Tanzania yatuma ujumbe mzito South Africa

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,917
31,157
Jana nilikuwa natazama mahojiano baina Mheshimiwa B Membe na Marin Hassan wa TBC1 kuhusiana na jaribio la mauaji Lt General Faustin K Nyamwasa.

Mheshimiwa B Membe alisema serekali imestuswa sana kusikia miongoni mwa watuhumiwa wa jaribio la mauaji ya Lt General F K Nyamwasa wapo watanzania wawili.Kuhusiswa raia wa Tanzania kwenye jaribio la mauaji ya Lt Gen Nyamwasa kumechafua sana sifa ya Tanzania kimataifa

Serekali ya Tanzania imetuma ujumbe mzito[ulinzi & Usalama] kwenda Afrika kusini kuchunguza uraia wa watuhumiwa hao.
 
Yetu macho..
 
Watawala wa Tanzania wanachekesha kweli.Hivi wakijua uraia iansaidia nini ?.Wauaaji wanaweza kuwa raia wa Tanzania au kenya au wakawa na uraia wa nchi yoyote ile it does not matter.

Issue kubwa hapa ni kujua ni nani aliyewatuma kufanya mauaji.Membe na genge la watawala wanapaswa kuwaeleza wananchi na dunia kwa ujumla kama tumekubali kumtumikia dikteta P Kagema kuendeleza mauaji ya watu wasiokubaliana na uzandiki wake.
 
Heshima kwako Bantugbro,

Fafanua kidogo sijakuelewa una maana gani ?.

Heshima kwako mkuu,

Namaanisha kwamba kuna mambo makubwa mawili ambayo yanaweza kutokea: 1) Jamaa wanaweza kuwa ni wabongo kweli lakini wakawa wametumiwa na nchi flani ili kuficha ukweli wa hali tete ya kisiasa huko kwao. 2) Jamaa wanaweza kuwa wabongo wakuchonga! yaani wanakila-karatasi ya bongo na wanongea kiswahili fasaha lakini si wabongo!
 
hata kama wakiwa watz they are contractors, sioni ni kwa vipi nchi imechafuka, as they dont represent utash wa watz wote na sioni sababu ya kutuma eti ujumbe mzito. Hiyo ni ufisadi mwingine kwa pesa za walipa kodi.
 
Per diems..

Heshima kwako Abdulhalim,

Mkuu afadhali wachote per diems wakafanye kazi ya kusafisha jina la nchi kuliko kukaa kimya tu bila kufanya juhudi zozote.Ni kweli upo uwezekano mkubwa tukakuta raia wanaodaiwa ni wa Tanzania kukutwa wala hawajui kiswahili vizuri.Unajua pasport za Tanzania zinauzwa holela kama njugu,wapo wasomali kibao wanahodhi pasport za Tanzania.

Kubwa zaidi inategemea wametumwa na nani ?.
 
Jana nilikuwa natazama mahojiano baina Mheshimiwa B Membe na Marin Hassan wa TBC1 kuhusiana na jaribio la mauaji Lt General Faustin K Nyamwasa.

Mheshimiwa B Membe alisema serekali imestuswa sana kusikia miongoni mwa watuhumiwa wa jaribio la mauaji ya Lt General F K Nyamwasa wapo watanzania wawili.Kuhusiswa raia wa Tanzania kwenye jaribio la mauaji ya Lt Gen Nyamwasa kumechafua sana sifa ya Tanzania kimataifa

Serekali ya Tanzania imetuma ujumbe mzito[ulinzi & Usalama] kwenda Afrika kusini kuchunguza uraia wa watuhumiwa hao.

Ubalozi wetu South Afrika hauwezi kutolea taarifa sahihi ya wanaohusishwa na tukio hili? Kwani wakijua Passport namba si wizara ya mambo ya ndani una taarifa zote? - another misuse of national resorces
 
hata kama wakiwa watz they are contractors, sioni ni kwa vipi nchi imechafuka, as they dont represent utash wa watz wote na sioni sababu ya kutuma eti ujumbe mzito. Hiyo ni ufisadi mwingine kwa pesa za walipa kodi.

Mkuu kumbuka huyo alietiwa mbaroni sio muuza madafu.......! Angekuwa muuza magazeti tu asingetumwa mtu toka Dar kwenda huko, si angetumwa messenger tu pale ubalozini akamjulie hali!
 
Safi sana. Familia fulani sasa wanasubiri zawadi kutoka kwa ndugu zao waliokwenda bondeni.

Yes, hela ya masurufu kwa kwenda mbele......... Acha na wao wafaidi.
 
As much as Tanzania played a "KEY ROLE" in Southern-Africa "Independence struggle" - It is playing the same role to "DISTABILIZE" the Great-Lakes region!

Role ya Tanzania ndani ya DR-Congo ni kubwa sana kuliko inavyosemekana -

Tanzania ilimeka madarakani M7 - M7 akamweka madarakani Kagame - Kagame akamweka madarakani Kabila Senior:

Kabila senior akauliwa na "mlinzi wake" - M7 na Kagame wakapigana vita "ndani ya DR-Congo" - Wapinzani wa Kagame wakakimbilia kwa M7:

Ni mduara tu wa "KUGOMBANIA MADARAKA - Power Struggle" na "RASILIMALI ZA DR-Congo"
 
As much as Tanzania played a "KEY ROLE" in Southern-Africa "Independence struggle" - It is played the same role to "DISTABILIZE" the Great-Lakes region! ...

Mkuu hapo unaingia kwenye mada nyingine. Suala hapa ni kuwa: kule kuhusishwa kwa watanzania katika skandali katika anga za kimataifa si lazima nchi ihusike. Wahuni hawana taifa. Wako watanzania katika kila fani ya jinai huko nje. Hatuwezi kudandia kila habari eti kwa vile mTZ katajwa. Inakuwaje basi leo hii Membe apande jazba na fununu hii kiasi cha kuamua kufuja rasilimali za nchi na muda kujaribu kusafisha kisichotuhusu kama taifa? Kuna walioilalamikia Serikali yetu? Huyu bwana naona ama IQ yake iko chini au ana kazi mbaya isiyohitaji soni. Ndio maana hata mshiko wa rada anauelezea kama kitu cha kawaida kabisa bila kuiona idhara inayoiandama Serikali baada ya kushindwa kuwawajibisha wahusika.
 
As much as Tanzania played a "KEY ROLE" in Southern-Africa "Independence struggle" - It is playing the same role to "DISTABILIZE" the Great-Lakes region! ...

Mkuu hapo unaingia kwenye mada nyingine. Suala hapa ni kuwa: kule kuhusishwa kwa watanzania katika skandali katika anga za kimataifa si lazima nchi ihusike. Wahuni hawana taifa. Wako watanzania katika kila fani ya jinai huko nje. Hatuwezi kudandia kila habari eti kwa vile mTZ katajwa. Inakuwaje basi leo hii Membe apande jazba na fununu hii kiasi cha kuamua kufuja rasilimali za nchi na muda kujaribu kusafisha kisichotuhusu kama taifa? Kuna walioilalamikia Serikali yetu? Huyu bwana naona ama IQ yake iko chini au ana kazi mbaya isiyohitaji soni. Ndio maana hata mshiko wa rada anauelezea kama kitu cha kawaida kabisa bila kuiona idhara inayoiandama Serikali baada ya kushindwa kuwawajibisha wahusika.

Ni mada ile ile mkuu - ila inakuja na sura nyingine:

Jaziba za Membe - ni sawa sawa na kukuta mtoto amelamba sukari nyumbani: unapomuuliza kwanini amefanya hivyo: yeye anapangusa midomo!
 
Baada ya kupitia maoni ya baadhi ya wachangiaji naanza kupata wasiwasi jinsi serekali inavyoshughulikia hii issue.Inavyoelekea hawa jamaa waliokamatwa si watu wa kawaida kama serekali inavyotaka kutuadaa.Yamkini kuna mambo makubwa yamejificha ndio maana serekali imekurupuka kulishughulikia hili jambo.
 
Heshima kwako mkuu,

Namaanisha kwamba kuna mambo makubwa mawili ambayo yanaweza kutokea: 1) Jamaa wanaweza kuwa ni wabongo kweli lakini wakawa wametumiwa na nchi flani ili kuficha ukweli wa hali tete ya kisiasa huko kwao. 2) Jamaa wanaweza kuwa wabongo wakuchonga! yaani wanakila-karatasi ya bongo na wanongea kiswahili fasaha lakini si wabongo!

3. Wanaweza kuwa wabongo.
 
Back
Top Bottom