Tanzania yazidi kushuka hadhi kwenye jumuiya ya kimataifa?

Poa tu, kwanza tanzania yenyewe ishakuwa shamba la bibi, kila mtu anavuna kwa wakati wake!
 
Sasa hivi Tanzania inabidi iufikirie upya huu unaoitwa jumuia/shirikisho la Afrika mashariki.....naona sie tunakubalika zaidi kusini mwa afrika kuliko hawa wabangaizaji wa ardhi yetuu...hebu tuamke kidogo tuanze kupeleka nguvu zetu kusini mwa Afrika coz huko wanatutambua na kutukubali zaidi kuliko hawa waroho wa rasilimali zetu...fyeeeeeee.
 
Hata mimi nilishtuka nilipoona Marais wote wanne wa EAC hawakuja kwenye sherehe hizi. Waliokuja ni Mutharika wa Malawi; Guebuza wa Mozambique na jamaa wa Comoros. Speech ya Rais Kikwete pia ilikuwa directed at showing the military prowess of TZ cf. that of the other EAC members. This may well be a sign that all is not well in the EAC. The fact that TZ refused to sign the recent EAC summit comminique in Bujumbura because of a joint defence clause may well be an illustration of the tensions within the EAC. One hopes that our neighbors in the EAC are not plotting anything against us. They will be doing so at their own peril - for once proveked TZ will not stop at the border - they should learn from Idd Amin.
 
Ukiona hivyo basi ujuwe wanaweza kuwasaidia "waasi wa Tanzania" endapo watakuwepo.

Msimamo wa vyama vya upinzani kwenye hiyo issue ukoje?

Ama mjadala huu ni wa wana CCM?
We don't need'em!
And definately we don't need people like you!!
Bring it on!!
And let them punks try us.
 
Mkenya eti ana rafiki? Toka lini? Ila tufanye urafiki na Museveni ili ajenge bomba ya mafuta toka Uganda mpaka hapa ninapokaa kariakoo. Ntawapiga bao wakinga wananitishia na hizi biashara zao mpya
 
Nakumbu hapo mwaka jana Rais wetu alienda Malawi kuhudhuria UZINDUZI WA KABURI la marehemu mke wa rais wa nchi hiyomwishoni mwa 2010.

Je, inamaana hata Prof Bingu wa Mutharika naye asiweze hata kuturudishia hisani hiyo kweli katika sherehe zetu hizi za kukata na shoka huku kimbunga cha mfumuko wa bei kikiendelea kila kona ya nchi!!!!!!!!!!!

Hapana, si bure hapa!
 
SOBY,

Taratibu mkuu!! Hizi kauli za SAUTI YA BATI si kawaida yako hata kidogo kwani imekuaje leo au ndio matokeo ya bia za bure Magogoni Mkuu??

Mtu ukiwa na hoja tena yenye mashika kama za wenzetu Mzee Mwanakijiji, William Malecela au Mchambuzi wote wa hapa JF, wala huhitaji kupiga kelele na hoja yako itasomeka tu.


We don't need'em!
And definately we don't need people like you!!
Bring it on!!
And let them punks try us.
 
Don't use your thought as conclusion my friend..watu wanaona ni uzindaki, ubakaji na ufisadi wa kodi za wananchi wao ndio maana hawajaja unadhani rais wa nchi kwenda nchi nyingine ni mchezo nini? eti kwenye sherehe za Uhuru wa tanganyika nchi na jina ambalo lishazikwa ni uwendawazimu...haikutakiwa hata wawakilishi wao kuja kwani ni ufujaji wa mali ya uma wao...na hawa wanaojiita wapigania uhuru walipigana na nani na vita hiyo ilikuwa na madhara gani kwani nijuavyo mimi hatujamwaga damu kudai uhuru sasa hao wapiganaji ni wapi? nijuzeni wataalamu wa

Mkuu hao marais nimewaita wanafiki sababu miaka ya nyuma walikuwa wanakuja katika hizi hizi sherehe, iweje leo wasije ukuzingatia hii ni sherehe kubwa kitaifa. Mbali ya kwamba wao ni majirani zetu, pia tupo kwenye mchakato wa kuwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo wao pia ni wahusika. Unafikiri wanatupa picha gani? Ndio maana ni rahisi ku-conclude kwamba wamekasirishwa na misimamo yetu katika mchakato wa EAC.
 
Bora hawajaja,wemepungu za gharama

Wametuma ujumbe e.g Kenya sent their Vice President Kalonzo Musyoka ,Rwanda sent their PM henceforth cost a.k.a gharama ziko pale pale! and remember they enjoy presidential status as they have been delagated those powers by the holders of the same!
 
Kaka usiende mbali sasa,

Hata Mwalimu Nyerere mwenyewe angekua hai angealikwa nadiriki kusema kwaa uhakika kwa Mchonga asingetokea kwa jinsi TULIVYOJITUTUMLISHA NA SHEREHE ZA KIFAHARI ya siku moja katika bahari ya umasikini wa zaidi ya miaka 50 kwa kutumbua Tshs 50 bn/-.

Wenye kuumwa na umasikini wa nchi ndio hivo hawapo tena kila siku ni sherehe tena yaa kukata na shoka huku hata na Ka-Rwanda kanatukimbia kabisa kiuchumi leo hii.

kale kaugonjwa ketu ka kupenda burdani kako kila kada - mtu mmoja mmoja hadi kule juu serikalini.
kijana jobless kufanyiwa sherehe ya harusi ya 20M, embu imagine!
 
Kwa marais wa nchi jirani zote kutohudhuria hii sherehe ni jambo la kushangaza. Na anaenishangaza zaidi ni Museveni! Kwa nini hajaja huyu baba? Kila kukicha amekuwa hapa kwa mambo madogo madogo leo imekuwaje? Kama sio Tanzania Museven asingekuwa hapo alipo sasa hivi. Pengine Prof Mukandara na wenzake UDSM wanatakiwa wakae kitako na kufikiri tena, ilikuwaje wakampa udaktari wa heshima huyu Museven?

Kama kuna tofauti kwenye masuala ya East Africa kwa nini wasitumie vikao badala ya kususa? Jamani hata huyu rais wa Burundi?

Hoja kwamba hawajui kama ni sherehe ya Tanzania au Tanganyika sio sahihi kwa sababu this is an internal issue na miaka yote hiyo wamekuwa wanatambua Tanzania. Kama tutaamua kurudisha Tanganyika tunaweza kufanya hivyo lakini kwa sasa jina linalotumika ni Tanzania.

Nionavyo mimi, Tanzania kwa sasa haina ujirani mwema. Tumezungukwa na watu wanaotutakia mabaya! Ni vizuri foreign policy iangaliwe vizuri.
 
SOBY,

Taratibu mkuu!! Hizi kauli za SAUTI YA BATI si kawaida yako hata kidogo kwani imekuaje leo au ndio matokeo ya bia za bure Magogoni Mkuu??

Mtu ukiwa na hoja tena yenye mashika kama za wenzetu Mzee Mwanakijiji, William Malecela au Mchambuzi wote wa hapa JF, wala huhitaji kupiga kelele na hoja yako itasomeka tu.
Ukiona mtu mzima anakosa patriotism huwa anatia hasira sana!
Mkuu ungejua wabeba maboksi wenzetu wa nchi jirani wanavyotubonda, halafu mafala wengine walio nyumbani wanavyotafuta affiliation na mambwiga hao hao wanaotubonda, unaweza kuua mtu.

Mwambie kama anataka support yao, awalete tu!!

Tutawafanya wote kuwa mishikaki, tutawapaka samli, tutawatundika kwenye vyuma na kuwawasha moto!!

I can't wait for that to happen..... Don't you dare mess with my MAMALAND!!
 
Leo nimeshindwa kushangaa kuona ni kwanini maraisi wa baadhi ya nchi hizo hawajona umuhimu huo na kuja kujumuika nasi kusherehekea miaka 50 ya Tanganyika yetu kama sisi tuliovyoona umuhimu wa utu wao katika kuwasaidia kupata uhuru wao?

1. Je hatuna maana kwao na thamani pia
2. Hatuaminiki na hatuna tena mchango kwao
3. nk

Wadau nisaidieni kutatua changamoto ndani ya kichwa changu

Kwa mambo yetu tunavyoyapeleka sasa, tunajidhalilisha wenyewe na kuishusha hadhi yetu mbele yao. Majirani wabaya hawa, ndo mana wananchi siku zote wamekuwa wakipiga kelele kuwakataa maana wanaajenda zao za siri hawa! Ole wenu viongozi wetu wanasiasa mkawakubali hawa waroho wa ardhi yetu!
 
labda hawakupewa elimu vizuri kuhusu cha maana tulichokifanya ktk miaka 50 hadi tunsherehekea kwa mbwembwe kihivyo
 
Sidhani kama kuna jambo la kushangaza hapa Tanzania imekataa na ardhi yake unategemea Kagame na Mwai Kibaki wangetia mguu Dar !.Suala la ardhi Kenya na Rwanda ni tata sana mipango na matarajio yao ilikuwa Tanzania.Kagame alijaribu kuchukua ardhi ya Congo akashindwa vibaya akadhani akiingiza nchi yake EAC atamaliza kiu ya ardhi kumbe safari hii waTZ walikuwa macho.Ng'ombe wa Rwanda wanategemea malisho Tanzania siku tukikataa ujue nusu ya ng'ombe lazima wauzwe haraka au wafee kwa kukosa malisho/majani.
 
Nimekuwa nafuatilia sana ziara na mialiko ya marais wa EAC hapa Tz,kila mara Kagame huwa anamtuma PM wake kuna shida gani hapa?au kuna kitu anaogopa??au anaogopa kukamatwa na wa tz wakawapa hao jumuoia ya kimataifa?kwa nn anaogopa kuja Tz?
 
Back
Top Bottom