Tanzania: Zanzibar na katiba ya Jamhuri ya Muungano

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
sikiliza sauti ya mahojiano ya Amina Abubakari liongo wa Sauti ya Ugerumani na Mbunge wa Kwamtipura Hamza Hassan.

AUDIO | DW.DE Leo tarehe13.06.2012, baraza la Wawakilishi Zanzibar limepokea Sheria Nambari 8 ya mwaka 2012 iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete

Sheria hiyo imewekwa sahihi na Rais Kikwete juu ya kuanzishwa kwa tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Wananchi kuelekea uandishi wa Katiba Mpya.
Lakini kama katiba ya Zanzibar inavyosemwa ni kwamba sheria hiyo iwasilishwe tu kwa taarifa na wala isijadiliwe katika baraza la wawakilishi visiwani humo. Hamza Hassan ni mwakilishi wa baraza hilo na anasema kuna vipengee vingi katika katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ambavyo vinapaswa kubadilishwa ili kuwpa nguvu ya kuamua maswala fulani yanayohusu mustakbal wa nchi.
Amina Abubakar amezungumza naye na mwanzo anatupa maoni yake juu ya kuwasilishwa kwa sheria hii.
(Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi Amina Abubakar
Mhariri Othman Miraji



[h=2]Sikiliza mazungumzo kati ya Amina Abubakar na Hamza Hassan[/h]
 
Back
Top Bottom