Tanzia: JK kafiwa na mtoto wa dada yake

Status
Not open for further replies.
Nimepita magomeni mapipa nyuma ya msikiti wa mchangani, rais wa Tanzania yu-katika hali ya majonzi ya kufiwa na dada yake, sifahamu marehemu akiitwa nani, mwenye taarifa za kina atujuze. POLE RAIS WETU, MUNGU AKUPE MOYO WA SUBIRA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MSIBA. RIP MAREHEM
,
Jogi, rekebisha, kwani msibani lazima ualikwe?. Wee si ulitakiwa upite, utoe pole, uulize msiba wa nani, ndipo uje uposti humu!.
Tunakupa habari bado hubadilishi, mode, please mtendeeni haki rais wetu!.

Mazishi ni saa 7:00 hii!.
 
lazima utakuwa kichaa wenzio waomboleza wewe wawaza kyeroro.ishia! Wacha tumalize kuzika.
 
Nimepita magomeni mapipa nyuma ya msikiti wa mchangani, rais wa Tanzania yu-katika hali ya majonzi ya kufiwa na mtoto wa dada yake, sifahamu marehemu aliitwa nani.

Mwenye taarifa za kina atujuze.

POLE RAIS WETU, MUNGU AKUPE MOYO WA SUBIRA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MSIBA.

RIP MAREHEM
Jogi, angalau, ila headline siyo lazima awe JK, aliyefiwa haswa ni Dada yake JK, kafiwa na mwanawe!.

Aliyefiwa na mwana ndie mfiwa zaidi, JK kafiwa mpwa, dada yake kafiwa na mwanae, najua big names makes news, lakini sio lazima kila news ndio mumtaje big name.

Ningekuwa mimi wewe ningeandika, "Dada wa JK, kafiwa na Mwanae!.
 
Naweza kukubaliana nawe kwan saivi nipo Magomeni katika matembezi yangu.Kuna gari za wizara zinaoneka kwenye maeneo ya Msikiti.
 
Nimepita magomeni mapipa nyuma ya msikiti wa mchangani, rais wa Tanzania yu-katika hali ya majonzi ya kufiwa na mtoto wa dada yake, sifahamu marehemu aliitwa nani.

Mwenye taarifa za kina atujuze.

POLE RAIS WETU, MUNGU AKUPE MOYO WA SUBIRA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MSIBA.

RIP MAREHEM

Kimsingi mimi sipendi matendo ya JK ila nafsi ya JK naipenda...pole JK Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu.....
 
Hiki kiswahili kinatupelekesha: hivi kweli kama JK kafiwa si tungeona msiba pale magogoni?!, kwanini usiandike hivi: "dada wa JK afiwa na mwanae"!

Nimepita magomeni mapipa nyuma ya msikiti wa mchangani, rais wa Tanzania yu-katika hali ya majonzi ya kufiwa na mtoto wa dada yake, sifahamu marehemu aliitwa nani.
Mwenye taarifa za kina atujuze.

POLE RAIS WETU, MUNGU AKUPE MOYO WA SUBIRA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MSIBA.
RIP MAREHEM
 
Aliyefariki ni mtoto wa dada yake, nimelisikia tangazo Radio One saa 4:00 asubuhi hii.

Mode please rekebisheni, JK hajafiwa na dadake, kafiwa na mtoto wa dadake, yaani mpwawe.

Wala haina haja ya Mode kurekebisha kwani mtoa mada amezungumza wazi kwamba ni mtoto wa dadake ila wapendao kuandika ili mradi wameandika ndio wameandika dadake!!!! kitu ambacho mtoa mada amesema hakukifahamu ni jina la huyo mtoto, lakini akina siye tunadai why kuleta unverified story kana kwamba jina ni issue muhimu sana!
 
kumbe bro kakulia migo!!! Nlidhani msoga

Kwao kabisa ni Bagamoyo na Msoga, lakini akiwa Dar es salaam kwao ni hapo mtaa wa Tosheka magomeni nyuma ya ule msikiti mkubwa unaotazamana na kanisa pale kwenye trafic lights za magomeni, kipindi kirefu cha ujana wake amekitumia mitaa ile akisoma kibaha na baadae chuo kikuu mlimani.

Hata baada ya kuupata uwaziri kipindi cha mwinyi kile akitoka kazini wizarani breki ya kwanza magomeni kwenye kijiwe chao pale mtaa wa Dossi na Takadiri magomeni mapipa yeye na swahiba wake marehemu Ditopile ilikua lazima watie timu pale kijiweni kwenye nyumba flani ipo kwenye kona hivi, kijiwe kizima walikua watu wa Yanga.

Pale kulikua na kina mzee mataka, mzee Tuwa(kaka yake jk) ambae kuna wakati fulani alikua mganga wa Yanga, basi mikakati ya kumfunga mnyama(simba)ilikua inafanyikia pale, maana jakaya mgonjwa ile mbaya kwa yanga yake.

Huyo mzee Tuwa kwenye ule mkasa wa marehemu Ditto kuua walikua pamoja kwenye gari siku ile ya tukio na baadae aliunganishwa kwenye ile kesi kama shahidi, yeye na mzee mataka wapo mpaka leo hapo Dossi na last time nilipokuja bongo kijiwe kilikuwepo lakini si kama kile cha zamani.

Jakaya alikua anakaa pale mpaka saa mbili usiku wakishasikiliza kipindi cha michezo ndio anaondoka kwenda uzunguni kwake.Baada ya kuwa waziri wa mambo ya nje au niseme kipindi cha mkapa ndio aliacha kwenda pale kijiweni! Sitaki tu kusema mengi lakini jk na ditto walikua na vituko sana,siku nikimuangalia yule brother huwa nakumbuka mbali,nacheka sana!

All in all poleni wafiwa wote.
 
Mara ya kwanza kuiona iyo heading nilishaelewa sasa ninyi mnaoleta kiswahili sanifu uku mmeelewa ambayo ndo maana kubwa ya lugha watu kuelewa kinachoongelewa!
Mnanikumbusha enzi za shekhe Gonga kile kipindi cha kiswahili pale TBC
Pole JK!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom