Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANZIA: Msanii Sajuki afariki dunia

Discussion in 'Celebrities Forum' started by C.T.U, Jan 2, 2013.

 1. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2013
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,522
  Likes Received: 687
  Trophy Points: 113
  Msanii Juma Kilowoko (SAJUKI) amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu.

  Sajuki kama ambavyo anajulikana na wengi kwa sinema zake za kashkash alikuwa akiugua maradhi ya muda mrefu mpaka kufikia hatua ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi (Ref: http://www.jamiiforums.com/celebrities-forum/244623-jamani-inasikitisha-hali-ya-afya-ya-sajuki-mme-wake-wastara.html )

  Sajuki ambaye ameacha mjane ambaye pia ni msanii aitwaye Wastara ambaye ni mlemavu wa mguu mmoja ambao ulisababishwa kwa kupata ajali mnamo mwaka 2008 siku chache kabla ya ndoa. Hata hivyo Sajuki aliamua kumuoa hivyo hivyo kwani alikuwa ameshapeleka posa kwa kina Wastara.

  Tukio hilo liligusa hisia za watu wengi na kumchukulia Sajuki kama shujaa na mwanaume mwenye mapenzi ya kweli kwa kitendo hicho alichokifanya.

  Mwaka 2011 haukuwa mzuri kwa Sajuki kwani ndio mwaka ambao maradhi yaliyomsumbua muda mrefu yalipamba moto

  Inajulikana kuwa Sajuki aliumwa na kufikia kipindi cha kudhoofu mwili wake kitu kilichopelekea wasanii wenzake na watu wengine waanzishe mchango wa kumchangia Sajuki (Ref: http://www.jamiiforums.com/celebrities-forum/261161-jamani-tumsaidie-msanii-sajuki.html ).

  Waasanii, wanasiasa, wananchi walifanikisha zoezi hilo na kumfanya aweze kwenda India kwa matibabu zaidi.

  Alirudi na kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo lilileta nyuso za furaha na amani miongoni mwa watanzania (Ref: http://www.jamiiforums.com/celebrities-forum/287965-picha-sajuki-shavu-dodo-sasa-mungu-mkubwa.html ).

  Hata hivyo alikuwa hajapona sawa sawa na alikuwa anajiandaa kurudi tena India kwa matibabu zaidi.. na hii alikiri kwenye kipindi cha 'Mkasi' kinachoendeshwa na kituo cha televisheni cha EATV.

  Sajuki ambaye ni mngoni ameshacheza maigizo na filamu na wasanii wengi karibia wote wenye majina hapa Tanzania.

  Sajuki kwa kusaidiana na mkewe walifungua kampuni ya productions kwa ajili ya filamu (movies) za hapa hapa nchini.

  Bwana ametoa, bwana ametwaa jina lake lihimidiwe


  Source: ITV
   
 2. J

  Jaslaws JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2013
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 3,823
  Likes Received: 310
  Trophy Points: 83
  Kama heading inavyo someka japo kwangu bdo ni tetesi ila kama kuna mtu mwenye taarifa kamili nadhani atasaidia kutuhabalisha.
   
 3. kaburu mdogo

  kaburu mdogo JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2013
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 330
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 18
  nipo hapa nyumbani naskiliza radio na mtanagazaji anatangaza kuwa muigizaji wa siku nyingi sajuki amefariki dunia leo asubuhi kutokana naradhari yaliyokua yanamsumbua.amefarikia katika hospital ya muhimbili.
  chanzo ni radio 88.5 fm
   
 4. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2013
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,405
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  jamani sajuki
   
 5. chris Juve

  chris Juve Member

  #5
  Jan 2, 2013
  Joined: Dec 29, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  R I P Sajuki
   
 6. J

  Jaslaws JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2013
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 3,823
  Likes Received: 310
  Trophy Points: 83
  Nasikia kafa,rest in peace arif.
   
 7. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2013
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,932
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  R.I.P, umeteseka sana
   
 8. Headless Person

  Headless Person JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2013
  Joined: Nov 30, 2012
  Messages: 307
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Who is Sajuki?
   
 9. magistergtz

  magistergtz JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2013
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 282
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  Kama ni kweli, R.I.P Sajuki
   
 10. b

  bogota the king Senior Member

  #10
  Jan 2, 2013
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  RIP sajuki
   
 11. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2013
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,849
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Bora apumnzike kwa amani Sajuki.
   
 12. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2013
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,579
  Likes Received: 317
  Trophy Points: 83
  RIP SAJUKI pole kwa ndugu na jamaa
   
 13. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2013
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Rip sajuk mbele yako nyuma yetu!!
   
 14. b

  bogota the king Senior Member

  #14
  Jan 2, 2013
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni true! Mm niko hapa! Amefariki leo alfajiri! RIP
   
 15. Ishina

  Ishina JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2013
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  Msanii wa bongo movie ambaye alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda sasa, amafariki dunia katika hospital ya taifa ya muhimbili. R.I.P Sajuki
  Source: power breakfast - clouds fm
   
 16. T

  Thando Senior Member

  #16
  Jan 2, 2013
  Joined: Jan 1, 2013
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenyenzi Mungu mrehemu mja wako
   
 17. Headless Person

  Headless Person JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2013
  Joined: Nov 30, 2012
  Messages: 307
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu ampumzishe mahali anapostahili.
   
 18. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2013
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,718
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 38
  RIP Juma Kilowoko a.k.a Sajuki
   
 19. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2013
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,522
  Likes Received: 687
  Trophy Points: 113
  He was sajuki
   
 20. Hayajamani

  Hayajamani JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2013
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 885
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 18
  Poleni sana
   

Share This Page