TANZIA: Mwenzetu NJEE amefariki dunia Leo Alfajiri

Status
Not open for further replies.

Reserved

JF-Expert Member
Sep 16, 2008
747
68
Kwa masikitiko makubwa kabisa nachukua fursa hii kuwatangazia Members wote wa JF kuwa kuna member mwenzetu kwa ID user name ya Njee, amefariki leo alfajiri baada ya kupatwa na mstuko wa Moyo!

Kupata profile yake tembelea - Njee (Senior Member)

Njee alijiunga Jamiiforums Disemba 28, 2012 na kuitumia Jf mwisho Mei 25, 2013 saa 11:31 jioni.

Member huyu alikuwa ni mwanaume mwenye familia yake.


MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI

========
Msiba upo nyumbani kwa marehemu maeneo ya Ukonga Mombasa,
Shughuri za Misa itafanyika kesho saa 5 Asubuhi hapa nyumbani, ambayo itafuatiwa na sadaka (Chakula).
Mchana ni kuaga mwili wa marehemu
Saa kumi safari ya kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Ifakara itaanza!

Kwa mawasiliano na MICHANGO unaweza kuwasiliana na mdogo wa marehemu: 0715 280 737
 
Pole kwa familia,ndugu,jamaa,marafiki na wanaJF wote,Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.Amina.Yafaa kujua msiba upo wapi na taratibu za mazishi zipoje ili kuwapa nafasi wanaJF ambao wapo karibu kushiriki pamoja katika msiba huu.
 
Yatosha msiba kuwa ni mawaidha kwa walio hai, mdau mwenzetu alipost juzi May 25 na leo hatunaye tena, ni ghafla mno nasi tujiandae kwa safari hii ya wote kwa kuenenda vyema tusijipe moyo kuwa tutatenda mema tukizeeka zeeka. Poleni sana wanandungu nasi wana jf wote kwa kumpoteza mwenzetu. Raha ya milele umpe eeh BWANA na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani.
 
Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe. Amen. Poleni sana wafiwa, Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kikuu cha majonzi. Poleni sana wanaJF wenzangu.
 
Mungu awafariji wafiwa..

Inaonekana hii ndiyo ilikuwa post yake ya mwisho hapa JF...tar 21 Mei 14:52

Ttatizo ccm wenzangu mnatumia lmg kuua swala. Haya mnazuia bajeti isisomwe mbona basi tena ilishatoka yote jana hiyohio?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom