Tanzania yazidi kupanda kwenye FIFA ranking

Belo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
12,882
10,193
Baada ya kufanikiwa kufuzu mashindano ya CHAN ,Tanzania imepanda juu kwa nafasi sita juu zaidi
Kutoka nafasi ya 105 hadi ya 99
Keep it up MAXIMO hadi tuingie kwenye top 50
 
Baada ya kufanikiwa kufuzu mashindano ya CHAN ,Tanzania imepanda juu kwa nafasi sita juu zaidi
Kutoka nafasi ya 105 hadi ya 99
Keep it up MAXIMO hadi tuingie kwenye top 50

Ivi vitu zamani tulikua tunaona ni kama ndoto tu
 
What I do believe is: TUNAWEZA!

Msimpongeze Maximo pekee, hata Tenga kwa kutokuwa na mizengwe kama ya waliomtangulia. Waliigeuza FAT (enzi hizo) shamba la bibi!
 
MAXIMO bado kibarua anacho cha kutengeneza STRIKERS nafikiri lazima TFF watamuongezea mkataba ,tunamhitaji kwa miaka kama 4 zaidi
 
What I do believe is: TUNAWEZA!

Msimpongeze Maximo pekee, hata Tenga kwa kutokuwa na mizengwe kama ya waliomtangulia. Waliigeuza FAT (enzi hizo) shamba la bibi!

In fact the congrats should go way up to big guy, I mean JK
 
Baada ya kufanikiwa kufuzu mashindano ya CHAN ,Tanzania imepanda juu kwa nafasi sita juu zaidi
Kutoka nafasi ya 105 hadi ya 99
Keep it up MAXIMO hadi tuingie kwenye top 50
hiyo imekaa freshi
ila tukumbuke kuwa haya mashindano ya CHAN hayatambuliwi na fifa.ingekuwa yapo kwenye kalenda ya fifa basi tungekuwa kwenye nafasi ya 60hivi.so kilichotusaidia hapo ni kuwafunga wale wazaramo(msumbiji)
 
Hapo umenena mkubwa,bila JK kufanya mpango wakumleta Maximo yanayotokea sasa kwa Stars yangekuwa ni ndoto

Kwa hiyo ametimiza moja ya ahadi zake alizotoa 2005 za kuinua kiwango cha soka nchini?

Haya mpeni kura ya ndio 2010 aendelee kula na mafisadi.
 
Originally Posted by Roya Roy
In fact the congrats should go way up to big guy, I mean JK

Originally Posted by Balantanda
Hapo umenena mkubwa,bila JK kufanya mpango wakumleta Maximo yanayotokea sasa kwa Stars yangekuwa ni ndoto

I agree, but msitusahau na sisi washangiliaji!!! wadau wako wengi sana!!!
 
Kwa hiyo ametimiza moja ya ahadi zake alizotoa 2005 za kuinua kiwango cha soka nchini?

Haya mpeni kura ya ndio 2010 aendelee kula na mafisadi.

Heshima yako mama..Kimsingi mimi nazungumzia kitendo cha JK kama rais kumleta kocha huyu(Maximo) kwa jinsi kilivyosaidia kubadilisha kiwango cha uchezaji wa timu yetu ya Taifa..sizungumzii(maana hapa si mahali pake) utelelezaji wa Ilani ya CCM bali nazungumzia ujio wa kocha Maximo ulivyobadilisha ufanisi wa Timu yetu ya Taifa kiasi kwamba imeweza kufuzu kushiriki katika CHAN pamoja na nchi yetu kupanda nafasi 6 juu(sasa hivi ni wa 99) katika ubora wa soka duniani....Ubarikiwe sana mama,tupo pamoja
 
I agree, but msitusahau na sisi washangiliaji!!! wadau wako wengi sana!!!

Ni kweli kabisa mkuu,bila hamasa ya Watanzania(mshikamano pamoja na kuikosoa pale inapokosea) timu hii isingefika hapo,so washangiliaji wanastahili pongezi nyingi tu..Heshima mbele mkuu...Be blessed
 
Huwezi ukaseparate ujio wa Maximo na ilani za CCM. Hiyo ilikuwa kwenye ilani yake...na pengine ndiyo iliyowaconvince wanamichezo wakampigia kura. Asingeukwaa Urais asingeweza kumleta Maximo, uongo?
 
Huwezi ukaseparate ujio wa Maximo na ilani za CCM. Hiyo ilikuwa kwenye ilani yake...na pengine ndiyo iliyowaconvince wanamichezo wakampigia kura. Asingeukwaa Urais asingeweza kumleta Maximo, uongo?

Ok mama yangu nimekusoma,hata hivyo binafsi sijui contents za ilani ya uchaguzi ya CCM,lengo la mchango wangu wa awali lilikuwa ni kumpongeza tu JK kwa kitendo chake cha kumleta Mtaalam Maximo ambaye mimi kama mnazi mkubwa wa soka nafurahishwa na kile anachokifanya katika kuibadilisha timu yetu ya Taifa..Nilichangia kama mwanamichezo zaidi bila kuangalia upande wa pili wa Ilani ya uchaguzi ya CCM...So kama mwanamichezo(bila kujali itikadi za kisiasa) bado nitazidi kushawishika kumpongeza Rais JK kwa kumleta Maximo....Nakushukuru mama kwa maoni yako..uzidi kubarikiwa
 
Hata mimi hapa mwanamichezo, ila inanibidi niliangalie swala hili pande zote, otherwise rahisi kuwa drowned na ushabiki.
 
What I do believe is: TUNAWEZA!

Msimpongeze Maximo pekee, hata Tenga kwa kutokuwa na mizengwe kama ya waliomtangulia. Waliigeuza FAT (enzi hizo) shamba la bibi!

Wapo wengi wa kupongezwa pamoja na sisi mashabiki kuwaunga mkono...vile vile Kondic wa Yanga kusaidia 90% ya kikosi cha kwanza... naua wengine hawatapenda...
 
vile vile Kondic wa Yanga kusaidia 90% ya kikosi cha kwanza... naua wengine hawatapenda...

Huyo KONDIC kamtengeneza nani hapo Yanga tangu aje hata Tegete anawekwa benchi kisa wakenya na bado anazidi kuleta wengine
Nsajigwa,Canavaro,Chuji,Maftah,Tegete,Ngasa wamenza kucheza Stars kabla hata ya huyo KONDIC
 
Nakubariana na Ushirombo, Maximo mbali na utaalam alionao pia hatuwezi kuwasahau makocha wa timu za Yanga na Simba kwa kazi nzuri wanayofanya mpaka Maximo akawa na pool nzuri ya wachezaji anaowataka. Angekuja miaka ile bado kisingeleweka kitu....
Kocha wa stars anakaa na wachezaji kwa muda mfupi sana, hivyo pongezi nusu lazima ziwaendee makocha wa timu kongwe!!!
 
Kila thread unayokwenda basi lazima utakuta neno ccm na siasa...yani kila kitu siasa tuu ebo....!!!
Nawapongeza wachezaji, kocha, TFF washabiki na Watanzania kwa ujumla maana nakumbuka miaka michache nyuma kutoka kwenye 100s ilikuwa ni mbinde na ndoto.
 
Back
Top Bottom