Tanzania yazidi kushuka hadhi kwenye jumuiya ya kimataifa?

kipuyo

JF-Expert Member
Jul 30, 2009
1,785
1,464
Wengi wa viongozi waalikwa kutoka kwenye mataifa marafiki wa Tanzania waliohudhuria kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika ni wawakilishi wa marais wa nchi watokazo.Hakuna rais hata mmoja kutoka jumuiya ya Afrika ya mashariki.Je hii ina maana gani kwenye heshima yetu nje ya nchi?
Sidhani kama wote walikuwa wamebanwa kwa shughuli za nchi zao kiasi cha kushindwa kuhudhuria jubilei yetu
 
Leo tutasikia mengi, mbona JK hakwenda kwenye kikao cha Jumuiya ya Afrika Mashariki juzi juzi na alimtuma Dr. Gharib...unadhani wale wenzake walijisikiaje? ukiangalia sana hapo waliokuja ni viongozi toka nchi za SADC (Malawi, Namibia, Mozambique etc), na kwa kweli SADC ndio nchi rafiki wa kweli wa Tanganyika...kuliko hao wengine (EAC) wanaolilia ardhi yetu:lol:.
 
Kuna uwezekano mkubwa sana EAC ikalegalega. Lengo la wenzetu ni ardhi yetu tu! Tangu tumegoma kuiweka kwenye shirikisho hawana raha na sisi, ila kwa skali hii legelege sijui kama itaendelea na huo msimamo.
 
Watanganyika toka miaka ya 1963 - 1985 tulikuwa maalufu sana katika kusaidia nchi nyingi za kiafrika kupata Uhuru wao Kama vile Uganda, Zimbabwe,Msumbiji,Afrika kusini, Rwanda, Burundi nk. Na katika vikao vyote vya maraisi au wakuu wa nchi akikosekana Mwl J.K. Nyerere hakionekani kama ni kikao harari umuhimu wake ulikuwa unaonekana na hekima zake pia.

Leo nimeshindwa kushangaa kuona ni kwanini maraisi wa baadhi ya nchi hizo hawajona umuhimu huo na kuja kujumuika nasi kusherehekea miaka 50 ya Tanganyika yetu kama sisi tuliovyoona umuhimu wa utu wao katika kuwasaidia kupata uhuru wao?

1. Je hatuna maana kwao na thamani pia
2. Hatuaminiki na hatuna tena mchango kwao
3. nk

Wadau nisaidieni kutatua changamoto ndani ya kichwa changu
 
Na bado naiona amani na maendeleo SADC kuliko EAC,falsafa ya EAC bado haiko bayana na imekaa kijanjakijanja (kihuni) zaidi,Tz tumechomekwa tu bila kurealise kwanini tuungane ama la
 
Waje kufanya nini wakati nchi wanayojua ilipata uhuru 9 december mlishaizika, hata bendera hamna si upuuzi huu?
 
Maraisi wa Afrika Mashariki wamepata dharura na kushindwa kuja kuhudhuria sherehe za kutimiza miaka 50 ya uhuru wetu.

Je,wamezira sababu tumekataa kuweka ardhi yetu rehani ktk shirikisho la A. Mashariki?

Hawa kweli ni wenzetu kama wanavyotaka tuwaamini?

Hivi hatuwezi kuendelea mpaka tuwe na 'ushosti' nao?
 
Tanzania Bara ilipewa uhuru mwaka gani ,ina bendera gani,mipaka yake ni upi ,sasa hao maraisi waje kwenye isiyona mipaka
 
Hao wanaojiita marafiki toka EA ni wanafiki wakubwa, wameona tumewanyima ardhi yetu ndio wamekasirika. Bora hata hawajaja maana wangetuchefua.
 
Niliandika kwa nini rais hatembelewi na marais wa nchi jirani, nikasema hakuna mipango ya pamoja kati yetu na hao. Matokeo yake ndio haya yaani wanaona hakuna haja ya kuimarisha mahusiano yasiyo na tija.
 
Jumuiya ya kiini macho hii... Kwani hukusikia majirani zetu Kenya walivyotushikia bango Tanzania tusiruhusiwe kuuza Ivory zilizotaifishwa kutoka kwa majangili?
 
Watanganyika toka miaka ya 1963 - 1985 tulikuwa maalufu sana katika kusaidia nchi nyingi za kiafrika kupata Uhuru wao Kama vile Uganda, Zimbabwe,Msumbiji,Afrika kusini, Rwanda, Burundi nk. Na katika vikao vyote vya maraisi au wakuu wa nchi akikosekana Mwl J.K. Nyerere hakionekani kama ni kikao harari umuhimu wake ulikuwa unaonekana na hekima zake pia.

Leo nimeshindwa kushangaa kuona ni kwanini maraisi wa baadhi ya nchi hizo hawajona umuhimu huo na kuja kujumuika nasi kusherehekea miaka 50 ya Tanganyika yetu kama sisi tuliovyoona umuhimu wa utu wao katika kuwasaidia kupata uhuru wao?

1. Je hatuna maana kwao na thamani pia
2. Hatuaminiki na hatuna tena mchango kwao
3. nk

Wadau nisaidieni kutatua changamoto ndani ya kichwa changu

Wanasiskitika sana kwa vile tumepoteza uhuru wetu, walituma wajumbe kuadhimisha siku tu. Hii ni kama watanzania wengi walivyokataa kushiriki. Je wewe ulishiriki?

Hii ni aibu kwa serikali na chama tawala, inafaa wajiulize kulikoni?

Jumuiya ya kiini macho hii... Kwani hukusikia majirani zetu Kenya walivyotushikia bango Tanzania tusiruhusiwe kuuza Ivory zilizotaifishwa kutoka kwa majangili?

Kama huwa unafuatilia taarifa za habari kuna Ivory zilipatikana zikiwa zinasafirishwa na gari ya polisi na zilikuwa za mwenyekiti wa CCM mkoa fulani wa nyanda za juu kusini.

Kwa hiyo kama itaruhusiwa kuuzwa hizo Ivory si ajabu na ''wakubwa'' wakapitisha humo humo Ivory haramu.

Nawaunga mkono wa kenya na wengine wote waliokwamisha hilo swala la kuuzwa hayo meno ya tembo...
 
Ukiacha marais wa EAC wote kuwa na dharura kwa mpigo na hivyo
kushindwa kuja, ni viongozi gani wengine wa nchi za nje wameshiriki?

Jirani yako akishindwa kuja kujumuika nawe kwenye jambo kubwa kama hili, inabidi
kujiuliza mara mbilimbili!
 
Tanzania bado inatawaliwa na wakoloni weusi. Wanashangaa Tanzania inapo adimisha uhuru wa nchi nyingine!
 
Wako bize kujenga Nchi zao. Wanawajibika wako kikazi zaidi na ndio maana wamepunguza utegemezi aa misaada ya kina Cameroon . Wa kwetu hata ingekuwa kwenda kufungua bar angekwenda kwani Hana kazi za kufanya anasubiri misaada tu.
 
Back
Top Bottom