Tanzania's CAG Report; March 2012

Inashangaza sana!barabara zote msaada toka japan,dawa zote toka global fund,vifaa shule na misitu danida,sida,norad,eu
 
naomba govt isikope tena,na mkopo wowote bora wananchi tushirikishwe!PERU gold inachangia 65%ya pato la taifa!sisi 0.1%
 
Huu wote ni upuuzi tu! Hakuna lolote ambalo CAG amelisema ambalo halijawahi kusemwa; hakuna lolote analosema serikali imefanya au kushindwa kufanya ambalo halijawahi kusemwa kabla. Wanaoambiwa ni watu wale wale, wa chama kile kile na Bunge linaongozwa na watu wale wale! Ni upuuzi tu wangetaka kudhibiti matumizi ya fedha wangeshadhibiti mwaka wa kwanza wa JK madarakani!

Yaani utafikiri ni zile enzi za kupiga makofi!!!!!!!!! Funny stuff haya mambo yakianza kujadiliwa na wabunge eti kunakuwa na sides, and guess what ule upande wa CCM siku zote utatetea matumizi hayo. Mwisho wa siku bunge halifanyi chochote kwa kisingizio kwamba majority wameamua wanabariki matumizi hayo.Lakini the majority of the majorities (Wananchi) badala ya kuwawajibisha hawa temporary majorities watapewa kanga na kofia sometimes pilau kuuza umajority wao......... Bongo tambarareeeeeeee hahaha ahahahah ahahaha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Huu wote ni upuuzi tu! Hakuna lolote ambalo CAG amelisema ambalo halijawahi kusemwa; hakuna lolote analosema serikali imefanya au kushindwa kufanya ambalo halijawahi kusemwa kabla. Wanaoambiwa ni watu wale wale, wa chama kile kile na Bunge linaongozwa na watu wale wale! Ni upuuzi tu wangetaka kudhibiti matumizi ya fedha wangeshadhibiti mwaka wa kwanza wa JK madarakani!

Wellsaid chakusikitisha zaidi uwingi wa magamba bungeni wanapitisha uozo kwa kura zao za ndiyo.
Shame on u magamba mwisho wenu waja.
 
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh jana aliwasilisha ripoti yake bungeni inayoonyesha kuendelea kuwapo kwa ufisadi wa kutisha serikalini huku deni la taifa likiongezeka kutoka Sh10.5 trilioni mwaka juzi na kufikia Sh14.4 trilioni mwaka jana.

CAG alisema Serikali imetumia Sh 544 bilioni bila kuidhinishwa na Bunge, Sh bilioni moja zimelipwa mishahara kwa watumishi hewa na Sh 3bilioni zimetumika katika Balozi za Tanzania nje ya nchi ambazo ziko nje ya bajeti iliyoidhinishwa na mhimili huo wa dola wa kuisimamia Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Utouh alisema deni la taifa limeongezeka kutoka Sh10.5 trilioni mwaka wa fedha wa 2009/2010 hadi kufikia Sh14.4 trilioni mwaka 2010/2011, sawa na ongezeko la asilimia 38.
“Kuna ongezeko kubwa la deni la taifa, lakini hoja hapa si kuongezeka kwa deni la taifa bali ni kwamba deni hili limeletwa kwa mikopo yenye manufaa kwa taifa na yenye kukuza uchumi wa nchi? Hii ndio hoja ya msingi ya kuangalia,”alisema.

SOURCE: MWANANCHI
Thursday, 12 April 2012 20:54

TUTAFIKA KWELI WATANZANIA WENZAGU? HAYA NDIO MAISHA BORA???.......
 
CAG aibua ufisadi wa kutisha serikalini Send to a friend
Thursday, 12 April 2012 20:54
0digg
sadi-cag.jpg
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti za mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2011, zilizowasilishwa jana Bungeni mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, John Cheyo. Picha na Edwin Mjwahuzi​
Daniel Mjema, Dodoma, Aidan Mhando, Dar
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh jana aliwasilisha ripoti yake bungeni inayoonyesha kuendelea kuwapo kwa ufisadi wa kutisha serikalini huku deni la taifa likiongezeka kutoka Sh10.5 trilioni mwaka juzi na kufikia Sh14.4 trilioni mwaka jana.

CAG alisema Serikali imetumia Sh 544 bilioni bila kuidhinishwa na Bunge, Sh bilioni moja zimelipwa mishahara kwa watumishi hewa na Sh 3bilioni zimetumika katika Balozi za Tanzania nje ya nchi ambazo ziko nje ya bajeti iliyoidhinishwa na mhimili huo wa dola wa kuisimamia Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Utouh alisema deni la taifa limeongezeka kutoka Sh10.5 trilioni mwaka wa fedha wa 2009/2010 hadi kufikia Sh14.4 trilioni mwaka 2010/2011, sawa na ongezeko la asilimia 38.
“Kuna ongezeko kubwa la deni la taifa, lakini hoja hapa si kuongezeka kwa deni la taifa bali ni kwamba deni hili limeletwa kwa mikopo yenye manufaa kwa taifa na yenye kukuza uchumi wa nchi? Hii ndio hoja ya msingi ya kuangalia,”alisema.

Ufisadi balozi na Mfuko wa Jimbo
Kuhusu ukaguzi katika balozi zote 32, Utouh, alisema ukaguzi uliofanywa katika ofisi hizo umebaini kuwapo matumizi yasiyoridhisha na kuwapo kwa Sh3 bilioni ambazo zimetumika nje ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge la Jamhuri.
Kuhusu Mfuko wa Jimbo (CDCF) ulioanzishwa kwa Sheria ya Bunge, ripoti hiyo inaonyesha kuwa Sh2.6 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za mfuko huo hazikutumika katika Halmashauri 51 zilizokaguliwa.

Kwa upande wa mashirika ya umma, alisema baadhi yake hayana bodi za wakurugenzi, vikao vya bodi haviitishwi kwa wakati na baadhi ya mashirika hayo huchelewa kukamilisha hesabu zao za mwaka kwa wakati.

Misamaha ya kodi na mfumo bajeti
Mbali na kukua huko kwa deni la taifa, CAG alisema pamoja na wananchi, wabunge na asasi za kiraia kupigia kelele misamaha ya kodi, ukaguzi umeonyesha kuwapo kwa misamaha ya kodi inayofikia Sh1.02 trilioni.

Alifafanua kuwa taarifa za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), zilionyesha kuwa misamaha ilitolewa kwa taasisi mbalimbali yenye thamani ya Sh1,016,320,300,000 ambazo ni sawa na asilimia 18 ya makusanyo yote nchini.
Kwa mujibu wa Utouh, kama kiasi hicho kisingesamehewa, TRA ingekusanya Sh6.5 trilioni ikiwa ni sawa na Sh717.4 bilioni zaidi ya kiasi kilichokadiriwa kukusanywa ambacho ni Sh6,566,525,544,378.

“Siku zote tumekuwa tukipiga kelele kuhusu misamaha ya kodi ingawa tunasema misamaha ya kodi haiepukiki, lakini lazima isimamiwe na iwe ni lazima kutolewa…kwa kweli eneo la misamaha ya kodi ni la kutazamwa,”alisema.

Alikosoa mfumo mzima wa mchakato wa kupitisha bajeti akisema, mjadala wa bajeti huanza Juni hadi Agosti kila mwaka wakati sheria ya matumizi ya fedha zinazopitishwa hutakiwa kuanza Julai mosi.

Alifafanua kwamba mjadala wa bajeti huanza kwa kujadili bajeti ya taifa ambayo pia hupitishwa kabla ya kuanza kujadili fungu moja moja la bajeti na hivyo, kufanya mchakato mzima wa kupitisha bajeti uonekane ni kugonga tu mhuri.
“Utaratibu huu unafanya mchakato mzima wa bajeti uonekane kama ni zoezi la rubber stamp (kugonga mhuri) kwani wabunge tayari walishapitisha bajeti ya taifa ambayo kimsingi inatokana na bajeti za fungu moja moja,” alisema.

CAG alipendekeza Serikali ijadiliane na Bunge kuhusu uwezekano wa kubadili mzunguko wa bajeti ya taifa ili kuruhusu mabadiliko ya tarehe za majadiliano kukamilika, kabla ya au ifikapo Juni 30 ya kila mwaka.

Katika mapendekezo hayo, CAG alisema mjadala wa wabunge kuhusu bajeti uanze kwa kujadili bajeti za fungu moja moja na bajeti ya taifa iwe ya mwisho kujadiliwa ili kuondoa ile dhana ya kuwa na bajeti isiyo na uhalisia.

Hali katika halmashauri
Alisema kuwa ukaguzi maalumu uliofanywa katika halmashauri za wilaya za Sengerema, Ludewa, Kishapu, Kilindi, Moshi,Monduli, Longido na Manispaa ya Ilala umebaini kuwapo kwa ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma.
CAG pia aliagiza kufanywa ukaguzi maalumu katika Halmashauri za Arusha, Songea, Morogoro, Kilindi na Misungwi kutokana na kutoridhishwa na taarifa za Halmashauri hizo kuhusu matumizi ya fedha za umma.

Akizungumzia ufisadi huo mara baada ya taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Augustino Mrema, alisema bado CAG ana kibarua kigumu kutokana na kuwepo mtandao wa mafisadi ndani ya halmashauri.

“Kwa ripoti hii ya CAG nchi inadidimia, nchi inasambaratika ni kama tunafanya mchezo wa kuigiza mimi napendekeza kiundwe kikosi kazi maalumu cha kupambana na mtandao wa wizi ndani ya halmashauri nyingi nchini," alisema Mrema
Alisisitiza kuwa nchi imezidiwa nguvu na wezi na mafisadi ndani ya halmashauri, ambao wamejipanga kila kona kutekeleza wizi wao kwa kuwa haiwezekani kila mwaka kuwepo ripoti za ubadhirifu wa mabilioni.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe, alisema CAG ametimiza wajibu wake kikatiba na sasa ni kazi ya wabunge kuhakikisha Bunge linatoka na maazimio juu ya ripoti hiyo.
Mbali na Zitto, kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuu(PAC), John Cheyo alionyesha kushangazwa na kuendelea kukua kwa deni la taifa wakati miradi mingi nchini haina fedha.

“Deni la taifa linatupa matatizo sisi wote hapa kwa sababu mimi sielewi maana tunakopa, lakini miradi yetu haina pesa hapa kuna kitendawili,”alisema Cheyo na kusema Bunge itabidi lijadili na kutegua kitendawili hicho.
Katika hatua nyingine, CAG Utouh amesema Ripoti ya Ukaguzi wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), tayari imekamilika na amekwishaikabidhi kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda tangu Aprili 6 mwaka huu.

Agosti 13 mwaka jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, George Mkuchika alikambidhi CAG kazi ya ukaguzi wa hesabu za UDA na mchakato wa uuzwaji wa hisa zake ambao unahusisha vigogo mbalimbali akiwemo, Idd Simba.

Akizungumza jijini Dares Salaam juzi, CAG Utouh alisema tayari ripoti iko kwa Waziri Mkuu kwa ajili ya hatua zaidi.
Alisema Aprili 6 mwaka huu baada ya kukamilika kwa ukaguzi, aliikabidhi kwa Waziri Mkuu kufuatia kukamilika kwa ukaguzi wa ripoti hiyo.

“Kwa sasa mimi nimeshamaliza kazi yangu ya ukaguzi wa UDA, ambapo Aprili 6 mwaka huu siku ya Ijumaa kuu, ndipo nilipo ikabidhi kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda,” alisema Utouh na kuongeza;

“Kitu ambacho kinatakiwa sasa ni kusubiri ripoti hiyo ipitiwe na Waziri Mkuu ndipo taarifa rasmi nini kilichokaguliwa na kilicho patikana katika ripoti hiyo kitawekwa wazi,” alisema.

CAG,alibainisha kwamba kwa sasa yeye kama mtu aliyepewa jukumu la kufanya kazi hiyo ya ukaguzi, amesha ikamilisha kwa kila kitu na kwamba ripoti hiyo haipo tena mikononi mwake.

“Ndugu zangu kwa sasa mimi sina tena hiyo ripoti ya UDA na kwamba kitu kinachotakiwa sasa ni kuwa wavumilivu kwani baada ya muda mfupi Waziri Mkuu akiipitia, kila kitu kitawekwa wazi,” aliseama.

Hatua hiyo inafuatia kuibuliwa kwa kashfa ya uuzaji UDA na wabunge wa Dar es Salaam Agosti mwaka jana kwamba, taratibu zilikiukwa wakati wa uuzaji dhidi ya Kampuni ya Simon Group, inayomilikiwa na Robert Kisena.


Baadhi ya vigogo wanaodaiwa kuhusika na kashfa hiyo, ni Meya wa Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi, Idd Simba, na Meneja Mkuu wa UDA, Victor Milanzi. Wote wamehojiwa na tume.

UDA ilikuwa inamilikiwa kwa pamoja na Halmashauri zote za Jiji la Dar es Salaam na Serikali Kuu kupitia Hazina, wakiwa na jumla ya hisa milioni 15, kila hisa moja ikiwa na thamani ya Sh100.

Kutokana na mchanganuo huo, Halmashauri ya Dar es Salaam ilikuwa inamiliki asilimia 51 ya hisa hizo, huku Hazina ikimiliki asilimia 49. 



Februari 11, mwaka jana, Bodi ya Wakurugenzi ya UDA, chini ya Idd Simba, ilikutana na uongozi wa Simon Group ikiongozwa na Kisena na kusaini mkataba, ambao ulithibitisha kwamba UDA ilikuwa imeiuzia Simon hisa milioni 7.8 sawa na asilimia 52.535 ya hisa zote kwa thamani ya Sh1.142 bilioni.



Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

[h=4]Comments [/h]


0#9 mkereketwa 2012-04-13 12:48Tatizo ni kuwa mafisadi wanaokamatwa hawachukuliwi hatua.Tumeona uwizi uliofanyika kwenye pesa za Halmashauri,unu nuzi wa Rada n.k.Tunawajua walioiba lakini hawachukuliwi hatua yoyote.Kweli jela ni ya maskini tu tajiri hawezi kwenda jela.Waziri mkuu na Raisi tunaomba mtuokoe na hawa mafisadi mbona mmekaa kimya?Au kwa sababu nyinyi hamupati madhara yoyote?Sisi wanainchi ndio tunaumia
Quote











0#8 Bora d 2012-04-13 12:01Mr CAG kazi nzuri!

Tatizo ni Serikali kuu imundwa kwa njia ya kujuana!
Mr Pinda hana ujasiri wa kupitisha maamuzi magumu kama ya kuiomba ofisi ya mwanasheria mkuu kufungua kesi kwa Wezi hawa.

Mr Mrema Watanzania hawahitaji kuundwa kwa sungusungu katka kuzuia wizi wa mali zao- tunazo Takukuru,Polisi ,Mahakama, mwanasheria Mkuu, CAG na vyombo vingine vingi vya kufanya kazi hizi. Kama unao ushawishi Waambie wafanye kazi zao-
Tatizo ni wizi ukibainika WEZI HAWACHUKULIWI HATUA yeyote.

Quote











+1#7 ORASINYHO 2012-04-13 10:46Yah. This is the work of Coconut Head.
Quote











0#6 SANGOVA 2012-04-13 09:54Hivi tutaendelea kusomewa taarifa za CAG mpaka lini bila kuchukua hatua?Mi naona hakuna haja ya kuwa na hyo CAG manake anafanya kazi muhimu ya kuionesha serikali madudu yanayofanyika kuhusiana na matumizi ya fedha lakini serikali inaishia kusikia tu haichukui hatua yoyote,tizama badala ya deni la taifa kupungua kutokana na taarifa ya kaguzi zilizopita imeongezeka kutoka trilion 10 -14,matumizi ya 544 bilion ambayo bunge halikuidhinisha ,kungekuwa na utekelezaji wa mapendekezo ya kaguzi za huko nyuma haya yasingejitokeza,serikali ijitazame upya na kama haioni haja ya kutekeleza mapendekezo ya CAG basi waifunge ofisi hiyo mara moja.
Quote











-1#5 S M Sikare 2012-04-13 08:39Kutokana na kipindi cha TV via TBC leo asubuhi, napenda kuunga mkono kuhusu 'unclaimed dividends' kuwa zisibaki mali ya Kampuni. Hizi ni 'dividends' za wenye hisa ndogo ndogo wengi na hivyo kwa uchache wake haziwafikii wenye hisa (include stailed chks?) - hisa moja ni ndogo lakini kwa pamoja ni nyingi sana.
Pendekezo ni kupeleka Hazina na mimi hii iwe hatua ya mwisho baada ya hatua hizi kushindwa (haki kwanza kwa waliozizalisha) :
(1) Kama inawezekana kila hisa zinapotolewa, wapelekewe 'cummulative amount' inayojumulisha 'uncollected dividends'.
(2) Kama (1) hapa juu haitekelezeki basi hiyo 'total uncollected dividents' igawiwe sawa (equal distribution) kwa kila mwenye hisa wanaoangukia katika kundi la hao 'shareholders' wadogo waliozalisha hizo 'unclaimed dividends'.

Quote











+2#4 rutashubanyuma 2012-04-13 08:11Bunge letu ni picha tu. Tunahitaji sheria ambayo taarifa za CAG zikiisha pi[NENO BAYA] na bunge zifanyiwe kazi na ofisi za DPP na Takukuru. Vinginevyo Bunge is just another talking shop..........waache domo na walete sheria ichukue mkondo wake wa kuwaadabisha wote wale ambao wanatajwa kwa matumizi mabaya ya fedha za umma....
Quote











+2#3 Jomoo 2012-04-13 03:41“Kwa ripoti hii ya CAG nchi inadidimia, nchi inasambaratika ni kama tunafanya mchezo wa kuigiza mimi napendekeza kiundwe kikosi kazi maalumu cha kupambana na mtandao wa wizi ndani ya halmashauri nyingi nchini," alisema Mrema
Mrema sasa umeanza kuzeeka! Tuna vithibitisho(ev idence) za wizi, tuunde kikosi tena???? Au tuwapeleke watu mahakamani?? wao ndio wakajitetee kuwa hawakuiba, wakithibitishwa ni wezi walipe/wafungwe. Nna uhakika hili likitendeka kwa halimashauri mbili tu HATUTAKUWA na kesi za wizi tena.
Hebu tulitendee haki hili Taifa jamani. Ntapenda kusikia wabunge "wetu" wataamua nini juu ya hili

Aksante

Quote











+3#2 vax 2012-04-13 03:35KAZI IPO KWELI KWELI.SERIKALI YA CCM INATIA AIBU SANA,KWANI KILA KUKICHA UTASIKIA TAARIFA ZA UFISADI NDANI YA SERIKALI.BILA AIBU WATATOKEA WAKINA NAPE NA KUDAI KWAMBA WANAPAMBANA NA UFISADI HIVI HAWAONAGI HAYA KUSIMAMA MBELE YA WATANZANIA NA KUELEZA UONGO USIO NA MASHIKO? MUNGU AWASEMEHE WANATESA WATU
Quote











+1#1 mzee hamis 2012-04-13 03:19Mhhh...sasa muheshimiwa JK unataka nini zaidi habari ndiyo hiyo....kama unapenda nchi yako funguka na utuwekee mambo sawa kabla hujeenda kupumzika baada ya miaaka 4.
Inauma sana

Quote









 
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh jana aliwasilisha ripoti yake bungeni inayoonyesha kuendelea kuwapo kwa ufisadi wa kutisha serikalini huku deni la taifa likiongezeka kutoka Sh10.5 trilioni mwaka juzi na kufikia Sh14.4 trilioni mwaka jana. CAG alisema Serikali imetumia Sh 544 bilioni bila kuidhinishwa na Bunge, Sh bilioni moja zimelipwa mishahara kwa watumishi hewa na Sh 3bilioni zimetumika katika Balozi za Tanzania nje ya nchi ambazo ziko nje ya bajeti iliyoidhinishwa na mhimili huo wa dola wa kuisimamia Serikali. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Utouh alisema deni la taifa limeongezeka kutoka Sh10.5 trilioni mwaka wa fedha wa 2009/2010 hadi kufikia Sh14.4 trilioni mwaka 2010/2011, sawa na ongezeko la asilimia 38. “Kuna ongezeko kubwa la deni la taifa, lakin

kufika ni mpaka mchwa wadhibitiwe
 
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amesema misamaha ya kodi imepunguza makusanyo ya taifa yenye thamani ya Sh. trilioni 1.02 sawa na asilimia 18. Utouh aliyasema hayo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana, wakati akizungumza na waandishi wahabari kuhusiana na ripoti zake za ukaguzi kwa mwaka wa fedha uliomalizika Juni 30, mwaka jana.

"Taarifa za mapato ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), zilionyesha misamaha iliyotolewa kwa taasisi mbalimbali yenye thamani ya Sh. 1,016,320,300,00 ikiwa ni sawa na asilimia 18 ya makusanyo yote ambayo ilikuwa ni Sh. 5,550,205,244,378," alisema. Hata hivyo, alisema kiwango cha misamaha ya kodi cha asilimia 18 ni kikubwa sana ikilinganishwa na viwango vya misamaha ya kodi vinavyotakiwa kwenye nchi jirani za Kenya, Uganda na Rwanda.

DENI LA TAIFA

Alisema deni la jumla la taifa nalo limeongezeka kwa asilimia 38 kutoka Sh. 10,503,806,011,884.90 (trilioni 10.5) mwaka 2009/10 hadi Sh. 14,441,617,939,770.20 (trilioni 14.4) mwaka 2010/11.

MIKATABA INA MAPUNGUFU

Kuhusu mikataba, Utouh, alisema katika kuchunguza utoshelevu wa usimamizi wa mikataba, uchambuzi uliofanywa na Mamlakaya Sheria ya Manunuzi ya Umma (PPRA), ulibaini mapungufu mengi. Aliyataja mapungufu hayo kuwa ni baadhi ya mikataba kukosa nyaraka muhimu kama vile masharti ya mikataba, michoro na maelezo ya kina ya jinsi ya kutekeleza mkataba.

Mengine ni kutotumika kwa kifungu cha fidia kwa kuchelewa kutekeleza mikataba na kutokuwepo mipango ya kudhibiti na kutoa hakikisho la ubora katika utekelezaji wa mikataba, kazi zilizokamilika hazikufanyiwa tathmini kuona kama zimekidhi matakwa ya utekelezaji aliyopewa mkandarasi katika mkataba.

Mapungufu mengine ni taarifa za utekelezaji na usimamizi kutoandaliwa, muda wa utekelezaji mikataba kuongezwa bila kufuata taratibu, malipo kufanywa kwa kazi ambazo hazijafanyika na kutokuteuliwa kwa kamati za mapokezi na ukaguzi wa bidhaa zinazonunuliwa kuthibitishwa usahihi pamoja na ubora na idadi wa bidhaa hizo.

BAJETI HEWA

Alisema pamoja na bajeti kupitishwa na Bunge, lakini serikali mara nyingi haijawahi kuitekeleza kama inavyopitishwa. "Sehemu kubwa ya bajeti ya wizara, idara na wakala hupunguzwa ili iendane na hali halisi ya mapato ya serikali," alisema. Alisema kuidhinisha shughuli ambazo hazitaweza kugharimiwa ndiko kunakosababisha kuwepo kwa madeni makubwa hasa katika ujenzi wa barabara, utoaji huduma na matumizi kwa shughuli zisizokuwa katika mipango.

"Ipo haja ya kuutazama upya mchakato mzima wa bajeti ili kuhakikisha kwa bajeti yenye uhalisia inaandaliwa kwa namna ambayo itakidhi mipango inayo kusudiwa kutekelezwa…Ni vyema bajeti iheshimiwe, izingatiwe na itumike kama chombo cha kudhibiti matumizi ya serikali," alisema.

HALI ZA BALOZI MBAYA

Kuna thread yake hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/250414-hali-ya-balozi-zetu-ni-mbaya.html

UFISADI SERIKALI ZA MITAA

Alisema jumla ya vitabu 682 vya stakabadhi za mapato kutoka halmashauri 36 havikuwasilishwa kwa ajili ya ukaguzi. Alisema halmashauri 47 zilikuwa na jumla ya Sh. 4,227,984,618 yakiwa ni mapato ambayo mawakala hawakuwasilisha katika halmashauri husika.

Utouh alisema ulegevu katika udhibiti wa ndani na ufuatiliaji wa makusanyo ya mapato ulisababisha kutokusanywa kwa mapato kutoka kwenye vyanzo vya ndani yenye jumla ya Sh. 8,332,985,545 kutokana kwa wadaiwa wa kodi mbalimbali katika sampuli ya halmashauri 22, kwamba mapungufu katika usimamizi wa matumizi yamesababisha hasara ya Sh bilioni 1.08. Alisema baadhi ya watumishi wa halmashauri wasio waaminifu wamekuwa wakishirikiana na wafanyakazi wa benki katika kuiibia serikali.

MISHAHARA HEWA

Alisema kutofanya usuluhisho wa mara kwa mara katika udhibiti wa mishahara kumesababisha malipo ya mishahara kwa wastaafu, watoro na walioachishwa kazi kumesababisha kulipwa kiasi cha Sh. 961,394,959 katika halmashauri 36.
Alisema pia watumishi 22 katika halmashauri tatu walilipwa mishahara ambayo ilikuwa ni zaidi ya viwango vyao vya mishahara yenye jumla ya Sh. 42,869,832.

MAKATO MAKUBWA

Aidha, CAG alisema kuwa tatizo la watumishi kukatwa zaidi kiwango kinachoruhusiwa katika mishahara bado linaendelea. "Ukaguzi uliofanyika katika halmashauri 55 umeonyesha kuwa zaidi ya watumishi 8,827 walikuwa wakipokea pungufu ya theluthi moja (1/3) ya mishahara yao," alisema. Alisema hiyo ni kinyume na matakwa ya waraka namba CCE.45.271/01/87 wa Machi 19, wa mwaka 2010 uliotolewa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

MISHAHARA VYUO VIKUU

Alisema mapitio katika vyuo vya umma 17 ukaguzi ulibaini kutowiana kwa kumbukumbu kati ya Hazina, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na vyuo vikuu. Pia alisema mishahara iliyolipwa kwa wafanyakazi walioacha kazi ni Sh. bilioni 1.9. "Ukaguzi ulibaini kuwa Hazina ilituma fedha katika vyuo kwa watumishi ambao walishaondoka katika ajira za vyuo vikuu husika," alisema.

Alisema Hazina ilituma Sh. milioni 612.1 kwenda Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, (MUCE), Sh. milioni 134.74 Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Sh. milioni 194.4 Chuo cha Mzumbe (MU), Sh. milioni 181.0 Chuo cha Ustawi wa Jamii na Sh. milioni 778.7 Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Dar es Salaam.


Aidha, alisema Hazina imekuwa ikipeleka fedha pungufu kwenye vyuo vikuu vya umma kiasi ambacho hakitoshelezi kulipa mishahara kwa watumishi. Alitolea mfano kwa Chuo Kikuu cha Mzumbe kuwa kwa miaka mitatu mfululizo kutoka mwaka 2008/09 hadi mwaka 2010/2011 upungufu wa fedha zilizopelekwa ulifikia Sh. bilioni 1.1.

USIMAMIZI WA RASLIMALI

Alisema ukaguzi huo umebaini kuwa majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma hayajaonyeshwa katika vitabu vya raslimali za chuo hicho na pia hayajaonyeshwa katika vitabu vya mifuko ya hifadhi ya jamii.

MIKOPO YA MIFUKO YA JAMII

Alisema ukaguzi pia umebaini kuwa kuna mikopo isiyorejeshwa yenye jumla ya Sh. bilioni 91.7 na Dola za Marekani milioni 9.65 iliyotolewa na mifuko ya jamii kwa ujenzi wa majengo mbalimbali. Ukaguzi huo umebaini kuwa fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, nyumba za polisi, jengo la machinga, kiwanda cha matairi Arusha na makampuni mengine binafsi.

Aliyataja makampuni hayo kuwa ni Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira, Kiwanda cha Saruji cha jijini Dar es Salaam, Kiwanda cha Sukari Kagera na Medtch Indestrial Co. Ltd chini ya udhamini wa serikali. Alisema kutorejeshwa kwa mikopo hiyo iliyodhaminiwa na serikali ni kinyume cha Sheria ya Udhamini ya mwaka 1974 na kunaiweka mifuko ya hifadhi katika hatari ya kupoteza fedha za wanachama na kuhatarisha uwezo wa mifuko hiyo kufanya uwekezaji zaidi kwa manufaa ya wanachama wake.

DAWA ZILIZOISHA MUDA

Utouh alisema kumekuwapo kwa mrundikano wa dawa zilizokwisha muda wake zenye thamani ya Sh. bilioni 8.4 katika Bohari Kuu ya Dawa (MSD). Alisema dawa zilikwisha muda wake zimekuwa zikilimbikizwa tangu mwaka 2002.

Hata hivyo, katika ukaguzi huo ilibainika kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii haipeleki MSD fedha zote zinazopokelewa kutoka Hazina kwa ajili ya manunuzi ya dawa na vifaa vya matibabu. Alisema walibaini kuwa Sh. milioni 658.9 hakikupelekwa MSD katika mwaka wa fedha 2010/2011.

Pia alisema serikali haijalipa deni la Sh. bilioni 40 zinazodaiwa na MSD Vile vile, ilibainika kuwa MSD imekuwa na mapungufu katika kuzingatia Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004 na kanuni zake za 2005 kwa kufanya manunuzi yenye thamani ya Sh. bilioni 7.0, manunuzi ya Dola za Marekani milioni 23.46 na mengine ya Euro milioni 4.7 bila kuzingatia sheria na kanuni hizo za manunuzi.

MFUKO WA BIMA YA AFYA

Alisema katika ukaguzi uliofanywa katika mfuko huo ulibaini kuwa mfumo funganifu wa utambuzi wa wanachama haukuweza kubaini wanachama batili waliopatiwa huduma za afya na mfumo huo kati ya watoa huduma waliokaguliwa katika kipindi cha ukaguzi.

Alisema mfuko huo una udhaifu katika udhibiti wa madai ya maabara yanayotolewa na watoa huduma kulingana na uhakiki uliofanyika katika Hospitali za KCMC, Kituo cha Faraja na Moshi Upendo, pia ilibainika kuwa taratibu zinazotumika katika utoaji wa dawa zina udhibiti dhaifu wa kumbukumbu zinazoingizwa katika madai.

FEDHA ZA MIRADI

Alisema fedha za miradi zimekuwa hazitumiki kama ilivyokubaliwa kwenye makubaliano na wafadhili. Alisema jumla ya Sh 248,005,002 hazikutumika hadi mwisho wa mwaka wa fedha 2010/2011. Alisema kutozingatiwa kwa makubaliano kati ya serikali na wafadhili kuhusu ununuzi wa vifaa na huduma kumesababisha hoja za Sh. bilioni 1.3.

USALAMA WA BARABARANI

Alisema makosa ya kibinadamu yalichangia asilimia 75 ya ajali za barabarani kwa mwaka 2008, na makosa mengine kama vile ufundi na ubovu wa barabara imechangia asilimia 25. Alisema sehemu kubwa ya ukaguzi wa Kikosi cha Usalama wa barabarani ulijikita katika makosa ambayo hayachangii sana katika ajali za barabarani.

MFUKO WA JIMBO

Alisema jumla ya Sh. 2,683,368,422 zilizotengwa kwa ajili ya Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo (CDCF), hazikutumika katika halmashauri 51 zilizofanyiwa ukaguzi wa majaribio. Alisema hilo lilisababishwa na usimamizi duni wa mfuko wa kamati za maendeleo ya mfuko wa jimbo.

ASILIMI 20 YA FEDHA HAZIPELEKWI VIJIJINI

Alisema pia mgawanyo wa mapato kati ya halmashauri na serikali za vijiji/mitaa, halmashauri nyingi hazipeleki vijijini au kwenye kata asilimia 20 ya fidia ya kodi iliyofutwa kinyume cha maelekezo ya serikali. Alisema katika ukaguzi katika halmashauri 50 walibaini kuwa halmashauri hizo hazikulipa Sh. 1,556,830,464 kwa ajili ya mgao wa vijiji.

CHANZO: NIPASHE
 
Watanzania wenzangu, ripoti za ukaguzi wa serikali kuu, serikali za mitaa, mashirika ya umma, donor funded projects etc ni public documents. Wanaopenda kuzipitia kujua nchi hii inavyotafunwa na wenye meno wanakaribishwa. Wasiojua lugha ya mkoloni, zipo hadi za kiswahili, asante kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali.

www.nao.go.tz
 
Wanabodi,

Niko hapa Dodoma kwenye ukumbi wa mikutano ya waandishi wa habari Bungeni, ambapo CAG, Ludovick Uttouh, anazungumza na waandishi wa habari, kuhusu ripoti yake.

Kubwa kuliko ni serikali, imelifungua lile fuko kuu la hazina lililoko Benki Kuu ya Tanzania, na kujitotea kutoka fuko hilo, Shilingi, Bilioni 5.8 bila idhini ya Bunge!.

Kwa lugha rahisi, ni serikali imejichotea fungu hilo na kujitafunia, yenyewe bila kuomba kibali cha wenye fedha zao!.

Kuchukua kitu bila ruhusa ni wizi, regardless umefanyia nini hicho ulichochukua, hivyo serikali yetu imeiba Shilingi Bilioni 5.8 zetu!.

Wakuu wa zile oversight commitee za PAC-Cheyo, LAAC-Mrema na POAC-Zitto wapo hapa kutueleza serikali yetu iliyafanyia nini mabilioni hayo?.

Pascal.
Naendelezea hapahapa~~chochote chenye public interest kina mawazo na maamuzi yanayotoka kwa watu kwa ajili ya watu,mwenyekiti wa ccm ndiye anejigeuza kuwa mwenyekiti wa Tanzania,yeye ndiye anayeamua nini kiwe for public interest na kipi kisiwe,alipomtimua mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali baada ya mkaguzi huyo kusimamia public interest wewe Pascal Mayalla hukumgombeza magufuli au kumkumbusha kuwa pesa iliyopotea ni ya umma,na mkaguzi ndiye jicho la umma,unamshangilia mwizi halafu unaongea habari za public interest,fool
Mkuu Capt Tamar ,
Asante,
Ubarikiwe
Japo sina uhakika, kwavile siwezi kusoma mabandiko ya watu wote humu, lakini humu JF, mimi ni miongoni mwa tuliomuongelea sana CAG, Ofisi ya CAG na Ripoti za CAG!.
Nakutakia Jumapili Njema
P
 
Back
Top Bottom