BornTown
JF-Expert Member
- May 7, 2008
- 1,716
- 481
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule, anasikitika kutangaza kifo cha Bw. Aziz Sheween, Afisa Mambo ya Nje Mkuu Daraja la I katika Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, kilichotokea huko Riyadh, Saudi Arabia. Taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuja nyumbani kwa mazishi zinaendelea na pindi zitakapokamilika taarifa rasmi itatolewa. Tunawapa pole familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki, watumishi wa Wizara na wote walioguswa na msiba huu mzito.
Source:www.foreign.go.tz
Source:www.foreign.go.tz