Tarnishing the name of Tanzania- US Researchers!

MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Jun 24, 2007
4,517
1,367
Wana JF,
Nimeona hii makala Majira ya jana over negative portray ya Tanzania kwa mwanamke wa US aliyepata PhD kwa data alizokusnya Bagamoyo. (http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=sayansi&habariNamba=4822).
My take;

1. Kuna mtu anawafahamu zaidi kwa undani zaidi Laura Edmonson- Profesa katika chuo kikuu cha Florida State na Thomas Riccio ambae nae ni Profesa katika Chuo Kikuu cha Texas –Dallas? Ili asaidie kuverify na kutoa mwanga zaidi habari hizo za Majira hapo juu?

2. Leo ni 46 years tangu tuwe huru- na watawala wetu wamekuwa kimya na kundelea kutoa vibali vya utafiti kwa Wazungu ambao leo hii wanatarnish good image of Tanzania. Ni taasisi gani ya serikali which monitors the conduct of research activities of hawa wageni- who bears responsibilities kama jina la nchi linakuwa tarnished?


3. Over 70% of findings from researchers conducted by West and America in Tanzania- they represent Tanzania so negatively! Je hakuna hata moja zuri wanaloliona? Should research findings represent negative view always? Je utafiti wao hulenga tu kufatuta mabaya?

4. This is not fair- Tanzania has many good things to offer- and we must fight- kwa nguvu zote, attempts to portray our beautiful country negatively!

Naomba kuwakilisha!
 
Makala yenyewe ni hii hapa:

taaluma ya kabwela: Maprofesa ‘feki’ wa sanaa

Habari Zinazoshabihiana
• Je, kigezo cha shahada ya Chuo Kikuu ni muhimu kwa mwandishi? 13.04.2007 [Soma]
• Mfumo huu wa elimu ubadilishwe kuepuka ubabaishaji 25.10.2007 [Soma]
• Nini kiliua kipindi cha Mambo Hayo? 14.10.2007 [Soma]

Katika makala zilizotangulia niliongelea mambo yanayoweza kulegeza nafasi ya sanaa Tanzania. Ni ukweli usiopingika kuwa kwa hali ilivyo sasa hivi, si ubora bali ni nguvu ya soko ndiyo inayofanya bidhaa iuzike. Hii inamaanisha kuwa kuna kila dalili kuwa ubora wa kazi ya sanaa utakuwa si kitu muhimu tena, bali nguvu ya soko. Baada ya muda mfupi, kutakuwa hakuna tofauti ya kazi bora na isiyo bora, mtaalamu na asiye mtaalamu. Sina nia ya kuwakatisha tamaa wasomi wa sanaa, ila hiyo ndio hali halisi. Binadamu wote tumeumbwa na tamaa, tamaa ya kuishi, kula na kulala vizuri. Katika tamaa hii hii mtu anaweza kufanya mambo mazuri au maovu ili kupata pesa. Pesa sasa ni kila kitu

Katika harakati hizi za kuhakikisha kuwa fweza inaingia mifukoni, ujanja na ubunifu ndio unaotumika zaidi. Na anayeweza kuwa mjanja, hata kwa kuongopa, huweza kuwazidi wenzie, na ukweli ukaonekana uongo na uongo ukawa ndio ukweli. Katika kufundishwa kwangu sikuwahi kuamini kuwa profesa anaweza kuandika uongo, yaani uongo uongo kabisa. Sasa ni bahati kubwa sana hawa maprofesa wanaoandika uongo safari hii wanatoka Marekani na wafuasi wake, na hao ndio wanajulikana kama wataalamu wa sanaa za maonyesho Tanzania (Tanzanian theatre/performing arts experts). Huko kwenye miradi ya UKIMWI, vijana, maji, afya, sijui miundombinu ndo usiseme.

Kutokana na ukarimu wetu wa kitanzania, tunawakubali kuja kusimamia miradi na kutukagua kama tumefanya vizuri au tumekula hela zao. Wanakuja kuranda randa kwenye mahoteli kwa jasho letu sisi tunawaita wataalamu na kuwalipa dola kibao, kisa ‘mzungu’. Lengo langu si kupandikiza mbegu ya ubaguzi na chuki ila ni kumtaka mtanzania ajue kuwa hasaidiwi ila anaibiwa nguvukazi na rasilimali zake. Ubeberu una sura nyingi sana, na ni vigumu mtu kuweza kung’amua. Hawa wataalamu wengi wao wamefukuzwa makwao au hawakubaliki kwa tabia mbovu. Wengine hawana elimu hata ya kuwenza mtawala mtu wa kidato cha nne. Lakini, akishuka na ndege, ni mtaalamu, haya.

Katika pekua pekua yangu nimekutana nao wengi, ila leo nitaanza na huyu mmoja anayejulikana kama Laura Edmonson. Huyu kwa sasa ni profesa katika chuo kikuu cha Florida (Florida State University) Marekani. Mbali ya machapisho yake kadhaa, mwaka huu 2007 ametoa kitabu chake kinachoitwa Performing and Politics in Tanzania: The Nation on Stage ambacho ndio kilichonirusha roho zaidi. Nitajitahidi kutafsiri hiki ‘kiinglish’ kadiri ninavyoweza, ila kule ambako nitakwama nitaacha ili nisipotoshe maana.

Mbali ya kuchapisha kitabu (ambacho nitakichambua katika makala nyingine), huyu Laura ameandika makala mbalimbali kuhusu sanaa za maonyesho Tanzania. Katika makala yake “Saving Whiteface” in Tanzania: Intercultural Discomforts iliyochapishwa na jaridala Theatre Topics. Ameelezea kiundani jinsi alivyokuwa akipata unyanyasaji wa kijinsia toka kwa wanafunzi wa kiume wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo waliokuwa wanamtamani kingono yeye akiwa kama mtafiti. Pia anasema kuwa kwa vile yeye ni mzungu alikuwa akipapatikiwa sana na wanafunzi hawa wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo waliokuwa wanataka kuwa na uhusiano nae ili waende ulaya na hasa Marekani. Anasema pia ilikuwa ni kitu cha kawaida kwake kusalimiwa kwa nia ya kutongozwa kama msichana wa kizungu. Anasema, “the greetings had become overtly sexual; for example, I soon lost count of the times my palm was scratched when I shook hand. Pia anafafanua kuwa kutokana na ukweli kuwa yeye ni mzungu na anatoka nchi za magharibi zenye uchumi imara, anajigamba kuwa “marriage with mzungu was considered a way to fulfill the African rags-to reaches dream” (Edmonson 1999:36-37)

Wakati akiandika haya, Laura alikuwa anafanya utafiti wake kwa ajili ya shahada ya falsafa (PhD). Kutokana na utaratibu gani sijui, alipewa darasa la kufundisha katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo. Wakati akiwa anafundisha, anadai kuwa wanafunzi wa kiume walikuwa wanapambana kuona ni kwa jinsi gani wataweza kumpata. Na yeye anasema kutokana na kujua hilo na kwa vile hakuwa na mpango huo, aliamua kuvaa sketi ndefu ili kupunguza mifadhaiko ya wanafunzi hao “I sought to disrupt these sexualized expectations by dressing ‘appropriately’ in long skirts.”

Anaendelea kujieleza, kuwa ili kuhakikisha anapunguza kasi ya kutongozwa, aliamua kubuni/kutafuta mwanaume kutoka Dar es Salaam. “I also invented a mzungu boyfriend living in Dar es Salaam to discourage the entourage of male visitors to my room” Laura yeye anavyosema, ingawa alitumia kila mbinu ili kuweza kuwafukuzilia mbali vijana wa kitanzania waliokuwa wakimtaka kinono/kimapenzi, bado vijana hao waliendelea kushindana ili kumpata.

Laura haukukomea kwa kuwasema vijana wa kiume pekee, pia amewasema wasichana waliokuwa wanasoma Chuo cha Sanaa Bagamoyo (ambao pia walikuwa wanafunzi wake). Anasema kuwa ingawa wasichana hao walikuwa marafiki zake, lengo lao ilikuwa ni kuhakikisha usalama wa wanaume wao hasa msichana mmoja ambae alikuwa rafiki yake wa karibu. Hata hivyo alimtosa huyo kijana aliyekuwa anamtaka. Laura anakongo’oli hivi, “I learned later that through our friendship she hoped to intimidate her lover, who was one of my most frequent visitors, from making advances. Apparently, she did not expect me, the prurient girl, to refuse him”.

Anasema wakati akiwa anafundisha, kulikuwa na ubishi hasa uliokuwa unafanywa na wanafunzi wa kike kwa lengo la kumdhalilisha. Yeye kama mtaalamu wa sanaa za maonyesho anaamini zaidi katika kutengeneza wahusika wanawake ambao ni jasiri (imperialism feminism) ingawa wasichana hao waliendelea kupenda kuwa na uhusika wa kujidhalilisha (yaani wahusika wanaume kuwa ndio wenye nguvu). Katika kazi alizokuwa anataka kuzitengeneza Kinjekitile iliyoandikwa na Ebrahim Hussein ambapo wanawake hawaonekani zaidi ya mke wa Kitunda na binti yao. Laura aliamini huo mchezo hauna usawa na alitaka kuuwekea usawa (wa kijinsia). Anadai wakati wakijadili hayo, wanafunzi wa kike walikuwa wabishi sana na mara zote walikuwa wakiongea kiswahili kwa haraka ambapo alikuwa hawezi kufuatilia “yet my relationship with these female students was marked by tension and power struggle; two of them would react with condescension and resistance to the ideas I presented in the class, speaking so rapidly in Swahili that they knew I was unable to follow”

Kazi hii ambayo asilimia zaidi ya 75 imekuwa akizungumzia matendo yake binafsi badala ya kilichomleta ambacho kwa tafsiri yangu ni tofauti na alichofanya, imejaa kauli nzito zenye kudhalilisha. Wakati anaandika haya kama nilivyelezea hao awali, alikuwa mwanafunzi wa Shahada ya Falsafa katika chuo Kikuu cha Texas Austin. Naomba niseme wazi, hao wanaoitwa wanafunzi (ambao amewataja) ni wasanii wanaofanya kazi zao za sanaa na wengi wemetoa mitizamo tofauti kabisa na maoni yake. Wengi wamepinga aliyoandika na wengine wameelezea tabia zake za ngono alizokuwa akiziendekeza. Huu ni mjadala tete, kwani kila mtu sasa anamrushia kesi mwenzie.

Kabla ya kuendelea kuchambua kazi zake nyingine kama vile National Erotica: The Politics of “Traditional” Dance in Tanzania, Sexing the Nation na kadhalika, ni vizuri nieleze dukuduku langu kuhusiana na hawa watafiti wanaokuja kutafiti Tanzania na sisi kwa ukarimu wetu tunawakaribisha, sebuleni wanaingia mpaka vyumba vya kulala.

Kwanza wengi waokuja na kazi zaidi ya moja, na huwa wanatumia vibali vya utafiti kutimiza kazi zao hizo nyingine. Pili watafiti hawa wamekuwa wakiandika kulingana na mitizamo yao ambayo ni ile ile ya kuendeleza nguvu ya ubeberu na ukoloni mambo leo. Tatu, mtu anakaa hotelini miezi miwili au mitatu, akiondoka ni mtaalamu wa sanaa za maonyesho Tanzania. Nne, wengi wao hawapendi kuandika upande wa pili wa shilingi, (mazuri na mafanikio hayaandikwi). Tano, wakishaandika ‘huu utumbo’ nchi zao zinawarudisha sasa kama wataalamu ‘experts’ wa kuja kutufundisha kucheza sindimba, lizombe, mkwaju ngoma na segere. Kwa kuwa sasa hivi hawajapata uwezo wa ‘kutwanga’, kumuvuzisha ‘ngwasuma’ , ‘kukwatua mgongo mgongo’ na hawawezi kuimba taarab, wanabakia kusema hizo ni tamaduni za muziki ambao kama si wazungu zisingepata umaarufu.

Kitu kinachostaajabisha ni kuwa, wakati wote wamekuwa waliandika kwa ujasiri wa ajabu mambo ambayo si tu yanawadhalilisha wasanii, pia na viongozi wao. Kwa mfano kuna huyu anayeitwa Thomas Riccio ambae nae ni profesa (katika Chuo Kikuu cha Texas –Dallas) na anajiita mtaalamu wa sanaa za maonyesho Tanzania, Afrika na Asia. Anadai pia alishawahi kufundisha Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonyesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1999 (darasa ambalo nilikuwepo ila sikumbuki kama alifanya hizo mbwembwe alizoziandika). Ukisoma The Drama Review, 45 Tanzanian Theatre: from Max to Market Theatre (T169. 128-152) ya mwaka 2001, anasema kutokana na umasikini wa Tanzania ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuweza kuishi. Hali ikiwa mbaya namna hiyo, thamani ya hela ya Tanzania inazidi kushuka. Noti za Tanzania ambazo zimejazwa picha ya rais Benjamin Mkapa si chochote si lolote nje ya mpaka wa Tanzania. “Its currency the shilling (which is emblazoned with the photo of the current president, Benjamin Mkapa) is not convertible and is essentially worthless outside of Tanzania” (Riccio 2001:130)

Hata mtoto mdogo wa Tanzania ukimuuliza kuhusu hili la noti na picha ya raisi atakupa jibu sahihi zaidi kuliko huyu profesa Thomas Riccio. Huyu profesa ameandika makala nyingi zenye chuki juu ya tamaduni za kitanzania. Machapisho mengi yamekuwa yakifadhiliwa na mashirika mabalimbali toka nchi tajiri zilizonendelea. Lengo kubwa ambalo limejificha ni kuonyesha kuwa ingawa mambo yanafanyika hakuna maendleeo yanayofanywa na watanzania. Hii ni kusaidia kufagia njia ya wao kuja kama constulants na kujipakulia malipo kama vile Tanzania hakuna watu wenye ujuzi kama wao. Wengi wao wanaamini njia moja wapo ya kupata kazi ni kuharibu ili upewe kazi ya kujenga na kurekebisha.

Ni vyema taasisi zinazohusika na kutoa vibali vya utafiti kwa wageni, wakaangalia upya mfumo mzima wa utoaji vibalai. Ni vizuri hawa wataaalamu tunaowakaribisha kufundisha watoto wetu wakachunguzwa kabla (kama wao wanavyochokonoa CV zetu ukitaka kufundisha watoto wao). Yaliyotokea kwa Sauper, tunajua wenyewe. Katika nchi za ulaya, ni vigumu sana kuonyesha filamu au video zinazoashiria maendeleo, kujitawala na kujikwamu kiuchumi. Filamu kama Sarafina, Catch the Fire na nyinginezo, hazionyeshwi kwani zinaonyesha wazi nguvu ya ushindi ambao waafrika wanayo. Kwa upande mwingine, filamu zinazopigiwa upatu ni zile zinazoonyesha Afrika na viongozi wao ni ‘choka mbaya’, The Blood Diamonds, Hotel Rwanda, The Last King of Scotland na nyinginezo. Filamu itaakayoonyeshwa ni ile ambayo mzungu ameweza kuwa shujaa na kumsasidia ‘mjinga’ mwafrika kuerevuka.

Nitaendelea kujadili hoja hii katika makala nyingine. Wengi wetu tungependa kufahamu ni nini kilichoendelea kati ya Laura Edmonson na wanafunzi wake baada ya yeye kumaliza utafiti wake katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo na Tanzania kwa ujumla. Wengi wa wasanii wanaelewa fika, ‘alikula matapishi yake’. Napenda kuomba nguvu ya pamoja katika kupambana na hawa maprofesa ‘feki’ wanaojiita wataalamu wa sanaa ya Tanazania. Hubert Sauper (Darwin’s Nightmare), James Watson (Watu weusi tuna akili ndogo) wako wengi na wafuasi wao wametapakaa dunia nzima. Wasanii wa Tanzania wasikubali kuendelea kutumikishwa sio tu na wanasiasa hasa na watafiti ‘uchwara’. Sio kila kinachong’aa ni dhahabu.

©Vicensia Shule 2007

Mwandishi wa makala hii ni msanii wa sanaa za maonyesho. Kwa maoni na mapendekezo unaweza kuandika kupitia vicensiashule@hotmail.com
 
Mbona makala inayoelezea mambo ambayo yana exist. Ishu labda kapata PhD kiulaini. Ila mambo mengine naona kuna ukweli mwingi. Si tulikuwa tuanaongelea vijana wa Mombasa na Zanzibar na vibibi wa kizungu wanaokuja likizo nchi zetu?
Ukweli sometimes unauma, kuna tofauti ya kuwa Patriotic na kuwa Realistic.
 
MzalendoHalisi:
Niliposoma 'posting' yako hapo juu nilianza kuwa na wasiwasi wa kuwepo 'mapanki' mengine.

Baada ya kusoma hiyo makala ya majira, sina wasi wasi tena na aibu ya taifa uliyoizungumzia wewe. Kwa kiasi kikubwa, mwandishi wa makala katika gazeti la majira ameyajibu maswali mengi.

Kwa kuanzia tu, sio kweli kwamba kila mzungu anayekuja kufanya utafiti hutupaka rangi mbaya waTanzania, au waAfrika.

Ni sahihi pia ukisema kuwa baadhi ya hao watafiti huwa wamekwishachukua hitimisho la matokeo ya tafiti zao hata kabla ya utafiti kufanyika.

Sioni taabu kwa huyo Laura kuwalalamikia vijana kwa kumtaka, hata kama ni kutaka pesa yake. Sioni tatizo kabisa na hilo; kama nisivyoona tatizo lolote, kwa hao akina dada kulinda vilivyo vyao kwa nguvu zote. Tunajua haya ndio yaliyoko huko USA aliko huyo Laura. Hiyo picha aliyoitoa haina tofauti yoyote na mahusiano yao, kati ya weupe na weusi wa huko huko kwao.

Kwa bahati mbaya sana, mwenye aliye nacho (yaani pesa) ndiye mwenye usemi katika dunia ya leo. Kwa kadri tutakavyokuwa tunawategemea hawa wataalam kutoka nje waje watufanyie mambo yetu, tutegemee na haya ya kusemwa vibaya.
Jambo linalotia matumaini kidogo sasa ni kwamba hata sisi tumeanza kuwajibu, hata kama ni kwa kidogo - mfano ni huo wa huyo mwandishi ya hiyo makala ya majira. Tuendelee kujenga huu utaratibu wa kujibu mapigo, ili kuweka upande wa pili wa shilingi.

Habari hiyo imenikumbusha habari ya mama mmjoja wa kizungu aliyekuja hapo chuo kikuu cha Dar es Sallam katika miaka, nadhani ni ya 80 hivi. Yeye alitaka kuwakomboa wanawake wote wa kiTanzania kwa kuwepo kwake pale miaka hiyo michache tu. She was utterly frustrated; hata hao akina dada walimwona mtu mpuuzi.
 
Celebrity culture si imeanzia kwao? Aliye nacho hutukuzwa zaidi. Hata hao vijana wa Afrika walikuwa wanataka kukamilisha malengo yao ya kupanda pipa kwenda USA bila matatizo sawa na wao wanavyopapalikia wenye nacho ili kuondokana na umaskini.

Mkuu usiogope watu wanaposema, wakati mwingine ndio tutajua mabaya yetu lakini pia yatatufumbua macho ili tupambane kwa hoja pale wanapokuwa na hoja finyu.

Nikitaka kuandika kitabu changu juu ya ujinga wa Wazungu, kuna mengi mno ya kuandika lakini pia nikitaka kuwasifia yapo mengi mno ya kuyasema. Inategemea motive yangu ya kuandika ni nini. Kwa West ukiandika kusagia Afrika, una nafasi ya kupata wasomaji wengi kuliko ukisifia.

Huyo dada anatengeneza pesa kupitia watu ambao si ajabu kila siku alikuwa anawaita ni marafiki, ndio maisha ya West, urafiki sio wa kudumu, kukiingia interest basi urafiki huwekwa pembeni.
 
Mzalendohalisi,
Nimesoma hii mada yako lakini naona mawazo yangu ni tofauti kabisa na yako. Kwanza lazima nikubali kwamba sijasoma yote yaliyoandikwa na hao maprofesa, lakini ulichotuandikia hapa sina tatizo nacho. Kama huyu mama alikuwa anasumbuliwa na wanaume, ana haki ya kusema hivyo. Na huyu mwingine aliyesema kwamba pesa yetu haina thamani kubwa, amesema ukweli. Sioni tatizo lolote na mambo uliyosema wameandika. Mengine zaidi ya hapo sijui. Labda unaweza kutupa mifano mingine.

Mimi nina tatizo na "academic freedom" Tanzania. Academics lazima wapewa uhuru wa kuandika wanachotaka hata kama hatukubaliani nacho. Acha wazungu waandike wanachotaka, ni wajibu wetu sisi wenyewe kuandika tunachoona ni ukweli. Maprofesa wetu waanze kuandika na wapunguze kwenda UDASA.

Pili, sio rahisi kupata kibali cha kufanya utafiti Tanzania. Hembu angalia cost ya kufanya utafiti Tanzania: http://www.costech.or.tz/research%20clearance.htm. Huu urasimu na cost unafanya watu wengi washindwe kufanya utafiti Tanzania. Kuna ambao wanakuja kuandika pumba, lakini kuna wengi wanaotaka kuandika mazuri, lakini wanachoswa na hiyo system. Nchi za ulaya, marekani, South Africa n.k. hamna haja ya kupata kibali cha utafiti, isipokuwa unapochunguzi baadhi ya vitu ambavyo bado vipo classified. Unaweza kwenda hapo London ukaingia archive ya serikali kufanya utafiti ukaandika chochote unachotaka; wapo wataokarika na wapo wataofurahi. Lakini maisha yanaendelea.

Tukianza kukataza watu waandike tusichopenda, tunaingia kwenye barabara itayotupeleka pabaya. Waliokasirishwa na mambo wanayoandika wazungu, wachukua nafasi hiyo kuandika book reviews, articles, na vitabu vinavyopinga wanachosema na kuchambua pumba wanazoandika.
 
Back
Top Bottom