Tanzia: Msanii YP wa kundi la 'Wanaume TMK' afariki dunia

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
51,662
68,617
YP.jpg


Ebwana namsikiliza Zembwela hapa kwenye supamix ndio amesema.

YP ni msanii wa wanaume TMK aliyeimba kwenye Dar mpaka Moro akishirikiana na Temba na Chege au kwenye wimbo wa twenzetu akiwa na Temba na Chege.

Msanii wa kundi la Wanaume Family “YP” amefariki Dunia jana usiku Hospitali ya TMK ambako alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa muda mrefu lakini hali ilikuwa mbaya katika wiki mbili kabla ya kifo chake.

Meneja wa kundi la TMK Wanaume Family amedhibitisha kifo hicho na msiba hupo Keko nyumbani kwa baba yake.

Msanii YP aliimba nyimbo kadhaa kama Ulipenda Pesa’, ‘Pumzika’, ‘Shemsha’ na nyimbo nyingi za TMK Wanaume Family kama ‘Twende zetu’ ya Chege, ‘Dar mpaka Moro’, ‘Kichwa kinauma’,

Chanzo: Mtandao ya kijamii
 
inasemekana akiugua kifua kikuu kwa mda mrefuu...tusubiri wenye taharifa zaidi.
 
Ebwana namsikiliza zembwela hapa kwenye supamix ndio amesema.

Yp ni msanii wa wanaume TMK aliyeimba kwenye dar mpaka moro akishilikiana na temba na chege au kwenye wimbo wa twenzetu akiwa na temba na chege.
omg! YP is gone! R.I.P man...
 
inasemekana akiugua kifua kikuu kwa mda mrefuu...tusubiri wenye taharifa zaidi.
Nimekaa na YP mara kibao na ingawaje sikuwahi kuhisi kwamba anaugua kifua lakini sasa ndo unanifungua macho... ni kweli alikuwa na dalili zote za mtu mwenye matatizo ya chest.
 
Yp ni msanii wa wanaume TMK aliyeimba kwenye dar mpaka moro akishilikiana na temba na chege au kwenye wimbo wa twenzetu akiwa na temba na chege.
Halafu kama kumbukumbu zangu zipo sawa, nadhani hata ile pini ya Y-Dash waliimba wote sema ndo hivyo tena... cjui inaitwa Hamisa ile, manake dah, long time!
 
Habari ambazo bado hazijathibitishwa, ni kwamba msanii aliyeunda kundi la T.M.K WANAUME FAMILY amefariki dunia. Sababu za kifo chake hazijajulikana bado. Nikipata taarifa zaidi nitaendelea kuwajuza. APEPE.
 
Tetes ni kwamba msanii wa bongo frever YP nikweli? mlioko temeke mtujuze,na alikuwa anaumwa nini!

Souce-mitandao ya kijamii.
 
Back
Top Bottom