Tanzanite yetu na barabara ya mererani!

Nyumbu-

JF-Expert Member
May 26, 2009
988
349
Vitu vingine ni vigumu kuelewa. Ukisafiri kwenda Mererani, mahali ambako Tanzanite inachimbwa hutaamini macho yako.Barabara mbaya mno, ikiwa imezuntgukwa na wanakijiji masikini waliokata tamaa. Magari ya kwenda huko ni Landrover mbovu maarufu kama mando. Kwa ujinga wangu nilitegemea kwamba kule mahali kungekuwa kumeendelea sana, lakini sivyo! Raisi Mkapa, na Raisi Kikwete wote wametembelea eneo hilo wakati wa kampeni zao na kuona kulivyo. Hivi inakuwaje hakuna maendeleo kiasi hiki? Au kuna faida gani basi ya kujitangaza kwamba sisi ndo wenye tanznite kama hatufaidiki nayo? Jamani tumerogwa au mimi ndo sielewi mambo yanavyotakiwa yawe? Naomba mawazo jamani, kichwa inazunguka!
 
tukiwa na shida zetu kwenda mererani tunakodi ndege,
nyie hangaikeni tu na barabara yenu.
na tanzanite ikiisha tunaachieni mashimo mhangaike nayo.
hiyo ndiyo sera yetu
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom