Taqwa Bus kutoka Dsm to Bujumbura

pole sana mkuu kama mtapita salama K9 Mungu atakuwa kawa nusuru na dhahama..
 
Kwa kawaida mabasi ya taqwa yanajaza sana mizigo had kwenye siti na hii inatokana na udogo wa but wa basi hizi. Mara nying wanapanda wafanya biashara na kwa kawaida hawana haraka ya safari, hebu angalia taqwa za dar to lusaka,dar to lubumbashi n.k. Nakushauri usipande tena haya mabasi kama unaharaka! Safar njema
 
Msije panda gari hili. Ni bovu sana, toka saa 12 alfajiri sasa ndio tunaingia Dodoma.
Limejaza sana mizigo ndani, korido haipitiki.
Polisi wanaliona na tumeongea, lakini hamna hatua walizochukuliwa wahudumu wa basi hili.
Polisi wamesema tuendelee na safari, dereva atalipia makosa yake akiwa anatoka Bujumbura.

Pole sana mkuu, kuna basi lingine la dar-mwanza linaitwa "Mastercity" ni kimeo kabisa linatembea siku mbili kutoka dar 2 mwanza, halafu ukifika pale ubungo wanadai ni luxury bus so unalipishwa 45,000/= halafu ukiliona basi lenyewe lazima ulie..!
 
Nimewahi kulipanda tokea Nzega-dar nilichoka make ilikuwa jioni saa12 na usafiri taabu njiani na nawahi kazini,nilisimama tokea Nzega-Mor.Limepakia wanyaru na wana roho mbaya kinyama,hapendi hata umsogolee na ukijitikisa tu wanakutusi kwenye kinyaru,sitakuja kulipanda tena basi kama daladala...nilibahatika kufika dar saa6 ksho yake niko hoi taabani

wabongo mmezidi umama yaani wewe wanyaru wanakutukana kwenye nchi yako unamtizama tu?
 
Back
Top Bottom