Tanzanians Diaspora Summit on 18th December 2009

...wakati wa ile mijadala ya dual citizen kuna wasio na aibu(majority) waliita watanzania wanaokaa nje ni traitor,wabangaizaji,wazamiaji,unpatriotic etc tena cha ajabu ni wasomi na wengine hata wali suggest kuwa na dual citizen itafanya watumike kama spy/vibaraka,sasa leo vipi wanaona nao kumbe wanaweza kuchangia maendeleo ya taifa?

Katika msafara wa Mamba, Kenge hawakosi.
 
Katika msafara wa Mamba, Kenge hawakosi.

Mzalendo Kandambili;

Ni kweli kabisa, wengine huwa wanaongezea kuwa Katika msafara wa Mamba, Kenge hawakosi na hata Mijusi n.k.

Ili mradi tumegundua kuwa kuna upungufu wa kimikakati na sera katika maeneo fulani fulani, ni vema basii sisi kama Watanzania tunaopenda Kujiletea mabadiliko ya kweli, tutafute njia mbadala ya kujiletea maendeleo badala ya kuendelea kulaumu tu bila kutenda.

Ninayo imani kuwa tuna nafasi kubwa kama tutakuwa serious.
 
Sanctus Mtsimbe,
Mkuu, mnayo site yenu ambayo naweza kutembelea na pengine kujiunga..
 
...hapa umekuja pazuri sana maana members wengi sana humu wapo nje na tungependa kuchangia na kupata faida nyumbani maana sio siri wengi wana $$$ na idea nzuri sana lakini wamekosa tuu maeneo ya kuchannel hizo $$$ na idea zao,hopefully TPN itasaidia na itaweka process ya kuaminika na rahisi as much as possible,mimi nakupa idea moja ....watanzania wengi wanaoishi states wana vyama vyao/society na wanakutana mara kwa mara na wana email za members wao kwa hiyo jaribu kuwasiliana na watanzania through hizo society na wanaweza kukupa emails za wanachama wao in bulky na kukusaidia kusukuma agenda za TPN kupitia vikao vyao,utawapata wengi kwa wakati mmoja...mfano Uzalendo HomePage (california), Umoja Society of Minnesota - Umoja ni Nguvu (minnesota na wana member zaidi ya 1000 hawa)..vipo vingi tuu kuanzia NY mpaka Dallas,Atlanta,Boston etc kwa hiyo unaweza kupitisha agenda na semina za diaspora kwa urahisi na usisahau wanapenda party ile mbaya...fanya party/BBQ za diaspora hata mimi nitakuja (ha haha haha..)
 
Big things start with small innovative ideas!

Mzalend;

Tuko pamoja Mkuu, tuendelee kutiana moyo na kushirikiana katika hili . . . I can foresee the beginning of the new era if we are serious.

Umesoma post inayohusu Diaspora wa Rwanda katika Thread hii?
 
...hapa umekuja pazuri sana maana members wengi sana humu wapo nje na tungependa kuchangia na kupata faida nyumbani maana sio siri wengi wana $$$ na idea nzuri sana lakini wamekosa tuu maeneo ya kuchannel hizo $$$ na idea zao,hopefully TPN itasaidia na itaweka process ya kuaminika na rahisi as much as possible,mimi nakupa idea moja ....watanzania wengi wanaoishi states wana vyama vyao/society na wanakutana mara kwa mara na wana email za members wao kwa hiyo jaribu kuwasiliana na watanzania through hizo society na wanaweza kukupa emails za wanachama wao in bulky na kukusaidia kusukuma agenda za TPN kupitia vikao vyao,utawapata wengi kwa wakati mmoja...mfano Uzalendo HomePage (california), Umoja Society of Minnesota - Umoja ni Nguvu (minnesota na wana member zaidi ya 1000 hawa)..vipo vingi tuu kuanzia NY mpaka Dallas,Atlanta,Boston etc kwa hiyo unaweza kupitisha agenda na semina za diaspora kwa urahisi na usisahau wanapenda party ile mbaya...fanya party/BBQ za diaspora hata mimi nitakuja (ha haha haha..)

Mzalendo Koba;

Asante sana kwa mawazo yako mazuri na bila ya shaka tutayafanyia kazi. Pia I promise kwamba yeyote ambaye atakuwa interested hapa JF nitawasiliana naye kupitia PM ili nimpatie details wakati mwafaka ukifika.

Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, waliahidi kutupa contacts zote za balozi zetu na Jumuiya zote za Watanzania zilizoko ughaibuni.

If we will be able to make it . . . I doubt if we can beg of having another Sullivan Summit.
 
Du kweli hii ni kubwa sana kama mtaweza kufanikisha jambo hili,naomba isiwe domo tu kwani watz wana mambo mazuri mengi sana vitendo kidogo,wazo zuri sana.
 
Du kweli hii ni kubwa sana kama mtaweza kufanikisha jambo hili,naomba isiwe domo tu kwani watz wana mambo mazuri mengi sana vitendo kidogo,wao zuri sana.

Mzalendo Pay2Play;

Kwanza nashukuru kwa post yako ya kwanza kuanzia katika thread hii. Kwa niaba ya wana JF wote napenda kukukaribisha hapa Jamvini. Jisikie huru kuongea na kuchangia kile unachoamini tena bila woga.

Tumedhamiria sana kufanikisha azma hii na ndiyo maana tuliwaona hata Mambo ya Nje. Kuna Watanzania in Diaspora ambao wengine walishatuma na Papers kabisa. Kuna wengine ambao walikuja hata Tanzania kuleta maoni yao.

Mkusanyiko wa maoni yao mabalimbali ndiyo uliofanya tubuni mkakati huu. Pia failurers za Sullivan na China-Africa Simmits zimechangia sana.
 
Muda ni mdogo sana inabidi anzeni kuwatangazia wabongo kwenye web mbalimbali,blog ,na balozi zote na inabidi kuwe na special website on this sumit.pia muunde kamati maalum kwa jambo hili iwe na watu wenye sifa na maadili na si wahuni,wazo lenu ni kubwa sana na pengine mnaweza mkawa ndio chanzo cha maendeleo ya taifa letu changa.
 
Idea inaweza kuwa nzuri, lakini kwa jinsi ulivyoandika bado sijaona kama inatekelezeka. Kama utafafanua jinsi unavyoforesee outcomes za huo mkutano inaweza kusaidia kuelewa umuhimu wake. Nionavyo mimi ni kwamba kama kweli lengo ni kuhusisha diaspora basi hakuna better venue than internet, otherwise hatutakuwa na mkutano wa diaspora kwa maana sahihi.Na ninachojiuliza haswa ni swali hili, je ni nini kinakosekana sasa ambacho kitapatikana kwa kufanyika mkutano huo? kwa sababu kumeshakuwa na mikutano ya aina hiyo ukiwepo ule wa London lakini mpaka sasa hakuna utekelezaji wa maamuzi wernye kuleta mabadiliko mazuri kwa diaspora.
 
Asante Mzalendo;

Point taken . . . Ushauri wako tutaufuata. By mwanzo wa April 2009 groundwork itakuwa imekamilika. Je, utapenda nikuhusishe?
 
Idea inaweza kuwa nzuri, lakini kwa jinsi ulivyoandika bado sijaona kama inatekelezeka. Kama utafafanua jinsi unavyoforesee outcomes za huo mkutano inaweza kusaidia kuelewa umuhimu wake. Nionavyo mimi ni kwamba kama kweli lengo ni kuhusisha diaspora basi hakuna better venue than internet, otherwise hatutakuwa na mkutano wa diaspora kwa maana sahihi.Na ninachojiuliza haswa ni swali hili, je ni nini kinakosekana sasa ambacho kitapatikana kwa kufanyika mkutano huo? kwa sababu kumeshakuwa na mikutano ya aina hiyo ukiwepo ule wa London lakini mpaka sasa hakuna utekelezaji wa maamuzi wernye kuleta mabadiliko mazuri kwa diaspora.

Mzalendo ZeMarcopolo,

Nashukuru sana kwa maoni yako mazuri na mapendekezo mbadala. Ungesoma kwa makini post kuu na michango ya wengine hapa, ungeona majibu ya maswali yako. Hata hivyo nitajitahidi kukujibu:

Outcome:

Hii itategemea jinsi wajumbe watakavyoamua na kukubaliana lakini inategemea pia na resolutions. Ya kwangu machache ninayofikiria binafsi ni haya:

- Kama TPN inavyofanya sasa, inawezekana kuanzisha serious business ikiwa na Partners kutoka Diaspora na wale waliopo TZ on a serious note. Role ya Diaspora partner ikiwa ni kuangalia masoko ya nje (kama biashara hiyo ina hilo), kuchangia mtaji, mawazo ya kibiashara nk.
na partner wa nyumbani kuendesha na kusimamia biashara. TPN inaweza ikaguarantee usalama na uaminifu wa wote kama kiungo.

- Moja ya malalamiko toka Diaspora ni kuwa TZ hakuna serious people to Trust. Kuna ambao wametuma pesa wajengewe, haikutokea, kuna ambao wanatuma pesa kwa mambo mbalimbali lakini bado kuna matatizo. Tunapenda kuona TPN inakuwa kiunganishi muhimu cha vitendo na kuleta mafanikio kama ambavyo inatokea sasa.

- Kunaweza kuwa na kuanzishwa kwa Databank and Labour & Business Exchange Centre on a serious note. Kuna Diaspora ambao wangependa kurudi nyumbani lakini hakuna basic information ya uhakika ya nini wanaweza kufanya wakirudi bila kuteteleka. Databank inaweza ku-provide practical details in the real current situations, business opportunities, partners, nafasi za kazi nk.

- Kuongeza kasi za kufungua Chapters au kuwalink wa TZ na Diaspora kupitia jumuiya zao kwa mambo yote muhimu ya kujiletea maendeleo.

- Wenzetu wa jamii ya Kiasia hapa TZ wana Jumuiya zao km Majamatini n.k. ambako huko wanapeana mitaji na masoko ya biashara wakati sisi inatuwia vigumu kusaidiana kwa hilo. Tunaweza kufanya Summit ikawa kama market place na mahali pa masoko.

- Tunaweza kuanzisha bank/fund yetu on a seriuos note. Niliona resolution hiyo kama hiyo summit ya UK ingawa sijui utekelezaji wake umefikia wapi maana wizara ya mambo ya nje pia hawajui. TPN imeshaanzisha fund tayari. Inahitaji kuboreshwa. Kwa mtazamo wangu inatakiwa team work ya waliopo ndani na nje ya nchi kufanikiwa zaidi katika hili.

- Kuanzishwa kwa mtandao mkubwa ambao unaweza ukawaunganisha wa TZ wa ndani na nje katika mambo ya kibiashara, masoko na mengine ya kuleta maendeleo.

- Kubadilishana uzoefu katika sekta mbalimbali, nk.

Binafsi ndoto yangu ni kuona Watanzania Wasomi na Wanataaluma wanaweza kujijengea uwezo wa kibiashara na kimitaji ili kuboresha maisha yao na kuleta maendeleo.

Juu ya hoja yako ya Internet Forum /Sumit. . . Ndugu yangu ni wazo zuri lakini utashangaa sana nikikwambia kuwa TZ walio na Access na Internet hawafiki hata laki tano. Na katika hao sijui ni wangapi wanaoweza kufika katika ONLINE FORUMS kwa kukosa nafasi, kukosa wakati mwafaka na hata uwezo wa kutumia. Pia si wengi ambao wanahamasika kwa njai hii. Mfano mdogo ni idadi ya wale tu ambao wanatembelea JF na hata thread hii. JF ina wanachama karibu 6000 lakini active kwa siku sidhani kama wanapita 1000 na katika thread hii hata 500 hawaajafika mpaka sasa.

Nia ya kukutana pamoja TZ (Si UK au USA nk) ni pia kupata kujua hali halisi ya Tanzania wakati tunaongelea mambo haya kwani wadau wote muhimu tutawaalika. Pia face to face meeting with potential partners wa ndani na nje ya nchi n.k.

Pia inaweza kuwa ni nafasi ya kuyafanyia kazi mapungufu yote yaliyotokana na summit kama hizo zilizofanyika huko nyuma.

Kama una mawazo zaidi ya kuboresha au hata mbadala yanayoweza kufanya kazi, tuendelee kushauriana ndugu yangu.
 
Mkuu Sanctus Mtsimbe

Hongera, Hii idea ni nzuri sana...kwa kweli ningekushauri utafute muda muafaka ukiwa pamoja na timu ya maandalizi mkae chini na Balozi wa UK Mrs Maajar akueleze kwa undani mchakato mzima wa Forum iliyofanyika London April 2008. Watanzania ni wazito sana...lakini kuna kila sababu ya "kutokukata tamaa".

Ushauri wangu kwenye hiyo forum; jaribuni sana kutokuingia kwenye masuala ya kisiasa kama dual citizenship etc. Angalieni mambo yatakayoweza kutekelezeka moja kwa moja bila kuhusisha siasa au hata wanasiasa; mfano masoko na mitaji kupitia nyenzo na taratibu zilizopo.

Wageni waalikwa: ningeshauri katika listi ya wageni waalikwa mjaribu kutafuta mgeni mwalikwa ambaye ni mtendaji na sio mwanasiasa. Mfano: Badala ya kumualika waziri wa fedha, aalikwe Kamishna wa TRA ambaye atajibu maswali kitaalamu na sio blah blah za kisiasa. Zaidi ya mgeni rasmi, tafadhali msikose na tena ikiwezekana wapewe nafasi kuzungumza na kuulizwa maswali; Kamishna wa TRA, Mkurugenzi Mkuu wa Bandari na Mkurugenzi Mkuu wa Swiss Ports. Natumai wadau mtakubaliana na mimi kuwa hawa waheshimiwa watakuwa mambo ya kutueleza kutoka maeneo yao ya tukio.

Naomba kuwakilisha.
 
Mzalendo Yebo Yebo;

maoni yamezingatiwa na yatafanyiwa kazi.
 
Wazalendo Wenzangu;

Yale mambo tuliyaongea kuhusu Diaspora Summit 2009 sasa yameiva.

Tulikuwa na Meeting na Coordinators wa TPN Chapter ya USA na Europe na kuna mikakati ya kimsingi tumekubaliana.

Kuna Concept Paper tunayoiandaa na Invitation ambayo next week itakuwa tayari na tutaipost hapa.

Mawazo yenu mliyoyatoa nyalizungumzwa na yatazingatiwa, na kama kuna ambaye ana mawazo ya ziada anakaribishwa maana tunakutana tena this Sunday.

Itakuwa ni meeting ya vitendo zaidi kuliko maneno. Na hivyo yoyote mwenye project au kampuni na anahitaji partnership au kama ana concern zozote au issues za kushare anakaribishwa. Kutatakiwa Profile ya page moja ili wadau wapate kufahamu mapema.

Kuna matumaini makubwa sana kuwa meeting hii inaweza ikasaidia kukabiliana na changamoto za kimiradi au biashara na hasa kwa kundi la Wanataaluma na Watanzania wa Kawaida.
 
sactus mtsimbe
hamna haja ya wewe kukutana na balozi wa uk katika hili, balozi na watu wake wa karibu ni moja ya matatizo....
watu wote wanaokushauri ukutane na balozi wa uk wana ukaribu na balozi wa uk na wanajua wewe kufanya hivyo kutawawezesha wao kuingia na vitu vyao vya kitapeli....
hiyo mikutano uk ni mingi sana na inatumia hela nyingi sana lakini mafanikio yake ni zero.
na kama kuna mtu yeyote ana mafanikio ya hiyo mikutano ya UK aweke hapa jamvini...
na hii ndio sababu ambayo inawa put off watu wengi kuudhuria hiyo mikutano, watu wanaona ni mradi mweingine tu....

unatakiwa uweke malengo ya mkutano clear, mpaka sasa hivi hayapo clear, na nini kinatakiwa kipatikane kwenye mkutano

hata website yenu inaonyesha hamko active (hayo ni mawazo yangu)
 
Semilong

Ukiangalia katika link hii hapa:

https://www.jamiiforums.com/habari-...iaspora-summit-december-2009-empowerment.html

Kila kitu kimeelezwa kwa undani. Tafdhali ipitia na kama kuna mapungufu yoyote tusaidiane ili kuweza kuboresha.

Website yetu ya: www.tnp.or.tz tutapost hizo taarifa hivi karibuni sasa.
 
Back
Top Bottom