Tathmini ya mapato ya kilimo cha michungwa 1000 baada ya miaka 3

Kahtan Ahmed

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
755
468
Habari wana jf mm ni kijana ambae nimekua nikifuatilia mishe mishe za mjini ambazo nikifanya naweza kutoka kimaisha mara moja nimekagua kila aina ya dili za hapa mjini na vilimo huko vijijini ila mwisho nimegundua kua kilimo cha michungwa kinalipa sana.

Hizi ni baadhi ya dondoo nilizozikusanya baada ya tathmini ya mapato kwa kupanda michungwa 1000 baada ya miaka 3

kila mchungwa baada ya miaka mitatu itazaa machungwa 4000
hivyo 4000 machungwa*1000 michungwa = 4,000,000 machungwa
jinsi ya quality ya chungwa katika kipindi cha mavuno sokoni linasimama 120 tsh kwa sasa baada ya miaka mitatu makadirio ni 150 150tsh
hivyo 150tsh *4,000,000 machungwa= 600,000,000/= tsh na ni misimu miwili kwa mwaka 600,000,000 * 2 = 1,200,000,000.

Nukuu
(a)Hii ni aina ya michungwa ambayo watu wengi hawaifahamu na kwa kiwango cha chini hapa tanzania katika mkoa wa pwani inazaa machungwa 6000 ila mm nimeweka 4000 na kwa kiwango cha juu ni 7000
(b)aina hii ya michungwa kadri inavyozidi kupea ndio machungwa yanazidi ubora wake pia kadri unavyochelewesha kuvuna ndio yanazidi kua mazuri na ukiyavuna mwisho wa msimu ndio vizuri zaidi mana bei itakua nzuri
(c)ni machungwa makubwa na matamu pia yanastahamili misukosuko mana ni magumu hata katika safari hayaharibiki wala kupasuka
(d)michungwa hii inahitaji utaalamu wa hali ya juu katika kuyashughulikia ila pia gharama zake ni ndogo katika kushughulikia!

ukiwa intrested na kilimo hiki kwa zaidi nitafute kwa 0712212220
 
Kwanini huu mchanganuo hauna gharama .... pamoja na kueleza tathmini ya mapato lakini gharama ndiyo elekezi ya mradi kuwa na faida au hasara ... i dont believe if this project has zero costs

unless otherwise it is too good to be true

all the best
 
,ghrama
ekari 1 = michungwa 76
michungwa 1000 = ekari 13.1

mwaka wa kwanza
miche 1000 kila mche tsh 1500 -- 1500*1000 =tsh 1,500,000/=
kutayarisha shamba ekari moja tsh 30000 -- 30000*13 =tsh 390,000/=
kuchimba mashimo kila shimo tsh 300 -- 300*1000 = tsh 300,000/=
kupanda kila kupanda mche mmoja tsh 200 -- 200*1000 = tsh tsh 200,000/=
mbolea samadi kila ekari tsh 20000 -- 20000*13 = tsh 260,000/=
dap(50 kg) kila ekari tsh 40000 -- 40000*13 = tsh 520,000/=
can(50 kg) kila ekari tsh 36000 --36000*13 = tsh 468,000/=
dawa kila ekari tsh 20000 -- 20000*13 = tsh 260,000/=
kupalilia kila ekari tsh 40000 -- 40000*13 = tsh 520,000/=

mwaka wa kwanza =4418,000/=

mwaka wa pili ni kupalilia tu 520000/= 520,000/=

mwaka wa tatu ni kupalilia na kuvuna
kupalilia 520,000
kuvuna 1,400,000
mwaka wa tatu = 1920,000/=

gharazama ya kumwagilizia kwa muda wa miezi 14

kisima kuchimba 3500,000
tank za maji 1200,000
irrigation system pipe 700,000 = 5400,000/=

total 12,258,000/=

kilimo cha umwagiliziaji ni bora kwasababu ukishapanda kila mche kwa kila siku unahitaji kumwagiliziwa lita mbili za maji kwa muda wa miezi 14 na kwa uhakika utavuna kile unachokihitaji
 
Naulizia kuhusu hiyo mbegu. Je unafanya grafting ili kupata mbegu bora yenye kuchukua muda mfupi mpaka kuzaa matunda?
 
kwa kweli mm si muandaaji wa taarifa nzuri ndio mana maelezo yangu hayajatulia na naomba munisamehe kwa hilo na penda kumjibu mmoja mmoja kama ifuatavyo
htuc: ni kweli ukishakua na maji bajeti ya laki saba inatosha kwa irrigation hemu mukipata muda niwapeleke shambani mujionee ninavyowafungia watu hizi iirigation na kila mche kwa siku unapata liter mbili bila ya wasi
zemacorpolo: sikiliza ardhi kwa sasa sehemu za ndani bado ni rahisi laki nne waweza kupata kwa hekari, michungwa ulinzi wake ni wanyama wa kula miche na ukiweka uzio tayari umeshaweka ulinzi na rabda kipindi cha msimu ni lazima uweke mlinzi kwa kipindi hicho cha msimu tu na kuhusu market machungwa kama haya ni ya kipekee na hakuna michungwa mingi aina hii ambayo watu wengi bado hawajaigundua mm nilikua nataka kupanda valencia ila kwa uchunguzi valencia ni mazuri ila hayana uzao mkubwa subiri niwawekee baadhi ya picha
chai chungu miche ipo ila kwa order mana inataka utaalamu kweli upandishia mana inapandishiwa kwa mlimau na inataka utaalamu kuunganishwa tofauti na valencia na jaffer

attachment.php
 
Attachments

  • 681x454.jpg
    681x454.jpg
    76.7 KB · Views: 2,179
Hongera sana mkuu kwa hatua uliyofikia,je hasa cha muhimu hapo ni kujua,endapo machungwa yakishavunwa je mauzo yanakuwaje??maana isije end of the day mtu amegharamia hicho kiasi chote kwa miaka 3 then machungwa yanakuwa tayari alafu hamna pa kuuzwa...

Vile vile upande wa shamba umesema linaweza kupatikana kwa kiasi cha 400,000 je hapo inakuwaje hasa??me nina shamba langu la ekari 80 huko Songea sasa unaweza kunifanyia utafiti zaidi kama haya machungwa yanaweza kukubali kwa huo mkoa??maana sio lazima wote tujazane kwenye hiyo mikoa uliyoitaja....labda ungeenda deep zaidi ingekuwa vizuri ili wengine washawishike zaidi kwenye hii project but for me so far naona sio mbaya sana.....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kanyagio nimesema 4000 na kama ikitokea mche haukukua vizuri na mche una maradhi basi utazaa si chini ya 1000
na anaetaka kuyaona machungwa ni bora nimfikishe shambani ajionee mana picha zinadanganya!

Hapo kwenye blue,
Hebu weka vizuri hizo takwimu za uzaaji wa michungwa hiyo tujijue vizuri.
Kweli mchungwa mmoja unaweza kuzaa matunda 4,000 ??? !!! kwa msimu mmoja ?? !!
Hapo kuna shaka katika takwimu zako, maana hata mti mkubwa kama muembe hauwezi kubeba maembe 4,000 kwa wakati mmoja.
Labda mimi sijawahi kuona hii.
 
nami nimepanda mchungwa hapa nyumbani lakini nikifikiria 4000 naona kama ni machungwa mengi. Labda kama ni ardhi ya ndani ya misitu ya Congo lakini kwa ardhi ya Tz nzima hata Muheza sioni
 
Hapo kwenye blue,
Hebu weka vizuri hizo takwimu za uzaaji wa michungwa hiyo tujijue vizuri.
Kweli mchungwa mmoja unaweza kuzaa matunda 4,000 ??? !!! kwa msimu mmoja ?? !!
Hapo kuna shaka katika takwimu zako, maana hata mti mkubwa kama muembe hauwezi kubeba maembe 4,000 kwa wakati mmoja.
Labda mimi sijawahi kuona hii.

Kumbe na wewe umeona eeh?! Mchanganuo wake wala sikutaka kuuzingatia mimi aliponitia ganzi ni kuhusu hiyo idadi ya machungwa kwa mti mmoja! Huyu anatuchezea akili tu hapa! Mchungwa wenye umri wa miaka 3 ukazaa machungwa 4000 hii inastahili kuingia kwenye Guiness book of records!! Tumezaliwa mashambani na tunafanyakazi kwenye michungwa, mchungwa wa miaka mitatu tena kwa michungwa grafted hiyo haipo maana sasa machungwa yanataka kuzidi hata idadi ya majani! Hayo ni machungwa au ndimu!
 
kwa kweli mm si muandaaji wa taarifa nzuri ndio mana maelezo yangu hayajatulia na naomba munisamehe kwa hilo na penda kumjibu mmoja mmoja kama ifuatavyo
htuc: ni kweli ukishakua na maji bajeti ya laki saba inatosha kwa irrigation hemu mukipata muda niwapeleke shambani mujionee ninavyowafungia watu hizi iirigation na kila mche kwa siku unapata liter mbili bila ya wasi
zemacorpolo: sikiliza ardhi kwa sasa sehemu za ndani bado ni rahisi laki nne waweza kupata kwa hekari, michungwa ulinzi wake ni wanyama wa kula miche na ukiweka uzio tayari umeshaweka ulinzi na rabda kipindi cha msimu ni lazima uweke mlinzi kwa kipindi hicho cha msimu tu na kuhusu market machungwa kama haya ni ya kipekee na hakuna michungwa mingi aina hii ambayo watu wengi bado hawajaigundua mm nilikua nataka kupanda valencia ila kwa uchunguzi valencia ni mazuri ila hayana uzao mkubwa subiri niwawekee baadhi ya picha
chai chungu miche ipo ila kwa order mana inataka utaalamu kweli upandishia mana inapandishiwa kwa mlimau na inataka utaalamu kuunganishwa tofauti na valencia na jafferView attachment 78093

Hii michungwa pichani ndiyo ina umri wa miaka 3?! Mbona inaonekana wazi ni miti yenye umri mkubwa tu! Na hayo machungwa umesema yako 4000 najaribu kuhesabu hapo yalipo sana sana labda yanaweza kufikia 300 hadi 400 ! Hayo hata hivyo ni machungwa kweli au machenja?! Hebu jitahidi ulete uthibitisho zaidi juu ya uwepo kwenye dunia hii wa michungwa yenye umri wa miaka 3 kuzaa machungwa makubwa 4000 msimu wa kwanza tutakusikiliza!!
 
kwa kweli mm si muandaaji wa taarifa nzuri ndio mana maelezo yangu hayajatulia na naomba munisamehe kwa hilo na penda kumjibu mmoja mmoja kama ifuatavyo
htuc: ni kweli ukishakua na maji bajeti ya laki saba inatosha kwa irrigation hemu mukipata muda niwapeleke shambani mujionee ninavyowafungia watu hizi iirigation na kila mche kwa siku unapata liter mbili bila ya wasi
zemacorpolo: sikiliza ardhi kwa sasa sehemu za ndani bado ni rahisi laki nne waweza kupata kwa hekari, michungwa ulinzi wake ni wanyama wa kula miche na ukiweka uzio tayari umeshaweka ulinzi na rabda kipindi cha msimu ni lazima uweke mlinzi kwa kipindi hicho cha msimu tu na kuhusu market machungwa kama haya ni ya kipekee na hakuna michungwa mingi aina hii ambayo watu wengi bado hawajaigundua mm nilikua nataka kupanda valencia ila kwa uchunguzi valencia ni mazuri ila hayana uzao mkubwa subiri niwawekee baadhi ya picha
chai chungu miche ipo ila kwa order mana inataka utaalamu kweli upandishia mana inapandishiwa kwa mlimau na inataka utaalamu kuunganishwa tofauti na valencia na jafferView attachment 78093

Mkuu mimi nipo interested na Irrigation,Je una utaalamu wa kuset up irrigation systems? what are the costs per acre? Nahitaji sana msaada wa kuset irrigation system kwa ajili ya kulima hortculture
Issue ya Machungwa I have to visit your farm before believing it
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom