Tathmini: M4C Fundraising Dar wapi hapakuwa sawa na nini Kifanyike

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Si busara sana kulalamika kwa mapungufu yaliyojitokeza katika tukio la leo na si vibaya kupongeza na kudumisha yote mazuri katika tukio hili hapo SERENA HOTEL.

Nini Tathmini yako Mpenda mbadiliko na nini kifanyike siku zijazo?

NYONGEZA KUFUATIA UZI HUU KUANZA KUPOTEZA MAANA:

Kukosekana kwa baadhi ya Makamanda kusichukuliwe kama kigezo cha kuonyesha umoja au uhai wa CHADEMA. Kumbukeni hizi ni Kampeni endelevu za Kanda kwa kanda, Kaskazini washamaliza, jana ilikuwa Pwani, Kanda ya ziwa wanafanya maandalizi, watafuata kusini na hatimaye kilipo kitovu cha kutunga sheria.

Kamanda Mbowe alikuwa pale kama mgeni rasmi, sawa tu na ambavyo kanda ya ziwa wakiamua mgeni rasmi awe PhD na Mbowe asiwepo.

Kukosekana kwa Makamanda wengine ZZK, Sugu, Msigwa, Mnyika, Mdee na wengineo hakumaanishi kuzorotesha nguvu ya CDM. CDM ni nguvu ya Umma na si kiongozi mmoja mmoja, wao ni watia hamasa tu na kuelekeza njia sahihi.

Utashangaa watu leo humu wameshupaa na Slaa, Zito jamani hawa si Chama. Kama alivyosema Mbowe ''NIKIFA MSILIE WEKENI MAITI YANGU PEMBENI NA ENDELEENI NA HARAKATI ZA UKOMBOZI''. Kwa unayefahamu kiswahili fasaha huu ujumbe haumaanishi kwamba itelekezeni maiti yangu basi iliwe na wanyama HAPANA bali yeye si Chama hata akifa au kutoka CDM itabaki na mapambano yataendelea kwa kuwa Chama hiki ni nguvu ya UMMA.


ADIOS
 
Hiki kitu kimetangazwa too late,imekuwa kama kushtukiza.Ilitakiwa kuwe na maandalizi na watu wajulishwe.MCs hawaku imanage shughuli vizuri.

Alafu eti ndo wanarudisha umeme kwetu
 
Malengo ni Bilioni 5, leo kwa hesabu ya mpaka sasa huku tukisubiri hesabu kamili zimechangishwa zaidi ya shilingi milioni 257
Mpaka hafla hiyo inahitimishwa hii thread pia ilikuwa na wachangiaji 257 (There are currently 257 users browsing this thread. (94 members and 163 guests)
 
tathmini ya nini?kwani tukio la kuchangisha limeisha au wamekata kwa sie ambao tulikuwa twaangalia na star tv,acha kiherehere muda wa tathmini yako ufanye by saa 7 usiku wakitoka ukumbini,aaaaarghh......
 
Ningepenga next tym kuwe na vi-earphone kama wanavyotumia usalama au kwenye tv kwa ajili ya mawasiliano sio lazima mpaka mtu aende kuongea kwenye mic moja kwa moja maana watu walikua wanasikia mtu anavyomnong'oneza mc(rose) na mwenyeketi wa m4c(alex) hilo tu hila mambo yote yameenda vizuri,bigup name nimechangia m4c thru m-pesa! Peoplessssssssssssss!!
 
Malengo ni Bilioni 5, leo kwa hesabu ya mpaka sasa huku tukisubiri hesabu kamili zimechangishwa zaidi ya shilingi milioni 257
Mpaka hafla hiyo inahitimishwa hii thread pia ilikuwa na wachangiaji 257 (There are currently 257 users browsing this thread. (94 members and 163 guests)

What a coincidence!!! Peoplesssssss!!
 
Malengo ni Bilioni 5, leo kwa hesabu ya mpaka sasa huku tukisubiri hesabu kamili zimechangishwa zaidi ya shilingi milioni 257 Mpaka hafla hiyo inahitimishwa hii thread pia ilikuwa na wachangiaji 257 (There are currently 257 users browsing this thread. (94 members and 163 guests)
kama tungetangaza vizuri hili zoezi naamini tungepata zaidi ya million 700 kwa leo tuu... ila it is a good begining.... next time tutangaze one month before ili wenye vimshahara vya kuunga tujiandae mwisho wa mwezi
 
Aiseee baba yangu mi ningeshauri m4c ingerushwa moja kwa moja na super sport 3 dstv manake vibanda vyote vya mipira wangeonesha kwa wingi
 
next time MC awe Godwin Gondwe na Salimu Mwaimu, huyu wa leo amezubaa, hajui hata mbunge wa viti maalum ni yupi anamuita kamanda Lema mbunge wa viti maalum.
 
Muendelezo wa kuchangia m4c ni mzuri isipo kuwa maandalizi ya shughuri hayatakiwi kufanywa kwa kushtukiza kama hii. Huu ulitakiwa kuwa hata mpango wa majuma matatu au hata mwezi, kuiandaa shughuri kuwa katika viwango vya uhakika kuanzia uandaaji, ma mc wabobezi na kuhamasisha sana kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Lakini lingine kubwa next m4c contributions gathering iwe inatoa mrejesho wa kilicho changwa na jinsi kilivyotumika. Mfano leo wangeweza ku breaka down mapato ya m4c Arusha na matumizi yake then impact yake kwa ujumla kwenye chama.

Muhimu.
Waziri kivuli wa fedha ambae pia ana cheo cha unaibu katibu mkuu kutokujihusisha na mambo ya chama kwenye fund rising ambayo naamini ni moja ya mambo muhimu na miongoni mwa majukumu ya pamoja ni dosari kubwa kwake. Hawezi kuwa raisi kwa kuota kwenye vyombo vya habari! Apambane ili chama kiopate fedha kifike kule anakota azipate kura za uraisi.
 
Joyce Mukya (Mb) alikuwa anaboa, kama alijua anakuja kwenye hiyo shughuli, alipaswa awe ameshaongea na hao aliokua anawaita "watu wangu" wa arusha, na pale alitakiwa aje kuwakilisha tu. It was like amekurupuka hivi. Otherwise, mengine ni ya kawaida tu
 
Hii inaonesha Chadema imeanza kuchokwa tokana na kutokuwa na mipango mizuri. Mara leo Morogoro, mara dar, mara Ulaya.
 
Back
Top Bottom