Tanzanite ONE tunavuliwa nguo .....

Hasara

Senior Member
Dec 29, 2006
138
9
Katika toleo la leo la gazeti hili habari kubwa katika ukurasa wa mbele ni ile inayohusu malalamko ya wafanyakazi wa kampuni ya madini ya Tanzanite One.

Pamoja na mambo mengine, wafanyakazi hao wanalalamikia unyanyasaji uliokithiri katika utendaji wao wa kazi wa kila siku.

Baadhi ya malalamiko hayo yanalenga katika udhalilishwaji ikiwa ni pamoja na kutukanwa matusi ya nguoni na kuvuliwa nguo hadharani wakati wa ukaguzi.

Aidha, wafanyakazi hao wanalalamikia kitendo cha kuvalishwa bukta wanapoingia mgodini pamoja na kukosekana kwa usalama wa kutosha kazini.

Katika kile kinachoonekana kuchoshwa na vitendo hivyo, wafanyakazi hao wameiomba Serikali kuingilia kati kuhakikisha kwamba misingi ya kazi inafuatwa katika kampuni hiyo.

Wanasema ni vizuri iwapo Serikali itatuma wakaguzi wake katika machimbo ya Tanzania One ili kuona hali halisi ilivyo katika machimbo hayo na kuchukua hatua ambazo wanafikiri zitafaa katika kuwanusuru na mateso wanayopata.

Kimsingi, ukiangalia madai ya wafanyakazi hao utaona kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa kilio chao kusikilizwa.

Tunasema hivyo kwa sababu hii si mara ya kwanza kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo kutoa kilio kama hicho pasipo wahusika kuchukua hatua zozote.

Malalamiko ya wafanyakazi hao yanaibuka tena huku kukiwa na malalamiko mengi ya aina hiyo kutoka kwa wadau mbalimbali wa sekta ya madini Tanzania.

Sisi, Arusha raha, tunaona kwamba sasa ni wakati muafaka kwa Serikali kuliangalia suala hili kwa marefu na mapana kwani tunaamini kulifumbia macho linaweza kuja kuleta madhara makubwa hapo baadaye.

Hivi, ni nani hasiyejua kuwa uvumilivu una mwisho wake?, unafikiri nini kitakachotokea iwapo wafanyakazi hao wa Tanzania One wataamua kuweka ‘sululu’ chini na kuchukua sheria mkononi.

Hivi, Serikali pamoja na vyombo vingine vinavyohusika na sekta hii ya madini wanashindwa nini kutatua tatizo hili?.

Sawa, tunaelewa umuhimu wa wawekezaji katika pato la Taifa lakini katika hili la Tanzanite One, tunaona kuna umuhimu mkubwa kwa Serikali na wadau wake kuingilia kati haraka iwezekanavyo kabla ya madhara zaidi hayajatokea.
source www.arusharaha.com
 
Labda ndio maana serikali haikuingia mkataba na hii kampuni?
 
Hii ni kampuni ya WAZALENDO, hawana mtaji wa kununua mashine za kisasa za kuchunguza kwi kwi kwi

Bongo bwana!
 
Tupia kapicha kama ni kweli au ukiona wamezidi acha kazi kudadeki!!!

Back
Top Bottom