TanzaniteOne yaajiri mtoto wa Kamishna wa Madini

DOUBLE AGENT

Member
Jul 3, 2011
38
34
Kuna tetesi kutoka serikalini kuwa kampuni ya TanzaniteOne ya Afrika Kusini inayofaidika na madini ya tanzanite kuliko serikali ya Tanzania na wachimbaji wote wazalendo imemwajiri kwa miaka kadhaa sasa mtoto wa Kamishna wa Madini kwenye Wizara ya Nishati na Madini, Gray Mwakalukwa, kama meneja wake na mwanasheria wa kampuni. Hili suala linaleta mgongano wa kimaslahi (conflict of interest) kwani baba hawezi kuisimamia kampuni iliyomwajiri mwanae. Hivi sasa Gray Mwakalukwa amehamishiwa kwenda Shirika la Madini la Taifa (Stamico), ambalo nalo pia linasimamia sekta ya madini nchini.

Anaye fahamu vizuri tetesi hizi atupe data tafadhali. Je, Lusekelo Mwakalukwa, ambaye ni Corporate Governance Manager and Company Secretary wa TanzaniteOne ana uhusiano gani na Gray Mwakalukwa, Kamishna wa Madini. Ni mtu na baba yake, wana undugu wowote au majina yamefanana tu?
Tanzanite supply will not be depleted soon-Staryee
 
Mkuu umeleta fitna, malalamiko au swali? Kama jamaa ameajiriwa on the basis of merit hakuna ubaya. Tatizo ni kuwa kama ameajiriwa kwa mizengewe na anafanya kazi kwa jina la baba, au aliingia kutokana na favour za baba yake.
 
Nijuavyo huyu baba hana mtoto wa kiume na hana mtoto mkubwa mkubwa wa kuajiliwa.

Kwanini usifanye uchunguzi kwanza kabla ya kulletea jamii tetesi zilizo kaa kiumbea umbea?
 
Nijuavyo huyu baba hana mtoto wa kiume na hana mtoto mkubwa mkubwa wa kuajiliwa.

Kwanini usifanye uchunguzi kwanza kabla ya kulletea jamii tetesi zilizo kaa kiumbea umbea
?

are u sure unawafahamu watoto wake wote,hadi wa nje ya ndoa.acha zako bana, ucijiamini katika hilo
 
Sio ajabu kusikia habari za namna hii katika tz ya leo. Makampini ya kinyonyaji yanatumia mbinu kama hii ya kuajiri watoto wa wakubwa ili yaendelee kutuibia bila kunyooshewa kidole. Bila vita ya ukombozi kama Libya upumbafu kama huu hautaisha
 
Napenda rejea maneno ya aliyekuwa katibu wa CCM yusuph makamba alipopata nafasi ya kuojiwa na waandishi wa habari kuhusu watoto wa wanasiasa kuwa nao wana siasa.makamba alitoa jibu fupi sana kwamba panya wa kanisani atakula biblia na yule wa msikitini atakula quran,hii inamaanisha nini kama baba yako ni mvuvi na mtoto atakuwa mvuvi.ivi ndo nchi yetu inavoendeshwa sijui lini tunaweza ondokana na huu mfumo wa dhuluma mungu tusaidie.
 
Kama ana sifa sioni sababu kwa nini asiajiriwe, ili mradi tu
taratibu zifuatwe maana tusipoteze wachapakazi kwa sababu
tu majina yao ya mwisho yanafanana na ya vigogo.
Mtoa mada labda utueleze mazingira ya ajira na sifa
za mtu huyo kama kuna utata...
 
uneyamtaja si mtoto wa kamishna mwakalukwa ila ni mtoto wa kaka yake anaitwa lusekelo james mwakalukwa ni ccoparate manager na mwanasheria wa tzone ninachofahamu ni kwamba hana uwezo sana kiutendaji na kampuni mara nyingi imekuwa nina hire wanasheria wa mjini arusha katika kesi mbalimbali zinazowakabilli na kuiingia gharama kubwa.kuhusu imgongano wa maslahi hilo nawaachia wachangiaji!
 
Hili ndo nililohitaji kufahamu kwenye posti yangu #9 ...
 
uneyamtaja si mtoto wa kamishna mwakalukwa ila ni mtoto wa kaka yake anaitwa lusekelo james mwakalukwa ni ccoparate manager na mwanasheria wa tzone ninachofahamu ni kwamba hana uwezo sana kiutendaji na kampuni mara nyingi imekuwa nina hire wanasheria wa mjini arusha katika kesi mbalimbali zinazowakabilli na kuiingia gharama kubwa.kuhusu imgongano wa maslahi hilo nawaachia wachangiaji!

Kwa kweli ni kinyume na maadili ya uoungozi wa umma kwa kiongozi kutoa vimemo kwa makampuni binafsi unayoyasimamia kwenye sekta ili yaajiri watoto wa ndugu zako. Sasa unadhani TanzaniteOne wakitaka leseni kutoka wizarani wakamtume Lusekelo akaongee na baba yake mkubwa matokeo yake si upendeleo tu kwa kampuni hii ya makaburu? Ni dhahiri kuwa hawajamwajiri kutokana na uwezo wake bali ni family connection zake.
 
Acheni umbea.kamishna wa madini ni Dr kafumu.

Kwa taarifa yako tu, Gray Mwakalukwa, alikuwa Kamishna wa Madini kwa miaka 8 na nusu kabla nafasi ya kupewa Dk. Kafumu. Alihamishiwa kutoka kuwa kamishna wa madini na kuteuliwa kuwa Director General of the State Mining Corporation (Stamico), shirika la serikali linalosimamia sekta ya madini. Hivyo conflict of interest ya Mwakalukwa iko palepale kwa kampuni ya TanzaniteOne kumuajiri ndugu yake. Si jambo jema kuona hili linafanyika.

Kwa mfano ukienda kwa AG huenda utasikia mtoto wake kaajiriwa na Mkono Advocates ambayo inapewa tenda za serikali za uwakili, Waziri wa Fedha mtoto wake yuko Benki Kuu, Waziri wa Nishati na Madini utaskia mke wake yuko Barrick, Waziri wa Mawasiliano mpwa wake anafanya kazi Vodacom, Waziri wa Maliasili na Utalii mdogo wake kaajiriwa na Grumeti, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani mpwa wake kaajiriwa Ultimate Security, JK mtoto wake Ridhwani kaajiriwa FK law chambers ambao wanapewa tenda za unashasheria na serikali.

Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond naye alipachika watoto wake BoT pamoja na vigogo wengine. Hii yote ni kukosa maadili ya uongozi wa umma. If only Mwalimu Julius Nyerere was living. Enzi zake kulikuwa hakuna upuuzi huu.

Hata kama watoto wa vigogo wana sifa, inaleta picha mbaya na si maadili mema kwa mawaziri na vigogo wengine kupeleka memos kwa taasisi zilizo chini yao kuajiri ndugu zao. Ni aina ya rushwa hii.
 
uneyamtaja si mtoto wa kamishna mwakalukwa ila ni mtoto wa kaka yake anaitwa lusekelo james mwakalukwa ni ccoparate manager na mwanasheria wa tzone ninachofahamu ni kwamba hana uwezo sana kiutendaji na kampuni mara nyingi imekuwa nina hire wanasheria wa mjini arusha katika kesi mbalimbali zinazowakabilli na kuiingia gharama kubwa.kuhusu imgongano wa maslahi hilo nawaachia wachangiaji!
Je unafahamu tofauti ya Manasheria na wakili?
 
Ndo maana akasema kuwa kuna tetesi
Nijuavyo huyu baba hana mtoto wa kiume na hana mtoto mkubwa mkubwa wa kuajiliwa.

Kwanini usifanye uchunguzi kwanza kabla ya kulletea jamii tetesi zilizo kaa kiumbea umbea?
 
Lusekelo Mwakalukwa, kweli kama ilivyoelezwa katika thread # 9 ni mtoto wa kaka yake Gray Mwakalukwa, huyu alieko stamico sasa. Baba yake mzazi yeye ni marehemu na mama yake anaishi Botswana kwa sasa. Huyu jamaa ni kilaza wa kutupwa, ana historia ndefu sana kwenye shule yake, alinzia kusome udaktari mwimbili huko maprof walimnyaka akadisco, baadaye akapenyeza ukwasi akaingia Faculty of Law (UDSM) licha ya kwamba alisoma PCB secondary. UD alimaliza kwa kuchechemea, alikuwa na sup za kufa mtu. Hiyo position aliyopo kuwa kapata kwa sababu ya baba yake mdogo wala haibishaniwi, hilo ni kweli. Lakini tukumbuke Tz ndio tupo stage hiyo, wala siyo yeye tu, ni utaratibu wa kawaida kwa sasa. Hakuna wa kumpigia kengere mwenzake. Nawakilisha
 
Mtoa mada uko sahihi kabisa,and i hope the message has been read.ths is disgusting and rubbish.Watu wachache wanagawana 'nationa keki' tena kwa bei chee.ee Mungu tuokoe na dhuluma hizi.Naamini iko siku nchi yetu itatoka mikononi mwa wanyang'anyi.kuanzia ikulu mpaka tarafani,kote kumegeuka mapango ya wanyang'anyi.
 
Back
Top Bottom