Mungu amlaze mahala pema peponi, poleni wanafamilia. Katiba mpya iangalie uwezekano anayekuwa wa pili kwa kura (Diwani kivuli) achukue nafasi kumalizia kipindi kilichobaki hii iende mpaka kwa mbunge kivuli na waziri kivuli mpaka rais kivuli. Kupunguza matumizi ya serikali, tunahitaji fedha za madarasa, madawati na kuajiri walimu wapya watoto wengi waliofaulu hawajachaguliwa kuingia sekondari, walimu bado wanadai fedha nyingi serikali za likizo, uhamisho na marimbikizo.