kizazi kipya
JF-Expert Member
- Jul 21, 2010
- 327
- 62
Huu ni upuuzi.Bado wana zile za kulindana,mbona hajaongea chochote kuhusu hatua zilizochukuliwa au zinazochukuliwa dhidi ya wauaji?Uchunguzi unaonyesha walipigwa risasi mgongoni jambo linaloonyesha walikuwa wanakimbia.Kwa nini nahodha anajaribu kulinda udhalimu huu.Haoni kwamba kutochukua hatua kutasababisha polisi wapate kiburi cha kuendelea kuua raia?Nahodha aueleze umma wa watanzania hatua zitakazochukuliwa juu ya polisi waliofanya mauaji hayo,ni wazi wanafahamika.Au intellijensia ni kwa wanasiasa wa upinzani pekee?