TANZIA: Mkurugenzi wa Mtandao wa WikiLeaks, MacFadyen(76) amefariki Dunia

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,783
Wasalaam,
Leo nimesikia kwamba mkurugenzi wa mtandao maarufu sana Wikileaks ambao kwa siku za karibuni umekuwa ukivujisha habari nyingi hapa duniani; hasa za uchaguzi wa Marekani amefariki dunia hii leo akiwa na umri wa miaka 76. Mpaka sasa chanzo cha kifo hakijafahamika.

Ikumbukwe kwamba ni takribani wiki moja sasa tangu Ubalozi wa Ecuador nchini Uingereza unyimwe mawasiliano ya kimtandao. Kwa bahati mbaya sana mle ndani ya ubalozo kuna mmiliki wa mtandao wa Wiki-leaks bwana Julian Assange. Kwa kipindi ambacho mtandao umezimwa hapo Ubalozi wa Ecuador nchini Uingereza marehemu bwana Gavin MacFadyen ndiye aliyekuwa anaongoza mtandao wa Wiki-leaks.

Mtandao wa Wiki-leaks umekuwa mwiba mchungu sana kwenye kampeni za Marekani. Mambo mengi ya siri ya mgombea Hillary Clinton yemevuja na kwa bahati mbaya siyo mambo mazuri sana. Tumejua dhahiri kwamba Marekani na Saudi Arabia ndiyo wafadhili wa ugaidi kule nchini Syria na Iraq; tumejua kwamba Hillary Clinton alipendelewa na chama chake dhidi ya Bernie Sanders; tumejua kwamba Hillary Clinton alipewa fedha nyingi na Benki ya Wayahudi "Goldman Sachs" ambapo Wamarekani wengi wameachwa gizani ni kwanini alipewa pesa nyingi mno.

Na kibaya zaidi imejulikana kwamba alikuwa hakubaliani na mpango wa OBAMA CARE.

Kikubwa katika wiki hii ni kile cha Wiki-leaks kutoa mawasiliano ya Barua pepe za siri za raisi Obama. Binafsi hata mimi walinishangaza, na hadi sasa baada ya Gavin kufariki ghafla leo sijajua kama Wiki-leaks itakuwa na nguvu kama mwanzo kwasababu Assange anasema bado ana mamlaka na mtandao japo hana mawasiliano kimtandao.

Wengi hawajayaamini haya maneno lakini kifo hicho kimestua na kuumiza mioyo watu wengi hasa pale wanapomkumbuka marehemu kama mwanzilishi wa CENTRE FOR INVESTIGATIVE JOURNALISM ambapo wanahabari wengi wakubwa duniani wamejifunza hapo.

Kufa kufaana kwa upande mwingine kifo cha huyu bwana kimeleta neema fulani kwa makundi ambayo yalikuwa wahanga wa WIKI-LEAKS hasa Hillary, Saudi Arabia, Israel, CIA na viongozi wengi wala rushwa hapa duniani.

Kuna msemo tulikuwa nao toka mwaka jana Hapa JamiiFroums-Kuelekea Uchaguzi Tutasikia mengi, nikajua ni Tanzania tu kumbe hata dunia ya kwanza yapo.

=====================================

WikiLeaks director and founder of the Centre for Investigative Journalism Gavin MacFadyen has died at age 76. The cause of death is yet unknown. His ‘fellows in arms’ have flocked online to post their farewells, including WikiLeaks co-founder Julian Assange.
We are extremely sad to announce the death of Gavin MacFadyen, CIJ’s Founder, Director and its leading light,” the Centre for Investigative Journalism team wrote on its Twitter.

MacFadyen was a pioneering investigative journalist and filmmaker, who back in 2003 founded the Centre for Investigative Journalism (CIJ), an organization that helped break several major stories and has trained a number of prominent journalists.

He was a mentor and friend to famous whistleblower and co-founder of WikiLeaks Julian Assange, as well as the director of the publication. Paying tribute to their head, WikiLeaks published a post on the group’s Twitter account saying MacFadyen “now takes his fists and his fight to battle God.”

The post is signed “JA,” indicating that the phrase belongs directly to Julian Assange, with WikiLeaks claiming that, despite the whistleblower being deprived of internet access in his suite in the Ecuadorian embassy for a week now, he has been able to contact them and is “still in full command.

The CIJ team also published an address from MacFadyen’s wife and member of Julian Assange’s Defense Fund, Susan Benn, who described her husband as a “larger-than-life person,” with gratitude and respect.

He was the model of what a journalist should be… He spearheaded the creation of a journalistic landscape which has irrevocably lifted the bar for ethical and hard-hitting reporting. Gavin worked tirelessly to hold power to account.

“His life and how he lived it were completely in sync with the principles that he held dear and practiced as a journalist and educator – to comfort the afflicted and afflict the comfortable,” Benn wrote.

Recounting her husband’s achievements, she said he had produced and directed more than 50 investigative documentaries covering diverse and multiple countries and problems. She also noted that he had been banned from apartheid South Africa and the Soviet Union for his investigative work, and was also attacked by British Neo-Nazis.

In his professional career, MacFadyen shed light on topics like child labor, pollution, the torture of political prisoners, neo-Nazis in Britain, UK industrial accidents, Contra murders in Nicaragua, the CIA, maritime piracy, election fraud in South America, South African mines, as well as many others. He worked on investigative television programs for PBS’s Frontline, Granada Television’s World in Action, the BBC’s Fine Cut, Panorama, The Money Programme, and 24 Hours, as well as Channel 4’s Dispatches.

The cause of MacFadyen’s death has not yet been made public. In the original post from his wife Susan, she wrote that he had died from “a short illness,” but that line has now been removed.

Twitter has been full of tributes from his colleagues and like-minded people. Even the hacktivist organization Anonymous has spoken out.


Source: RT


CC: Bukyanagandi , Bowie , Apollo , maalimu shewedy, MSEZA MKULU
 
Mr Gavin MacFadyen amefariki lakini asilimia kubwa ya kazi yake amekamilisha hii si mara ya kwanza kufa ghafla kwa hawa Investigating Journalists.
Tarehe 18 June 2013 alifariki mwandishi wa mambo ya uchunguzi Michael Hasting kwa ajali ya gari ambayo mpaka sasa umeleta utata sana na imeonekana huyu aliuawa na CIA baada ya huyu mwandishi kuanza uchunguzi dhidi ya Mkurugenzi wa CIA John Brennan kwa mkakati mbaya wa shirika hilo dhidi ya waandishi wa habari wanaochunguza maovu ya serikali ya Rais Obama. Huyu mwandishi Michael alikuwa akipinga vitendo vibaya vya wa utawala wa Obama, chama cha democratic, udokozi wa taarifa za raia wa Marekani kupitia (NSA), na ya ukandamizaji wa waandishi wanaotumbua mabaya ya serikali ya Marekani. Michael alifanya kazi kama mwandishi huru huko Iraq na Afghanistan. Na alipokuwa Afghanistan aligundua maovu mengi yaliyokuwa yakifanywa na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi NATO General Stanley McChrstal, huyu General ilibidi ajiuzulu baada ya Michael kuanika maovu yake hadharani. Waandishi wa habari ambao siku zote wako mstari wa mbele kutoa taarifa za ukweli maisha yao yako hatarini. Kabla ya kukutana na kifo chake hicho Michael Hasting alikuwa na wasiwasi na maisha yake, alifariki akiwa na umri wa miaka 33 tu.
Mwenyezi Mungu aziwekee roho za hawa waandishi mahala pema peponi mpaka the Day of Judgement
 
Mimi siyo shabiki saana wa mtandao tajwa ila nathamini sana kazi zao.

Ninaimani mtandao huu ni taasisi so pengo litakuwepo hususani kwa kufa kwake lakini humo humo watainuka majemedari wengine wengi.

Imagine Assange yupo nje ya ofisi yapata sasa miaka zaidi ya mitatu ila mzigo unatemwa tu kila sekunde. Ndo umuhimu wa kujenga taasisi thabiti.
 
Mkuu Malcom, Julian Asange nae amekatiwa internet pale ubalozi wa Equador.

Lakini kwa ufundi wa ajabu abado anaendelea kurusha habari za uhakika.
 
So the Clinton's wanaendelea kufungua butcher!!!

Hawana Mchezo hata kidogo.
Na huko ubalozini sidhani kama Assange anaweza kuwa salama.
Ecuador wamesema wamezima mtandao kwasababu hawataki kufungamana na upande wowote ule,
Lakini ni lazima wametiwa mkwara na Marekani, sasa sijui hata kama Assange anaweza kuwa salama.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Mkuu Malcom, Julian Asange nae amekatiwa internet pale ubalozi wa Equador.

Lakini kwa ufundi wa ajabu abado anaendela kurusha habari za uhakika.

Mkuu Richard Ecuador wamekosea sana kwasababu anayerusha hizo habari siyo Assange bali ni Netherlands na kwingine.
 
Sijui Jamii Forums imejiandaa vipi na mamlaka mapya ya serikali ya kudhibiti uenezaji mawazo na habari yanayokuja na sheria mpya ya habari.
 
Sijui Jamii Forums imejiandaa vipi na mamlaka mapya ya serikali ya kudhibiti uenezaji mawazo na habari yanayokuja na sheria mpya ya habari.
Wamesalimu amri toka long time mkuu. Ile kauli mbiu ya where we dare talk openly unaiona tena? Hata wewe ukijipendekeza ukapost humu kindezi hawatachelewa kukuuza
 
Hawana Mchezo hata kidogo.
Na huko ubalozini sidhani kama Assange anaweza kuwa salama.
Ecuador wamesema wamezima mtandao kwasababu hawataki kufungamana na upande wowote ule,
Lakini ni lazima wametiwa mkwara na Marekani, sasa sijui hata kama Assange anaweza kuwa salama.


Malcolm if anything they'll prefer awe salama. They'd rather catch him alive than dead so they can squeeze him for information, seems he has a lot.
 
Malcolm if anything they'll prefer awe salama. They'd rather catch him alive than dead so they can squeeze him for information, seems he has a lot.

Agreed.
Majuzi ya tarehe 22 Wiki-Leaks waliandika Tweeter kwamba tarehe 23 wangetoa tamko kuhusu hali ya Assange.
Tukasubiri lakini tukapata tamko la Ubalozi wa Ecuador pekee, humo Ubalozini kinachoendelea anajua Mungu mwenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Agreed.
Majuzi ya tarehe 22 Wiki-Leaks waliandika Tweeter kwamba tarehe 23 wangetoa tamko kuhusu hali ya Assange.
Tukasubiri lakini tukapata tamko la Ubalozi wa Ecuador pekee, humo Ubalozini kinachoendelea anajua Mungu mwenyewe.


Kama ni hivi, usikute walipewa mkwara.
 
Biological weapon imemng'oa huyo.Ni mkakati wa yule shetani mkuu duniani na washirika wake.
 
Kuna watu ni wataalamu wa computer asee...hawa jamaa huwa najiuliza wana uwezo mkubwa kias gani aseee
Hicho ni kipaji mtu anazaliwa nacho.
Kwanza unaeza ona mtu anakipaji kama hivyo na anapenda kujifunza daima ili kupata ujuzi zaidi na zaidi anakuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana.

Heri kipaji kile kinachotumika na kuwa msaada kwa dunia ya wapenda haki na amani.

Hata akiuawa wanakuwa hawajafanikiwa kuua kile alichokuwa anakisimamia na kukipigania.
 
Back
Top Bottom