,,

ama weye mbovu,,, nasepa,,,

my take,,,
chukua kioo ujiangalie,,, uone unaona nini, chunguza njia na mapito yako uone ulipojikwaa ukamkifu mumeo, jihoji bila kujihesabia haki,,, kuna mahali wewe ni chanzo, itafute kweli itakuweka huru,,, malezi yako yakoje? Umeshika yapi na yapi umeacha juu ya suala la ndoa?

Wengi tunaolea utamaduni tu na mazoea, lakini faraja ipo kwa hawara, malengo ya hawara ni dhahiri ila malengo ha mke asiye na heshma akutesaye ni tata, uzeeni je? Heri mapemaaa nisife na bp,,, tunaisaka faraja na security unapoona ni tata kwa mke au kuna mambo ulimficha ameyagundua mshakua pamoja,,,

mambo ni mengi, umemkamata mama yake kwa kipato chako unamtumia kanma silaha kumpelekesha mumeo!

My dear,,,,tulia jitafakari muombe mungu,,,tubu dhambi zako na makosa yako kwa mungu na kwa mumeo,,upate hekima muite mahali pa sirinmuongee,,umueleze ulipokosea,,,kisha muombe asiendelee kukuumiza kwani ushatubu na ujirekebishe,, kweli wapeden wtt wenu, pole,
 
Pole sana! Chukua hatua huyo mwanaume hakupendi angekua anakupenda asinge kufanyia hayo its too much aisee!kama ingekua ni mtu wa kubadilika angeshabadilika toka mwanzo ulipoanza kugombana na hao kina ashura wake!kwa sasa hata mkikaa vikao vya ndugu na wazazi it won't help hiyo ndio asili yake hawezi kuiacha! Nenda ustawi wa jamii ili ujihakikishie matunzo ya watoto asipojirudi then fanya process za divorce!
 
ndio ndoa hizo shoga unazani uko mwenyewe mko kibao mnaoteseka na ndoa ukienda kwenye maombi na mikutano ya injili utakutana
na wenzio wanalia, ndoa0 mama ndio ndoa hizo
 
Back
Top Bottom