Tanzania's GDP: Hivi tunajua hili?

Sasa mkuu mbona unaleta mambo ya shule sasa data ni za nchi tatu dunia ina nchi zaidi ya 230

1.Kama utakubali GDP ni formula in the economic perspective wewe utaweka figure tu na chombo kinacho aminika ni World Bank nd IMF to give you fair results kwani hata Watanzania wapo wanafanya kazi kule
2. sasa ukiltaka ranking ya mortality rate or maternal death, and life expectancy for each country WHO wanazo na wanatumia sama rules na nchi zipo ranked
3. kama ukitaka iliterate rate kuna UNICEF
4. Wakimbizi ipo UNHCR na hii sisi ndio tunaongoza

na vitu vyote vipo ranked separately na hao walioderive hivyo vitu wamabobea kwenye fani hiyo sio wanafunzi
Kwa kuwa mtu anaanza kutambaa halafu kutembea ndio akimbie lazima walisoma hiyo attachment Shuleni
Na wameweka nchi tatu kwa sababu ya kurahisisha kuelewa
Huwezi kuweka mambo ya life expectacy kwenye GDP every thing was considered well before agreed by every country sasa kama hutaki hutaki tuu

Nilikuelezea umuhimu wa kuzingatia vigezo vingine vya maendeleo na siyo GDP peke yake,hapo ndiyo kwenye hoja yangu.
Ukataka data.Nimekutumia hako ka file kusisitiza hoja yangu ya mapungufu ya GDP,bado hunielewi?
Nani asiyejua dunia ina nchi zaidi ya 3?Wamekuchanganulia kama nilivyokuambia mwanzo kuwa nchi moja inaweza ikawa juu katika baadhi ya vielelezo vya maendeleo na ikawa chini katika vingine.Na wenyewe nao wametumia baadhi ya ripoti hizohizo za WB/IMF unazoziamini.Wakakupa mfano wa umri wa kuishi kama kielelezo kimojawapo cha maendeleo.Utaona kuna nchi zina GDP sawa lakini vilevile zina viwango tofauti katika umri wa kuishi.
Wakakupa mfano wa Literacy rates kama kielelezo kimojawapo cha maendeleo.Mfano Saudi Arabia ina GDP kubwa kuliko Zambia lakini Zambia inaongoza kwa literacy rates.
Sasa kigumu kiko wapi mkuu?
Usipoielewa hoja yangu mpaka hapa basi mkuu umeshinda.Tukutane kwenye thread nyingine!!
 
Haya file hilo wakuu
Labda litatuongezea ufahamu kidogo kuhusu GDP na economic indicators nyingine
NB;Tuko pamoja katika hopa za kujiletea maendeleo na kuondokana na umasikini.

Ndg Mtarajiwa,
Nashukuru kwa kisehemu hicho toka kwenye hiyo module.LAKINI NAPENDA NIKUHAKIKISHIE KUWA MWANDISHI WA MODULE HIYO ALIACHA MAMBO MEEEENGI SANA YA KUZUNGUMZIA JUU YA INDICAROTORS OF ECO DEV na akasite vijisehemu tu vya kuandika ili asambaze module hizo ili watu wasomee somo la GS huko vyuoni hasa Diploma za ualimu.kimsingi alifanya biashara.

Kumbuka kuwa hiyo module ilitokana na ile warsha ya bagamoyo na watu walikaa mwezi mzima.Mimi baada ya kuona kijimodule hicho kidogo nitapike kwani aliandika utadhani ana-account for something.

Nashangaa sana unavyobisha juu ya GDP na kubeza world Bank wakati wewe unatupa reference ya module ya warsha ya Bagamoyo.I cant picture it.

Tukisema vigezo vya maendeleo ya kiuchumi vipo vingi sana lakini baba lao ni GDP.Nikirudi kwako nashangaa huweki hizo indicators unazodai zipo bali unabeza tu.Labda nikukumbushe kuwa ukiwa unajadili usije ukafananisha na Indicators of poverty japo zinashabiana SANA.Sitorudia haya hapa chini:-
-GD
-Life expectanc
-Literacy
-Measures of poverty
-Disease
-Mortarity rate na vifo vya watoto wachanga.

mimi nakubali wazi kuwa Tanzania ni masikini.Nashauri tuache kubisha kwa ajili tu ya siasa bali huo ndo ukweli.Mimi nataka kuangalia baadhi ya sababu zilizo fanya Tanzania tuwe masikini wa kunuka kiasi hiki.

1:WAKATI WA NYERERE
Sababu kubwa iliyotufanya tuwe masikini ni Nyerere na ujamaa wake aliotulazimisha kuuabudu ana kuunga huku ukikinzana na ujamaa nyingine huku akituletea maazimio meengi yasiyo na kichwa wala miguu na kutufanya tumuogope hata kumbishia ama kumwelekeza na kusababisha kuwepo na pengo kubwa kati ya watawala na watawaliwa huku tukiwaogopa kama miungu mtu.kifupi sababu ya kuwa masikini kipindi hiki ni Ujamaa na kujitegemea wa nyerere.

2:WAKATI WA MWINYI:
Serikali haikuwa makini na iliendeshwa utafikiri hapakuwa na wasomi wala watu wa kuongoza.Bra bra nyiiiingi huku mfumko wa bei na kushuka kwa thamani ya hele yetu kukiwa na kasi ya ajabu.

3:WAKATI WA MKAPA.
Serikali ilikuwa MAKINI sana na uchumi wetu ulikuwa SANA tofauti sana na awamu 2 zilizomtangulia.Hapa hakuna ubishi.Uchumi uliimarika na thamani ya hela yetu ilikuwa imara na alidhibiti mfumko wa bei.(Najaribu kumlinganisha mkapa na waliomtangulia pia aliyepo sasa) simlinganishi na waTZ wote tafadhari.Shida inayokuja sasa tumeweka siasa nyiiingi kiasi kwamba sasa hivi mkapa anaonekana kama choo popote litamkwapo jina lake.Lakini ukweli ni kuwa huyu baba wa watu upande wa Uchumi ALIJITAHIDI.

4:WAKATI HUU WA KIKWETE.
Hapa hakuna kitu.Sioni hata moja la ku-comment.Silaumu siasa yake kwani hana siasa,wala Ujamaa wake kwani hana ujamaa,wala maazimio yake kwani hana maazimio.USANII TU NA KUCHEKA CHEKA.Inakera sana kuona anapokea nchi ikiwa imara toka kwa Mkapa sasa imekuwa utafikiri danguro.Hivi kwa nini mlimchagua nyie watanzania nyie?????enough is enough.2010 yaja.

HITIMISHO.
Mambo yote yameongelewa huko juu ila shida ni UONGOZI SAFI ndo hatuna.Tuanazijua indicators zoote za uchumi,indicators zote za poverty na jinsi ya kuzishughulikia.Tuna raslimali nyiingi tu,Watu,Siasa,na Elimu Swafi kabisa.Huwezi kusema sisi ni wajinga wakati tuna mavyuo makuu sijui mangapi tuu na watu kila mwaka wanamaliza pale.Tuchague viongozi imara na thabiti ili watuwekee strategies bora za maendeleo.
Mkishindwa njooni tuvue samaki huku majita
 
Sasa mkuu mbona unaleta mambo ya shule sasa data ni za nchi tatu dunia ina nchi zaidi ya 230

1.Kama utakubali GDP ni formula in the economic perspective wewe utaweka figure tu na chombo kinacho aminika ni World Bank nd IMF to give you fair results kwani hata Watanzania wapo wanafanya kazi kule
2. sasa ukiltaka ranking ya mortality rate or maternal death, and life expectancy for each country WHO wanazo na wanatumia sama rules na nchi zipo ranked
3. kama ukitaka iliterate rate kuna UNICEF
4. Wakimbizi ipo UNHCR na hii sisi ndio tunaongoza

na vitu vyote vipo ranked separately na hao walioderive hivyo vitu wamabobea kwenye fani hiyo sio wanafunzi
Kwa kuwa mtu anaanza kutambaa halafu kutembea ndio akimbie lazima walisoma hiyo attachment Shuleni
Na wameweka nchi tatu kwa sababu ya kurahisisha kuelewa
Huwezi kuweka mambo ya life expectacy kwenye GDP every thing was considered well before agreed by every country sasa kama hutaki hutaki tuu

Saafi sana, hapa tupo ukurasa mmoja mkuu!
 
Kwani hao benki ya dunia ni Mungu au biblia au msaafu wakisema kitu hakiwezi kuwa uongo au kubadilika?

nadhani sasa una lako na benki ya dunia, tupe vigezo vyako vya kuonyesha angalau wao wamekosea, kwa kuwa tukitumia kigezo hiki na hiki tanzania itakuwa labda ya 20 duniani. kukkandia tu tafiti za world bank haitasadia

kama ni ukubwa wa nchi mbona zaire na sudan ni kubwa sana? mbona haziko kwenye kundi letu?
 
Mtarajiwa, ni sawa lakini GDP ndio mara nyingi inatumika kama proxy indicator ya 'human development and well-being'. Kwa maana hiyo mimi kama investor au social-scientist kwanza nitaanza simply kuangalia GDP kabla sijazama kwenye other indicators ili kupata picha kubwa zaidi.

Kwa hiyo kama ni investor, GDP tu ikiwa ovyo inaweza kunikatisha tamaa sana kuinvest kama natarajia kuinvest with big capital......kwa sababu ukiwa na low GDP ni likely, kuwa na huduma mbovu za afya, miundombinu mibovu, limited skilled labour n.k.....

The opposite ya hili (GDP kubwa au inayoonekana kukua kwa kasi) inacreate interest especially kwa investor kuona kuwa kuna opportunity kwenye specific country.

Nani kasema GDP ndiyo representative indicator?Mimi siyo mtaalam wa uchumi na uwekezaji lakini ninavyojua sasa kuna ongezeko kubwa la ushindani wa kimataifa katika kuvutia wawekezaji hasa wa kigeni.Nchi sasa zinatenga hata bajeti kwa ajili ya kushindana na nchi nyingine katika kunadi sera za kuvutia wawekezaji.Ingekuwa wawekezaji wanaangalia GDP tu ndiyo wanaamua wapi wakawekeze,basi kusingekuwa na haja ya hawa watu kupoteza muda,nguvu na pesa nyingi katika kunadi hizo sera.Wengine wanasema wanatoa misamaha ya kodi,wengine wanaringia geografical location,arable land,security,vivutio vya kitalii,Wengine wanaringia cheap labor,Rais wetu amefanya misafara mingi nje na sababu tunayoambiwa ni kutafuta wawekezaji.
Unajua kwamba Kenya ina wawekezaji wengi kuliko Uganda na kwa viwango vya GDP,Uganda iko juu kuliko Kenya?
 
GDP kisiwe kipimo pekee cha kusema nchi gani ni tajiri zaidi duniani na nchi gani ni masikini wa kutupa.
Watu wa development studies wana kitu wanaita INDICATORS OF DEVELOPMENT,ambayo ina vitu vingi ma hiyo GDP ikiwa ni kasehemu tu ambavyo kwa pamoja ndivyo vinapima uwezo wa kimaendeleo wa nchi tofauti.
Kuna vitu kama huduma za kijamii kwa mfano shule,hospitali,zahanati,maji safi na salama,kuna walimu wangapi katika nchi,uwiano wa madaktari na wagonjwa,vitanda hospitalini nk
Kuna vitu kama miundombinu,barabara,reli,,anga,simu,mzunguko wa pesa,upatikanaji wa ajira,nk nk
Mambo yako mengi.Kwahiyo unaposema GDP pekee ndiyo kipimo cha maendeleo,si kweli.Inabidi uziangalie hizo indicators zote halafu ndiyo utupangie list ya matajiri na masikini.
Halafu hiyo GDP yenyewe inatafutwaje?iko even?Nchi kama Luxembourg ina watu wasiozidi 500,000(laki tano),hiyo population ni kama mara sita ndiyo ifikie population ya watu wa jiji la Dar Es Salaam kwa mfano.Sawasawa na Rwanda na Burundi ambazo nazo zina idadi ndogo ya watu.
Manake kanchi kenye watu wadogo kama Luxembourg,ni sawa na mkoa fulani wa Tanzania au mji fulani wa Marekani au nchi nyingine kubwa.ukikafanyia hiyo GDP ni sawa labda kwa mfano ufanye GDP kwa sehemu nyingine kwa uwiano huohuo.Kwamfano ukifanya GDP ya mkoa wa Dar Es Salaam,utapata nzuri sana zaidi ya hiyo 600.
Kwahiyo point hapa ni hiyo uneven distribution of incomes in different parts of different populations in a big country like Tanzania.
Ndiyo utaona bajeti ya ulinzi ya Marekani ni zaidi ya bajeti ya nchi tano za ulaya lakini kwenye GDP inashika nafasi ya 2/3/5
Kwahiyo usidanganyike na hizo figure mkuu

Mkuu nimeweka msisitizo kwenye highlight lakini karibia hayo yote uliyataja hapo juu yako included kwenye GDP calculations either direct ama inderect kutokana na the fact kwamba since GDP ni gross domestic product ambayo ofcourse ni mapato gawanya kwa population...Then utaona ukweli kuwa uzalishaji huweza kuwa juu kama kukiwa na efficiency pamoja na good infrustructures.

Tunaweza pia ku assume kuwa uzalishaji unakuwa juu kama hali ya wananchi ni nzuri na social services ulizozitaja pia ni satisfactory.

All in all ni kwamba GDP hutumika kama kigezo kikubwa kwasababu ni kweli nchi masikini zote GDP zao ni low.
 
Ndg Mtarajiwa,
Nashukuru kwa kisehemu hicho toka kwenye hiyo module.LAKINI NAPENDA NIKUHAKIKISHIE KUWA MWANDISHI WA MODULE HIYO ALIACHA MAMBO MEEEENGI SANA YA KUZUNGUMZIA JUU YA INDICAROTORS OF ECO DEV na akasite vijisehemu tu vya kuandika ili asambaze module hizo ili watu wasomee somo la GS huko vyuoni hasa Diploma za ualimu.kimsingi alifanya biashara.

Kumbuka kuwa hiyo module ilitokana na ile warsha ya bagamoyo na watu walikaa mwezi mzima.Mimi baada ya kuona kijimodule hicho kidogo nitapike kwani aliandika utadhani ana-account for something.

Nashangaa sana unavyobisha juu ya GDP na kubeza world Bank wakati wewe unatupa reference ya module ya warsha ya Bagamoyo.I cant picture it.

Tukisema vigezo vya maendeleo ya kiuchumi vipo vingi sana lakini baba lao ni GDP.Nikirudi kwako nashangaa huweki hizo indicators unazodai zipo bali unabeza tu.Labda nikukumbushe kuwa ukiwa unajadili usije ukafananisha na Indicators of poverty japo zinashabiana SANA.Sitorudia haya hapa chini:-
-GD
-Life expectanc
-Literacy
-Measures of poverty
-Disease
-Mortarity rate na vifo vya watoto wachanga.

mimi nakubali wazi kuwa Tanzania ni masikini.Nashauri tuache kubisha kwa ajili tu ya siasa bali huo ndo ukweli.Mimi nataka kuangalia baadhi ya sababu zilizo fanya Tanzania tuwe masikini wa kunuka kiasi hiki.

1:WAKATI WA NYERERE
Sababu kubwa iliyotufanya tuwe masikini ni Nyerere na ujamaa wake aliotulazimisha kuuabudu ana kuunga huku ukikinzana na ujamaa nyingine huku akituletea maazimio meengi yasiyo na kichwa wala miguu na kutufanya tumuogope hata kumbishia ama kumwelekeza na kusababisha kuwepo na pengo kubwa kati ya watawala na watawaliwa huku tukiwaogopa kama miungu mtu.kifupi sababu ya kuwa masikini kipindi hiki ni Ujamaa na kujitegemea wa nyerere.

2:WAKATI WA MWINYI:
Serikali haikuwa makini na iliendeshwa utafikiri hapakuwa na wasomi wala watu wa kuongoza.Bra bra nyiiiingi huku mfumko wa bei na kushuka kwa thamani ya hele yetu kukiwa na kasi ya ajabu.

3:WAKATI WA MKAPA.
Serikali ilikuwa MAKINI sana na uchumi wetu ulikuwa SANA tofauti sana na awamu 2 zilizomtangulia.Hapa hakuna ubishi.Uchumi uliimarika na thamani ya hela yetu ilikuwa imara na alidhibiti mfumko wa bei.(Najaribu kumlinganisha mkapa na waliomtangulia pia aliyepo sasa) simlinganishi na waTZ wote tafadhari.Shida inayokuja sasa tumeweka siasa nyiiingi kiasi kwamba sasa hivi mkapa anaonekana kama choo popote litamkwapo jina lake.Lakini ukweli ni kuwa huyu baba wa watu upande wa Uchumi ALIJITAHIDI.

4:WAKATI HUU WA KIKWETE.
Hapa hakuna kitu.Sioni hata moja la ku-comment.Silaumu siasa yake kwani hana siasa,wala Ujamaa wake kwani hana ujamaa,wala maazimio yake kwani hana maazimio.USANII TU NA KUCHEKA CHEKA.Inakera sana kuona anapokea nchi ikiwa imara toka kwa Mkapa sasa imekuwa utafikiri danguro.Hivi kwa nini mlimchagua nyie watanzania nyie?????enough is enough.2010 yaja.

HITIMISHO.
Mambo yote yameongelewa huko juu ila shida ni UONGOZI SAFI ndo hatuna.Tuanazijua indicators zoote za uchumi,indicators zote za poverty na jinsi ya kuzishughulikia.Tuna raslimali nyiingi tu,Watu,Siasa,na Elimu Swafi kabisa.Huwezi kusema sisi ni wajinga wakati tuna mavyuo makuu sijui mangapi tuu na watu kila mwaka wanamaliza pale.Tuchague viongozi imara na thabiti ili watuwekee strategies bora za maendeleo.
Mkishindwa njooni tuvue samaki huku majita

Mkuu hilo siyo desa mlilomezeshwa bagamoyo kwenye semina yenu.Liangalie vizuri mkuu,naona umelifananisha!!
 
Jamani mna namba za zamani Tanzania per capita ya 2007 ni $1,300 Source CIA factbook na siyo $600 kama zamani
 
Jamani its true Tanzania ni masikini ila sio kihivyo. Tanzania kama nchi ni tajiri kwa rasilimali ila watu wake ndio masikini.
Hii GDP ni Gross Domestic Product Per Capital Income maana yake pato la ndani la taifa ukaligawanya kwa idadi ya watu.
Tuko chini kwa sababu tunaimport zaidi kuliko tunacho export simply kwa sababu almost hakuna tunachozalisha for export market. Sisi ni consumers tuu kwenye global market.
Good news ni kuwa our Annual Growth Rate ni zaidi ya 7% according to UNDP data. This is 2% above avarage rate ambayo ni 5%. Inamaana nchi yoyote yenye kuanzia 6% inadalili nzuri ya kukua kiuchumi.

Sina uhakika kama pato la madini linajumuishwa kwa sababu makampuni ya madini yanadai hayatengenezi faida kulingana na mitaji waliowekeza.
They haven't break even!.
 
.....kama Lowassa Richmond katuibia mabilioni na ushahidi uko wazi kabisa lakini hakuna kilichofanyika kumfikisha kwenye vyombo vya sheria,then leo tunashangaa tupo bottom of the bottom...we deserve that!
 
There are misrepresentations and even lies here. GDP (Gross Domestic product) is the total market value of all final goods and services produced in a country in a given year. Gaza Strip is not, and has never been, a country. Only a mischievous person would compare our GDP with that of a non-country.

More importantly, I put it to you that most of the market value of all final goods and services produced in Tanzania in a given year is not recorded and is therefore not added to the World Bank’s measure of our GDP. For instance, large numbers of huts and houses are informally constructed in our villages each year, but their market value is not included when the Bank computes our GDP.

Let us not compare oranges with mangoes. An economy like ours that is overwhelmingly informal, cannot be compared with a formalized one like that of Switzerland.

It is true that we are poor, but that does not justify discouraging us by miscalculating our output. It seems to me that the World Bank knows that it has false GDPs of most Third World Countries, but it likes to perpetuate this as an instrument of emasculation. Nothing weakens a community more than a feeling that they are no good.

The WB wants us to be so sorry for ourselves that we will hate ourselves and loose our self confidence. Do not succumb to that.
 
Nilikuelezea umuhimu wa kuzingatia vigezo vingine vya maendeleo na siyo GDP peke yake,hapo ndiyo kwenye hoja yangu.
Ukataka data.Nimekutumia hako ka file kusisitiza hoja yangu ya mapungufu ya GDP,bado hunielewi?
Nani asiyejua dunia ina nchi zaidi ya 3?Wamekuchanganulia kama nilivyokuambia mwanzo kuwa nchi moja inaweza ikawa juu katika baadhi ya vielelezo vya maendeleo na ikawa chini katika vingine.Na wenyewe nao wametumia baadhi ya ripoti hizohizo za WB/IMF unazoziamini.Wakakupa mfano wa umri wa kuishi kama kielelezo kimojawapo cha maendeleo.Utaona kuna nchi zina GDP sawa lakini vilevile zina viwango tofauti katika umri wa kuishi.
Wakakupa mfano wa Literacy rates kama kielelezo kimojawapo cha maendeleo.Mfano Saudi Arabia ina GDP kubwa kuliko Zambia lakini Zambia inaongoza kwa literacy rates.
Sasa kigumu kiko wapi mkuu?
Usipoielewa hoja yangu mpaka hapa basi mkuu umeshinda.Tukutane kwenye thread nyingine!!

Mkuu naona bora ushinde wewe
GDP is Gross Domestic Product (yaani total output inside the country sasa iliterate utaiweka wapi ?
kwa kifupi ni mshahara wangu na wapo total income yamabosi wetu nakila mtu mapato yake tanzania
Hayo mengine yana chart zake na kuna World ranking as well
 
Usiingize life expectancy,literacy rates nk kwenye GDP.Hivyo ni vigezo vinavyojitegemea.Unapojadili vigezo vya maendeleo,haviingii kwenye GDP bali vinajadiliwa separately.
 
Jamani its true Tanzania ni masikini ila sio kihivyo. Tanzania kama nchi ni tajiri kwa rasilimali ila watu wake ndio masikini.
Hii GDP ni Gross Domestic Product Per Capital Income maana yake pato la ndani la taifa ukaligawanya kwa idadi ya watu.
Tuko chini kwa sababu tunaimport zaidi kuliko tunacho export simply kwa sababu almost hakuna tunachozalisha for export market. Sisi ni consumers tuu kwenye global market.
Good news ni kuwa our Annual Growth Rate ni zaidi ya 7% according to UNDP data. This is 2% above avarage rate ambayo ni 5%. Inamaana nchi yoyote yenye kuanzia 6% inadalili nzuri ya kukua kiuchumi.

Sina uhakika kama pato la madini linajumuishwa kwa sababu makampuni ya madini yanadai hayatengenezi faida kulingana na mitaji waliowekeza.
They haven't break even!.

Mkuu hakuna political symphassy ni kuweka fugure tu kiasi ulichozalisha gawa na population sasa kama hizo pesa za maendeleo viongozi wanaweka Swiss bank unategemea nini
mtu anacheza bao kutwa nzima wenyewe tuna usemi naenda kijiweni kupoteza muda
 
Mbunge,

ACHA kuota ndoto za mchana. CCM iachie mikoa? Wenyewe si unaona ni product ya recycling toka enzi za Uhuru na hawana lolote jipya.

Ukitaka maendeleo ya kweli ni lazima tuwe na decentalization na wakati huo huo inegration ndani ya kitu kikubwa zaidi. Hili lina faida kubwa ya kila mmoja kutaka kubaki ndani ya eneo kubwa la uchumi kwa faida na maslahi ya watu wao. Lakini ukiwapata wababaishaji kama hawa jamaa wa visiwani hili hata hawalioni. Wakati watu wanazungumzia a free market area kubwa hapa Afrika wao wanazungumzia vitambulisho ili jamaa wapate ten percent toka kwa printer.Njaa tupu. Sasa njaakali na siasa safi havikai pamoja hata siku moja. Sahau!

Na kipofu akimuona tembo pale macho yanapofunguka kwa sekunde moja tu kweli inakuwa kazi kubwa kumsikiliza. Luxemburg tu ndiyo ndugu yetu kaiona. Angelifungua Kaka Iga alipoelekeza angeligundua kuna Bermuda, Iceland, Hongkong pekee sio China,Aruba ,Liechtenstein, Monaco,Jersey ,Faroe Islands ,Isle of Man, Seychelles, Mauritius, Israel na kadhalika, na kadhalika anajua ukubwa wa nchi au vijinchi hivi.

Mimi ningelitoa ushauri kwamba Mkuu apunguze safari za Marekani na sasa apange ratiba ya kwenda kwenye vijinchi hivi tudogo tudogo na kuviuliza siri ya mafanikio yao ni nini. Ili na sisi tuige. Tusikubali kuwa mkiani mwaka ingia, mwaka ondoka!

Profesa Ndulu pale BOT tafadhali wawezeshe na young enrepreneurs kwenda vijinchi hivyo na nina hakika watakuja kuibadilisha nchi.
 
I think this is a pre-independence product, child, if not my God bless him or her!

same excuses, same scapegoats and such a hatred for a very,very white and opaque ttuth.

Has he or she ever been to the rural areas and find for self how hardhit is the ordinary Tanzanian.

For a job application I will without hesitation recommend him to work for CCM or National Bureau of Statisstics or the old BOT ( I don't think the current CEO will welcome this kind of a passover type of a person!)
 
Nchi kama Burma, Botswana (imetuzidi mara 15), Bangladesh, Cameroon
Mauritania, Gambia, Cambodia, Laos, Haiti, Marshall Islands, Cape Verde na kadhalika siri yao ni bei nzuri na matumizi safi ya MALI ASILI yao ikiwemo dhahabu na almsai; UTALII kwa kuweka nchi yao katika hali ya usafi na mandhari bora (mambo yanayotushinda japo hayana gharama kubwa isipokuwa tu kubadili tabia zetu); uzalishaji vitu vinavyouzwa nje kama NGUO, viatu na kadhalika pamoja na HUDUMA za kuridhisha za mahoteli, starehe, usafiri na vitu kama hivyo.

Pamoja na kuiogopa Kenya lakini Rwanda na Uganda ziko juu ya Kenya kwa hiyo ina maana kama tukifanya biashara kubwa zaidi na nchi hizo sisi tutaweza kulingana nao. Lakini je, bandari itaamka? Tutajenga reli hadi Uganda? ATC itanunua midege ya mizigo badala ya ndege za abiria ambazo ni hasara tupu.

TATIZO ni kwamba hatujajipanga. Kiongozi bora Tanzania ni yule atakayepanga kwanza, masuala ya uchumi yakakaa vyema na tukawa na mikakati na malengo yanayoeleweka na kutathminika. Kisha ndio aanze kurandaranda duniani.

Vinginevyo, wewe unayetoka katika nchi ya 226 kiuchumi duniani (kwa taarifa hata Gaza ni nchi kwa tafsiri ya eneo la uchumi linalojitosheleza na kujitegemea na WB si wajinga kiasi cha kutotambua hilo) hivi watu wanakuchukuliaje hata kama umevaa suti ghali kuliko za viongozi wenyeji wako? Si maskikini tu wakutupwa na mleta bakuli la sadaka???

Tumuombe Profesa Lipumba atufanyie uchambuzi au upembuzi sijui yakinifu wa hili na aache porojo za kisiasa yeye kasoma bwana na hili saizi yake tena linamfiti kabsaaa!
 
Watu watasema sana watasingizia data za world bank sio credible lakini world bank hawaji kukusanya hizi data wenyewe wanazipata kutoka kwenye idara mbalimbali za serikali yetu kama BOT na NATIONAL BUREAU OF STATISTCIS wasiofahamu mnaweza kutembelea website yao na utaona .....National Bureau of Statistics Tanzania Official Website
Suala lingine world bank wanaposema GDP yetu ni $600, nadhani ni challenge kwetu sisi na sio kuwa tukae tujione kuwa hatuwezi tena ....mbona wengine wanakuja nyuma yetu na kutupita. Inachotakiwa ni kuamka na kupanga mikakati ya kuhakikisha nchi kama nchi tunazalisha, kuuza nje na kutumia every opportunity na resources tulizonazo kwa maendeleo yetu. Lakini hayo yote hayawezekani bila kuwa na visionary leaders na sisi wananchi tuwachallenge vile vile.
 
Mwalimu Augustine,

Mkuu hata huko Somalia kuna mibanda na nyumba vijijini ambavyo pia havikuwekwa ktk hesabu.. Unajua mkuu tunapojaribu kutetea kitu ni muhimu sana tukubali ukweli ili kesho tuweze kujirekebisha... Hivi visingizio vya hiki ama kile haviwezi kabisa kutupeleka kokote..
Gaza strip pamoja na kwamba sio nchi lakini hadi leo hii wana bunge lao, wizara, Budget kama tulivyo sisi iweje leo wasiitwe nchi kwa sababu tu Dunia yako haitaki kuwatambua..Na inasaidia nini kutokuwepo kama nchi kuongeza pengine pato la Tanzania!
Kitu muhimu hapa ni kutazama kweli dollar 600 kwa mwaka ni hesabu inayokubalika?..kama una takwimu tofauti zinazopingana na hiyo hesabu, then tunamjadalka mwingine...

Mtarajiwa,
Watu wa development studies wana kitu wanaita INDICATORS OF DEVELOPMENT,ambayo ina vitu vingi ma hiyo GDP ikiwa ni kasehemu tu ambavyo kwa pamoja ndivyo vinapima uwezo wa kimaendeleo wa nchi tofauti.
Kuna vitu kama huduma za kijamii kwa mfano shule,hospitali,zahanati,maji safi na salama,kuna walimu wangapi katika nchi,uwiano wa madaktari na wagonjwa,vitanda hospitalini nk
Kuna vitu kama miundombinu,barabara,reli,,anga,simu,mzunguko wa pesa,upatikanaji wa ajira,nk nk
Mambo yako mengi.Kwahiyo unaposema GDP pekee ndiyo kipimo cha maendeleo,si kweli.Inabidi uziangalie hizo indicators zote halafu ndiyo utupangie list ya matajiri na masikini.
Ni kweli kabisa kuwa GDP haiwezi kuwa kipimo halali cha maendeleo ila kinaweza kabisa kuwa kupimo cha Umaskini..
Leo hii Mtanzania mwenye kipato ca mwezi laki moja hawezi kuwa na maendeleo hata kama mbuzi na kuku wake hawahesabiwi...Huna kipato na kipatoi hicho ndicho kinachokuwezesha wewe kununua vitu vya kujiendeleza..
Kipimo cha maendeleo ni zaidi ya GDP lakini tutaweza vipi kuwa na hivyo ikiwa GDP yetu iko chini kiasi hicho!...Hizo barabara na Hospital zinajengwa na kitu gani hata ikiwa mikopoo kumbuka tu inatakiwa kulipwa...
 
Kama definition ya GDP, ambayo ni

the total market value of all final goods and services produced in a country in a given year

mnaikubali basi sioni kwanini msione yafuatayo:

Sehemu kubwa ya "goods and services" zinazozalishwa na Watanzania hazioorodheshwi na kupata thamani yake kwani haziko katika uchumi rasmi.

Wakata nywele, mama ntilie, makondakta, watumishi wa ndani, wauza nyama mabuchani vijijini, machinga, etc ni sehemu kubwa sana ya wazalisha mali Tanzania, lakini mchango wao hauko kweye hilo li-GDP lenu.
 
Back
Top Bottom