Tanzania yawatuliza wanaopinga uuzaji meno ya tembo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,295
33,079
menotembo.jpg
Meno ya Tembo yakiwa yamehifadhiwa

Na mwandishi wetu, DodomaMAZUNGUMZO ya kidiplomasia kati ya Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda yamefanyika, ili kuzifanya nchi hizo zisiweke pingamizi wakati Tanzania itakapopeleka tena mswada wa kuomba kuruhusiwa kuuza sehemu yake ya meno ya ndovu .

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, ambaye alisema chini ya mazungumzo hayo, serikali ilizieleza nchi hizo nia yake ya kutaka kuuza sehemu ya pembe za ndovu.

Alisema kwa msingi huo, serikali haitegemei tena kama kutakuwa na kikwazo kutoka katika nchi hizo wakati mswada huo utakapowasilishwa tena ili kuomba ruhusa ya kuuza pembe hizo.


Maige alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi wananchama wa mkataba wa kimataifa wa kudhibiti biashara ya kimataifa wa wanyama na mimea iliyo hatarini kutoweka (Cites), uliosainiwa mwaka 1973 na kuanza kutekelezwa mwaka 1975.

Alisema kwa upande wake, Tanzania iliridhia mkataba huo mwaka 1980.

Alisema kutokana ongezeko la ujangili dhidi ya tembo na biashara ya meno ya wanyama hao, mwaka 1988, Tanzania ilisimamisha biashara ya meno ya tembo, jambo linaloonyesha nchini ilikuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za Cites.

Kwa mujibu wa Naibu waziri, tangu wakati huo meno ya tembo hapa nchini yamekuwa yakihifadhiwa katika maghala ya kuhifadhia nyara za serikali bila kufanyiwa biashara.


Alisema kuongezeka kwa idadi ya tembo hapa nchini, kutoka 55, 000 mwaka 1989 hadi kufikia 110,000 mwaka 2009 pia kumesababisha kuongezeka kwa meno ya tembo kwenye ghala.

"Lakini pia hali hiyo imesababisha kuongezeka kwa gharama za kutunza meno hayo. Kwa hiyo mwaka 2010 Tanzania iliamua kuwasilisha kwa Sektrerieti ya Cites muswada wa kuuza meno ya tembo ili ujadiliwe katika mkutano mkuu wa 15 wa nchi wanachama," alisema.

Alisema uamuzi wa kuwasilisha muswada kama huo ni wa kawaida ingawa hata hivyo kuna propaganda dhidi ya Tanzania.

Alisema propaganda hizo zilifanywa na mashirika mbalimbali ya kimataifa yasiyo ya kiserikali na baadhi ya nchi za Afrika zikiwemo nchi jirani.


Alisema kwa jumla, propaganda hizo ziliathiri kusudio la Tanzania kwa sababu zilitoa picha potofu.

Maige alisema baadhi ya wapotoshai hao walidai kuwa fedha ambazo zingepatikana kwa kuuza meno hayo zingetumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na si kwa uhifadhi wa tembo.


Maige alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kongwa,Job Nduai aliyetaka kauli ya serikali kuhusu hatma ya meno ya ndovu yaliyohifadhiwa ghalani.

Chanzo Tanzania yawatuliza wanaopinga uuzaji meno ya tembo

Serikali badala ya kulimaliza tatizo la Ujangil wa Meno ya Tembo. Serikali inataka meno ya Tembo yaliyokuwepo yauzwe kasheshe kweli. Jamani huko kwetu kuna Serikali?
 
"Kuongezeka kwa tembo kutoka 55,000 hadi 110,000 kumesababishaje kuongezeka kwa meno ya tembo katika ghala?" Yaani tembo wakiongezeka na meno yao yanaongezeka katika ghala? Hawa tembo waliuwawaje? Hilo mbona serikali haielezi?
 
Back
Top Bottom