Losambo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 2,612
- 864
Rejao acha wivu wa kisiasa, kama mtu anatekeleza majukumu yake basi ni haki yake kusifiwa. Kuna jamaa yangu yupo Arusha alikuwa anamponda sana aliyekuwa mbunge wa CCM Felix lakini alikuja kuona Lema anaweza kuwa suluhisho kwa matatizo ya wana Arusha baada ya kumsikia na kusikiliza baadhi ya maoni ya wanaArusha.
Hapo ni bla bla tu, tulishafanyia analysis ya kila kitu. Kati ya hayo uliyoyataja, kipi kilikuwa kwenye kampeni zake? Alitoa ahadi nyingi sana na hamna hata moja ameitekeleza. Umeleta hapa vitu ambavyo ni irrelevant, ambavyo hata mtu wa kawaida asiye mbunge anaweza kuvifanya.
Kusomesha hao wanafunzi 400 tulifanya calculations ni around 16m kwa mwaka, hela ambayo ni ndogo sana kwa mbunge plus wafadhili wanaomsaidia.
Jipangeni tena mje na hoja za kumtetea na wala si habari za kutetea.
Halafu huyu mbunge mwambieni pia aache kujitangaza sana kupitia hapa JF na kwenye media nyingine. Kuna wabunge wanafanya mambo mazito na makubwa ya kimaendeleo lakini hawapigi domo.