Taratibu za kufuata ili kupata TIN Number

Nenda kasajili jina la biashara Brela kwanza wakishakupa Cheti, unakipeleka TRA ukiwa na nakala ya mkataba wa ulipopanga ofisi ya biashara yako na vitu vingine kadhaa wanavyovihitaji. Watakupatia TIN

Kisha unaambatanisha Copy ya TIN, Cheti Cha Usajili ( Brela ), Mkataba wa eneo la ofisi, Copy ya kitambulisho Nk. vyote hivi unaenda navyo kwa afisa biasha katika wilaya husika huyu ndiye atakayekupatia Leseni ya Biashara.

Nimejaribu kukumbuka kumbuka, ila uwe tayari na usumbufu wa kipuuzi kutoka kwa watumishi wa umma.

USITOE WALA KUPOKEA RUSHWA TAFADHARI.
 
HABAR WAKUUU,


Nnaomba msaada kwa anaejua ni njia zipi nizitumie kupata Tin number ya TRA kwa ajili ya kampuni, nmesajili kampuni brela la usambazaji wa vifaaa, nnahitaj nipate TIN ya mlipa kodi ndo nianze operation,,, msaada kwa mwenye ujuza tafadhar
 
Kama ni kampuni ni hivi,
1. MOA
2. Registration
3. Extract
4. Mkataba wa mahala pa biashara ulioshuhudiwa na wakili
5. Utambulisho wa shareholders
6. Barua ya utambulisho wa serikali za mitaa pale unapofungua biashara, yaani ulipopanga
7. Kama ni pako uwe na uthibitisho
8 Picha mbili zilizogongwa mhuri wa mwenyekiti wa serikali za mitaa
9. Jiandae kulipa kodi ya mwaka huu yaani unaweza kukadiriwa 150K na kutakiwa kulipa nusu.
10. Usumbufu wa hapa na pale
 
Kama ni kampuni ni hivi,
1. MOA
2. Registration
3. Extract
4. Mkataba wa mahala pa biashara ulioshuhudiwa na wakili
5. Utambulisho wa shareholders
6. Barua ya utambulisho wa serikali za mitaa pale unapofungua biashara, yaani ulipopanga
7. Kama ni pako uwe na uthibitisho
8 Picha mbili zilizogongwa mhuri wa mwenyekiti wa serikali za mitaa
9. Jiandae kulipa kodi ya mwaka huu yaani unaweza kukadiriwa 150K na kutakiwa kulipa nusu.
10. Usumbufu wa hapa na pale

Mbona mambo ni mengi hivi?

MOA inatosha kabisa.
 
Me nilipotaka kuitoa gari yangu bandarini nilikwenda TRA na kupata TIN ndani ya Dk 40 Bure Dodoma. Chakufanya nenda TRA utapewa form ya kujaza, baadae utapigwa picha na kusaini digitally. Then you wait. kama watu ni wengi sn watakukwambia uje kuchukua muda gani.

Utaratibu ndio huo. Ila kuhusu wewe kwa vile ni kampuni utahitaji uwe na viambata pia kama alivyokushauri Hossam hapo juu.
 
Habari wadau,nina duka dogo nahitaji kujua taratibu za kupata tin namba na leseni,duka lina wiki sasa naishi dar tabata.Katika hilo naomba nifahamishwe pia
gharama zake na wapi Huduma hizo nitazipata.
 
Nenda ofisi za TRA utapewa utaratibu.Kusajili TIN ni bure mkuu wangu.
 
Nami nahitaji sana tin number,TRA niende na vitambulisho gani ili niipate?
 
Unaenda TRA kuna fom unapewa unajaza then unapigwa pastpot unawekwa kwenye stistmu zao unalipia elfu kumi CRDB thn kesho yake waenda na risit ya bank unapewa tn no yako na lesen
 
Mkuu Tin ni buree Hakuna Cha kwenda kulipia Benk.
Nenda ofisi Za TRA iliyo karibu Yako. Naomba kuonana Na Afisa anayeshugulikia mambo Ya Elimu Kwa walipa kodi atakupa majibu sahihi zaidi.
 
Back
Top Bottom